Hamjambo Wazazi/Walezi na Watoto wangu Wapendwa? Summer Time....Wakati wa Jua umewadia,Hiki ni kipindi kizuri sana hapa Ng'ambo kwa Michezo ya Nje,Unaweza kuvaa vizuri na si nguo nyiingi yaani makoti,Masweta na.......Pia kunakuwa na Likizo[Summer Holiday].
Maandalizi Ya "Family Fun Day" zaidi itakuwa Michezo;Kuchora,Kuimba,Kucheza,Mitindo,Kuangalia Vipaji vya Watoto wetu,Nyama Choma na VyaKula vingine, Kufurahi Pamoja... na Watoto.
Wengi huwa wanakwenda Likizo Afrika na sehemu nyingine kwa wale watakao kuwepo kwa mwaka huu tutafanya tukutane na kucheza pamoja.
Itakuwa baada ya mfungo wa Ramadhani ili wote tufurahi pamoja.
Tarehe 02/08 panapo Majaaliwa.
Kama kuna Ushauri,Msaada katika kuandaa na Mengine yote,Usisite kuwasiliana nami.
Email;rasca@hotmail.co.uk.
Simu;0750 44 100 40.
Wote Mnakaribishwa katika Yote.
kuhusu mambo ya Watoto zaidi;http://watotonajamii.blogspot.co.uk/
Swali;Kwanini watoto wetu ni waoga?
Kwanini Hawajiamini?
Kwanini wana Aibu?