Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru kwa yote... Asante Baba wa Mbinguni, Baba yetu na Mungu wetu,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuiona Leo hii..Tazama Jana imepita Baba Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Jehovah..!! Tunakuja mbele zako na tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Yahweh..!!Tunaomba utubariki katika maisha yetu,Utamalaki na kutuatamia,Ulinzi upo nawe Baba,Furaha,Upendo,Tumaini,Wema na Fadhili zipo kwako Jehovah..!! Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote.. Tukawe Barua njema na tusomeke vyema Baba.. Ukatuongezee Hekima,Busara,utuwema na Kukutafuta wewe zaidi..
Tupendane sisi kwa sisi na tupende wengine..Jehovah..!!
Mwanga wa mwili
(Mat 5:15; 6:22-23)
“Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa debe, bali huiweka juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga. Jicho lako ni taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza. Uwe mwangalifu basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza. Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwili huo utangaa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia kwa mwanga wake.”
Tunakwenda kinyume na Mwovu na kazi zake zote.. Tunakuja mbele zako Tunaomba Utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..kwakuwaza,Kwakunena/kutenda,kwakujua/kutojua.Baba Utupe Neema ya kuweza kuwasaheme nasi waliotukosea..
Mfano wa mwana mpotevu
Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu mmoja mwenye watoto wawili wa kiume. Yule mdogo alimwambia baba yake: ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Naye akawagawia mali yake. Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo. Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika. Akaomba kazi kwa mwananchi mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe. Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu. Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa? Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’ Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu. “Mwanae akamwambia: ‘Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.’ Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: ‘Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu! Mchinjeni ndama mnono; tule na kusherehekea! Kwa sababu huyu mwanangu; alikuwa amekufa, kumbe yu hai; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’ Wakaanza kufanya sherehe. “Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani, akasikia vifijo na ngoma. Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: ‘Kuna nini?’ Huyo mtumishi akamwambia: ‘Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.’ Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie. Lakini yeye akamjibu: ‘Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwanambuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu! Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba, mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.’ Baba yake akamjibu: ‘Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni chako. Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’”
Asante kwa Neema/Rehema zako zatutosha hakuna cha kulinganisha nawe Mfalme wa Amani..Tunayaweka haya yote mikononi mwako tukisifu, tukiamini na kushukuru..
Amina..!! Mungu aendelee kuwabariki katika yote..wote mliopita hapa nawapenda na Asanteni sana..
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote...
Amina.
|