Showing posts with label waTanzania/Mahojiano. Show all posts
Showing posts with label waTanzania/Mahojiano. Show all posts
Wednesday, 1 October 2014
Tuesday, 19 August 2014
[VIDEO]: Mazungumzo na Liberatus Mwang'ombe na Solomon Chris baada ya Uchaguzi DMV
Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano |
Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu.
Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014.
Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga
Mazungumzo na Salma Moshi kuhusu uchaguzi DMV
Salma Moshi akizungumza na Mubelwa Bandio kwenye mahojiano haya
Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu.
Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Mmoja wa wagombea hao, Salma Moshi amaketi nasi kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014 chini ya utayarishaji wa Vijimambo Blog
Karibu uungane nasi kusikia anachopinga
Thursday, 7 August 2014
Monday, 23 June 2014
Mahojiano ya Kwanza Production na Haika Lawere. Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel
Haika Lawere akizungumza na wanawake kwenye tukio la wanawake waTanzania Washington DC
Photo Credits: IskaJojo Studios
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Haika Lawere.Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mbezi Garden Hotel ya Dar Es Salaam Tanzania.
Amezungumzia mengi kuhusu maisha yake, kazi yake, changamoto anazokumbana nazo katika kazi, ziara yake hapa Marekani na hata ushauri wake kwa wasikilizaji
Amezungumza mengi mema
Karibu uungane nasi
Kwa maoni ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail dot com
Monday, 26 May 2014
Mahojiano ya Idd Ligongo (Bicco) na Kwanza Production
Photo Credits: Idd's Facebook Page |
Msanii na mwanahabari makini ambaye amezungumza mengi mema kuhusu Sanaa na Habari ya Tanzania.
Amezungumzia historia yake katika fani hizi, ilipo na anapoiona ikielekea
Ni kati ya mazungumzo ninayoamini utapata mengi ya kujifunza.
KARIBU UNGANE NASI
Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com
Monday, 19 May 2014
Mahojiano ya Maggid Mjengwa na Kwanza Production
Maggid Mjengwa |
Karibu katika mahojiano mwanahabari makini na wa muda mrefu ambaye pia ni mmiliki wa Kwanza Jamii, Maggid Mjengwa na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production.
Amegusia mambo mbalimbali kama masuala ya uandishi, siasa (kama mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba) na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.
Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu masuala tofauti yaliyo muhimu kwa mustakabali wa nchi za Afrika Mashariki

Karibu
Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com
Monday, 28 April 2014
Mhe Mwigulu Nchemba akizungumzia suala la uraia pacha Washington DC
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akihojiana na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production Washington DC. Photo Credits: Habari Kwanza blog |
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa anajivunia kiasi cha UZALENDO walichonacho waTanzania hapa nchini, jambo linalompa moyo kuendeleza harakati zake za kusaidia kupatikana kwa uraia pacha, ombi lililo kuu kwa waTanzania waishio nje ya nchi katika mabadiliko ya katiba mpya.
Mhe Nchemba, ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika jijini Washington DC nchini Marekani, amesema kuwa ushiriki wa waTanzania na rafiki zao katika maadhimisho haya, umemdhihirishia nia na mapenzi yao kwa nchi yao, na hilo limemsukuma zaidi kusaidia kupitishwa kwa suala la uraia pacha kwenye katiba mpya.
Hii ni ripoti katika kipindi cha Morning Jam

Wednesday, 4 December 2013
HUYU NA YULE: Mahojiano na waTanzania Evans Mhando na Fatuma Matulanga wakiwa CHINA
Katika huyu na yule wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa
wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga
aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja
tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana
Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo
1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA
2:TOFAUTI
KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi
ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?
3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?
4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?
5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?
6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)
Na mengine mengi
Ni
huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma
Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la
Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China
Kwa maoni ama ushauri, usisite kutuandikia kupitia jamiiproduction@gmail.com
--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"
Subscribe to:
Posts (Atom)