Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Watoto na Malezi/Elimu. Show all posts
Showing posts with label Watoto na Malezi/Elimu. Show all posts

Tuesday, 24 March 2020

Watoto na Malezi-Shule ya Nyumbani Na Rachel-siwa...






8:00-Kuamka watoto na kujiandaa/kuwa andaa

8:30-Kifungua Kinywa
9:00-Kazi ya shule, 
10:30-Muda wa vitafunwa 
11:00-Kutembea/kunyoosha miguu
11;30-Kusoma na kufanya kazi za shule
1:00- Chakula cha mchana 
1:30-Muda wa kupumzika
2:00-Kazi za Shule;Muziki,kuchora n.k
3:00-Michezo/mazoezi 
3:45-Usafi/kufungasha na kazi zingine za kusadia nyumbani
4:00- Muda wa kupumzika,vitafunwa
5:30-Kujifunza Dini/Imani, 
6:00-Wakati wa chakula cha jioni, kupumzika/TV
7:30-Kujiandaa kulala;kusoma vitabu,kusali
8;30-  Kwenda kulala
9:00- Taa zizimwe ... 

Shule ya Nyumbani, Shule ya mama Na Rachel Siwa


Mpendwa unaweza kuchangia mawazo yako pia
kupunguza/kuongezea na kusahihisha kwa upendo.
ili tusaidiane kwa wakati huu Watoto wapo Nyumbani..

Nitumie;email-rasca@hotmail.co.uk
Comment na unaweza ku share na wengine..

Asante.

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.



Tuesday, 20 June 2017

Samwel Mwanyika Anyakua tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.


Habari na Picha za Freddy Macha



TUMEZOEA kuwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Ila sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....

Monday, 8 December 2014

Tunaweza Badilika - Mzee Yusuf & Khadija Kopa


Collabo ya kihistoria kati ya Mfalme Mzee Yusuf na Malkia Khadija Kopa katika wimbo na video ya pamoja yenye malengo ya kuhamasisha jamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake.

Video hii iliyorekodiwa mkoani Morogoro inamuonyesha Mzee Yusuf na Khadija Kopa kama mume na mke ambao wamebahatika kupata watoto wawili 'Kulwa' na 'Doto' ambao ni mapacha. Mzee Yusuf ni dereva wa daladala wakati Khadija ni mama wa nyumbani lakini pia mjasiriamali.

Pamoja na kwamba watoto wao ni mapacha ambao wanafanana na kulingana kwa karibu kila kitu ikiwemo umri lakini tofauti ya jinsi yao inaonekana kumpa haki zaidi mtoto wa kiume ambaye anaonekana kuelekea shuleni wakati pacha mwenzie anaonekana kuhangaika na shughuli za nyumbani ikiwemo kutafuta maji, kufanya usafi n.k.

Kwa upande mwingine, Mzee anaonekana kutokuijali familia yake haachi pesa ya matumizi nyumbani na hata anapoulizwa anakuwa mkali sana wakati huo huo anaonekana kuchezea mabinti wengine akiwa kazini.

Stori inabadilika kabisa pale mzee anapokutana na Mwanamabadiliko ambaye anafanikiwa kumshawishi kubadili tabia hizo kwa ajili ya manufaa ya familia yake. Kuanzia hapo Mzee anaonekana akinunua nguo za shule za mwanae wa kike na kubandika ujumbe wa mabadiliko katika gari na nyumba yake.

Baada ya hapo maisha yanaonekana kuwa ya raha mustarehe.

"Tukae na tu-starehe tule raha na maisha." Kinasema kibwagizo katika wimbo huo.



Shukrani,zaidi ingia;Tunaweza

Tuesday, 15 October 2013

Mahojiano na wadau wa darasa la Kiswahili Washington DC‏

Photo Credits: Panafricanvisions.com
Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi kusini mwa jangwa la sahara.

Kama
tunavyojua, ni lugha ya taifa kwa nchi za Tanzania naKenya, na pia
yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi,
Rwanda, Uganda na visiwa vya Comoro.

Ikizungumzwa na watu
wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee
ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na
inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani

Na matumizi
yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi
kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na
biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.

Kiswahili sasa
kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia
inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.

Kiswahili
ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na
hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya
waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha
darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.

Na leo,
wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV
(Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha
Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami
katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.

KARIBU UUNGANE NASI

Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Iddi Sandaly akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Bernadeta Kaiza ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Asha Nyang'anyi akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Twawapenda....Tukutane juma lijalo kwa kipindi kingine cha HUYU NA YULE tutakapohojiana na wadau wengine juu ya jambo jingine MUHIMU kwa jamii yetu

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Wednesday, 12 June 2013

Kueleke Siku Ya Mtoto Wa Afrika; Wazo La Leo na Emu-Three!!!!!!



WAZO LA LEO:,Kumbuka ipo siku maalumu, inayotambulikana kama ya siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16 June, sijui kama upo makini na siku hii, huenda kwako ni historia tu ya Mauaji ya Soweto…kwani unaishi kwenye kisiwa cha amani, huna shida…una kazi nzuri, gari..nk. Lakini kumbuka kuna hawa watoto wa mitaani, unawakumbuka?

 Je siku ya mtoto kwako inakugusaje?


Je wewe kama mzazi, unahisije ukiwaona watoto wa mitaani, au ndio huko kusema, `hawa watoto wanaomba omba tu, hawaendi shule…’ hawa kwa mateso wanayoyapata hawana tofauti na wale watoto waliouwawa kikatili,…..wewe hutumii, silaha, lakini unatumia njia nyingine, isiyoonekana, ya kutokutimiza wajibu wako kama mzazi.


Kumbuka mateso wanayopata hawa watoto, kwanza kisaikolojia pale wanapoona wenzao wakiwa kwenye sare za shule, au wakipita na magari wakiepelekwa mashuleni.  Lakini pia kuwa mateso ya afya zao, kwani wengine wanaishia majalalani kuokota yale mabaki ya vyakula mliyokula na kusaza. Huyu ni mtoto wako hata kama hukumzaa wewe, kumbukeni kila mtoto ana mzazi, na mzazi wake ni mimi na wewe.

Imeandikwa na emu-three wa Diary Yangu.



Zaidi ingia kwa ndugu wa mimi,Pia kwa Visa vya kusisimua na Mambo meengi;http://miram3.blogspot.co.uk/




Kwa Habari na mambo meengi ya watoto,wazazi/walezi nifuate huku;http://www.watotonajamii.blogspot.co.uk/



Wednesday, 12 September 2012

Tujikumbushe;Baraza la Watoto - Mahojiano na Rais, A,B,,C..!!!!!!!!


Waungwana; Tujikumbushe na kama hujaona,Baraza la Watoto,Mahojiano na Rais wa Jamuhuri ya Tanzania.Muheshimiwa .JAKAYA  KIKWETE.
Kuna lolote,Umejifunza/ unataka kutueleza kupita Video hizi?Karibu sana Tuelimishane kwa Upendo.Video hizi zinaendelea, kuona zaidi na kujifunza meengi ingia;CreativeGenesTZ pia unaweza kufuatana nao kupitia; twitter@creativegenesTz.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.