Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 22 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo25..

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Asante Mungu Baba kwa Mapenzi yako na kutupa kibali cha kuiona siku hii.
Wengi walitamani kuiona lakini imeshindikana, Sisi si kwamba ni wema sana,Wajuaji,wenyenguvu/Utashi hapana ni kwa Neema/Rehema yako Baba wa Mbinguni,Baba wa Mbinguni Ukatamalaki katika Nyumba zetu,Ndoazetu, Watoto/Familia zetu,Elimu,Kazizetu,Biashara na Maisha yetu.Mfalme wa Amani ukawaguse na kuwaponya wanaopitia Magumu/Majaribu, Shida/Tabu,Vifungo mbalimbali..
Mungu Baba ukavibariki na kuvitakasa vyote tunavyoenda kutumia/kugusa.
Roho mtakatifu akatuongoze kwenye kunena na Kutenda,Kutambua/kujitambua.
Baba ukatupe na kutuongezea Upendo,Amani,Furaha,Msamaha/kusamehe,kuchukuliana na kueleweshana/kukumbushana kwa wema.
Tunakwenda kinyume na mwovu,Tunajiachilia mikononi mwako Baba wa mbingu na nchi..
Tunashukuru na kuamini wewe ni Bwana na mwokozi wetu..
Amina..!!
Upendo wa Mungu Ukatamalaki kwa kila mmoja wetu.


Wazawa wengine wa Abrahamu

(1Nya 1:32-33)
1Abrahamu alioa mke mwingine, jina lake Ketura. 2Ketura alimzalia Abrahamu: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. 3Yokshani alimzaa Sheba na Dedani; wazawa wa Dedani walikuwa Waashuru, Waletushi na Waleumi. 4Watoto wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura.
5Abrahamu alimrithisha Isaka mali yake yote. 6Lakini watoto wa kiume wa masuria wake akawapa zawadi, na wakati alipokuwa bado hai, aliwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka mwanawe.

Kifo cha Abrahamu

7Abrahamu aliishi miaka 175. 8Alifariki baada ya kuishi maisha marefu na ya fanaka, akajiunga na wazee wake waliomtangulia. 9Isaka na Ishmaeli, wanawe Abrahamu, wakamzika baba yao katika pango la Makpela, mashariki ya Mamre kwenye shamba lililokuwa la Efroni, mwana wa Sohari, Mhiti. 10Abrahamu alikuwa amenunua shamba hilo kwa Wahiti. Huko ndiko alikozikwa Abrahamu na mkewe Sara. 11Baada ya kifo cha Abrahamu, Mungu alimbariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akawa anaishi karibu na kisima cha Beer-lahai-roi.

Wazawa wa Ishmaeli
(1Nya 1:28-31)
12Hawa ndio wazawa wa Ishmaeli mwanawe Abrahamu ambaye Hagari Mmisri, aliyekuwa mjakazi wa Sara, alimzalia Abrahamu. 13Hii ni orodha yao kufuatana na kuzaliwa kwao: Nebayothi, mzaliwa wa kwanza, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 14Mishma, Duma, Masa, 15Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. 16Hao ndio watoto wa kiume wa Ishmaeli, waliokuwa asili ya makabila kumi na mawili; makazi na vijiji vyao vilijulikana kwa majina yao. 17Ishmaeli alikuwa na umri wa miaka 137 alipofariki, akajiunga na wazee wake waliotangulia. 18Wazawa wa Ishmaeli walikaa katika eneo lililo kati ya Hawila na Shuri, mashariki ya Misri, kuelekea Ashuru. Walikaa kwa utengano na wazawa wengine wa Abrahamu.

Kuzaliwa kwa Esau na Yakobo

19Hawa ndio wazawa wa Isaka mwana wa Abrahamu. 20Isaka alipokuwa na umri wa miaka arubaini alimwoa Rebeka, binti Bethueli, Mwaramu wa Padan-aramu. Rebeka alikuwa dada yake Labani. 21Rebeka alikuwa tasa, kwa hiyo Isaka akamwomba Mwenyezi-Mungu. Naye Mwenyezi-Mungu akakubali ombi lake, Rebeka akapata mimba. 22Mimba hiyo ilikuwa ya mapacha. Watoto hao wakashindana tumboni mwake Rebeka, naye akasema, “Kama hivi ndivyo mambo yalivyo, ya nini kuishi?” Basi, akaenda kumwuliza Mwenyezi-Mungu. 23Mwenyezi-Mungu akamwambia,
“Mataifa mawili yamo tumboni mwako;
makabila mawili yatakayozaliwa nawe, yatafarakana.
Moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine;
mkubwa atamtumikia mdogo.”
24Siku zake za kujifungua zilipotimia, Rebeka alijifungua mapacha. 25Wa kwanza alikuwa mwekundu, mwenye nywele mwili wote; hivyo wakamwita Esau. 26Wa pili alizaliwa akiwa amemshika Esau kisigino, hivyo wakampa jina Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati Esau na Yakobo walipozaliwa.
Esau anauza haki yake
27Watoto hao wakakua; Esau akawa mwindaji hodari, mpenda maisha ya mbugani, na Yakobo akawa mtu mtulivu, mpenda maisha ya nyumbani. 28Basi, Isaka akampenda Esau kwa sababu alipenda kula mawindo yake, lakini Rebeka akampenda Yakobo.
29Siku moja, Yakobo alipokuwa anapika dengu, Esau alirudi nyumbani kutoka mawindoni ana njaa sana. 30Kwa hiyo akamwambia Yakobo, “Nafa njaa; tafadhali, nigawie chakula hicho chekundu nile.” (Ndiyo maana walimpanga jina Edomu yaani mwekundu). 31Yakobo akajibu, “Kwanza niuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza.” 32Esau akasema, “Sawa! Niko karibu kufa; haki yangu ya mzaliwa wa kwanza itanifaa nini?” 33Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Basi, Esau akamwapia na kumwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. 34Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na dengu kiasi. Esau akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo ndivyo Esau alivyoidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
Mwanzo25;1-34

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 21 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo24....

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Nimatumaini yangu mmeanza siku hii na Mungu..
Tumshukuru sana Mungu kwa Pumzi/Uzima,Afya na kutupa kibali cha kuiona leo hii..Ikawe yenye Baraka,Amani,Upendo,Furaha na Kumpendeza Mungu wetu muumba wa vyote..
Akatubariki Kuingia/Kutoka kwetu,Kazi,Biashara,Elimu,Vilaji/Vinywaji, Vyombo vya usafiri na tutembeapo Baba wa mbinguni awe nasi na kuvitakasa vyote tunavyoenda kugusa/kutumia..
Roho mtakatifu akatuongoze kwenye kunena na kutenda,Mungu baba aka
tupe na ukutuongezea Hekima,Busara,Uvumilivu,Utambuzi/kujitambua na kuheshimiana.
Mfalme wa Amani ukawafariji wafiwa,Ukawaponye na kuwaokoa Wenye Shida/Tabu,Wagonjwa,waliokata tamaa, wenyevifungombalimbali na wote wanaopitia Magumu/Majaribu yoyote.
Mfalme wa Amani ukatawale maisha yetu na ukatupe sawasawa na Mapenzi yako..
Tunajikabidhi mikononi mwako Baba wa mbinguni,Tukishukuru na kuamini kwamba wewe ni Bwana na mwokozi wetu..
Amina...!!
Muwe na Imani na Amani.


Isaka anaoa
1Sasa Abrahamu alikuwa mzee wa miaka mingi, naye Mwenyezi-Mungu alikuwa amembariki katika kila hali. 2Siku moja Abrahamu akamwambia mtumishi wake aliyekuwa mzee kuliko wengine na msimamizi wa mali yake yote, “Weka mkono wako mapajani mwangu, 3nami nitakuapisha kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa mbingu na dunia, kwamba hutamwoza mwanangu msichana yeyote miongoni mwa binti za Wakanaani ninaoishi nao. 4Niapie kwamba utakwenda mpaka katika nchi yangu, kwa jamaa zangu, umtafutie mwanangu Isaka mke.” 5Mtumishi akamwambia, “Huenda mwanamke huyo atakataa kufuatana nami kuja huku, ikiwa hivyo, je, ni lazima nimrudishe mwanao nchini ulikotoka?” 6Abrahamu akamwambia, “La! Angalia sana usimrudishe mwanangu huko. 7Mwenyezi-Mungu, Mungu wa mbingu, aliyenitoa nyumbani kwa baba yangu na kutoka katika nchi nilimozaliwa, na ambaye alisema nami, aliniapia kwamba atawapa wazawa wangu nchi hii. Yeye atamtuma malaika wake mbele yako ili umletee mwanangu mke kutoka huko. 8Iwapo mwanamke huyo hatapenda kufuatana nawe hadi huku, basi kiapo changu hakitakufunga, lakini kwa vyovyote vile usimrudishe mwanangu huko.” 9Basi, mtumishi huyo akaweka mkono wake mapajani mwa Abrahamu, bwana wake, akaapa kuhusu jambo hilo.
10Kisha, huyo mtumishi akachukua ngamia kumi wa bwana wake akaondoka akiwa na zawadi nzuri za kila aina. Akasafiri kwenda katika mji alimokaa Nahori, nchini Mesopotamia. 11Alipowasili, aliwapigisha magoti ngamia wake kando ya kisima kilichokuwa nje ya mji. Ilikuwa jioni wakati ambapo wanawake huenda kisimani kuteka maji. 12Naye akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nakuomba unijalie nifaulu leo na umfadhili Abrahamu bwana wangu. 13Niko hapa kando ya kisima ambapo binti za wenyeji wa mji huja kuteka maji. 14Basi, msichana nitakayemwambia atue mtungi wake wa maji anipatie maji ninywe, naye akanipa mimi pamoja na kuwanywesha ngamia wangu, na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka. Jambo hilo litanionesha kwamba umemfadhili bwana wangu.”
15Kabla hajamaliza kuomba, mara Rebeka, binti Bethueli, mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu yake Abrahamu, akafika amebeba mtungi wake begani. 16Msichana huyo alikuwa na sura ya kuvutia sana, na bikira ambaye hakuwa amelala na mwanamume yeyote. Basi, akateremka kisimani, akaujaza mtungi wake maji na kupanda. 17Ndipo yule mtumishi akaharakisha kukutana naye, akamwambia, “Tafadhali, nipatie maji ya kunywa kutoka mtungi wako.” 18Msichana akamjibu, “Haya kunywa bwana wangu.” Na papo hapo akautua mtungi wake, akiushikilia ili amnyweshe. 19Alipokwisha kumpatia maji, akamwambia, “Nitawatekea maji ngamia wako pia, wanywe mpaka watosheke.” 20Basi, akafanya haraka, akawamiminia ngamia maji ya mtungi wake katika hori, akakimbia kisimani kuteka maji mengine na kuwanywesha ngamia wake wote. 21Yule mtu akawa anamtazama kwa makini bila kusema lolote, apate kufahamu kama Mwenyezi-Mungu ameifanikisha safari yake au sivyo.
22Ngamia walipotosheka kunywa maji, yule mtu akampa huyo msichana pete ya dhahabu yenye uzito upatao gramu sita, na bangili mbili za dhahabu za gramu kumi kila moja. 23Akamwuliza, “Niambie tafadhali: Wewe ni binti nani? Je, kuna nafasi ya kulala nyumbani kwenu?” 24Rebeka akajibu, “Mimi ni binti Bethueli, mwana wa Milka, mkewe Nahori. 25Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha na mahali pa kulala wageni.” 26Ndipo yule mtu akainamisha kichwa chake, akamwabudu Mwenyezi-Mungu 27akisema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hajasahau fadhili zake na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mwenyezi-Mungu ameniongoza mimi mwenyewe moja kwa moja hadi kwa jamaa ya bwana wangu!”
28Kisha yule msichana akakimbia kwenda kuwapa habari jamaa za mama yake. 29Rebeka alikuwa na kaka yake aitwaye Labani. Labani akatoka mbio kukutana na yule mtu kisimani. 30Labani alikuwa ameiona ile pete na bangili mikononi mwa dada yake, na kusikia mambo Rebeka aliyoambiwa na huyo mtu. Labani alimkuta yule mtu amesimama karibu na ngamia wake kando ya kisima. 31Labani akamwambia, “Karibu kwetu wewe uliyebarikiwa na Mwenyezi-Mungu. Mbona unasimama nje? Mimi mwenyewe nimekwisha tayarisha nyumba na mahali kwa ajili ya hawa ngamia wako!” 32Basi, mtumishi huyo wa Abrahamu akaingia nyumbani. Labani akawafungua ngamia na kuwapatia majani ngamia wake, akampa yeye na watu wake maji ya kunawa miguu. 33Basi, wakamwandalia chakula, lakini yeye akasema, “Sitakula mpaka nimesema ninachotaka kusema.” Labani akamwambia, “Haya, tuambie.”
34Yule mtu akasema, “Mimi ni mtumishi wa Abrahamu. 35Mwenyezi-Mungu amembariki sana bwana wangu, naye amekuwa mtu maarufu. Amempa makundi ya kondoo na mifugo mingi, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda! 36Sara, mke wa bwana wangu katika uzee wake, alimzalia bwana wangu mtoto; na bwana wangu amempa huyo mtoto mali yake yote. 37Bwana wangu aliniapisha mimi akisema, ‘Hutamwoza mwanangu msichana yeyote miongoni mwa binti za Wakanaani ambao ninaishi katika nchi yao. 38Bali utakwenda mpaka nchi yangu, kwa jamaa zangu, ili umtafutie mwanangu Isaka mke.’ 39Nami nikamwambia bwana wangu, ‘Huenda mwanamke huyo akakataa kufuatana nami kuja huku.’ 40Lakini yeye akasema, ‘Mwenyezi-Mungu aniongozaye maishani mwangu, atamtuma malaika wake aende pamoja nawe na kukufanikisha katika safari yako; nawe utamtwalia mwanangu mke kutoka kwa jamaa yangu na nyumba ya baba yangu. 41Kama utakapofika kwa jamaa zangu hawatakupa huyo msichana, basi, hutafungwa na kiapo changu.’
42“Leo nilipofika kisimani nimeomba, ‘Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nakuomba nifaulu leo katika safari yangu na umfadhili Abrahamu bwana wangu. 43Niko hapa kando ya kisima. Msichana atakayekuja kuteka maji ambaye nitamwomba anipatie maji kidogo ya kunywa kutoka mtungi wake, 44naye akanipa na kuwatekea maji ngamia wangu, basi huyo na awe ndiye uliyemchagua kuwa mke wa mwana wa bwana wangu.’
45“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, mara Rebeka alifika na mtungi wake wa maji begani, akateremka kisimani na kuteka maji. Nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ya kunywa.’ 46Naye akautua mtungi wake haraka kutoka begani mwake, akasema, ‘Haya, kunywa bwana wangu. Nitawatekea maji ngamia wako pia.’ Basi mimi nikanywa na ngamia wangu pia akawapa maji. 47Ndipo nilipomwuliza, ‘Je, wewe ni binti wa nani?’ Akaniambia, ‘Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Milka, mkewe Nahori.’ Ndipo nilipompa pete na kumvisha bangili mikononi. 48Kisha nikainama na kumwabudu Mwenyezi-Mungu; nikamtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye ameniongoza moja kwa moja kwa binti wa ukoo wa bwana wangu kwa ajili ya mwanawe. 49Sasa, basi, niambieni kama mko tayari kumtendea bwana wangu kwa uaminifu na haki; kama sivyo, basi semeni, nami nitajua cha kufanya.”
50Baada ya kusikia hayo, Labani na Bethueli wakamjibu, “Jambo hili limetoka kwa Mwenyezi-Mungu, sisi hatuwezi kuamua lolote. 51Rebeka huyu hapa; mchukue uende. Na awe mke wa mwana wa bwana wako kama Mwenyezi-Mungu alivyosema.” 52Mtumishi wa Abrahamu aliposikia maneno hayo, alimsujudia Mwenyezi-Mungu. 53Kisha akatoa vito vya fedha na dhahabu na nguo, akampa Rebeka. Pia aliwapa ndugu na mama yake Rebeka mapambo ya thamani kubwa.
54Mtumishi wa Abrahamu na watu aliokuja nao wakala, wakanywa na kulala huko. Walipoamka asubuhi, mtumishi yule akasema, “Naomba kurudi kwa bwana wangu.” 55Lakini ndugu na mama yake Rebeka wakasema, “Mwache msichana akae nasi muda mfupi, kama siku kumi hivi; kisha anaweza kwenda.” 56Lakini yeye akasema, “Tafadhali, msinicheleweshe, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amekwisha fanikisha safari yangu; naomba mniruhusu kurudi kwa bwana wangu.” 57Nao wakasema, “Basi, tumwite msichana mwenyewe, tumwulize.” 58Wakamwita Rebeka na kumwuliza, “Je, utakwenda na mtu huyu?” Naye akajibu, “Nitakwenda.” 59Basi, wakamwacha Rebeka na yaya wake aende na mtumishi wa Abrahamu na watu wake. Yaya wake Rebeka pia aliandamana naye. 60Basi, wakambariki Rebeka wakisema,
“Ewe dada yetu!
Uwe mama wa maelfu kwa maelfu;
wazawa wako waimiliki miji ya adui zao.”
61Kisha, Rebeka na wajakazi wake wakapanda ngamia na kumfuata huyo mtumishi wa Abrahamu; nao wote wakaondoka.
62Wakati huo, Isaka alikuwa ameondoka Beer-lahai-roi, akawa anakaa huko pande za Negebu. 63Siku moja jioni, Isaka alikwenda mashambani kutafakari. Basi, akatazama akaona ngamia wanakuja. 64Naye Rebeka alipotazama na kumwona Isaka, alishuka chini 65na kumwuliza mtumishi wa Abrahamu, “Ni nani yule mtu anayetembea kule shambani, anakuja kutulaki?” Yule mtumishi akasema, “Ni bwana wangu.” Basi, Rebeka akatwaa shela yake, akajifunika uso. 66Yule mtumishi akamsimulia Isaka yote aliyokuwa ameyafanya. 67Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.
Mwanzo24;1-67
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 20 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo23...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana, Anastahili kusifiwa,Anastahili kuabudiwa,Ahimidiwe,Mungu wetu asiyelala,Mungu wetu aponyae,Mungu wetu afanyae njia pasipo na njia,Yeye ni Alpha na Omega..!!
Tunamshukuru sana  kwa Neema/Rehema  ya kuiona leo hii,
Asante Baba wa Mbinguni kwa kutupa kibali cha kuendelea kuwepo leo hii..
Sisi si kwamba ni wema sana,Wazuri sana,Wajuaji, wenyenguvu/Utashi..Hapana ni kwa mapenzi yako tuu wewe uliyetuumba, na kuumba Mbingu na nchi na vyoote vilivyopo..
Ukaibariki siku hii Baba wa Mbinguni, Tuingiapo/Tutokapo,Vyombo vya Usafiri,Tutembeapo,Vilaji/Vinywaji,Kazi,Biashara,Elimu na vyote tunavyoenda kutumia/kugusa Mfalme wa Amani ukavitakase..
kuwaguse na kuwaponya wote wanaopitia Magumu/Majaribu,Vifungo mbalimbali vya mwovu,Wagonjwa,Wafiwa,Waliokata tamaa,wenyeshida/Tabu mbalimbali..
Mfalme wa Amani ukatawale katika maisha yetu, Ukatawale na kuwaongoza wanaotuongoza wakaongoze kwa haki na kweli,Ukaibariki nchi hii tunayoishi Baba,Ukaibariki Tanzani,Afrika na Dunia yote Mfalme wa Amani ukatawale..
Tunakwenda kinyume na Mwovu, Tunajiachilia mikononi mwako Bwana Mungu wetu, Tunashukuru na Tukiamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu..
Amina..!!!!!!
Tuanze wiki na Mungu yeye atosha..
Mbarikiwe.


Kifo cha Sara
1Sara aliishi miaka 127. Hiyo ndiyo iliyokuwa miaka ya maisha yake Sara. 2Alifia huko Kiriath-arba, yaani Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akaomboleza na kumfanyia matanga Sara mkewe. 3Abrahamu akaiacha maiti ya mkewe, akatoka kwenda kuzungumza na Wahiti, akawaambia, 4 “Mimi ninaishi kama mgeni miongoni mwenu. Nipatieni sehemu ya ardhi ya kaburi, ili nipate kumzika marehemu mke wangu.” 5Wahiti wakamjibu, 6“Ee bwana wetu, tusikilize; wewe ni kiongozi maarufu miongoni mwetu. Mzike marehemu mkeo katika kaburi lolote utakalojichagulia; hakuna yeyote miongoni mwetu atakayekunyima kaburi lake, wala kukuzuia kumzika marehemu mkeo.” 7Hapo Abrahamu akasimama na kuinama kwa heshima mbele ya wananchi Wahiti, 8akawaambia, “Ikiwa mnaniruhusu nimzike marehemu mke wangu, tafadhali mwombeni Efroni mwana wa Sohari, kwa niaba yangu, 9aniuzie lile pango lake la Makpela lililo mpakani mwa shamba lake. Msihini aniuzie nilifanye makaburi yangu; anipatie kwa bei ya haki papa hapa mbele yenu.”
10Efroni mwenyewe alikuwa miongoni mwa Wahiti hao waliokuwa wamekutanika penye lango la mji. Basi, Efroni Mhiti, akamjibu Abrahamu, mbele ya Wahiti wote hapo langoni, 11“La, bwana; tafadhali unisikilize. Ninakupa shamba lote na pango lililomo humo; tena ninakupa mbele ya wananchi wenzangu. Mzike humo marehemu mkeo.”
12Abrahamu akainama tena kwa heshima mbele ya wananchi, 13akamwambia Efroni, wananchi wote wakisikia, “Nakuomba, tafadhali unisikilize. Nitakulipa bei kamili ya shamba lako, na ninakuomba upokee malipo haya, ili nipate kumzika humo marehemu mke wangu.” 14Efroni akamjibu Abrahamu, “Bwana, nisikilize; 15shamba lenye thamani ya shekeli 400 tu za fedha ni nini kati yako na mimi? Mzike marehemu mke wako.” 16Abrahamu akakubaliana na Efroni, akampimia kiasi cha fedha alichotaja mbele ya Wahiti wote, fedha shekeli 400, kadiri ya vipimo vya wafanyabiashara wa wakati huo.
17Basi, shamba la Efroni lililoko huko Makpela, mashariki ya Mamre, pango na miti yote iliyokuwamo pamoja na eneo zima, likawa lake 18Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokutanika penye lango la mji. 19Baada ya hayo, Abrahamu akamzika Sara mkewe katika pango hilo lililokuwamo katika shamba la Makpela, mashariki ya Mamre (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani. 20Shamba na pango lililokuwamo humo lilithibitishwa na Wahiti liwe mali yake Abrahamu apate kuzika humo wafu wake.
Mwanzo23;1-20

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (BHN):
Jifunze zaidi
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday 17 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo22..

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Mungu wetu ni mwema sana,Tunamshukuru na Kumsifu, Unastahili kuabudiwa ee Mungu Baba wa Mbinguni,Sifa na Utukufu ni kwake Mungu wetu,Bwana wa Mabwana,Mume wa wajane,Baba wa Yatima,Mungu asiye lala,Mungu anayejibu,Aponya,Anaokoa,Yeye anatosha kwa kila uliombalo Ukimkabidhi yeye na kuamini anatenda...
Yanini kung'ang'ana na mizigo yako?kwanini wakata tamaa?Kwanini kupoteza muda,Gharama,Kutafuta kisicho chako?Yupo awezae yote,Njoo kwakwe naye atakutua mizigo yako,Mgeukie Baba Mungu muumba nchi na Mbingu yeye ni Mfalme wa Amani,Upendo,Faraja,Furaha,Ushindi,mpe/mkabidhi maisha yako leo na hutojutia,Omba na kusifu pasipo kikomo,Muite leo ataitika, Mwambie yote yeye anasikia..
Acha kutangatanga kwa wanadamu/mataifa hawatakusaidia kitu pasipo Mungu...
Mungu aendelee kutubariki/Kutulinda, Kuingiakwetu/Kutokakwetu,Vilaji/Vinywaji,Vyombo vya Usafiri,Tutembeapo,Kazi,Biashara,Masomo na Vyote tunavyoenda kugusa/Kutumia Baba wa Mbinguni akavitakase..
Akatupe sawa sawa na Mapenzi yake.
Tunakwenda kinyume na mwovuTunajikabidhi na kujiachilia mikononi mwako baba wa Mbinguni, Tukiamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu sasa na hata milele..
Amina..!!!
Mungu awe nanyi katika yote.


Abrahamu anamtoa Isaka sadaka
1Baada ya muda fulani, Mungu alimjaribu Abrahamu. Mungu alimwita, “Abrahamu!” Naye akaitika, “Naam nasikiliza.” 2Mungu akamwambia, “Mchukue mwanao, Isaka, mwanao wa pekee umpendaye, uende mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuonesha.” 3Basi, kesho yake, Abrahamu akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwanawe. Akatayarisha kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akaanza safari kuelekea mahali alipoambiwa na Mungu. 4Mnamo siku ya tatu, Abrahamu aliinua macho akapaona mahali hapo kwa mbali. 5Akawaambia wale watumishi wake, “Ngojeni hapa na huyu punda. Mimi na mwanangu tutakwenda mpaka kule, tukamwabudu Mungu, kisha tutawarudiani.”
6Basi, Abrahamu akazitwaa zile kuni, akamtwika Isaka mwanawe; yeye mwenyewe akachukua moto na kisu mkononi; wakaondoka pamoja. 7Isaka akamwuliza baba yake, “Baba, moto na kuni tunazo; lakini mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa yuko wapi?” 8Abrahamu akamjibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atatujalia mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa.” Basi, wakaendelea na safari yao.
9 Walipofika mahali ambapo Mungu alimwagiza, Abrahamu akajenga madhabahu na kupanga kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe na kumlaza juu ya kuni juu ya madhabahu. 10Abrahamu akaunyosha mkono wake, akatwaa kisu tayari kumchinja mwanawe.
11Lakini malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita kutoka mbinguni, “Abrahamu! Abrahamu!” Naye akaitika, “Naam, nasikiliza!” 12Malaika akamwambia, “Usimdhuru mtoto wala usimfanye lolote! Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwani hukuninyima hata mwanao wa pekee.” 13Ndipo Abrahamu akatazama, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake kichakani. Basi, akaenda, akamchukua huyo kondoo, akamtoa sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14Kwa hiyo, Abrahamu akapaita mahali hapo, “Mwenyezi-Mungu hujalia.” Kama isemwavyo hata leo, “Katika mlima wa Mwenyezi-Mungu, watu hujaliwa.”
15Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni, 16 akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeapa kwa nafsi yangu kwamba kwa kuwa umefanya hivi, wala hukuninyima mwanao wa pekee, 17 hakika nitakubariki, na wazawa wako nitawazidisha kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ufuoni mwa bahari. Wazawa wako wataimiliki miji ya adui zao. 18 Kutokana na wazawa wako mataifa yote duniani yatabarikiwa kwa sababu wewe umeitii amri yangu.” 19Basi, Abrahamu akawarudia wale watumishi wake, nao kwa pamoja wakaondoka, wakarudi Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.

Watoto wa Nahori

20Baada ya matukio hayo Abrahamu alipata habari kwamba Milka pia amemzalia Nahori, nduguye, watoto wa kiume: 21Usi mzaliwa wa kwanza, Buzi ndugu yake, Kemueli baba yake Aramu, 22Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli. 23Bethueli alimzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori, ndugu yake Abrahamu, watoto hao wanane. 24Zaidi ya hayo, Reuma, suria wa Nahori, pia alimzalia watoto: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.
Mwanzo22;1-24
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 16 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi; Mwanzo21..


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Nimatumaini yangu mmeamka salama..Tunamshukuru Mungu kwa leo hii,Ametupa kibali cha kuiona tena..Wengi walitamani kuiona siku hii lakini wameshindwa,wengine ni wagonjwa wanashindwa hata kuinuka,Wengine hawana hata kauli, Sisi ni nani basi tumepewa hii Neema /Rehema ya kuwa Hai na wenye Afya na tushindwe kumuabudu Mungu,Kumshukuru Mungu,Kumsifu Mungu?
Tumempanini Mungu kwa uzima huu, sisi si kwamba ni wema sana zaidi ya wenzetu,si kwa nguvu/utashi wetu kuiona leo hii bali ni kwamapenzi ya Mungu wetu Muumba nchi na mbingu, Yeye ni mwingi wa Neema/Rehema, Yeye ni mtetezi wetu,Yeye asiye lala,Yeye ni mwokozi wetu,Yeye atupaye ridhiki zetu, Yeye awezae yote,Yeye ni mwamzo na yeye ni mwisho,Hakuna kama Yeye na hatokuwepo..
Mkabidhi Shida/Tabu zako,Magonjwa,Vifungo mbalimbali,Waliokata tamaa lipo Tumaini la kweli,Wafiwa yupo mfariji wa kweli,Wanaopitia Magumu/Majaribu yoyote mgeukie Mungu yeye anaweza..Akisema atakubariki hakuna wakupinga,Weka juhudi ya kumtafuta naye utamuona, Omba pasipokuchoka,Mwite na ataitika na kukutendea sawasawa na mapenzi yake.
Mungu Baba ukabariki Kuingia/Kutoka kwetu,Kazi,Biashara,Masomo,Vyombo vya usafiri na tutembeapo,Baba ukavitakase na damu yako vyote Tunavyoenda kuvitumia/kuvigusa..
Ukatuokoe na mwovu..Tunakuja mbele zako na kujiachilia mikononi mwako,Tukiamini wewe ni Bwana na mwokozi wetu..
Amina..!!!
Mbarikiwe.

Kuzaliwa kwa Isaka

1Mwenyezi-Mungu alimkumbuka Sara, akamtendea kama alivyoahidi. 2Basi, Abrahamu akiwa mzee, Sara akapata mimba, akamzalia mtoto wa kiume, wakati uleule Mungu alioutaja. 3Abrahamu akampa huyo mwanawe ambaye Sara alimzalia jina Isaka. 4Isaka alipotimiza umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri kama alivyoamriwa na Mungu. 5Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 100 wakati mwanawe Isaka alipozaliwa. 6Naye Sara akasema, “Mungu amenipatia kicheko; yeyote atakayesikia habari hizi, atacheka pamoja nami.” 7Kisha akaongeza, “Ni nani angeweza kumwambia Abrahamu kwamba mimi Sara nitanyonyesha watoto? Tena nimemzalia mtoto wa kiume katika uzee wake!”
8Isaka akaendelea kukua, na siku alipoachishwa kunyonya, Abrahamu akafanya sherehe kubwa.

Hagari anafukuzwa
9Baadaye Sara alimwona Ishmaeli, mtoto wa Abrahamu aliyezaliwa na Hagari, Mmisri, akicheza na Isaka mwanawe. 10Basi, Sara akamwambia Abrahamu, “Mfukuzie mbali mjakazi huyu na mwanawe. Haiwezekani kabisa mtoto wa mjakazi kurithi pamoja na mwanangu Isaka.” 11Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa kuwa Ishmaeli pia alikuwa mtoto wake. 12Lakini Mungu akamwambia Abrahamu, “Usihuzunike kwa sababu ya mtoto huyu, wala huyo mtumwa wako wa kike. Lolote akuambialo Sara lifanye; kwa kweli wazawa wako watatokana na Isaka. 13Na kuhusu huyo mwana wa mjakazi wako, nitamfanya awe baba wa taifa kubwa kwa kuwa yeye pia ni mtoto wako.”
14Hivyo, asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari na kumtwika begani; akamfukuza pamoja na mwanawe. Hagari akaondoka, akawa anatangatanga nyikani Beer-sheba.
15Ikawa maji yalipomwishia katika kile kiriba, Hagari akamlaza mwanawe chini ya mti. 16Naye akaenda kando, akaketi umbali wa kama mita 100 hivi, akisema moyoni mwake, “Heri nisimwone mwanangu akifa.” Na alipokuwa ameketi hapo, mtoto akalia kwa sauti.
17Mungu akamsikia mtoto huyo akilia, na malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni, akamwambia, “Una shida gani Hagari? Usiogope; Mungu amesikia sauti ya mtoto huko alipo. 18Simama umwinue mtoto na kumshika vizuri mikononi mwako, kwani nitamfanya awe baba wa taifa kubwa.” 19Mungu akamfumbua Hagari macho, naye akaona kisima cha maji. Akaenda akajaza kiriba maji, akamnywesha mtoto wake.
20Mungu akawa pamoja na huyo mtoto, naye akaendelea kukua. Alikaa nyikani na akawa mpiga upinde hodari sana. 21Alikuwa akikaa katika nyika za Parani, na mama yake akamwoza mke kutoka nchi ya Misri.
Agano kati ya Abrahamu na Abimeleki
22Wakati huo, Abimeleki pamoja na Fikoli, mkuu wa jeshi lake, alimwendea Abrahamu, akamwambia, “Mungu yuko pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. 23Kwa hiyo niapie kwa jina la Mungu kwamba hutanifanyia hila mimi au watoto wangu au wazawa wangu. Kadiri mimi nilivyokuwa mwaminifu kwako, vivyo hivyo nawe uwe mwaminifu kwangu na kwa nchi hii unamokaa.” 24Abrahamu akasema, “Naapa.”
25Wakati huo Abrahamu alikuwa amemlalamikia Abimeleki juu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamemnyanganya. 26Abimeleki akamwambia, “Mimi sijui nani aliyefanya hivyo; mpaka leo hii wewe hukuniambia; wala mimi sijapata kusikia habari hizi hadi leo.” 27Basi, Abrahamu akachukua kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki nao wawili wakafanya agano baina yao. 28Abrahamu akatenga wanakondoo wa kike saba. 29Abimeleki akamwuliza Abrahamu, “Kwa nini unawatenga hao wanakondoo wa kike saba?” 30Abrahamu akamjibu, “Hawa wanakondoo wa kike saba ninakupa kwa mkono wangu mwenyewe kama shahidi wangu kwamba mimi ndimi niliyechimba kisima hiki.” 31Kwa hiyo kisima hicho kikaitwa Beer-sheba, maana wote wawili walikula kiapo mahali hapo. 32Hivyo, wakafanya agano huko Beer-sheba. Abimeleki na Fikoli, mkuu wa jeshi lake, akaondoka na kurudi katika nchi ya Wafilisti. 33Abrahamu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaomba kwa jina la Mwenyezi-Mungu, akamwabudu Mungu, Mungu wa milele. 34Abrahamu alikaa katika nchi ya Wafilisti muda mrefu.
Mwanzo21;1-34
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 15 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo20..

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Natumaini mmeamka salama na Mungu yu pamoja nanyi..
Asante Baba wa Mbinguni kwa siku hii uliyo tupa kibali kuiona tena..
Si kwa uwezo/Utashi wetu bali kwa Neema/Rehema zako..
Tunaomba uibariki ikawe njema yenye mafanikio, Heri na Fanaka..
Ukabariki kuingiakwetu/Kutoka kwetu,Vilaji/Vinywaji,Vyombo vya Usafiri,Tutembeapo,Kazi,Biashara,Masomo na Vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba ukavitakase..
Roho mtakatifu akatuongoze kwenye kunena na kutenda..Sema nasi Baba wa Mbinguni ..
Ukawaguse na kuwaponya wote wanaopitia Magumu/Majaribu, Vifungo mbalimbali vya mwovu,Wagonjwa,Wafiwa,Walio Magerezani pasipo na hatia..Wewe ni Mungu uwezaye yote,Ufanya njia pasipo na njia,Unastahili kuabudiwa,Bwana wa Mabwana,Mungu usiye lala,Mfalme wa Amani ukatawale Nchi hii na Ukatawale Tanzania,Afika nzima na Dunia yote..Ukawaongoze wanaotuongoza na waongoze katika haki na kweli siku zote..Mamlaka ni yako,Nguvu na Utukufu,Jana,Leo,Kesho na hata Milele..
Amina..!!!!
Mungu awe nanyi katika yote ,Muwe na wakati mwema.


Abrahamu na Abimeleki

1Toka Mamre, Abrahamu alisafiri kuelekea eneo la Negebu, akafanya makao yake kati ya Kadeshi na Shuri, kisha akaenda kukaa kwa muda huko Gerari. 2Akiwa huko, Abrahamu alisema kuwa mkewe Sara ni dada yake. Kwa hiyo, mfalme Abimeleki wa Gerari akamchukua Sara. 3Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto usiku, akamwambia, “Wewe utakufa kwa sababu ya mwanamke uliyemchukua, kwani ana mumewe.”
4Abimeleki ambaye bado hakuwa amelala na Sara, akajibu, “Bwana, utawaua watu wasio na hatia. 5Abrahamu mwenyewe ndiye aliyesema kuwa huyu ni dada yake. Tena hata Sara mwenyewe alisema kuwa Abrahamu ni kaka yake! Mimi nimefanya nilivyofanya kwa moyo mnyofu na sina hatia.” 6Basi, Mungu akamwambia katika hiyo ndoto, “Sawa. Najua kwamba umefanya hivyo kwa moyo mnyofu, na mimi ndiye niliyekuzuia kutenda dhambi dhidi yangu; ndiyo maana sikukuruhusu umguse huyo mwanamke. 7Sasa mrudishe huyo mwanamke kwa mume wake. Abrahamu ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini usipomrudisha, ujue kwa hakika kwamba wewe utakufa pamoja na watu wako wote.”
8Basi, Abimeleki akaamka asubuhi na mapema, akawaita watumishi wake wote na kuwaeleza mambo aliyoyaona katika ndoto; nao wakaogopa sana. 9Ndipo Abimeleki akamwita Abrahamu, akamwuliza, “Umetutendea nini? Nimekukosea nini hata ukaniletea balaa hili mimi na ufalme wangu? Umenitendea mambo yasiyostahili kutendwa.” 10Tena Abimeleki akazidi kumwuliza, “Ni kitu gani kimekusukuma kufanya hivyo?”
11Abrahamu akamjibu, “Nilifanya hivyo kwa kuwa hakuna amchaye Mungu mahali hapa, na kwamba mngeniua ili mumchukue mke wangu. 12Zaidi ya hayo, kwa kweli, yeye ni dada yangu: Baba yake na baba yangu ni mmoja, lakini mama tofauti; ndiyo maana akawa mke wangu. 13Wakati Mungu aliponifanya niiache nyumba ya baba yangu na kwenda ugenini, nilimwambia mke wangu, ‘Popote tutakapokwenda tafadhali useme kwamba mimi ni kaka yako!’”
14Abimeleki akamrudishia Abrahamu mke wake Sara, akampa na kondoo, ng'ombe na watumwa wa kiume na kike. 15Tena Abimeleki akamwambia Abrahamu, “Tazama, nchi hii yote ni yangu! Basi, chagua popote upendapo, ukae.” 16Kisha, akamwambia Sara, “Tazama, mimi nimempa ndugu yako vipande 1,000 vya fedha ili kuwaonesha wote walio pamoja nawe kwamba huna hatia; umethibitishwa huna lawama.”17Kisha Abrahamu akamwomba Mungu, naye akamponya Abimeleki, mkewe na mjakazi wake, hata wakaweza kupata tena watoto. 18Hapo kwanza Mwenyezi-Mungu alikuwa amewazuia wanawake wote wa nyumba ya Abimeleki kupata watoto kwa sababu ya Sara, mke wa Abrahamu.
Mwanzo20;1-18

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 14 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo19..

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tunamshukuru Sana Mungu kwa leo hii na ikawe yenye Baraka,Amani, Furaha,Upendo na Faida...Mungu akawe nasi katika Kazi,Biashara,Masomo na akabariki Vyombo vya usafiri,Tutembeapo, Tuingiapo/Tutokapo,Vilaji/Vinywaji na akatakase vyote tunavyoenda kugusa/kutumia na Damu yake..
Akawakomboe/Kuwaponya wenye Shida/Tabu, Waliokata tamaa,Waliokataliwa/Kutengwa, Wenye vifungo mbalimbali na wote wanaopitia Magumu/Majaribu..
Akatupe sawaswa na mapenzi yake..
Yeye akisema atakubariki hakuna wa kupinga, Akisema ndiyo nani aseme hapana?Mungu wetu yu macho na anaweza yote..Mkadhi leo mizigo yako naye atakutua..Tuombe pasipo kukoma..
Mungu anatosha..!!!
Muwe na Wakati mwema.


Uovu wa watu wa Sodoma
1Wale malaika wawili wakawasili mjini Sodoma jioni. Loti ambaye alikuwa ameketi penye lango la mji wa Sodoma, alipowaona, aliinuka kuwalaki, akainama kwa heshima, 2akasema, “Bwana zangu, karibuni nyumbani kwangu mimi mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala kwangu usiku wa leo. Asubuhi na mapema mtaweza kuendelea na safari yenu.” Lakini, wao wakasema, “La! Sisi tutalala huku mtaani.” 3Loti akawasihi sana, mwishowe wakakubali, wakageuka na kuingia nyumbani kwake. Loti akawaandalia karamu, akaoka mikate isiyotiwa chachu, wakala.
4Lakini kabla ya kulala usiku, wanaume wote wa mji wa Sodoma, vijana kwa wazee, bila kubaki hata mmoja, wakaizingira nyumba ya Loti. 5Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.”
6Loti akatoka nje, akafunga mlango nyuma yake, 7akawaambia, “Ndugu zangu, nawasihi msitende uovu huo. 8Tazama, ninao binti wawili ambao bado hawajalala na mwanamume. Mniruhusu niwapeni hao wasichana muwatendee kama mpendavyo. Lakini msiwatende lolote wanaume hawa kwa sababu ni wageni wangu.”
9Lakini wao wakasema, “Tupishe! Wewe ulikuja huku ukiwa mgeni na sasa wajifanya hakimu! Basi, tutakutenda mabaya zaidi ya hao wageni wako.” Hapo wakamsukuma Loti nyuma hata karibu wauvunje mlango wake. 10Lakini wale wageni wakanyosha mikono yao, wakamvuta Loti ndani ya nyumba na kuufunga mlango. 11Kisha wakawapiga kwa kuwapofusha macho wanaume wote waliokuwapo mlangoni, wakubwa kwa wadogo, hata wakataabika kuutafuta ule mlango, wasiupate.
Loti anatoka Sodoma
12Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Je, una mtu mwingine hapa, pengine wana, mabinti, wachumba wa binti zako au watu wengine wa jamaa yako wanaoishi mjini humu? Watoe mahali hapa haraka, 13kwa maana kilio kilichomfikia Mwenyezi-Mungu dhidi ya wakazi wa hapa ni kikubwa mno, naye ametutuma tuje kuwaangamiza.”
14Basi, Loti akawaendea wachumba wa binti zake, akawaambia, “Haraka! Tokeni mahali hapa, maana Mwenyezi-Mungu atauangamiza mji huu.” Lakini wao wakamwona kama mtu mcheshi tu.
15Kulipokucha, malaika wakamhimiza Loti wakisema, “Amka, mchukue mkeo na hawa binti zako wawili msije mkaangamia wakati mji huu unapoadhibiwa.” 16Loti akawa anasitasita. Lakini kwa vile Mwenyezi-Mungu alivyomhurumia Loti, wale malaika wakamshika yeye, mkewe na binti zake wawili, wakamtoa nje ya mji. 17Walipowatoa nje ya mji, malaika mmoja wao akawaambia, “Kimbieni kwa usalama wenu. Msiangalie nyuma wala kusimama popote bondeni. Kimbilieni milimani, msije mkaangamia.”
18Loti akawaambia, “La, bwana zangu! 19Ni kweli kwamba mimi mtumishi wenu nimepata fadhili mbele yenu, nanyi mmenionea huruma sana kwa kuyaokoa maisha yangu; lakini milimani ni mbali mno. Maangamizi haya yatanikuta kabla sijafika huko, nami nitakufa. 20Tazameni, kule kuna mji mdogo ambao naweza kuukimbilia kwani uko karibu. Basi, mniruhusu nikimbilie huko. Ule ni mji mdogo tu, na huko nitasalimika.”
21Naye akamjibu, “Sawa, nimekubali ombi lako. Sitauangamiza mji ulioutaja. 22Harakisha! Kimbilia huko, nami sitafanya lolote mpaka utakapowasili huko.” Hivyo mji huo ukaitwa Soari.
Kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora
23Jua lilikuwa limekwisha chomoza wakati Loti alipowasili mjini Soari. 24Ndipo Mwenyezi-Mungu akateremsha moto mkali wa kiberiti kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora, 25akaiangamiza miji hiyo, bonde lote, wakazi wake wote na mimea yote katika nchi hiyo. 26Lakini mkewe Loti aliyekuwa nyuma ya Loti, akatazama nyuma, akageuka nguzo ya chumvi.
27Asubuhi na mapema, Abrahamu alikwenda mahali alipokuwa amesimama mbele ya Mwenyezi-Mungu. 28Akiwa hapo, akatazama chini pande za Sodoma na Gomora na eneo lote la bondeni, akashangaa kuona moshi ukipanda, moshi kama wa tanuri kubwa. 29Mungu alipoiangamiza miji ya bondeni alimokuwa anakaa Loti, alimkumbuka Abrahamu kwa kumtoa Loti katika miji hiyo, ili Loti asije akaangamia pamoja nayo.
Asili ya Wamoabu na Waamoni
30Loti aliogopa kuishi mjini Soari, kwa hiyo akauhama mji huo, yeye pamoja na binti zake wawili, wakaenda kuishi pangoni, milimani. 31Wakiwa huko, binti mkubwa akamwambia dada yake, “Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanamume nchini wa kutuoa tupate watoto. 32Basi, tumlevye baba kwa divai, ili tupate kulala naye na kudumisha uzawa kwa kupata watoto kwake.” 33Usiku huo wakamlevya baba yao kwa divai, na yule binti wa kwanza akaenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati bintiye alipolala naye, wala alipoondoka.
34Kesho yake, yule binti wa kwanza akamwambia yule mdogo, “Jana usiku mimi nililala na baba; leo pia tumlevye kwa divai, kisha wewe utalala naye, na hivyo sote tutadumisha uzao kwa kupata watoto.” 35Basi, usiku huo pia wakamlevya baba yao kwa divai, kisha yule binti mdogo akaenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati bintiye alipolala naye, wala alipoondoka. 36Hivyo, binti wote wawili wa Loti wakapata mimba kutokana na baba yao. 37Yule binti wa kwanza akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Moabu. Huyo ndiye baba wa Wamoabu hadi leo. 38Yule mdogo pia akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Ben-ami. Huyo ndiye baba wa Waamoni hadi leo.
Mwanzo19;1-38

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 13 February 2017

Viongozi Wetu;DIRA YA MWL NYERERE UTANGULIZI PART I,11,111









Shukrani;ikulu mawasiliano

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo18

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Ni siku nyingine  tena Mungu ametupa kibali cha kuiona tena,Si kwa uwezo wetu au nguvu na utashi wetu bali ni kwa Neema/Rehema ya Muumba Mbingu na Nchi...
Tunamshukuru Mungu kwa siku hii na tunaomba Akaibariki Kuingia/Kutoka kwetu,Vilaji/Vinywaji,Kazi,Biashara,Masomo,Vyombo vya usafiri na tutembeapo..Mungu akawaguse na Kuwaponya Wenye Shida/Tabu,Wagonjwa walio mahospitalini/Majumbani,Walio magerezani pasipo na hatia,wenye vifungo vyovyote vya mwovu,Mungu akawafungue na kuwaponya..
Mungu Baba ukawaguse wenzetu wanaotafuta wachumba (Ndoa)
Baba mke mwema/Mume mwema hutoka kwako,Baba ukawaongoze katika harakati hizi ili wapate kilicho chako..
Ukabariki Ndoa zetu Baba wa Mbinguni,Ukatuongoze katika maamuzi,Kunena,Kutenda, hekima,Busara na kuchukuliana..
Kila mmoja akawe mpya kila siku,Mapenzi kwa mwenzake na kuheshimiana..Tukafurahi pamoja katika Neno lako,na Kila mtu awajibike ipasavyo kwenye majukumu yake..Bwana wa Majeshi ukawe mlinzi mkuu wa familia zetu,Kipato na vyote tunavyovimiliki..
Tunakwenda kinyume na mwovu kuvunja na kuharibu kazi zake zote...
Mfalme wa Amani ukatawale kwa kila jambo..
Tunajikabidhi mikononi mwako Baba wa Mbinguni,
Tukiamini wewe ni Bwana na mwokozi wetu..Tunashukuru na kukusifu..
Amina..!!
Anza na Mungu na umalize na Mungu..
Muwe na wiki njema.


Mungu anathibitisha ahadi yake

1Mwenyezi-Mungu alimtokea Abrahamu penye mialoni ya Mamre. Abrahamu alikuwa ameketi penye mlango wa hema lake wakati wa joto la mchana, 2na alipoinua macho yake, akaona watu watatu wamesimama mbali kidogo mbele yake. Mara alipowaona, akapiga mbio kutoka mlangoni mwa hema lake, akaenda kuwalaki. Alipowafikia aliinama kwa heshima na kusema, 3“Bwana zangu, kama mnanipenda tafadhali msinipite mimi mtumishi wenu ila mshinde kwangu. 4Mtaletewa maji kidogo ili mnawe miguu na kupumzika chini ya mti. 5Wakati mnapopumzika, nitaandaa chakula kidogo, mle, ili mpate nguvu za kuendelea na safari yenu; maana mmenijia mimi mtumishi wenu.” Nao wakasema, “Sawa! Fanya kama ulivyosema.”
6Abrahamu akarudi haraka hemani akamwambia Sara, “Tayarisha haraka vipimo vitatu vya unga bora, uukande, uoke mikate.” 7Kisha akatoka haraka akaenda kwenye kundi la ng'ombe, akachagua ndama mmoja mzuri na mnono, akamkabidhi mtumishi ambaye aliharakisha kumchinja na kumpika. 8Halafu Abrahamu akachukua siagi, maziwa na ile nyama iliyotayarishwa, akawaandalia wageni hao chakula; naye akasimama karibu nao kuwahudumia walipokuwa wakila chini ya mti.
9 Wale wageni wakamwuliza, “Mkeo Sara yuko wapi?” Abrahamu akawajibu, “Yumo hemani.” 10Mmoja wao akasema, “Hakika nitakurudia wakati kama huu mwakani, na mkeo Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa huko nyuma mlangoni mwa hema, akisikiliza. 11Abrahamu na Sara walikuwa wakongwe, naye Sara mambo ya kawaida ya wanawake yalikuwa yamekoma kitambo. 12Kwa hiyo, Sara alicheka kimoyomoyo akisema, “Mimi ni mzee, na mume wangu hali kadhalika. Je, nikiwa mzee hivi, nitaweza kufurahi na kupata watoto?” 13Hapo Mwenyezi-Mungu akamwuliza Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kujiuliza kama kweli itawezekana apate mtoto akiwa mzee? 14Je, kuna jambo lolote lisilowezekana kwa Mwenyezi-Mungu? Nitakurudia wakati uliopangwa, wakati kama huu mwakani, na Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” 15Lakini Sara, akiwa na hofu, akakana akisema, “Sikucheka!” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Sivyo! Kucheka, ulicheka.”
Abrahamu anawaombea wakazi wa Sodoma
16Ndipo wale watu wakaondoka, wakafika mahali walipoweza kuona mji wa Sodoma; naye Abrahamu akawasindikiza. 17Basi, Mwenyezi-Mungu akawaza: Je, nimfiche Abrahamu jambo ambalo nimepanga kutenda? 18Yeye atakuwa baba wa taifa kubwa na kwake mataifa yote ya ulimwengu yatabarikiwa! 19Nimemchagua yeye na wazawa wake. Yeye atawafunza wazawa wake kushika njia yangu: Wawe waadilifu na wenye kutenda mambo ya haki, nami nipate kuwatimizia ahadi zangu.
20Basi, Mwenyezi-Mungu akasema, “Kuna malalamiko mengi dhidi ya watu wa Sodoma na Gomora, na dhambi yao ni kubwa mno. 21Hivyo nitashuka kwenda huko nijionee mwenyewe kama kweli wamefanya kadiri ya kilio kilichonifikia. Nataka kujua.”
22Kutoka hapo, wale watu wakashika njia kuelekea Sodoma, lakini Mwenyezi-Mungu akawa amebaki, amesimama pamoja na Abrahamu.23Basi, Abrahamu akamkaribia Mwenyezi-Mungu, akamwuliza, “Je, kweli utawaangamiza watu wema pamoja na waovu? 24Huenda ikawa mna watu wema hamsini humo mjini. Je, utauangamiza mji mzima badala ya kuuacha kwa sababu ya hao wema hamsini waliomo humo? 25Sidhani kama utafanya hivyo! Kuwaua watu wema pamoja na waovu; wema kutendewa sawa na waovu! La, hasha! Hakimu wa dunia yote hataacha kutenda yaliyo sawa!” 26Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nikikuta watu wema hamsini kule mjini Sodoma, basi nitauacha mji wote salama kwa ajili yao.”
27Abrahamu akasema, “Nimethubutu kuzungumza na Bwana, mimi niliye mavumbi na majivu tu. 28Huenda wakapatikana watu wema arubaini na watano badala ya hamsini. Je, utauangamiza mji mzima kwa sababu wamepungua watu watano?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Sitauangamiza mji ikiwa kuna watu wema arubaini na watano.”
29Abrahamu akaongeza kusema, “Pengine watu arubaini watapatikana humo.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Kwa ajili ya watu wema arubaini, sitafanya hivyo.”
30Abrahamu akaongeza kusema, “Ee Bwana, naomba usinikasirikie, nami nitasema tena. Huenda wakapatikana watu wema thelathini.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Sitafanya hivyo nikiwakuta hao thelathini.”
31Abrahamu akasema, “Nimethubutu kuzungumza na Bwana. Labda watapatikana watu wema ishirini.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Kwa ajili ya hao ishirini, sitauangamiza.”
32Hatimaye, Abrahamu akasema, “Ee Bwana, nakuomba usikasirike, ila nitasema tena mara moja tu. Je, wakipatikana watu wema kumi, itakuwaje?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Kwa ajili ya hao watu wema kumi, sitauangamiza mji huo.”
33Mwenyezi-Mungu alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, alikwenda zake; naye Abrahamu akarudi nyumbani kwake.
Mwanzo18;1-33

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Sunday 12 February 2017

Natumaini Jumapili ilikuwa/Inaendelea Vyema;Burudani-Your Presence Is Heaven,Victor's Crown by Darlene Zschech from REVEALING JESUS

Wapendwa/Waungwana Natumaini Jumapili ilikuwa Njema/Inaendelea Vyema kabisa..
Hapa kwetu ilikuwa nzuri kabisa Tunamshukuru Mungu kwa siku hii kwetu..
Waliokwenda Nyumbani mwa Bwana ninaimani hawakuondoka hivihivi na walichobeba kitawasaidia
wao, Familia na wengine pia..
Kama ulishindwa kufika nyumbani mwa Bwana kwa sababu iliyokuwa nje ya uwezo wako pole sana na Bwana atafanya njia
na upate kufika wakatimwingine..
Kama ni Uvivu,Uzembe au kifungo chochote Mungu akakuamshe na kukukumbusha wakati mwingine usikose
nawe jibidishe/jitahidi kumshinda mwovu na kuungana na wengine nyumbani mwa Bwana..
Mungu aendelee kuwabariki katika yote na tukumbushane kwa Upendo...



“Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa visiweko tena. Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa. 

Jiwe kuu
“Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa visiweko tena. Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni mwema.” Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa. Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea tambiko za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama! Naweka jiwe huko Siyoni, jiwe la msingi, teule na la thamani. Mtu atakayemwamini huyo hataaibishwa.” Kwenu nyinyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.” Tena Maandiko yasema: “Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuwaangusha watu.” Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini ule ujumbe; na ndivyo walivyopangiwa tangu mwanzo. Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu. Wakati mmoja nyinyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa nyinyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa mmepokea huruma.”
‭‭1 Petro‬ ‭2:1-10‬ ‭BHND‬‬
http://bible.com/393/1pe.2.1-10.bhnd






"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Friday 10 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo17

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Asante Baba Mungu kwa Neema/Rehema,Umetupa kibali cha kuiona siku hii tena..Tunakushukuru na Kukusifu na Kulitukuza Jina lako linaloyashinda yote,Wewe Mwenye-Enzi,Muumba mbingu na dunia,Mungu uponyaye,Mungu utoshaye, Mwenye huruma,Husamehe,Hufariji,Mshauri wa Ajabu,Mwenye Nguvu,na Muweza wa yote tunakuja mbele zako Baba
ukatuongoze kwa kila jambo,Tuingiapo/Tutokapo,Vilaji/Vinywaji,Kunena/Kutenda,Kazi,Biashara,Elimu na yote tusiyoyataja Baba wewe unatujua zaidi,Ukatupe sawasawa na Mapenzi yako Mfalme wa Amani uendelee kutawala...
Ukawaponye wanaopitia Magumu/Majaribu mbalimbali,Wagonjwa,Wafiwa,Wenye Shida/Tabu..Wakakutane nawe Baba..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako tukiamini na kushukuru ..
Amina...!!
Muwe na wakati mzuri.


Agano na tohara

1Wakati Abramu alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Mwenyezi-Mungu alimtokea, akamwambia, “Mimi ni Mungu mwenye nguvu. Fuata mwongozo wangu na kuishi bila lawama. 2Nami nitafanya agano nawe na kuwazidisha wazawa wako.” 3Hapo Abramu akasujudu. Naye Mungu akamwambia, 4“Ninafanya agano hili nawe: Utakuwa baba wa mataifa mengi. 5Tangu sasa, hutaitwa tena Abramu, bali utaitwa Abrahamu, maana nimekufanya kuwa baba wa mataifa mengi. 6Nitakufanya uwe na wazawa wengi sana; kwako nitazusha mataifa mengi na wafalme. 7Nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele; tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele. 8Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambamo unaishi kama mgeni; yaani nchi yote ya Kanaani iwe mali yenu milele; nami nitakuwa Mungu wao.”
9Kisha Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, wewe utalishika agano langu, wewe binafsi, wazawa wako na vizazi vyao vyote. 10Hili ndilo agano utakaloshika kati yangu na wewe na wazawa wako: Kila mwanamume miongoni mwenu lazima atahiriwe. 11Mtatahiriwa kwa kukata magovi yenu, na hii itakuwa ndiyo alama ya agano kati yangu nanyi. 12Kila mtoto wa kiume wa siku nane miongoni mwenu ni lazima atahiriwe. Kila mwanamume katika vizazi vyenu, awe mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwenu au aliyenunuliwa kwa fedha zenu kutoka kwa mgeni asiye mzawa wako; 13naam, kila mmoja wao aliyezaliwa katika nyumba yako na hata aliyenunuliwa kwa fedha zako ni lazima atahiriwe. Hiyo ni alama ya agano langu katika miili yenu, agano la milele. 14Mwanamume yeyote asiyetahiriwa atatengwa na watu, kwani atakuwa amevunja agano langu.”
Abrahamu anaahidiwa mtoto
15Kisha Mungu akamwambia Abrahamu, “Kuhusu mkeo, hutamwita tena jina lake Sarai, bali jina lake litakuwa Sara. 16Nitambariki, naye atakuzalia mtoto wa kiume. Naam, nitambariki Sara, naye atakuwa mama wa mataifa mengi na wafalme wa mataifa watatoka kwake.” 17Hapo Abrahamu akasujudu, akacheka moyoni mwake akiwaza, “Ati, itawezekana kweli mtoto kuzaliwa kwa mzee wa miaka 100? Na je, Sara ambaye umri wake ni miaka tisini, ataweza kupata mtoto?” 18Basi, Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti ungekubali ahadi yako hiyo imhusu Ishmaeli.” 19Mungu akamjibu, “La! Ila mkeo Sara atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita Isaka Nitaliimarisha agano langu kwake na wazawa wake, kuwa agano la milele.
20“Na, kuhusu Ishmaeli, nimesikia ombi lako. Nitambariki, nitamjalia watoto wengi na kuwazidisha sana. Ishmaeli atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya kuwa baba wa taifa kubwa. 21Lakini agano langu litathibitika kwa Isaka ambaye Sara atakuzalia mwakani wakati kama huu.” 22Basi, Mungu alipomaliza kuongea, akamwacha Abrahamu.
23Kisha, siku hiyohiyo, Abrahamu akamtahiri mwanawe Ishmaeli na kuwatahiri watumwa wote wa kiume waliozaliwa nyumbani mwake na walionunuliwa kwa fedha zake, kama Mungu alivyomwamuru. 24Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 99 alipotahiriwa. 25Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka 13 alipotahiriwa. 26Abrahamu na mwanawe Ishmaeli 27pamoja na wanaume wote wa nyumba yake, watumwa wote waliozaliwa nyumbani mwake na walionunuliwa kwa fedha zake walitahiriwa siku hiyohiyo.
Mwanzo17;1-27

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 9 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo16...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Mungu wetu ni mwema na Muaminifu..
Tunamshukuru kwa kutuamsha tena siku hii tukiwa wenye afya na kuendelea na maisha ya kila siku ya Duni hii yenye mambo meengi,
Akatuongoze katika kazi zetu,Biashara, Masomo,akavibariki vyombo vyote vya usafiri,tutembeapo,Tuingiapo/Tutokapo baba akawe nasi daima...
Akawaguse na Kuwaponya Wagonjwa,Wanaopitia Magumu/Majaribu, Shida/Tabu zozote Mungu yu pamoja nanyi msiache kumkabidhi yote mnayopitia yeye ni mkombozi wa yote..
Mungu wetu ukawaongoze watoto wetu shuleni wakapate kukumbuka na kuelewa wanayofundishwa,
Ukawalinde na kuwavusha salama katika ujana wao, wakakujue Mungu katika ujana wao mpaka mwisho,Ukawaokoe katika vishawishi vyote vya dunia hii yenye mambo mengi na kufuata mkumbo..
wawe na hofu yako na wasikuonee haya watajapo jina lako mahali popote.
Wazazi/Walezi Mungu ukawape hekima na Busara katika maamuzi na malezi yao.
Tunakwenda kinyume na Mwovu, Nguvu za Giza na vifungo vyote vya shetani.
Tunajiachilia kwako Baba Wambinguni na ukatusamehe pale tulipokosea kwa makusudi/kujua au kutojua..Ukatupe kunena yaliyo yako Mfalme wa Amani uendelee kutawala katika maisha yetu.
Amina..!!!
Mungu awabariki.


Sarai na Hagari
1Basi, Sarai, mkewe Abramu, alikuwa bado hajamzalia mumewe mtoto. Lakini alikuwa na mjakazi aliyeitwa Hagari, kutoka Misri. 2Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.
3Kisha, Sarai akampa Abramu Hagari, mjakazi wake ambaye alikuwa Mmisri, awe mke wake. Haya yalitokea baada ya Abramu kukaa katika nchi ya Kanaani kwa muda wa miaka kumi. 4Abramu akamchukua Hagari, naye Hagari akapata mimba. Lakini mara tu alipoona amepata mimba, Hagari akaanza kumdharau bimkubwa wake. 5Sarai akamwambia Abramu, “Wewe utawajibika kwa ubaya ninaotendewa. Mimi nilikupa mjakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake! Mwenyezi-Mungu na ahukumu kati yako na mimi!” 6Lakini Abramu akamwambia Sarai, “Mjakazi wako yuko chini ya mamlaka yako; mfanyie upendavyo.” Basi, Sarai akamtesa Hagari mpaka akatoroka.
Ishmaeli anazaliwa
7Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamkuta Hagari penye chemchemi ya maji jangwani, chemchemi iliyoko njiani kuelekea Shuri. 8Malaika akamwuliza, “Hagari, mjakazi wa Sarai! Unatoka wapi na unakwenda wapi?” Hagari akamjibu, “Namkimbia bimkubwa wangu Sarai.” 9Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Rudi kwa bimkubwa wako Sarai na umtii.” 10Zaidi ya hayo, malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Hagari, “Nitawazidisha wazawa wako hata wasiweze kuhesabika kwa wingi wao.” 11Kisha huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Wewe ni mjamzito na utajifungua mtoto wa kiume; utamwita Ishmaeli, maana Mwenyezi-Mungu amesikia mateso yako. 12Ishmaeli ataishi kama pundamwitu; atakuwa adui wa kila mtu na kila mtu atakuwa adui yake. Ataishi akiwa adui wa jamaa yake.” 13Basi, Hagari akampa jina Mwenyezi-Mungu aliyezungumza naye huko, “Wewe ni Mungu Aonaye” kwa maana alifikiri, “Kweli hapa nimemwona yeye anionaye!” 14Ndiyo maana kile kisima chaitwa Beer-lahai-roi. Kisima hiki kipo kati ya Kadeshi na Beredi.
15Hagari akamzalia Abramu mtoto wa kiume. Abramu akamwita mtoto huyo Ishmaeli. 16Abramu alikuwa na umri wa miaka 86 wakati Hagari alipomzaa Ishmaeli.
Mwanzo16;1-16
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 8 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo15...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Natumaini mmeamka salama na mnaendelea vyema/Mmeanza vyema na Mungu,Andelee Kutubariki katika Kazi,Biashara,Masomo,kwenye Vyombo vya usafiri,njiani/Tutembeapo,Vilaji/Vinywaji,Tuingiapo/Tutokapo,
Mungu baba akatupe/Akatufanyie sawaswa na Mapenzi Yake.
Wagonjwa,Walio Magerezani pasipo na hatia,Wafiwa,wanaopitia Magumu/Majaribu,Shida/Tabu,Mungu Baba akawaguse na kuwaponya...
Baba Mungu ukaibariki na kuiponya Nchi yetu Tanzani,Ukabariki Afrika nzima Baba,Baba pia na Ubariki hapa tunapoishi, Na Dunia Nzima Mfalme wa Amani ukatawale na Kuongoza...Mfalme wa Amani ukawaguse wanaotuongoza ukawape kutenda sawasawa na mapenzi yako...
Tunajiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni katika yote...
Tunaomba na Kushukuru..Amina.!!!!
Mungu akawe nanyi.


Agano la Mungu na Abramu

1Baada ya mambo hayo, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Abramu katika maono, “Abramu! Usiogope! Mimi ni ngao yako. Tuzo lako litakuwa kubwa!” 2Lakini Abramu akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu, utanipa nini hali naendelea kuishi bila mtoto, na mrithi wangu ni Eliezeri wa Damasko? 3Tazama! Hujanijalia mtoto; mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye atakayekuwa mrithi wangu!”
4Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Huyu hatakuwa mrithi wako! Mwanao halisi ndiye atakayekuwa mrithi wako.” 5Hapo Mwenyezi-Mungu akamleta Abramu nje na kumwambia, “Tazama mbinguni! Zihesabu nyota, kama kweli utaweza kuzihesabu! Hivyo ndivyo wazawa wako watakavyokuwa wengi!” 6Abramu akamwamini Mwenyezi-Mungu, naye Mwenyezi-Mungu akamkubali Abramu kuwa mwadilifu.
7Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyekuleta toka Uri, mji wa Wakaldayo, ili nikupe nchi hii uimiliki.” 8Lakini Abramu akamwambia, “Ee Mwenyezi-Mungu, nitajuaje kwamba nitaimiliki nchi hii?” 9Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Niletee ndama wa miaka mitatu, mwanambuzi jike wa miaka mitatu, kondoo dume wa miaka mitatu, na hua na kinda la njiwa.” 10Abramu akamletea hao wote, akamkata kila mnyama vipande viwili, akavipanga katika safu mbili, vikielekeana; lakini ndege hakuwakata vipande viwili. 11Na tai walipoijia hiyo mizoga, Abramu akawa anawafukuza.
12Jua lilipokuwa likitua, Abramu alishikwa na usingizi mzito; hofu na giza nene vikamfunika. 13Hapo Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Ujue hakika ya kwamba wazawa wako watakaa kama wageni katika nchi isiyo yao, watakuwa watumwa na watateswa kwa muda wa miaka 400. 14Hata hivyo, nitaliadhibu taifa watakalolitumikia, na hatimaye watatoka wakiwa na mali nyingi. 15Lakini wewe mwenyewe utaishi maisha marefu na kufariki kwa amani. 16Wazawa wako watarudi hapa katika kizazi cha nne, kwa sababu uovu wa Waamori haujakamilika bado.”
17Jua lilipokwisha tua na giza kuingia, tanuri ifukayo moshi na mwenge uwakao moto vikapita katikati ya vile vipande vya nyama. 18Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu akafanya agano na Abramu akisema, “Wazawa wako ninawapa nchi hii, toka mto wa Misri hadi ule mto mkubwa wa Eufrate, 19yaani nchi za Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, 20Wahiti, Waperizi, Warefai, 21Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”
Mwanzo15;1-21

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN): 
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 7 February 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo14...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Mungu wetu yu mwema sana na tuzidi Kumtukuza,Kumsifu,Kumshukuru ,Yeye aliyetupa kuiona Leo hii
kwa mapenzi yake na si kwa utashi,nguvu zetu au kwamba sisi ni wema sana..ni Kwa Neema/Rehema zake tuu kwakutuchagua sisi...
Asante sana Mungu wetu uliye mkuu,Uliyetukuka,Unayetupa ridhiki,Uliyetupa Afya,Uliyetupa kibali chako cha kuendelea  nasi katika maisha haya ya Dunia hii yenye mambo meengi...Ukatulinde na kutubariki katika Kazi zetu,Biashara,Masomo,Vyombo vya usafiri na tutembeapo,ukabariki Kuingia/Kutoka kwetu,Vilaji/Vinywaji..Na vyote tunavyoenda kugusa/Kutumia Baba ukavitakase na Kuvifunika/Kuviosha kwa Damu yako..
Tunakwenda kinyume na Roho chafu,Nguvu za giza,Kukata tamaa,Kukataliwa,Magonjwa Shida/Tabu
Baba ukatulinde na kutuokoa...Tunayakabidhi haya yote tuliyoyanena, tunayoyawaza/Yaliyo moyoni mwetu Baba yote unayajua..
Tunaomba na Kushukuru,Tukiamini wewe ni Baba Mungu wetu na Mwokozi wetu..Amina..!!
Muwe na wakati mwema.


Abramu anamwokoa Loti
1Wakati huo, mfalme Amrafeli wa Shinari, mfalme Arioko wa Elasari, mfalme Kedorlaomeri wa Elamu na mfalme Tidali wa Goiimu, 2walipigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, dhidi ya Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na dhidi ya mfalme wa Bela (yaani Soari). 3Wafalme hao watano waliyaunganisha majeshi yao katika bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi). 4Kwa muda wa miaka kumi na miwili walikuwa wakimtii mfalme Kedorlaomeri, lakini mnamo mwaka wa kumi na tatu, walimwasi. 5Mnamo mwaka wa kumi na nne, mfalme Kedorlaomeri na wale wafalme wenzake walikuja na kuwashinda watu wa Refaimu huko Ashtaroth-karnaimu, na Wazuzi huko Hamu, na Waemi huko Shawe-kiriathaimu, 6na Wahori huko mlimani kwao Seiri, wakawafukuza hadi Elparani, mpakani mwa jangwa. 7Kisha wakarudi nyuma mpaka Enmishpati (yaani Kadeshi), wakaivamia nchi yote ya Waamaleki, na kuwashinda Waamori waliokaa Hasason-tamari.
8Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu na mfalme wa Bela 9(yaani Soari), wakaingia vitani katika bonde la Sidimu kupigana na Kedorlaomeri mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goiimu, Amrafeli mfalme wa Shinari na Arioko mfalme wa Elasari; wafalme wanne dhidi ya wafalme watano. 10Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami; kwa hiyo wafalme wa Sodoma na Gomora walipokuwa wakiikimbia vita, wakatumbukia humo, lakini wengine wakatorokea mlimani. 11Basi, wale walioshinda, wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora, kadhalika na mazao yao, wakaenda zao. 12Walimteka hata Loti, mwana wa nduguye Abramu aliyekuwa anakaa Sodoma, pamoja na mali yake, wakaenda zao.
13Mtu mmoja aliyeponyoka, akaenda kumwarifu yule Mwebrania Abramu ambaye alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mwamori Mamre. Mamre alikuwa ndugu yake Eshkoli na Aneri. Wote walikuwa wamefanya agano na Abramu. 14Abramu alipopata habari kwamba mpwa wake amechukuliwa mateka, akatoka na watu wake stadi 318 waliozaliwa katika nyumba yake, akawafuatia adui mpaka Dani. 15Huko, akaligawa jeshi lake katika makundi. Usiku, akawashambulia adui zake, akawashinda na kuwafukuza hadi Hoba, kaskazini mwa Damasko. 16Basi, Abramu akaikomboa mali yote iliyotekwa na adui, na kumkomboa Loti mpwa wake, mali yake, pamoja na wanawake na watu wengine.
Melkisedeki anambariki Abramu
17Abramu aliporudi baada ya kumshinda mfalme Kedorlaomeri na wenzake, mfalme wa Sodoma alitoka kwenda kumlaki katika bonde la Shawe, (yaani Bonde la Mfalme). 18Naye Melkisedeki, mfalme wa mji wa Salemu, ambaye alikuwa kuhani wa Mungu Mkuu, akaleta mkate na divai, 19akambariki Abramu akisema,
“Abramu na abarikiwe na Mungu Mkuu,
Muumba mbingu na dunia!
20Na atukuzwe Mungu Mkuu,
aliyewatia adui zako mikononi mwako!”
Naye Abramu akampa Melkisedeki mchango wake sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo.
21Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu, lakini jichukulie mali yote wewe mwenyewe.” 22Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, aliyeumba mbingu na dunia, 23kwamba sitachukua uzi au kamba ya kiatu, wala chochote kilicho chako, usije ukajivuna na kusema kwamba umenitajirisha. 24Basi, sitachukua chochote isipokuwa tu vile vitu vijana wangu walivyokula na sehemu ya wale waliokuwa pamoja nami, Aneri, Eshkoli na Mamre ambao wana haki nayo.”
Mwanzo14;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 6 February 2017

Kikombe Cha Asubuhu;Mwanzo 13...

Shalom,Habari za Asubuhi,Mmeamkaje,Wapendwa/Waungwana?
Siku/wiki Nyingine tena kwa Neema/Rehema za Mungu tumebarikiwa kuiona leo hii..
Tunamshukuru sana Mungu kwa Neema hii,Tuanze wiki hii vyema kwa kumrudishia Mungu Utukufu na Sifa yeye
Astahiliye yote,Mungu wetu aliyeumba Mbingu na Nchi, Yeye ni kimbilio la wote,Yeye akatubariki kuingia/Kutoka kwetu
kwenye Vyombo vya usafiri,Akabariki Kazi zetu,Biashara,Akawaguse na kuwaongoza wanafunzi katika masomo yao, Wapate kukumbuka na kuelewa wanayofundishwa.
Akawaponye Wagonjwa walio Mahospitalini/Majumbani,Wenye Shida/Tabu,Wanaopitia Magumu/Majaribu wamgeukie Mungu na kuomba pasipo kikomo yeye anatosha..
Akawafariji wafiwa,Akawaguse Yatima na Wajane...Wafungwa walio Magerezani pasipo na hatia baba akawaguse, Waliofungwa kwa shida mbalimbali za kidunia,Shetani na minyororo yoyote ya nguvu za Giza Baba ukawafungue na Wakapate Uponyaji..
Tumshukuru Mungu na Kumtukuza,Kuomba na Kuamini yeye ni mwingi wa Huruma na Uponyaji..
Anza na Mungu naye hatokuacha....!!!!
Mungu awabariki Sana.



Abramu na Loti wanatengana

1Abramu akarudi kutoka Misri, akaingia upande wa Negebu. Alikuwa na mkewe na mali yake yote pamoja na Loti. 2Wakati huo, Abramu alikuwa ametajirika sana. Alikuwa na mifugo, fedha na dhahabu. 3Akaendelea kusafiri toka eneo la Negebu hadi Betheli. Alifika mahali alipokuwa amepiga kambi ya hema hapo awali, kati ya Betheli na Ai, 4ambapo alikuwa amejenga madhabahu. Hapo Abramu akamwomba Mwenyezi-Mungu kwa jina lake. 5Kadhalika, Loti, ambaye alifuatana na Abramu, alikuwa na kondoo, mifugo na hema. 6Idadi ya mifugo yao ilikuwa kubwa mno hata nchi ile haikuweza kuwatosha Abramu na Loti kuishi pamoja. 7Basi, kukazuka ugomvi kati ya wachungaji wa Abramu na wachungaji wa Loti. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo.
8Basi, Abramu akamwambia Loti, “Kusiwe na mafarakano kati yetu wala kati ya wachungaji wako na wachungaji wangu, kwa sababu sisi ni jamaa moja. 9Tazama nchi hii yote mbele yako. Na tutengane. Ukienda kushoto, mimi nitakwenda kulia; ukienda kulia, mimi nitakwenda kushoto.”
10Loti akatazama, akaliona bonde la mto Yordani, akaona kuwa lina maji ya kutosha kila mahali, kama bustani ya Mwenyezi-Mungu na kama nchi ya Misri upande wa Soari. (Hii ilikuwa kabla Mwenyezi-Mungu hajaiangamiza miji ya Sodoma na Gomora). 11Kwa hiyo, Loti akajichagulia bonde lote la mto Yordani, akaelekea mashariki, na hivyo wakatengana. 12Abramu akabaki nchini Kanaani na Loti akakaa kati ya miji iliyokuwa bondeni, akahamishia kambi yake Sodoma. 13Watu wa Sodoma walikuwa waovu na watenda dhambi wakuu dhidi ya Mwenyezi-Mungu.

Abramu anaoneshwa nchi

14Baada ya Loti kujitenga na Abramu, Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Angalia toka hapo ulipo utazame pande zote: Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi. 15Nchi hii yote unayoiona nitakupa wewe na wazawa wako iwe yenu milele. 16Wazawa wako nitawafanya wawe wengi wasiohesabika, kama vile mavumbi ya nchi yasivyoweza kuhesabika! 17Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.” 18Kwa hiyo, Abramu akangoa hema, akaenda kukaa karibu na mialoni ya Mamre kule Hebroni; huko akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu.
Mwanzo 13;1-18

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili Mbarikiwe.

Friday 3 February 2017

Wanawake na Maisha;Mwanamke/Mama huyu Mjane amenigusa..;Wanawake wengi wanapitia haya...







Shukrani;BongoStars

Haya mambo yanawakuta wanawake wengi wanapofiwa na waume/wenza wao,Inafikia baba wadogo/Ndugu wa mume wanawagombanisha mama na watoto...
Wewe imeshakukuta/kupitia haya matatizo, Au mtu wako wa karibu?
Mungu awabariki wamama wote na wote wanaopitia/waliopitia haya.

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo12..

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tunamshukuru Mungu muumba wa Mbingu na Nchi,
Muweza wa yote,Bwana wa Mabwana,
Baba wa Yatima,Mume wa Wajane..
Tumsifu,Tumuabudu,Tumuombe,Tumkabidhi mizigo yetu...
Asante Mungu wetu kwa Neema/Rehema hii Baba ya kuiona siku nyingine tena
wengi walitamani kuiona Baba lakini imeshindikana,
 si kwamba si wema au wakosefu sana bali ni kwa Mapenzi yako..
Ukabariki  Kuingia/Kutoka kwetu,Vyombo vya usafiri,kazi zetu Baba wa mbinguni,Biashara,Masomo na ukatupe sawasawa na mapenzi yako.
Utulinde na kutuokoa katika Shida/Tabu,Ukawafariji wafiwa,Utusamehe Baba wa Mbinguni nasi tupate kuwasamehe waliotukosea,Tunakwenda kinyume na Shetani na Tunakutanguliza/Kuja kwako Mfalme wa Amani..Ukatuongoze katika Maisha yetu.
Ameeeen..!!!!
Mungu yu Macho na  Anasamehe,Anasikia, Omba pasipo  kuchoka.
Mbarikiwe sana.


Mungu anamwita Abramu aiache nchi yake

1Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, acha jamaa yako na nyumba ya baba yako, uende katika nchi nitakayokuonesha. 2Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka.
3Anayekubariki, nitambariki;
anayekulaani, nitamlaani.
Kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”
4Kwa hiyo, Abramu akaondoka kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru; na Loti akaenda pamoja naye. Abramu alikuwa na umri wa miaka 75 alipotoka Harani. 5Alimchukua Sarai mkewe, na Loti mwana wa ndugu yake, pamoja na mali yao yote na watu wote waliokuwa wamejipatia huko Harani, wakaondoka kuelekea nchi ya Kanaani. Walipoingia nchini Kanaani, 6Abramu akapita katikati ya nchi mpaka Shekemu, mahali patakatifu, penye mti wa mwaloni wa More. Wakati huo, Wakanaani walikuwa ndio wenyeji wa nchi hiyo. 7Ndipo Mwenyezi-Mungu akamtokea Abramu, akamwambia, “Wazawa wako nitawapa nchi hii.” Basi, Abramu akajenga madhabahu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu aliyemtokea. 8Baadaye Abramu akaondoka, akaelekea mlimani mashariki ya Betheli akapiga hema kati ya mji wa Betheli, upande wa magharibi, na mji wa Ai upande wa mashariki. Hapo pia akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu na kumwomba kwa jina lake. 9Kisha Abramu akaendelea kusafiri kuelekea upande wa Negebu.

Abramu nchini Misri

10Wakati huo, njaa ilitokea nchini. Njaa hiyo ilikuwa kali, hivyo Abramu akalazimika kwenda Misri kukaa huko kwa muda. 11Alipokaribia Misri, Abramu alimwambia Sarai mkewe, “Najua kuwa wewe ni mwanamke mzuri na wa kuvutia. 12Wamisri watakapokuona watasema, ‘Huyu ni mkewe,’ kisha wataniua lakini wewe watakuacha hai. 13Basi, waambie kuwa wewe ni dada yangu ili mambo yaniendee vema, niachwe niishi kwa ajili yako.” 14Basi, Abramu alipowasili nchini Misri, wenyeji wa huko walimwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana. 15Maofisa wa Farao walipomwona Sarai, wakamsifia kwa Farao. Basi, Sarai akapelekwa nyumbani kwa Farao. 16Basi, kwa ajili yake, Farao alimfadhili Abramu, akampa kondoo, ng'ombe, punda dume, watumishi wa kiume na wa kike, punda jike na ngamia.
17Lakini Mwenyezi-Mungu akamtesa Farao na watu wote wa nyumba yake kwa mapigo makali kwa sababu ya Sarai, mkewe Abramu. 18Farao akamwita Abramu, akamwuliza, “Ni kitu gani hiki ulichonitendea? Mbona hukunijulisha kwamba Sarai ni mkeo? 19Kwa nini ulisema ni dada yako hata nikamchukua kuwa mke wangu? Basi, sasa mkeo ndiye huyo. Mchukue uende zako!” 20Kisha Farao aliwaamuru watu wake, nao wakamsindikiza Abramu njiani akiwa na mke wake na mali yake yote.
Mwanzo 12;1-20
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.