Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 22 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..20..


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Ni siku nyingine tena Mungu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Kwa wema na fadhili zake ametulinda usiku na wakati wote,Ametupa neema/rehema hii ya kuamka salama wenye afya na kuendelea na kazi/mambo yetu katika kutafuta ridhiki na yote yanayotukabili mbele yetu yeye akatuongoze  kwa maana peke yetu hatutaweza..


Mwenyezi-Mungu asipoijenga nyumba, waijengao wanajisumbua bure. Mwenyezi-Mungu asipoulinda mji, waulindao wanakesha bure.
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Tunaomba utusamehe pale tulikwenda kinyume nawe kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..

Ututakase Miili yetu na Akili zetu,Utufunike kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo..Yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa visiweko tena. Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni mwema.” Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa. Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea tambiko za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama! Naweka jiwe huko Siyoni, jiwe la msingi, teule na la thamani. Mtu atakayemwamini huyo hataaibishwa.” Kwenu nyinyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.” Tena Maandiko yasema: “Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuwaangusha watu.” Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini ule ujumbe; na ndivyo walivyopangiwa tangu mwanzo. Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu. Wakati mmoja nyinyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa nyinyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa mmepokea huruma.


Mungu wetu ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na mapezni yako..


Asante Mungu wetu tunaomba ukaibariki siku hii na ukabariki vyote tunavyoenda kutenda/kufanya na tukafanye sawaswa na mapenzi yako..
Vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Mungu wetu ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu tuliyanena na tusiyoyanena Mungu wetu unayajua na kutujua vyema kuliko tujijuavyo sisi..
Tunakushukuru na kukusifu Daima..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..

Amina..!

Asanteni sana kwakuwanami/kunisoma..
Mungu aendelee kuwabariki na msipungukiwe na neema yake..
Nawapenda sana.



Adhabu kwa ajili ya maovu

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Waambie Waisraeli hivi: Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayekaa miongoni mwenu, akimtoa sadaka mtoto wake yeyote kwa mungu Moleki ni lazima mtu huyo auawe. Wananchi wa hapo watamuua kwa kumpiga mawe. 3Mimi mwenyewe nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake kwa sababu alimtoa mmoja wa watoto wake sadaka kwa mungu Moleki na hivyo kupachafua mahali pangu patakatifu na jina langu takatifu. 4Kama wananchi wa mahali hapo hawatamwadhibu mtu huyo kwa kumuua, 5mimi mwenyewe nitamkabili mtu huyo na jamaa yake. Nitawatenga kutoka watu wao, yeye mwenyewe pamoja na wote waliokosa uaminifu kwangu kwa kumwendea mungu Moleki.
6“Kama mtu yeyote anawaendea waaguzi wa mizimu na wachawi na hivyo kukosa uaminifu kwangu, nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake. 7Kwa hiyo, jiwekeni wakfu muwe watakatifu; kwani mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. 8Shikeni masharti yangu na kuyatekeleza. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewatakasa. 9Mtu yeyote amlaaniye baba yake au mama yake, ni lazima auawe. Amemlaani baba au mama yake, kwa hiyo damu yake itakuwa juu yake.
10“Kama mwanamume akizini na mke wa jirani yake, ni lazima wote wawili wauawe. 11Mwanamume akilala na mmoja wa wake za baba yake, anamwaibisha baba yake; wote wawili ni lazima wauawe. Damu yao itakuwa juu yao wenyewe. 12Mwanamume yeyote akilala na mke wa mwanawe, wote wawili ni lazima wauawe. Wamefanya zinaa ya maharimu; wanawajibika kwa umwagaji wa damu yao wenyewe. 13Kama mwanamume yeyote akilala na mwanamume mwenzake kana kwamba ni mwanamke, basi, wote wawili ni lazima wauawe kwani wamefanya jambo lililo chukizo; watawajibika kwa umwagaji wa damu yao wenyewe. 14Kama mwanamume akioa mke na pia kumwoa mama yake, huo ni uovu; wote watatu ni lazima wateketezwe kwa moto kwani wamefanya uovu. Mtafanya hivyo ili uovu usiwe miongoni mwenu. 15Kama mwanamume yeyote akilala na mnyama ni lazima auawe; na mnyama huyo lazima auawe. 16Kama mwanamke akimkaribia mnyama na kulala naye ni lazima mwanamke huyo auawe na mnyama huyo pia; damu yao itakuwa juu yao wenyewe.
17“Kama mwanamume yeyote akimwoa dada yake, binti ya baba yake au mama yake, na binti huyo akakubaliana na mwanamume huyo ambaye ni kaka yake, na kulala naye, hilo ni chukizo, ni lazima watengwe na rika lao kwani wamefanya jambo la aibu. Ni lazima mwanamume huyo awajibike kwa uovu wake. 18Kama mwanamume akilala na mwanamke aliye mwezini, wote wawili ni lazima watengwe na watu wao; huyo mwanamume amelala na mwanamke aliye na hedhi, na huyo mwanamke amelala na mwanamume akiwa na hedhi. 19Usilale na dada ya mama yako wala na shangazi yako, maana hao ni jamaa yako wa karibu. Wote watendao hayo watawajibika kwa uovu wao. 20Kama mtu akilala na mke wa baba yake, mkubwa au mdogo, anamwaibisha baba yake mkubwa au mdogo; wote wawili watawajibika kwa dhambi yao; wote wawili watakufa bila watoto. 21#Taz Lawi 18:16 Kama mwanamume akimwoa mke wa ndugu yake, anamwaibisha ndugu yake, huo ni unajisi; wote wawili watakufa bila watoto.
22“Mnapaswa kushika na kutekeleza masharti na maagizo yangu yote; la sivyo nchi ile ambamo ninawapeleka itawatapika. 23Msizifuate desturi za taifa ninalolifukuza mbele yenu; kwani waliyafanya hayo yote, nami nikawachukia sana. 24Lakini, nimekwisha waambia, ‘Mtarithi nchi yao, mimi nawapa nchi hiyo muimiliki, nchi inayotiririka maziwa na asali.’ Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu niliyewatenga na mataifa mengine. 25Kwa hiyo, ni lazima mtofautishe kati ya mnyama asiye najisi na aliye najisi, kati ya ndege asiye najisi na aliye najisi. Msijifanye kuwa najisi kwa kugusa mnyama au ndege au chochote kitambaacho duniani ambacho nimekitenga kuwa ni najisi. 26Kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu ni mtakatifu, nami nimewatenga nyinyi na mataifa mengine ili muwe mali yangu, mtakuwa watakatifu.
27“Mwanamume au mwanamke yeyote aliye mlozi au mchawi, ni lazima auawe kwa kupigwa mawe. Wote watawajibika kwa umwagaji wa damu yao wenyewe.”

Mambo Ya Walawi20;1-27


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 21 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..19...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu katika yote..
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..

Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Asante kwa pumzi na kutuasha wenye afya njema..

Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mfalme wa Amani tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizofanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu,utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote, Ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Mfalme wa Amani tunaomba ukatamalaki na kutuatamia katika nyumba zetu/maisha yetu..

Ukabariki kazi zetu,Biashara,Masomo na ukatuongoze katika utendaji na ukatupe ubunifu na maarifa katika kazi /biashara zetu..
Pale tunapokosea Baba ukatuonyeshe njia,ukatupe mwanga  katika kuendeleza/kuanzisha na tukafanye kama itavyokupendeza wewe..
Mungu wetu ukatupe kutambua na kuelewa nini tunatakiwa kufanya  tukafanye nini wapi na wakati gani katika mazingira tunalinayo..
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu na tusipungukiwe katika mahitaji yetu..na ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuwabariki wanaohitaji..
Mungu wetu ukaonekane popote tunapopita, tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Tazama waliokata tamaa,waliokwama,wenye hofu/mashaka,waliokataliwa,waliokatika vifungo mbalimbali,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,wenye shida/tabu..Mungu wetu ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye kiroho na kimwili pia..Mungu wetu ukawainue na kuwabariki,Ukaonekane katika mahitaji yao..Mungu wetu ukasikie kulia kwao,ukajibu maombi yao,ukawatendee na kuwafadhili..Ukawape sawasawa na mapenzi yako..


Mungu wetu tunakwenda kinyume  na adui yule mwovu, na nguvu zote za giza,Nguvu za mapepo,nguvu za mizimu,za mpinga Kristo.Maagano yote ya mwovu,yeyote anayetunenea mabaya,tunavunja kwa Jina la YESU na tunajifunika kwa Damu ya Bwana wetu YESU Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...


Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu. Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara. Basi, kaeni tayari. Ukweli na uwe kama mkanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu. Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu. Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Injili kwa uthabiti. Mimi ni balozi kwa ajili ya Injili hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.
Asante Mungu wetu tunapokwenda kupokea katika Jina la YESU..
Amani ikatawale moyoni mwetu,Upendo na udumu,Tuendelee kusaidiana na kuhurumiana,tuchukuliane na tusameheane,Tuijue kweli yako nayo ituweke huru..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Tunashukuru na kukusifu daima..


kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!


Asante sana kwakunisoma/kuwa pamoja..
tuendelee kumuomba Mungu pasipo kuchoka..
Munguaendelee kuwabariki katika maisha yetu..
Nawapenda.


Kutenda mema

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2#Taz Lawi 11:44-45; 1Pet 1:16 “Iambie jumuiya yote ya watu wa Israeli hivi: Ni lazima muwe watakatifu kwani mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ni mtakatifu. 3Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. 4Msizigeukie sanamu za miungu, wala msijitengenezee sanamu za kusubu za miungu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
5“Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa. 6Sadaka hiyo ni lazima iliwe siku hiyohiyo inapotolewa au kesho yake. Chochote kinachobaki hadi siku ya tatu ni lazima kiteketezwe kwa moto. 7Kama sehemu ya nyama yake italiwa siku ya tatu, tendo hilo ni chukizo; na sadaka hiyo haitakubaliwa, 8naye atakayekula nyama hiyo ni lazima awajibike kwa uovu wake kwa sababu amekitia unajisi kitu kitakatifu cha Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo atatengwa na watu wake.
9 # Taz Lawi 23:22; Kumb 24:19-22 “Utakapovuna mavuno ya nchi yako, usivune kabisa hadi mpakani mwa shamba wala usirudi nyuma kukusanya mabaki. 10Msirudie kukusanya kila kitu katika shamba la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini; utawaachia maskini na wageni. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
11 # Taz Kut 20:15-16; Kumb 5:19-20; Kut 20:7; Kumb 5:11; Mat 5:33 “Msiibe, msidanganye wala kuambiana uongo. 12Msiape uongo kwa jina langu hata kulikufuru jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
13 # Taz Kumb 24:14-15 “Usimdhulumu jirani yako wala kumwibia. Mshahara wa mtu aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi. 14#Taz Kumb 27:18 Usimlaani kiziwi wala kuweka kizuizi mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
15 # Taz Kut 23:6-8; Kumb 16:19 “Unapotoa hukumu uamue kwa haki; usimpendelee maskini wala kumwogopa mwenye cheo. Bali ni lazima kumwamua jirani kwa haki. 16Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
17 # Taz Mat 18:15 “Usimwekee kisasi ndugu yako moyoni mwako, bali upatane daima na jirani yako ili usije ukatenda dhambi. 18#Taz Mat 5:43 Usijilipize kisasi au kuwa na kinyongo dhidi ya wazawa wa watu wako bali umpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
19 # Taz Kumb 22:9-11 “Yakupasa kuyashika masharti yangu. Usiiache mifugo yako ipandwe na wanyama wa aina nyingine. Shambani mwako usipande mbegu za aina mbili. Usivae vazi lililofumwa kwa aina mbili za nguo.
20“Mwanamume akilala na mwanamke mtumwa ambaye ameposwa na mwanamume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamke huyo hakuwa bado huru. 21Mwanamume huyo ataleta mbele ya hema la mkutano sadaka yake ya kondoo dume ya kuondoa hatia na kunitolea mimi Mwenyezi-Mungu. 22Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.
23“Mtakapofika katika nchi ya Kanaani na kupanda aina zote za miti ya matunda, matunda hayo hamtayala; hamtaruhusiwa kuyala kwa muda wa miaka mitatu. 24Mnamo mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa matakatifu, yatatolewa kuwa sadaka ya sifa,#19:24 sifa: Au shukrani. kwa Mwenyezi-Mungu. 25Lakini matunda ya kuanzia mwaka wa tano hayo mnaweza kula, na mavuno yenu yataongezeka. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
26 # Taz Mwa 9:4; Lawi 7:26-27; 17:10-14; Kumb 12:16,23; 15:23; 18:10 “Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi. 27#Taz Lawi 2:5; Kumb 14;1 Nywele zenu msizikate pembeni wala kunyoa ndevu zenu. 28Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
29 # Taz Kumb 23:17 “Usimchafue binti yako kwa kumfanya kahaba, nchi nzima isije ikaangukia katika ukahaba na hivyo kujaa uovu. 30#Taz Lawi 26:2 Mtazishika Sabato zangu na kupaheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
31 # Taz Kumb 18:11; 1Sam 28:3; 2Fal 23:4; Isa 8:19 “Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
32“Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
33“Kama kuna mgeni katika nchi yako usimtendee vibaya. 34Huyo mgeni anayekaa nawe atakuwa kwako kama mwenyeji nawe utampenda kama unavyojipenda mwenyewe, kwa kuwa nawe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
35 # Taz Kut 22:21; Kumb 24:14-18; 27:19 “Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo. 36Ni lazima mtumie mizani halali, na vipimo vilivyo halali. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. 37Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”

Mambo Ya Walawi19;1-37


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 20 June 2017

Samwel Mwanyika Anyakua tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.


Habari na Picha za Freddy Macha



TUMEZOEA kuwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Ila sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..18...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu katika yote..
Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo ni mali yako,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako Baba..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendele kuiona leo hii..
Mfalme wa Amani tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..

Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
utuepushe katika majaribu na utuokoe na  yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..


Basi, sisi tunajua umuhimu wa kumcha Bwana, na hivyo tunajitahidi kuwavuta watu. Mungu anatujua waziwazi, nami natumaini kwamba nanyi pia mnatujua kinaganaga. Si kwamba tunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ila tunataka kuwapa nyinyi sababu zetu za kuona fahari juu yenu, ili mpate kuwajibu wale wanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsi walivyo moyoni. Ikiwa tumeonekana kuwa wendawazimu, hiyo ni kwa ajili ya Mungu; na ikiwa tunazo akili zetu timamu, hiyo ni kwa faida yenu. Maana mapendo ya Kristo yanatumiliki sisi ambao tunatambua ya kwamba mtu mmoja tu amekufa kwa ajili ya wote, na hiyo ina maana kwamba wote wanashiriki kifo chake. Alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa, akafufuliwa kwa ajili yao. Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena. Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika. Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye. Ndiyo kusema: Mungu, amekuwa akiupatanisha ulimwengu naye kwa njia ya Kristo, bila kutia maanani dhambi zao binadamu. Yeye ametupa ujumbe kuhusu kuwapatanisha watu naye. Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia sisi kuwasihi nyinyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. Kristo hakuwa na dhambi, lakini Mungu alimfanya ahusike na dhambi kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungana naye, tupate kuushiriki uadilifu wake Mungu.

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukapate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..

Ee Mungu wetu Tunakutukuza na kutukuza Jina lako..
Ee Mungu wetu tunakusifu na kusifu Jina lako..
Ee Mungu wetu asante kwakutupenda kwanza..
Ee Mungu wetu utupe neema ya kupendana nasi,Utupe neema ya kushinda majaribu,Utupe neema ya kufuata Neno lako,Sheria na Amri zako..
Ee Mungu wetu utuepushe na Kiburi,choyo,chuki,majivuno,kujisifu,kujitukuza,dharau,masimango,wivu na kuneneana mabaya..
Ukatupe macho ya Rohoni na masikio ya kusikia..Mdomo wa kukusifu na kutangaza Neno lako,Hekima,Busara,Utuwema,Upendo,Maarifa,Ubunifu na tukatambue nini chakufanya/tunatakiwa kufanya..ukatuonyeshe njia iliyo yako na kila mmmoja akajue jukumu lake na kazi zake ulizomtuma hapa Duniani..

Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Ukaibariki  siku hii na ukatubariki katika yote ..
Vyote tunavyoenda kutenda/kugusa na ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Asante Mungu wetu wewe watosha..

Hakuna na  hatokuwepo kama wewe..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu..
tuliyoyanena na tusiyoyanena Mungu wetu unayajua na kutujua sisi zaidi ya tunavyojijua wenyewe..
Sifa na Utukufu ni wako..Tunakushukuru Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..

 Amina...!

Asanteni sana sana Wapendwa kwa kuwa nami/kunisoma..

Mungu akawaongoze kwa kila jambo..
Nawapenda.

Matendo maovu ya ndoa

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Waambie watu wa Israeli hivi: Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. 3Kamwe msifanye kama wafanyavyo watu wa nchi ya Misri ambako mlikaa; wala msifanye kama wafanyavyo watu wa nchi ya Kanaani ambako nawapeleka. Kamwe msifuate mitindo yao. 4Nyinyi mtafuata maagizo yangu na kuyashika masharti yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. 5#Taz Neh 9:29; Eze 18:9; 20:11-13; Luka 10:28; Roma 10:5; Gal 3:12 Kwa hiyo, ili mtu apate kuyaokoa maisha, mnapaswa kuyashika masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
6“Mtu yeyote wa Israeli haruhusiwi kumkaribia mtu wa jamaa yake wa karibu ili kulala naye. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. 7Kamwe usimvunjie heshima baba yako kwa kulala na mama yako aliyekuzaa. Usimwaibishe; yeye ni mama yako. 8Kamwe usimvunjie heshima baba yako kwa kulala na mmoja wa wake zake. Hao ni mama zako. 9Kamwe usilale na dada yako, awe ni dada yako halisi au dada yako wa kambo. 10Kamwe usilale na mjukuu wako, mtoto wa mwanao au binti yako; maana sehemu zao za siri ni kama zako mwenyewe. 11Kamwe usilale na msichana aliyezaliwa na mama yako wa kambo aliyeolewa na baba yako; msichana huyo ni dada yako. 12Kamwe usilale na shangazi yako; kwani huyo ni dada wa baba yako. 13Kamwe usilale na dada wa mama yako; kwani huyo ni mama yako mkubwa au mdogo. 14Kamwe usilale na mke wa baba yako mkubwa au mdogo; huyo ni mama yako. 15Kamwe usilale na mke wa mwanao; huyo ni mkewe mwanao. Kamwe usilale naye. 16Kamwe usilale na mke wa ndugu yako; huyo ni shemeji yako. 17Ukilala na mwanamke, basi, kamwe usilale naye na binti yake, wala wajukuu zake. Hao ni ndugu. Kuwachanganya ni kufanya uovu. 18Kamwe usimwoe dada wa mkeo wakati mke wako yungali hai; hiyo itasababisha ushindani.
19 # Taz Neh 9:29; Eze 18:9; 20:11-13; Luka 10:28; Roma 10:5; Gal 3:12 “Kamwe usilale na mwanamke awapo mwezini. 20#Taz Lawi 20:10 Kamwe usilale na mke wa jirani yako na hivyo kujitia mwenyewe najisi naye.
21 # Taz Lawi 20:1-5 “Kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utalikufuru jina langu mimi Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
22 # Taz Lawi 20:13 “Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni mwanamke. Hilo ni chukizo. 23#Taz Kut 22:19; Lawi 15-16; Kumb 27:21 Kamwe usilale na mnyama ili usijitie najisi; mwanamume au mwanamke yeyote kamwe asifanye hivyo; kufanya hivyo ni upotovu.
24“Msijitie najisi kwa kufanya mambo hayo kwani kwa sababu ya mambo hayo nayafukuza mataifa yaliyo mbele yenu kwa vile wao hufanya hayo na kujitia najisi. 25Nchi yao ilitiwa unajisi nami nikaiadhibu, nayo ikawakataa wakazi wake. 26Lakini nyinyi na wageni wanaokaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti na maagizo yangu na wala msifanye machukizo hayo. 27Machukizo hayo waliyafanya watu waliokaa katika nchi ya Kanaani kabla yenu, nao wakaitia nchi unajisi. 28Basi, nyinyi msifanye mambo hayo, la sivyo nchi hiyo itawatapika kama ilivyolitapika taifa lililokuwa kabla yenu. 29Watu wote watakaofanya mambo hayo ya kuchukiza ni lazima watengwe mbali na watu wao. 30Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”

Mambo Ya Walawi18;1-30


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 19 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..17...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Ni siku/wiki nyingine tena Mungu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona..
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako..
Asante kwa ulinzi wako usiku na wakati wote..
Tunakuja mbele zako Baba wa Mbinguni tukijinyenyekeza,kujishusha na kujiachilia mikononi mwako Jehovah..!!
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbingini tulizifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wote waliotukosea..

utuepushe na majaribu na utuokoe na hila za mwovu na kazi zake zote..
Ututakase miili yetu na Akili zetu na ukatufunike kwa Damu ya mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti....
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote,tupatekutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..
Baba wa Mbinguni tunaiweka siku hii  na maisha yetu  hii mikononi mwako,ukatubariki,ukatuongoze ,ukatupe Amani,Upendo,Wema,Fadhili,Hekima,Busara,Upole kiasi..
Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda na ukabariki ridhiki zetu ziingizo/zitokazo..

Tazama wenyeshida/tabu,wanaopitia majaribu mbalimbali,waliokwenyevifunguo mbalimbali,waliokata tamaa,wenye hofu na mashaka Baba wambinguni ukawatendee sawasawa na mapenzi yako..


Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambo haya. Napenda mkumbuke maneno yaliyosemwa na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi mliyopewa na mitume wenu. Awali ya yote jueni kwamba siku za mwisho watakuja watu ambao mienendo yao inatawaliwa na tamaa zao mbaya. Watawadhihaki nyinyi na kusema: “Aliahidi kwamba atakuja! Je, sasa yuko wapi? Mambo ni yaleyale tangu babu zetu walipokufa; hali ya vitu ni ileile kama ilivyokuwa mwanzo wa ulimwengu!” Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na dunia zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji; na kwa maji hayo, yaani yale maji ya gharika kuu, dunia ya wakati ule iliangamizwa. Lakini mbingu na dunia ya sasa zahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa ajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya siku ile ambapo watu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa. Lakini, wapenzi wangu, msisahau kitu kimoja! Mbele ya Bwana, hakuna tofauti kati ya siku moja na miaka elfu; kwake yote ni mamoja. Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu. Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake. Maadamu kila kitu kitaharibiwa namna hiyo, je, nyinyi mnapaswa kuwa watu wa namna gani? Mnapaswa kuishi kitakatifu na kumcha Mungu, mkiingojea siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi – siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto. Lakini sisi, kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingu mpya na dunia mpya ambayo imejaa uadilifu. Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnaingojea siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye. Mnapaswa kuuona uvumilivu wa Bwana kuwa ni nafasi anayowapeni mpate kuokolewa, kama Paulo ndugu yetu mpenzi alivyowaandikia akitumia hekima aliyopewa na Mungu. Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe. Lakini nyinyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara. Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwe kwake, sasa na hata milele! Amina.
Mungu wetu tunayaweka haya yote mikononi mwako..
tukiamini na kushukuru  kwa upendo wako kwetu na katika yote..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!


Mungu aendelee kuwabariki..
Asanteni sana kwakuwa nami..
Nawapenda..



Mwongozo kuhusu damu

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Mwambie Aroni, wanawe na watu wote wa Israeli amri zifuatazo: 3Kama mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli akichinja ng'ombe au mwanakondoo au mbuzi ndani au nje ya kambi, 4badala ya kumleta mnyama huyo kwenye mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu mbele ya maskani yake takatifu, mtu huyo atakuwa na hatia ya kumwaga damu; amemwaga damu na atatengwa na watu wake. 5Kusudi la sheria hii ni kwamba Waisraeli wanapaswa kuleta wanyama ambao wangewachinjia mashambani ili wawalete kwa Mwenyezi-Mungu kwa kuhani kwenye mlango wa hema la mkutano, naye atawachinja na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za amani. 6Basi, kuhani atainyunyizia damu madhabahu ya Mwenyezi-Mungu iliyoko mlangoni mwa hema la mkutano na kuyateketeza yale mafuta yawe harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu. 7Kwa hiyo Waisraeli watakoma kabisa kutambikia yale majini, jambo ambalo limewafanya wakose uaminifu kwangu. Sharti hili ni la kudumu milele katika vizazi vyao vyote.
8“Waambie kwamba mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayeishi kati yao, anayetoa sadaka ya kuteketezwa au tambiko, 9lakini haileti mbele ya mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atatengwa na watu wake.
10 # Taz Mwa 9:4; Lawi 7:26-27; l9:26; Kumb 12:16,23; 15:23 “Kama mtu yeyote wa jumuiya ya Israeli au mgeni anayeishi kati yao anakula damu yoyote, mimi nitamwandama mtu huyo aliyekula damu na kumtenga mbali na watu wake. 11#Taz Ebr 9:22 Itakuwa hivyo kwa sababu uhai wa kiumbe umo katika damu. Nimewaagiza kuitolea damu madhabahuni ili kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili ya roho zenu; kwa sababu damu hufanya upatanisho maana uhai umo katika damu. 12Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli hivi: Mtu yeyote miongoni mwenu wala mgeni anayeishi kati yenu kamwe asile damu.
13“Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayekaa miongoni mwao akienda kuwinda mnyama au ndege, ni lazima aimwage damu chini na kuifunika kwa udongo. 14Maana, uhai wa kila kiumbe umo katika damu. Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli, kamwe wasile damu ya kiumbe chochote kwani uhai wa kiumbe chochote ni damu yake. Yeyote atakayekula damu atatengwa.
15“Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi. 16Lakini asipoyafua mavazi yake na kuoga, ni lazima mtu huyo awajibike kwa uovu wake.”

Mambo Ya Walawi17;1-16


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.


Sunday 18 June 2017

Natumaini Jumapili ilikuwa njema/inaendelea vyema;Happy Father's Day..Burudani-Phil Wickham - This Is Amazing Grace,At Your Name (Yahweh Yahweh)



Shalom wapendwa/waungwana;Nimatumaini yangu mnaendelea vyema na mmekuwa kuwa na wakati mzuri Jumapili hii..
Hapa kwetu leo kijua kimewaka haswaaa kama tupo Dar..
Tunamshukuru Mungu katika yote..

Niwatakie heri na baraka wa Baba wote.."Happy Father's Day" kwa wazazi/Baba wote wanaojua majukumu yao ..
Mungu aendelee kuwaongoza katika malezi ya watoto wenu na kwa watoto wengine wote..

Nimshukuru Baba wa watoto wangu kwa kuwa karibu na watoto wake na kujua/kutumikia majukumu yake..Mungu aendelee kumuongoza..
R.I.P. Baba yangu haupo nasi lakini kila leo tunakukumbuka katika yote..
ulipokuwa unatuasa/kutufundisha ,Kutushauri yooote tunayaona  sasa..
Ulipokuwa unasema wakati ule tulikuwa tunaona kama unaimba au unaongea sana[unatuzingua]
Maneno hayaozi...
Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo yeye nimwema tuu..



Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema. “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.” Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.


Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu, tegeni sikio mpate kuwa na akili.

Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha nyinyi, bali kwa ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi. Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema. Kwa hiyo, nawasihi: Fuateni mfano wangu. Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.








"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Friday 16 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..16...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu katika yote..

Yeye aliyetuamsha salama,Yeye atulindaye kila wakati,Yeye ni Mungu wetu na Muumba wetu,Yeye ni Baba yetu, Yeye ni Muweza wa yote,Yeye akisema ndiyo hakuna wakupinga,Yeye Ndimi Mwenyezi-Mungu..!!Yeye hubariki watu wake,,Yeye ni  mwenye huruma,Yeye husamehe,Yeye asifiwe,Yeye huponya,Yeye apokea maombi yetu,Yeye aokoa,Yeye asiye sinzia wala kulala,Mungu wetu yu mwema sana...


Hapo, Balaamu akamtolea Balaki kauli yake: “Inuka, Balaki, usikie, nisikilize ewe mwana wa Sipori. Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize? Tazama, nimepewa amri ya kubariki, naye amebariki wala siwezi kuitangua. Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo, wala udhia kwa hao wana wa Israeli. Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao, Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao, yeye huzipokea sifa zao za kifalme. Mungu aliyewachukua kutoka Misri, huwapigania kwa nguvu kama za nyati. Hakika ulozi hauwezi kuwapinga watu wa Yakobo, wala uchawi dhidi ya watu wa Israeli. Sasa kuhusu Israeli, watu watasema, ‘Tazameni maajabu aliyotenda Mungu!’ Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike, wanasimama kama simba dume. Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake, na kunywa damu ya mawindo.”
Mungu akatupiganie,Mungu akatutendee,Mungu akatulinde na kutuongoza,Mungu akatuokoe katika nguvu za giza,nguvu za mpinga Kristo zishindwe katika jina Kuu kushinda majina yote  la Bwana wetu Yesu Kristo,Mungu akatuinue na tukasimame imara..

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na Fadhili zako..

Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Mfalme wa Amani tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikoni mwako Mungu wetu..
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe walio tukosea..
Utuokoe na mwovu na kazi zake zote,Ututakase Miili yetu na Akkili zetu kwa Damu ya mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..Yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika maisha yetu tupate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..

Mungu wetu tunaomba utubariki na ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda,kugusa/kutumia na ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Baba wa Mbinguni tunaomba ulinzi wako kwetu  sisi na vyote tunavyovimiliki vilivyo ndani na vilivyo nje Mungu wetu ukavifunike kwa Damu ya Bwana  wetu Yesu Kristo..
Mungu Baba ukaonekane kwenye maisha yetu na tusipungukiwe kwenye mahitaji yetu, popote tunapokuwa na chochote tunachofanya Mungu wetu ukajiinue na tukatende sawasaswa na mapenzi yako..
Tazama wenye shida/tabu,Yatima na Wajane,wagonjwa,wafiwa ukawe mfariji wao,waliokata tamaa,wenye hofu/mashaka,waliokataliwa/kutengwa pasipo sababu,waliokatika vifungo mbalimbali,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukawaponye na kuwatendea sawasawa na mapenzi yako..

Sifa na utukufu ni kwako Mungu wetu..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu..
Tuliyoyanena na tusiyoyanena Mungu wetu unayajua na kutujua vyema kuliko tujijuavyo wenyewe..

Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwa kuwa nami..
Mungu awe nanyi Daima..
sina neno zuri zaidi ya kusema..
Nawapenda.


Siku ya msamaha wa dhambi

1Mwenyezi-Mungu alizungumza na Mose, baada ya wana wawili wa Aroni kufa wakati ule walipomkaribia. 2#Taz Ebr 6:19 Alimwambia, “Mwambie ndugu yako Aroni asiingie mahali patakatifu nyuma ya pazia wakati usiokubaliwa. Asiingie mahali hapo kwani ndipo nitakapotokea katika wingu juu ya kiti cha rehema. Asipotii, atakufa. 3#Taz Ebr 9:7 Aroni ataingia mahali patakatifu sana akiwa na fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. 4Ataoga mwili wote katika maji, kisha atavaa mavazi matakatifu. Ataingia mahali hapo akiwa amevaa mavazi matakatifu: Joho la kitani baada ya nguo ya ndani ya suruali ya kitani na akiwa amevaa kanzu ya kitani na kujifunga mkanda wa kitani. 5Atatwaa kutoka jumuiya ya watu wa Israeli beberu wawili kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na kondoo dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.
6“Aroni atamtoa huyo fahali sadaka ya kuondoa dhambi kwa ajili yake mwenyewe, na kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na jamaa yake. 7Kisha, wale beberu wawili atawaweka kwenye mlango wa hema la mkutano. 8Atawapigia kura hao beberu wawili, kura moja kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na nyingine kwa ajili ya Azazeli. 9Atamleta yule beberu ambaye kura ilimtaka kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na kumtolea sadaka ya kuondoa dhambi. 10Lakini yule beberu aliyetakiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atatolewa mbele ya Mwenyezi-Mungu akiwa hai ili kufanya ibada ya upatanisho kuhani atamwacha aende jangwani kwa Azazeli, ili kuondoa dhambi za jumuiya.
11“Aroni atamtoa fahali wa sadaka ya kuondoa dhambi kwa ajili yake mwenyewe, na kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya jamaa yake, kisha atamchinja fahali huyo sadaka ya kuondoa dhambi. 12Halafu atachukua chetezo na kutwaa makaa madhabahuni mbele ya Mwenyezi-Mungu na ubani konzi mbili uliosagwa vizuri sana. 13Ili asije akafa, atauleta ubani huo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuutia katika moto ili moshi wa ubani huo ukifunike kifuniko cha sanduku la agano. 14Atachukua kiasi cha damu ya yule fahali na kunyunyiza kwa kidole chake upande wa mashariki juu ya kiti cha rehema kisha atainyunyizia mbele ya sanduku la agano mara saba kwa kidole chake.
15 # Taz Ebr 9:12 “Halafu atamchinja yule beberu wa sadaka ya kuondoa dhambi kwa ajili ya watu wote. Damu ya mbuzi huyo ataileta ndani mahali patakatifu sana na kufanya kama alivyofanya na damu ya yule fahali; atainyunyiza juu ya kiti cha rehema, upande wake wa mbele. 16Hivyo atafanya ibada ya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu kwa sababu ya unajisi, makosa na dhambi zote za Waisraeli. Ndivyo atakavyofanya pia kwa ajili ya hema la mkutano lililo miongoni mwa watu hao walio najisi. 17Wakati Aroni anafanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe, jamaa yake na jamii nzima ya Israeli, kamwe asiwepo mtu yeyote ndani ya hema la mkutano hadi atakapokuwa amemaliza na kutoka nje. 18Kisha atatoka na kwenda kwenye madhabahu iliyo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuifanyia ibada ya upatanisho. Atachukua kiasi cha damu ya yule fahali na ya yule mbuzi na kuzipaka pembe za madhabahu pande zote. 19Atainyunyizia madhabahu hiyo damu kwa kidole chake mara saba na hivyo kuiweka wakfu na kuitakasa unajisi wote wa watu wa Israeli.
20“Baada ya Aroni kumaliza kupatakasa mahali patakatifu, hema la mkutano na madhabahu, ndipo atamtoa yule beberu kwa ajili ya Azazeli,#16:20 Azazeli: Taz Lawi 16:8. akiwa hai. 21Aroni ataweka mikono yake juu ya kichwa cha huyo beberu hai na kuuungama juu yake dhambi zote za watu wa Israeli, makosa yao yote na dhambi zao zote, ili kumwajibisha huyo. Kisha atamwacha huyo beberu aende jangwani akipelekwa huko na mtu yeyote anayejitoa kwa hiari. 22Atamwacha huyo beberu aende jangwani, mahali pasipokuwa na watu, akiwa ameyachukua maovu yao yote.
23 # Taz Eze 44:19 “Kisha Aroni atarudi ndani ya hema la mkutano, atavua yale mavazi aliyovaa alipoingia mahali patakatifu sana na kuyaacha humo. 24Ataoga humo ndani katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake. Atatoka na kutoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka ya kuteketezwa ya watu wa Israeli, ili kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote. 25Mafuta ya sadaka ya kuondoa dhambi atayateketeza juu ya madhabahu. 26Yule mtu aliyempeleka yule beberu kwa Azazeli kwanza atayafua mavazi yake na kuoga ndipo atakapoweza kuingia kambini. 27#Taz Ebr 13:11 Yule fahali na mbuzi waliotolewa sadaka ya kuondoa dhambi ambao damu yao ilipelekwa mahali patakatifu sana ili kufanya ibada ya upatanisho, watapelekwa nje ya kambi na kuteketezwa. Ngozi zao, nyama na mavi yao, vyote vitateketezwa. 28Yule mtu atakayewateketeza atayafua mavazi yake na kuoga, ndipo atakapoweza kuingia kambini.
29 # Taz Lawi 23:26-32; Hes 29:7-11 “Hili ni sharti ambalo mnapaswa kulifuata milele: Siku ya kumi ya mwezi wa saba, nyinyi wenyewe na hata wageni wanaoishi miongoni mwenu, ni lazima mfunge siku hiyo na kuacha kufanya kazi. 30Mtafanya hivyo kwa sababu siku hiyo ndiyo siku ambayo mtafanyiwa ibada ya upatanisho, msafishwe dhambi zenu, nanyi mtakuwa safi mbele ya Mwenyezi-Mungu. 31Siku hiyo ni siku ya mapumziko kamili nanyi mtafunga. Kanuni hiyo ni ya kudumu milele. 32Kuhani aliyepakwa mafuta na kuwekwa wakfu ashike nafasi ya baba yake, ndiye atakayefanya ibada ya upatanisho akiwa amevaa mavazi matakatifu ya kitani. 33Atafanya ibada ya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu sana, kwa ajili ya hema la mkutano, madhabahu, makuhani na kwa ajili ya jumuiya nzima ya Israeli. 34Hili, basi ni sharti la kudumu milele; ni lazima mlifuate ili kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili ya watu wa Israeli mara moja kila mwaka na kusamehewa dhambi zao.” Mose akafanya yote kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.

Mambo Ya Walawi16;1-34


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 15 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..15...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Ni siku nyingine tena Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu,Muumba wa Vyote,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..Yahweh..!Elohim..!El Shaddai,El Olam..!Jehova Nissi..!Jehovah Jireh..!Jehovah Rapha..!Jehovah Roi..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shalom..!
Muweza wa yote,Hakuna kama wewe Baba..!!
Asante Mungu wetu kwa wema na Fadhili zako..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote...
Asante kwa kutuamsha tena na kutuchagu,Umetupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Tunakushuru Mungu wetu  katika yote wewe ni wakuabudiwa Daima..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Jehovah..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizoziwaza,tulizonena,tulizotenda,tunazozijua/tusizozijua..

Mungu wetu tunaomba nasi ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale walio tukosea..
Ukatuepushe na majaribu yote Mungu wetu,Ukatuokoe na yule mwovu na kazi zake zote,Ukatutakase Miili yetu na Akili zetu na ukatufunike na Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tupate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..
Baba wa Mbinguni ukatamalaki na kutuatamia  katika nyumba zetu/maisha yetu, Ndoa zetu Baba wa Mbinguni tunaziweka mikononi mwako,Ukatuongoze vyema na kila mmoja akajue wajibu wake,Wanawake ukatupe neema ya Kutii na Wanaume ukawaongoze katika mapenzi yao kwetu,Ukatuepushe na mifarakano isiyo na faida,ukatupe kutambua Amri na Sheria zako..

Ukawafunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo na ukawalinde na kuwaokoa watoto wetu na hatari zote,ukawaongoze vyema na hatua zao ziwe nawe Baba wa Mbinguni,kwenye masomo yao Baba ukawape ufahamu,Uelewa na kumbukumbu kwa yote waliyofundishwa,kwenye michezo na maisha yao yapo juu yako Mungu wetu..
Ukatupe Hekima,Busara katika malezi yetu,ukatuongoze Mungu wetu na tukawe wazazi/walezi wema na wenye kuwafundisha yaliyo yako.



Maisha ya kale na maisha mapya

Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao. Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana. Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa. Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana. Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu. Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana! Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.
Tunakushukuru ee Mungu wetu na tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana Wapendwa kwakunitembela/kunisoma..
Mungu akawaongoze katika yote..
Nawapenda.

Vitu najisi vya mwili

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose na Aroni, 2“Waambieni Waisraeli hivi: Mwanamume yeyote akitokwa na usaha, usaha huo wamfanya kuwa najisi. 3Na ufuatao ni mwongozo kuhusu najisi hiyo: Muda wote anapotokwa na usaha au usaha unapokuwa umezuiwa ndani yake, mtu huyo ni najisi. 4Kitanda chochote atakacholalia au atakachokalia, kitakuwa najisi. 5Mtu yeyote atakayegusa kitanda chake mtu huyo ni lazima ayafue mavazi yake, na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. 6Mtu yeyote atakayekalia kitu chochote alichokalia huyo mtu mwenye kutokwa na usaha, ni lazima ayafue mavazi na kuoga; na atakuwa najisi hadi jioni. 7Mtu yeyote atakayemgusa mtu atokwaye na usaha, lazima afue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. 8Mtu yeyote akitemewa mate na mtu anayetokwa usaha ni lazima mtu huyo aliyetemewa mate ayafue mavazi yake, na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. 9Tandiko lolote la mnyama aliloketia mtu anayetokwa na usaha litakuwa najisi. 10Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote alichokalia mtu huyo, atakuwa najisi mpaka jioni. Mtu yeyote anayebeba kitu chochote kilichokuwa cha mtu huyo ni lazima ayafue mavazi yake, na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. 11Mtu yeyote anayetokwa na usaha akimgusa mtu bila kusafisha kwanza mikono yake na kuoga, aliyeguswa atakuwa najisi mpaka jioni. 12Chombo chochote cha udongo kilichoguswa na mtu anayetokwa na usaha ni lazima kivunjwe. Lakini chombo chochote cha mbao ni lazima kisafishwe kwa maji.
13“Mwanamume yeyote anayetokwa na usaha akiponywa ugonjwa wake, ni lazima huyo mtu angoje siku saba kabla ya kuondolewa unajisi wake. Atayafua mavazi yake na kuoga kwa maji ya mtoni; naye atakuwa safi. 14Siku ya nane, ni lazima alete hua wawili au makinda mawili ya njiwa mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano na kumkabidhi kuhani. 15Kuhani atawatoa hao, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumwondolea unajisi wake wa kutokwa na usaha.
16“Kama mwanamume yeyote akitokwa na shahawa yake, ni lazima aoge mwili mzima kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. 17Vazi lolote lililodondokewa shahawa au ngozi yoyote iliyoguswa na shahawa hiyo ni lazima ioshwe kwa maji, na itakuwa najisi mpaka jioni. 18Kama mwanamume akilala na mwanamke, akatokwa na shahawa, basi, ni lazima wote wawili waoge kwa maji, nao watakuwa najisi mpaka jioni.
19“Mwanamke yeyote anapokuwa mwezini, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba. Mtu yeyote atakayemgusa mwanamke huyo atakuwa najisi mpaka jioni. 20Kitu chochote anacholalia au kukalia wakati yu najisi, kitakuwa najisi. 21Mtu yeyote atakayegusa kitanda cha huyo mwanamke ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji; naye atakuwa najisi mpaka jioni. 22Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. 23Mwanamume yeyote atakayegusa kitu chochote alicholalia au kukalia huyo mwanamke, atakuwa najisi mpaka jioni. 24Kama mwanamume akilala na mwanamke huyo na damu ya huyo mwanamke ikamdondokea huyo mwanamume, basi, mwanamume huyo atakuwa najisi kwa muda wa siku saba. Kitanda chochote atakacholalia huyo mwanamume kitakuwa najisi.
25“Kama mwanamke anatokwa na damu kwa muda wa siku nyingi kuliko ilivyo kawaida au anatokwa damu wakati usio wa majira yake ya kutokwa damu, basi, ataendelea kuwa najisi muda wote damu inapomtoka. 26Kitanda chochote anacholalia wakati huo au kiti chochote anachokalia, kitakuwa najisi sawa kama wakati wa unajisi wake wa kutokwa damu. 27Mtu yeyote atakayegusa vitu hivyo, atakuwa najisi na ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. 28Baada ya kukauka damu yake mwanamke huyo atangoja hadi siku saba ili kuwa safi; na baada ya muda huo atakuwa safi. 29Siku ya nane atachukua hua wawili au makinda mawili ya njiwa na kumletea kuhani mlangoni mwa hema la mkutano. 30Kuhani atamtoa mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Hivyo kuhani atamfanyia huyo mwanamke ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumwondolea unajisi wake wa kutokwa damu.
31“Ndivyo mtakavyowatahadharisha Waisraeli na unajisi wao, wasije wakaikufuru maskani yangu takatifu iliyo miongoni mwao wakiingia humo na unajisi wao; wakifanya hivyo watauawa.”
32Hiyo ndiyo sheria kuhusu mwanamume anayetokwa na usaha na anayetokwa na shahawa na kuwa najisi. 33Sheria hiyo yamhusu pia mwanamke anayetokwa damu na kuwa najisi. Sheria hiyo yamhusu mwanamume au mwanamke yeyote anayetokwa na chochote na pia yahusu mwanamume anayelala na mwanamke ambaye ni najisi.

Mambo Ya Walawi15;1-33


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 14 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..14...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo ni mali yako,Hata sisi ni mali yako Baba,Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo..
Asante kwa wema na fadhili zako Mungu wetu..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote Yahweh..!
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Mngu wetu..
Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Muumba wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..

Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Baba wa Mbinguni utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti .
Yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukapate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako tunaomba utubariki na kubariki kazi zetu,Biashara,Masomo,tuingiapo/tutokapo,vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri na tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahaweh..
Ukabariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Tazama wenye shida/tabu, wanapoitia magumu/majaribu mbalimbali,waliokatika vifungo mbalimbali Mungu wetu ukawaguse na mkono wako wenye nguvu ukawaponye na kuwaokoa katika mapito yao..


Wapendwa/Waungwana; Mungu akatupe Kibali Leo na wakati mwingine cha kuwaombea Ndugu/jamaa zetu na watu wengine..

Jehovah tunaweka nyumba zetu,familia,ndugu,jamaa na wote wanaotufahamu kwa namna moja au nyingine na wote wanaosoma hapa..

Baba wa Mbingu tunaomba ukatulinde na kutuokoa,ukatuponye kiroho na ukatupe amani ya moyo, ukatujenge kiroho/kiimani,tukaijue kweli yako na kukufuata wewe Mungu na kufuata sheria zako,Agano lako na Amri zako..Ukatufadhili ee Mungu wetu na kutuhurumia,Ukatusamehe na ukatuepushe na Hasira,Chuki,Wivu,Tamaa,Masimango,Kujisifu/kujikweza, kisasi na yote yasiyo kupendeza wewe..
Ee Mungu wetu ukatuinue na kutusimamisha, tazama ndugu zetu walio asi Mungu wakurudie pasipo na aibu wakapate Nuru na Mwanga kwenye maisha yao...

Lifuatalo ni simulizi la Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa, nilipokuwa katika mji mkuu wa Susa, katika mwezi wa Kislevu wa mwaka wa ishirini, Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akaja pamoja na baadhi ya watu toka nchini Yuda. Nikawauliza kuhusu Wayahudi wenzetu waliosalimika, yaani ambao hawakuhamishiwa Babuloni na kuhusu mji wa Yerusalemu. Wao wakaniambia, “Wayahudi waliosalimika na kubaki katika mkoa ule, wako katika taabu na aibu. Ukuta wa mji wa Yerusalemu umebomolewa na malango yake yameteketea.” Niliposikia hayo nilikaa chini na kulia, nikaomboleza kwa siku kadhaa. Nikafunga na kumwomba Mungu wa mbinguni, nikisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa mbinguni, wewe u Mungu aliye mkuu na wa kutisha, unalishika agano lako na unawafadhili wale wakupendao na kuzishika amri zako. Yasikilize kwa makini maombi yangu, na uniangalie mimi mtumishi wako, ninapokuomba kwa ajili ya watumishi wako, watu wa Israeli, usiku na mchana. Ninaungama dhambi za watu wa Israeli, tulizofanya mbele yako. Mimi pamoja na watu wa jamaa yangu tumefanya dhambi. Tumetenda mabaya mbele yako, hatujazishika amri zako, kanuni na maagizo yako uliyomwagiza mtumishi wako Mose. Kumbuka sasa lile ulilomwambia mtumishi wako Mose, uliposema, ‘Kama hamtakuwa waaminifu, nitawatawanya miongoni mwa mataifa. Lakini mkinirudia, mkazishika amri zangu na kuzifuata hata ingawa nitakuwa nimewatawanya mbali kabisa, nitawarudisha mahali nilipochagua kuwa mahali pangu pa kuabudiwa.’ Watu wa Israeli ni watumishi wako na watu wako uliwakomboa kwa uwezo wako na mkono wako wenye nguvu. Ee Bwana, yasikie maombi yangu mimi mtumishi wako na ya watumishi wako wanaofurahia kukutii wewe. Nakuomba unifanikishe leo, mimi mtumishi wako, na kunijalia kuhurumiwa na mfalme.” Basi, mimi nilikuwa na jukumu la kumpa mfalme kinywaji.
Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu na ukatupe sawasawa na mapenzi yako
ee Mungu wetu na ukasikie kulia kwetu na kupokea maombi/sala zetu..
Asante Mungu wetu na tunayaweka haya yote mikononi mwako...
Tunakushukuru na kukusifu Daima..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana kwakunisoma/kutembelea hapa..
Mbarikiwe na Ninawapenda.



Utakaso baada ya kuugua magonjwa ya ngozi

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Ifuatayo ni sheria kumhusu mwenye ukoma katika siku ya kutakaswa kwake. Baada ya kupona ataletwa kwa kuhani. 3Kuhani atakwenda kumwangalia huyo mtu nje ya kambi. Ikiwa ukoma huo umepona, 4basi, kuhani ataamuru watu walete ndege wawili safi walio hai, kipande cha mwerezi, sufu ya rangi nyekundu na tawi la husopo kwa ajili ya huyo mtu atakayetakaswa. 5Kuhani atawaamuru wamchinje ndege mmoja katika chungu chenye maji safi ya chemchemi. 6Kuhani atamchukua yule ndege mwingine hai, kipande kile cha mwerezi, sufu ya rangi nyekundu na lile tawi la husopo na kuvitumbukiza vyote katika damu ya yule ndege aliyechinjwa. 7Kisha, atamnyunyizia huyo mwenye kutakaswa ile damu mara saba, halafu atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Yule ndege hai atamwacha aende zake mashambani nje ya mji. 8Huyo mtu atayafua mavazi yake, atanyoa nywele zake, na kuoga; naye atakuwa safi. Baada ya hayo atarudi kambini, lakini atakaa nje ya hema lake kwa muda wa siku saba. 9Siku ya saba atanyoa nywele zake zote, ndevu na kope za macho yake. Kisha atafua mavazi yake na kuoga, ataoga kwa maji; naye atakuwa safi.
10“Siku ya nane ataleta wanakondoo madume wawili wasio na dosari, kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na dosari, kilo tatu za unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka pamoja na mafuta theluthi moja ya lita. 11Kuhani atakayemtakasa mtu huyo atamleta mbele ya Mwenyezi-Mungu karibu na mlango wa hema la mkutano pamoja na vitu alivyoleta. 12Kuhani atachukua mwanakondoo dume mmoja na kumtolea sadaka ya kuondoa hatia pamoja na yale mafuta theluthi moja ya lita. Atafanya ishara ya kuvitolea mbele ya Mwenyezi-Mungu. 13Kisha atamchinja huyo mwanakondoo katika mahali patakatifu, wanapochinjia wanyama wa sadaka ya kuondoa dhambi na sadaka ya kuteketezwa. Sadaka hii ya kuondoa hatia, kama ilivyo sadaka ya kuondoa dhambi, ni mali yake kuhani; ni sadaka takatifu kabisa. 14Kuhani atachukua kiasi cha damu ya sadaka ya kuondoa hatia na kumpaka mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia na kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia. 15Kisha, kuhani atachukua kiasi cha ile theluthi moja ya mafuta na kuyatia katika kiganja cha mkono wake wa kushoto. 16Atachovya kidole cha mkono wake wa kulia katika mafuta hayo na kumnyunyizia huyo mtu anayetakaswa mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu. 17Kiasi cha mafuta yanayobaki katika kiganja chake atampaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia na kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia. 18Yale mafuta yaliyobaki atampaka huyo mtu kichwani. Hivyo kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu. 19Kuhani atatolea sadaka ya kuondoa dhambi na kumfanyia huyo mtu anayetakaswa ibada ya upatanisho ili kumwondolea unajisi wake. Kisha atamchinja mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa. 20Kuhani atatolea ile sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka juu ya madhabahu. Hivyo kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho, naye atakuwa safi.
21“Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini, hana uwezo wa kutoa vitu hivyo, basi ataleta mwanakondoo dume mmoja kuwa fidia ya sadaka ya kuondoa hatia ambaye atafanyiwa ishara ya kutoa sadaka ili kumfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho. Ataleta pia kilo moja ya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka na mafuta theluthi moja ya lita. 22Ataleta pia hua wawili au makinda mawili ya njiwa kadiri anavyoweza mmoja atakuwa kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. 23Siku ya nane atamletea kuhani vitu hivyo mbele ya mlango wa hema la mkutano kwa ajili ya utakaso wake mbele ya Mwenyezi-Mungu. 24Kuhani atamchukua huyo mwanakondoo dume wa sadaka ya kuondoa hatia pamoja na yale mafuta theluthi moja ya lita na kufanya ishara ya kuvitolea mbele ya Mwenyezi-Mungu. 25Atamchinja huyo mwanakondoo dume wa sadaka ya kuondoa hatia. Kuhani atachukua kiasi cha damu na kumpaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia, katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia. 26Kuhani atatia kiasi cha mafuta hayo katika kiganja cha mkono wake wa kushoto. 27Kisha atamnyunyizia huyo mtu kwa kidole chake cha kulia kiasi cha hayo mafuta yaliyomo katika kiganja chake cha kushoto mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu. 28Kuhani atampaka huyo mtu anayetakaswa mafuta katika ncha ya sikio lake la kulia, katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia, na kidole gumba cha mguu wake wa kulia. Atampaka mahali pale ambapo alimpaka ile damu ya sadaka ya kuondoa hatia. 29Mafuta yanayosalia mkononi mwake atampaka huyo mtu kichwani, ili kumfanyia ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu. 30Kisha kuhani atamchukua mmoja wa wale hua au njiwa wawili kadiri mtu huyo anavyoweza kuleta. 31Hua atakuwa kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Pamoja na hao, atatoa sadaka ya nafaka; naye kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu. 32Huo ndio mwongozo kuhusu mtu mwenye ukoma asiyeweza kutoa sadaka za kumtakasa.”

Upele katika nyumba

33Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose na Aroni, 34“Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani ambayo ninawapa kuwa milki yenu, nami nikafanya namna ya upele wa ukoma uote katika ukuta wa nyumba fulani katika nchi mtakayoimiliki, 35basi, mwenye nyumba hiyo ni lazima amwambie kuhani kwamba namna ya upele wa ukoma umeonekana katika nyumba yake. 36Kuhani ataamuru vitu vyote ndani ya nyumba hiyo vitolewe kabla yeye mwenyewe hajaanza uchunguzi wake; visije vyote kutangazwa kuwa najisi. Kisha kuhani ataingia kuiangalia nyumba hiyo. 37Atauchunguza upele huo; kama upele huo umeonekana ukutani na umesababisha madoa ya rangi ya kijani kibichi au nyekundu na kuonekana kuwa yamepenya ndani ya kuta, 38basi, kuhani atatoka nje mlangoni na kuifunga nyumba hiyo kwa muda wa siku saba. 39Siku ya saba kuhani atarudi na kuiangalia tena nyumba hiyo. Ikiwa upele huo umeenea katika kuta za nyumba hiyo, 40kuhani ataamuru mawe yaliyoko kwenye sehemu zenye upele yatolewe na kutupwa mahali najisi nje ya mji. 41Lipu ya nyumba hiyo itabanduliwa na kifusi chake kutupwa mahali najisi nje ya mji. 42Kisha watachukua mawe mapya na kujenga mahali walipobomoa; nao wataipiga nyumba hiyo lipu upya.
43“Ikiwa upele huo utatokea tena baada ya kutoa mawe hayo na kukwangua lipu na kuipiga lipu upya, 44yapasa kuhani aje kuichunguza. Ikiwa upele umeenea katika nyumba hiyo, basi huo ni upele wa kufisha; nyumba hiyo ni najisi. 45Nyumba hiyo ni lazima ibomolewe na mawe yake, miti yake na lipu vipelekwe mahali najisi nje ya mji. 46Zaidi ya hayo, yeyote atakayeingia ndani ya nyumba hiyo wakati itakapokuwa imefungwa, atakuwa najisi mpaka jioni. 47Yeyote anayelala katika nyumba hiyo au kulia chakula ndani yake, lazima ayafue mavazi yake.
48“Lakini ikiwa baada ya kuikagua nyumba hiyo, kuhani ataona kuwa upele haujaenea baada ya kupigwa lipu, basi, kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi kwani upele umekwisha. 49Ili kuitakasa nyumba hiyo, mwenye nyumba ataleta ndege wawili pamoja na kipande cha mwerezi, sufu nyekundu na tawi la husopo. 50Atamchinja ndege mmoja katika chungu chenye maji safi ya chemchemi. 51Atachukua kipande cha mwerezi, tawi la husopo na ile sufu nyekundu pamoja na yule ndege mwingine aliye hai na kuvitumbukiza vyote katika damu ya yule ndege aliyechinjwa. Kisha atainyunyizia nyumba hiyo damu mara saba. 52Hivyo ndivyo atakavyoitakasa nyumba hiyo kwa damu ya ndege, maji safi ya chemchemi, ndege hai, kipande cha mwerezi, tawi la husopo na ile sufu nyekundu. 53Yule ndege hai atamwacha aende zake mashambani nje ya mji. Hivyo ndivyo atakavyoitakasa nyumba hiyo, nayo itakuwa safi.”
54Hii ndiyo sheria kuhusu aina yoyote ya namna ya upele wa ukoma; 55upele katika nguo au nyumba, 56uvimbe, jipu au kipaku, 57ili kuonesha ni kitu gani kilicho najisi na kisicho najisi. Hiyo ndiyo sheria kuhusu namna ya upele wa ukoma.

Mambo Ya Walawi14;1-57


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.