Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 7 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..4


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu kwa mema yote aliyotutendea/anayoendelea kutenda..

Mtakatifu Baba wa Mbinguni..Tunakushukuru  kwa ulinzi wako
wakati wote..
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha,tukijiachilia mikononi mwako Jehovah..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu Mungu wetu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazreti..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukapate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..
Tunakwenda kinyume na nguvu zote za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu na nguvu za mpinga Kristo katika Jina lipitalo majina yote jina Bwana wetu Yesu Kristo..

“Kama mtu yeyote anawaendea waaguzi wa mizimu na wachawi na hivyo kukosa uaminifu kwangu, nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake. Kwa hiyo, jiwekeni wakfu muwe watakatifu; kwani mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Shikeni masharti yangu na kuyatekeleza. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewatakasa.

31 #Taz Kumb 18:11; 1Sam 28:3; 2Fal 23:4; Isa 8:19 “Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.[walawi19;31]

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako..
Tunaomba utubariki na kubariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda..
Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mfalme wa Amani nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe sawasawa na mapenzi yeko..
Tukawe Barua njema na tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..

Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! Upole wenu ujulikane kwa watu wote. Bwana yu karibu. Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.


Asante Baba wa Mbinguni..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Tunashukuru na kukusifu daima..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami..
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.


Wajibu waliopewa Wakohathi

1Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose na Aroni, 2“Wahesabu watu wa ukoo wa Kohathi, mmoja wa koo za Lawi, kufuatana na jamaa zao na koo zao; 3utawaorodhesha wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano. 4Hii ndio itakayokuwa huduma ya wana wa Kohathi, kuhusu vitu vitakatifu kabisa.
5“Wakati wa kuvunja kambi, Aroni na wanawe wataingia katika hema, na kulishusha pazia lililoko mbele ya sanduku la agano, kisha walifunike kwa pazia hilo. 6Juu yake wataweka kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi, kisha watatandaza kitambaa cha rangi ya buluu safi. Halafu wataingiza mipiko ya kulichukulia sanduku hilo.
7“Juu ya meza ya kutolea mikate inayowekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu watatandaza kitambaa cha buluu ambacho juu yake wataweka sahani, visahani vya ubani, bakuli na bilauri, kwa ajili ya kutolea tambiko za kinywaji. Daima kutakuwa na mkate juu ya meza. 8Kisha, watavifunika vyombo hivi vyote kwa kitambaa chekundu, na juu yake wataweka kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi. Halafu wataingiza mipiko yake ya kulibeba.
9“Watachukua kitambaa cha buluu ambacho watafunikia kinara cha taa na taa zake, makasi zake, sinia zake na vyombo vyote vinavyotumiwa kukiwekea mafuta. 10Watakiweka pamoja na vyombo vyake vyote ndani ya ngozi laini ya mbuzi na kukiweka juu ya mipiko ya kuchukulia.
11“Halafu watatandaza kitambaa cha buluu juu ya madhabahu ya dhahabu na kuifunika kwa ngozi laini ya mbuzi juu yake. Halafu wataingiza mipiko yake ya kuichukulia. 12Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika mahali patakatifu, watavifunga kwa kitambaa cha buluu na kuvifunika kwa ngozi laini ya mbuzi, kisha wataviweka juu ya mipiko yake ya kuchukulia. 13Watayaondoa majivu kutoka madhabahuni na juu yake watatandaza kitambaa cha zambarau. 14Juu yake wataviweka vyombo vyote vitumikavyo katika ibada kwenye madhabahu: Vyetezo, nyuma, miiko na mabakuli. Kisha, juu yake watatandaza kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi na kuiingiza mipiko yake ya kulibebea. 15Baada ya Aroni na wanawe kupafunika mahali patakatifu pamoja na vyombo na vifaa vyake vyote, wakiwa tayari kuanza safari, watu wa ukoo wa Kohathi watakuja na kuvibeba. Lakini wao, hawaruhusiwi kabisa kuvigusa vyombo hivyo vitakatifu, wasije wakafa. Hiyo ndiyo kazi ya ukoo wa Kohathi kila wakati hema la mkutano linapohamishwa. 16Eleazari mwana wa kuhani Aroni itampasa kuyatunza mafuta ya taa, ubani wa kunukia, tambiko za nafaka za kila siku, mafuta ya kupaka ili kuweka wakfu na kila kitu kilichowekwa wakfu katika hema hilo.”
17Kisha Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose na Aroni, 18“Msiache ukoo wa familia za Kohathi miongoni mwa Walawi uangamizwe. 19Basi, ili kuwaepusha wasije wakauawa kwa kuvikaribia vyombo hivyo vitakatifu sana utafanya hivi: Aroni na wanawe wataingia na kumpangia kila mmoja wao wajibu wake na kazi yake. 20Lakini wazawa wa Kohathi hawataingia kamwe kuvitazama vitu hivyo vitakatifu sana; wakifanya hivyo watakufa.”

Huduma za Walawi wa ukoo wa Gershoni

21Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 22“Wahesabu watu wa ukoo wa Gershoni, kufuatana na familia na koo zao; 23utawahesabu wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano. 24Wajibu wao utakuwa huu: Watabeba mapazia ya hema takatifu na hema la mkutano pamoja na 25kifuniko chake, kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi kilicho juu yake, pazia la lango, 26mapazia na kamba za ua ulio kandokando ya hema na madhabahu, mapazia ya lango la kitalu, na vifaa vyote vinavyotumika pamoja na vitu hivi. Wao watashughulika na mambo yote yanayohusika na vitu hivi. 27Aroni na wanawe makuhani ndio watakaoamrisha huduma zote za Wagershoni kuhusu vitu watakavyobeba na kazi watakazofanya. Utawapangia vitu vyote vile ambavyo wanapaswa kubeba. 28Hii ndiyo huduma ya jamaa za Gershoni kwenye hema la mkutano; watafanya kazi chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa kuhani Aroni.

Huduma za Walawi na ukoo wa Merari

29“Kadhalika, utawahesabu wana wa Merari, kufuatana na jamaa zao na koo zao. 30Utawahesabu wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano. 31Wao, watakuwa na wajibu na kubeba mbao, mataruma, nguzo na misingi ya hema la mkutano. 32Kadhalika na nguzo za ua za kuzunguka pande zote, vikalio, vigingi na kamba pamoja na vifaa vyake vyote na vyombo vyake vingine vyote. Nawe utawapangia kufuata majina yao vitu watakavyopaswa kubeba. 33Hii ndiyo itakayokuwa kazi ya wana wa ukoo wa Merari katika huduma yao yote ndani ya hema la mkutano, chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa kuhani Aroni.”

Sensa ya Walawi

34Basi, Mose, Aroni na viongozi wa jumuiya yote wakafanya sensa ya watu wa ukoo wa Kohathi, kufuatana na familia zao, 35wakawaorodhesha watu wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, kila aliyefaa kuingia katika huduma ya hema la mkutano. 36Idadi yao kufuatana na jamaa zao ilikuwa watu 2,750. 37Hii ndiyo idadi ya watu wa jamaa ya Kohathi, ambao walihudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
38Idadi ya watu wa ukoo wa Gershoni kufuatana na familia zao, 39wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, waliofaa kuhudumu katika hema la mkutano, 40ilikuwa watu 2,630. 41Hii ndiyo iliyokuwa idadi ya watu wa familia za wana wa Gershoni wote waliohudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza. 42Idadi ya watu wa ukoo wa Merari kufuatana na jamaa zao na familia zao, 43wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, waliofaa kuhudumu katika hema la mkutano, 44ilikuwa watu 3,200. 45Hii ndiyo idadi ya watu wa ukoo wa Merari ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza Mose.
46Hivyo, Walawi wote walioandikishwa na Mose, Aroni na viongozi wa watu, kwa kufuata jamaa zao na koo zao, 47wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, na ambao walifaa kwa huduma na uchukuzi katika hema la mkutano, 48jumla walikuwa watu 8,580. 49Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Hesabu4;1-49


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 6 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..3



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu Baba yetu..Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwakutulinda wakati wote na kutuamsha salama tukiwa wenye afya..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah..!Tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe na majaribu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote
Ututakase kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Baba utuhurumie na kutuweka huru..utupe neema ya kufuata na kusimamia neno lako...


Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa. Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote. Nasema tena wazi: Kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika sheria yote. Kama mnatazamia kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu. Kwa upande wetu, lakini, sisi tunangojea kwa matumaini kwa nguvu ya Roho tufanywe waadilifu kwa njia ya imani. Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo. Mwenendo wenu ulikuwa mzuri! Nani, basi, aliyewazuia kuuzingatia ukweli? Aliyesababisha hali hiyo si Mungu ambaye amewaiteni. “Chachu kidogo tu huchachusha donge lote la unga!” Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba nyinyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni – awe nani au nani – hakika ataadhibiwa. Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote. Laiti hao wanaowavurugeni wangejihasi wenyewe! Nyinyi ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo. Maana sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe!
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Basi, nasema hivi: Mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia. Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka nyinyi wenyewe. Kama mkiongozwa na Roho, basi, hamko tena chini ya sheria.
[Wagalatia 5:16-18]



Baba wa mbinguni tuyaweka maisha yetu mikononi mwako..
Tunaomba utubariki na kubariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda..
Jehovah..!tukafanye kama itakavyokupendeza wewe..
Tukawe barua njema na tukasomeke sawasawa na mapenzi yako..

Yahweh..tazama wenye shida/tabu,wagonjwa,waliokata tamaa,waliokataliwa,waliokatika vifungo mbalimbali,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali..Baba ukawaguse na kuwaongoza
ukawape neema ya kujua kweli yako,wakapate kufuata Amri na sheria zako..wajue jinsi wewe ulivyo na ukawaponye kimwili na kiroho pia..
wafiwa ukawafariji na kuwapa nguvu na uvumilivu..
Mungu wetu ukaonekane kwenye maisha ya wanao wanao kulilia ukawafute machozi,wanaokuomba ukawajibu Mungu wetu..
wanaokutafuta kwa bidii ukapatikane..wape macho ya rohoni na wape masikio ya kusikia na ukawape ufahamu wa kujitambua na kufuata Neno lako..



19Mwenyezi-Mungu asifiwe siku kwa siku!
Yeye hutubebea mizigo yetu;
yeye ndiye Mungu wa wokovu wetu.
20Mungu wetu ni Mungu mwenye kutuokoa;
Bwana Mungu pekee ndiye aokoaye katika kifo.
[Zaburi 68:19-20]

Asante Mungu wetu..Sifa na utukufu tunakurudishia wewe..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Mbarikiwe sana wapendwa..
Asanteni kwakuwa nami..
Nawapenda.

Wana wa Aroni

1Wafuatao ndio wazawa wa Aroni na Mose wakati Mwenyezi-Mungu alipozungumza na Mose mlimani Sinai. 2#Taz Hes 26:60 Haya ndiyo majina ya wana wa Aroni: Nadabu, mzaliwa wake wa kwanza, Abihu, Eleazari na Ithamari. 3Hawa waliwekwa wakfu kwa kupakwa mafuta wawe makuhani. 4#Taz Lawi 10:1-2; Hes 26:61 Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakati walipomtolea Mwenyezi-Mungu moto usio mtakatifu katika jangwa la Sinai. Wao hawakuwa na watoto kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakawa wanahudumu kama makuhani wakati wa uhai wa Aroni baba yao.

Walawi wanateuliwa kuwahudumia makuhani

5Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 6“Walete karibu watu wa kabila la Lawi, uwaweke mbele ya kuhani Aroni ili uwape jukumu la kumtumikia. 7Watafanya kazi kwa niaba yake na ya jumuiya yote kwenye hema la mkutano wanapohudumu mahali patakatifu, 8wataangalia na kutunza vyombo vyote vya hema la mkutano na kuwasaidia Waisraeli wanapotoa huduma zao kwenye mahali patakatifu. 9Walawi utampa Aroni na wazawa wake makuhani; hao wametolewa kati ya Waisraeli wawahudumie kabisa. 10#Taz Hes 1:51 Utawateua Aroni na wanawe ili waweze kutekeleza huduma zao za ukuhani; lakini kama mtu yeyote mwingine atakaribia, atauawa.”
11Mwenyezi-Mungu akaendelea kumwambia Mose, 12“Angalia, sasa nimewateua Walawi miongoni mwa Waisraeli wote, badala ya kila mzaliwa wa kwanza wa kiume kifunguamimba katika kila familia ya Israeli. Walawi ni wangu, 13#Taz Kut 13:2 kwani kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli ni wangu. Wakati nilipowaua wazaliwa wa kwanza wote wa Wamisri nilijiwekea wakfu kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli; kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu hata wa mnyama; wao watakuwa wangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”

Sensa ya Walawi

14Baadaye Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose katika jangwa la Sinai, 15“Wahesabu wana wa Lawi wote kulingana na koo zao na familia zao, kila mwanamume kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi.” 16Basi, Mose akawahesabu kufuatana na neno la Mwenyezi-Mungu, kama alivyomwamuru.
17Wafuatao ndio waliokuwa wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari. 18Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni kwa kufuata familia zao: Libni na Shimei. 19Wana wa Kohathi kwa kufuata familia zao: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. 20Wana wa Merari kwa kufuata familia zao: Mahli na Mushi. Hizi zilikuwa jamaa za Walawi kulingana na koo zao.
21Familia za Walibni na Washimei zilitokana na Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wagershoni. 22Idadi yao kwa kadiri ya hesabu ya wanaume wote kuanzia waliokuwa na mwezi mmoja na zaidi ni 7,500. 23Familia za Wagershoni, iliwapasa kupiga kambi yao upande wa magharibi, nyuma ya hema takatifu 24naye Eliasafu mwana wa Laeli akiwa mkuu wa ukoo wa Wagershoni. 25Kazi ya wana wa Gershoni ilikuwa kulitunza hema takatifu, hema pamoja na kifuniko chake, pazia la mlango wa hema la mkutano, 26mapazia ya ua ulioko kati ya hema takatifu na madhabahu, na pazia la mlango wa ua, na kamba zake. Huduma zote zilizohusu vitu hivi zilikuwa zao.
27Familia za Waamrami, Waishari, Wahebroni na Wauzieli zilitokana na Kohathi; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wakohathi. 28Kadiri ya hesabu ya wanaume wote kuanzia wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ilikuwa 8,600, waliohusika na huduma za mahali patakatifu. 29Familia za wana wa Kohathi zilitakiwa kupiga kambi yao upande wa kusini wa mahali patakatifu, 30naye Elisafani, akiwa mkuu wa ukoo huo wa familia za Wakohathi. 31Wajibu wao ulikuwa kulitunza sanduku la agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, vyombo wanavyotumia makuhani mahali patakatifu na pazia; huduma zote zilizohusu vitu hivi zilikuwa zao.
32Naye Eleazari mwana wa kuhani Aroni aliwekwa kuwa mkuu wa wakuu wa Walawi, na msimamizi wa wahudumu wote wa mahali patakatifu.
33Familia za Wamahli na Wamushi zilitokana na Merari. 34Hizi ndizo familia za Merari. Idadi yao kadiri ya hesabu ya wanaume wote kuanzia wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ilikuwa watu 6,200. 35Mkuu wa ukoo wa familia za Merari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kupiga kambi yao upande wa kaskazini wa hema takatifu. 36Wao walipewa kazi ya kutunza mbao za hema takatifu, mataruma, nguzo, vitako na vifaa vyote vya kushikilia hema; huduma zote zilizohusu vitu hivi zilikuwa juu yao. 37Pia walihitajika kutunza nguzo za ua zilizouzunguka na vitako vyake, vigingi na kamba zake.
38Mose na Aroni na wana wao walitakiwa kupiga kambi yao mbele ya hema takatifu upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua. Wajibu wao ulikuwa kutoa huduma kwenye mahali patakatifu kwa lolote lililohitajika kufanyika kwa ajili ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyesogea karibu ilibidi auawe. 39Idadi ya Walawi kulingana na familia zao, wanaume wote kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi ambao Mose na Aroni waliwahesabu kwa amri ya Mwenyezi-Mungu, ilikuwa watu 22,000.

Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza

40Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Wahesabu kwa majina wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli kuanzia wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi. 41Nawe utatenga Walawi kwa ajili yangu mimi Mwenyezi-Mungu; pia utatenga kwa ajili yangu mifugo yote ya Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo ya watu wa Israeli.” 42Basi, Mose akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa watu wa Israeli kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru. 43Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume kadiri ya hesabu ya majina, kuanzia wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi, kufuata walivyohesabiwa, walikuwa 22,273.
44Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 45“Sasa, watenge Walawi wote kuwa wangu badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli. Kadhalika, watenge ng'ombe wa Walawi wote badala ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe wa Waisraeli. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. 46Kwa ajili ya fidia ya wazaliwa wa kwanza wa kiume wa watu wa Israeli 273, wanaozidi idadi ya wanaume Walawi, 47utapokea kwa kila mwanamume fedha shekeli tano, kulingana na kipimo cha mahali patakatifu, ambayo ni sawa na gera ishirini, 48na fedha hizo kwa ajili ya fidia ya hao waliozidi idadi yao utampa Aroni na wanawe.” 49Mose akatii, akachukua fedha hizo za fidia ya hao waliozidi idadi ya waliofidiwa na Walawi; 50alipokea kutoka wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli fedha kiasi cha shekeli 1,365, kulingana na kipimo cha mahali patakatifu, 51akawapa Aroni na wanawe fedha hizo za fidia sawa na neno la Mwenyezi-Mungu kama alivyomwamuru.

Hesabu3;1-51


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 5 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..2

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..! Baba wa Mbinguni,Mungu wetu na Baba yetu..Muumba wetu na Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Yahweh..!Jehovah..!El shaddai..!Elohim..!Muweza wa Yote..!
Asante kwa wema na fadhili zako Baba..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote na kutuamsha salama na wenye afya
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendele kuiona Leo hii..
Si kwa uwezo wetu wala nguvu zetu..si kwamba sisi ni wema sana..
Ni kwa Neema/rehema zako Mungu Baba na Mapenzi yako kwetu..
Si kwamba waliotangulia/ni wabaya mno au si wema Baba..
Imekupendeza wewe Mungu wetu ...!!

Basi, ndivyo ilivyo pia wakati huu wa sasa: Ipo idadi ya waliobaki ambao Mungu aliwateua kwa sababu ya neema yake. Uteuzi wake unatokana na neema yake, na si kwa sababu ya matendo yao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemea matendo ya watu, neema yake haingekuwa neema tena.
Tunakuja mbele zako Mungu Baba tukijinyenyekeza,tukijishusha na tukijiachilia mikononi mwako Jehovah..
 Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mungu wetu
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..Mungu Baba..
Tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damau ya Mwanao Mpendwa..
Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...


Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wa kuingia Mahali Patakatifu. Yeye ametufungulia njia mpya, njia ya uhai, kupitia lile pazia, yaani mwili wake mwenyewe. Basi, tunaye kuhani maarufu aliye na mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa kutokana na dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi. Tuzingatie kabisa tumaini letu tunalokiri, maana Mungu aliyefanya ahadi zake ni mwaminifu. Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema. Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, siku ile ya Bwana inakaribia. Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna tambiko iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi. Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga. Mtu yeyote asiyetii sheria ya Mose, huuawa bila huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu. Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani? Maana tunamfahamu yule aliyesema, “Mimi nitalipiza kisasi, mimi nitalipiza,” na ambaye alisema pia, “Bwana atawahukumu watu wake.” Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno! Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, nyinyi mlistahimili. Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo. Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyanganywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele. Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatia tuzo kubwa. Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili muweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi. Maana kama yasemavyo Maandiko: “Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia. Lakini mtu wangu aliye mwadilifu ataamini na kuishi; walakini akirudi nyuma, mimi sitapendezwa naye.” Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa.
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tupate kutambua/kujitambua
na tukawe na kiasi..
Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yake...

Mungu wetu tunayaweka maisha yetumikononi mwako..
Tunaomba utubariki na ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda..
Mungu wetu ukatuongoze tukatende kama itakavyokupendeza wewe..
Ukabariki kuingia kwetu/kutoka kwetu vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Mungu Baba ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu na ukatupe kulingana na mapenzi yako
Asante Mungu wetu tunarudisha sifa na utukufu ni wako..
tunayaweka haya yote mikononi mwako tukiamini na kushukuru...

Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni wapendwa/waungwana kwakuwa pamoja..
Mungu Baba akaonekane kwenye maisha yenu..
Mungu awabariki muingiapo/mtokapo..
Msipungukiwe katika mahitaji yenu kama ikatavyompendeza yeye..
Nawapenda.



Kupangwa kwa makabila

1Mwenyezi-Mungu aliwapa Mose na Aroni, maagizo yafuatayo: 2“Waisraeli watapiga kambi zao, kila mmoja akikaa mahali penye bendera yake, penye alama za ukoo wake. Watapiga kambi zao kulizunguka hema la mkutano.
3“Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua watakuwa kikundi cha watu walio chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu, 4kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 74600. 5Wale watakaofuata kupiga kambi baada ya watu wa Yuda watakuwa kabila la Isakari, kiongozi wao akiwa Nethaneli mwana wa Suari, 6kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 54,400. 7Kisha kabila la Zebuluni, kiongozi wao akiwa Eliabu mwana wa Heloni, 8kikosi chake kulingana na hesabu ni wanaume 57,400. 9Jumla yote ya watu watakaokuwa katika kambi ya Yuda kulingana na makundi yao ni watu 186,400. Hao ndio watakaotangulia kusafiri.
10“Kwa upande wa kusini, wale walio chini ya bendera ya kundi la Reubeni kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elisuri mwana wa Shedeuri, 11kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 46,500. 12Kisha wale watakaopiga kambi kando ya watu wa Reubeni watakuwa ni watu wa kabila la Simeoni, kiongozi wao akiwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai, 13kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 59,300. 14Hatimaye kabila la Gadi, kiongozi wao akiwa Eliasafu mwana wa Reueli, 15kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 45,650. 16Jumla ya wanaume watakaokuwa katika kambi ya Reubeni kulingana na makundi yao ni watu 151,450. Hawa ndio watakaokuwa katika msafara wa pili.
17“Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.
18“Kwa upande wa magharibi, wale walio chini ya bendera ya kundi la Efraimu watapiga kambi kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elishama mwana wa Amihudi, 19kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 32,200. 20Mara tu baada ya Waefraimu litafuata kabila la Manase: Kiongozi wake akiwa Gamalieli, mwana wa Pedasuri, 21kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa watu 32,000. 22Hatimaye kabila la Benyamini: Kiongozi wake ni Abidani, mwana wa Gideoni, 23kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 35,400. 24Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Efraimu kulingana na makundi yao ni watu 108,100. Kundi hili la Efraimu litakuwa katika msafara wa tatu.
25“Kwa upande wa kaskazini, watapiga kambi katika makundi yao wale walio chini ya bendera ya Dani, kiongozi wao atakuwa Ahiezeri, mwana wa Amishadai, 26kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 62,700. 27Kisha wale watakaopiga kambi baada yao watakuwa watu wa kabila la Asheri, kiongozi wao akiwa Pagieli mwana wa Okrani, 28kikosi chake kulingana na hesabu kitakuwa na watu 41,500.
29“Hatimaye watu wa kabila la Naftali, kiongozi wake akiwa Ahira mwana wa Enani, 30kikosi chake kulingana na hesabu, kitakuwa na watu 53,400. 31Jumla ya watu watakaokuwa katika kambi ya Dani kulingana na makundi yao ni watu 157,600. Kundi hili la Dani litakuwa katika msafara wa mwisho, bendera baada ya bendera.”
32Hao ndio Waisraeli waliohesabiwa kulingana na koo zao, katika kambi na vikosi vyao; wote walikuwa 603,550. 33Lakini Walawi hawakuhesabiwa miongoni mwa watu wa Israeli kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
34Hivyo ndivyo, Waisraeli walivyofanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Walipiga kambi zao, kufuata bendera zao na walisafiri kila mmoja akiandamana na jamaa yake kwa kufuata ukoo wake.

Hesabu2;1-34


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 4 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Leo tunaanza kitabu cha Hesabu..1



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu..
Asante Mungu wetu, Baba yetu kwa ulinzi wako na kutuamsha salama..
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu,Tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizoziwaza,tulizozinena,tulizozitenda,tunazozijua/tusizozijua..
Jehovah tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukoasea..
Utuepushe na majaribu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu..
Aliumizwa kwasababu ya maovu yetu...
Kwakuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai..
Kwakupigwa kwake sisi tumepona...!!!
Mwanadamu yupi anayeweza kujitoa kiasi hiki?
Nani anaweza kuvumilia haya yote kwa sababu wewe upate kupona/usamehewe dhambi?..

Si kwamba sisi tulikuwa tunampenda Mungu kwanza..
Bali kwamba yeye alitupenda hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kuondolea dhambi zetu..
Wapenzi wangu ikiwa Mungu alitupenda hivyo,basi nasi tunapaswa kupendana...[1Yohane 4:10-11]

Nani aliyeamini mambo tuliyosikia? Nani aliyetambua kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu ulihusika? Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu, mtumishi wake alikua kama mti mchanga, kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza, wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia. Alidharauliwa na kukataliwa na watu, alikuwa mtu wa uchungu na huzuni. Alikuwa kama mtu kinyaa kwa watu; alidharauliwa na tukamwona si kitu. Hata hivyo alivumilia majonzi yetu, na kubeba huzuni zetu. Sisi tulifikiri amepata adhabu, amepigwa na Mungu na kuteswa. Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu, aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu. Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai; kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote tumepotea kama kondoo, kila mmoja wetu ameelekea njia yake. Lakini Mwenyezi-Mungu alimtwika adhabu, ambayo sisi wenyewe tuliistahili. Alidhulumiwa na kuteswa, lakini alivumilia kwa unyenyekevu, bila kutoa sauti hata kidogo. Alikuwa kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni, kama kondoo akaavyo kimya anapokatwa manyoya. Hakutoa sauti hata kidogo. Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa; na hakuna mtu aliyejali yanayompata. Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai, kwa sababu ya makosa ya watu wangu. Walimzika pamoja na wahalifu; katika kifo aliwekwa pamoja na matajiri, ingawa hakutenda ukatili wowote, wala hakusema neno lolote la udanganyifu. Mwenyezi-Mungu alipenda kumwumiza na kumweka katika huzuni. Alijitoa mhanga kwa ajili ya kuondoa dhambi. Mtumishi wa Mungu atakuwa na wazawa; ataishi maisha marefu. Yeye ndiye atakayetimiza mpango wa Mwenyezi-Mungu. Mungu asema: “Baada ya kutaabika sana, mtumishi wangu atafurahi. Kwa kuwajibika kwake kikamilifu, atatosheka na matokeo hayo. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwadilifu atawafanya wengi wawe waadilifu Yeye atazibeba dhambi zao. Kwa hiyo, nitamweka katika cheo cha wakuu, atagawa nyara pamoja na wenye nguvu; kwa kuwa alijitolea mwenyewe kufa, akawekwa katika kundi moja na wakosefu, alizibeba dhambi za watu wengi, akawaombea msamaha hao wakosefu.”

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na Upendo wa kweli,Utuwema,Fadhili,Hekima,Busara,kuchukuliana,Upole na kiasi..

Jehovah..! tunakabidhi nyumba zetu,Ndoa na familia vyote mikononi mwako..
Ukatubariki na kubariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda na tukatende sawasawa na mapenzi yako...

Asante Mungu wetu kwa neema ya kusoma Neno lako..
Tumemaliza/tumepitia na kujifunza mengi katika kitabu cha walawi na Leo tunaanza Kitabu hiki cha Hesabu..Mungu wetu tunaomba tukaelewe na kusimamia yote tunayojifunza..isiwe tunasoma tuu kama gazeti au hadithi..
Mungu wetu tunaomba Neno lako likakae ndani yetu na likawe kinga..
likatufae sisi na wengine pia..
Tukapate shauku/hamu ya kujifunza zaidi na kujua ukuu wako Mungu wetu...
Na tuendane/tufuate Amri na sheria zako Mungu wetu..
Ukatupe macho ya kuona zaidi,Masikio ya kusikia na akili ya kutambua/kujitambua katika mema na mabaya...
Tunakushukuru na kukusifu daima..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Wapendwa/waungwana asanteni sana..
Mungu aendelee kuwabariki..
Asanteni kwakuwa pamoja na Mungu akatuongoze
Msipungukiwe katika mahitaji yenu na Mungu akawape sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

Hesabu ya kwanza ya Waisraeli

1 # Taz Hes 26:1-51 Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa pili, mwaka wa pili baada ya wana wa Israeli kutoka Misri, Mwenyezi-Mungu aliongea na Mose ndani ya hema la mkutano jangwani Sinai, akamwambia hivi: 2“Wewe na Aroni fanyeni sensa ya jumuiya yote ya Waisraeli, familia mojamoja kwa kufuata koo zao na idadi ya majina yao kila mwanamume mmojammoja; 3wale wote katika Israeli wanaoweza kwenda vitani, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, mtawaweka katika orodha ya vikosi vikosi. 4Tena mwanamume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi, kila mmoja aliye kiongozi wa jamaa za kabila lake. 5Haya ndiyo majina ya watu watakaokusaidia:
Kabila la Reubeni: Elisuri, mwana wa Shedeuri;
6Kabila la Simeoni: Shelumieli mwana wa Suri-shadai;
7Kabila la Yuda: Nashoni mwana wa Aminadabu;
8Kabila la Isakari: Nethaneli mwana wa Suari;
9Kabila la Zebuluni: Eliabu mwana wa Heloni;
10Kabila la Efraimu: Elishama mwana wa Amihudi;
Kabila la Manase: Gamalieli mwana wa Pedasuri;
11Kabila la Benyamini: Abidani mwana wa Gideoni;
12Kabila la Dani: Ahiezeri mwana wa Amishadai;
13Kabila la Asheri: Pagieli mwana wa Okrani;
14Kabila la Gadi: Eliasafu mwana wa Deueli;
15Kabila la Naftali: Ahira mwana wa Enani.”
16Hawa ndio viongozi waliochaguliwa miongoni mwa jumuiya yote ya watu wa Israeli, kama viongozi wakuu wa makabila yao na viongozi wa koo za Israeli.
17Basi, Mose na Aroni wakawachukua watu hawa waliotajwa, 18na mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa pili, wakaikusanya jumuiya yote ya watu waliokuwa wamehesabiwa kila mmoja kulingana na familia yake na ukoo wake. Kufuatana na majina ya watu waliokuwa na umri wa miaka ishirini na zaidi, mmojammoja, 19kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. Mose akawahesabu watu hawa kule jangwani Sinai.
20Watu waliotoka katika kabila la Reubeni aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, kwa kufuata vizazi vyao, kulingana na familia zao na jamaa zao, kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, kila mwanamume aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na zaidi, aliyefaa kuingia jeshini, 21walikuwa watu 46,500.
22Kutoka kabila la Simeoni kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 23walikuwa watu 59,300.
24Kutoka kabila la Gadi kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 25walikuwa watu 45,650.
26Kutoka kabila la Yuda kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 27walikuwa watu 74,600.
28Kutoka kabila la Isakari kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 29walikuwa watu 54,400.
30Kutoka kabila la Zebuluni kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 31walikuwa watu 57,400.
32Kutoka kabila la Efraimu, mwanawe Yosefu, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 33walikuwa watu 40,500.
34Kutoka kabila la Manase, mwanawe Yosefu, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi waliofaa kuingia jeshini, 35walikuwa watu 32,200.
36Kutoka kabila la Benyamini, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 37walikuwa watu 35,400.
38Kutoka kabila la Dani kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 39walikuwa watu 62,700.
40Kutoka kabila la Asheri, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 41walikuwa watu 41,500.
42Kutoka kabila la Naftali, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina ya mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, 43walikuwa watu 53,400.
44Hawa ndio watu waliokuwa wamehesabiwa ambao Mose na Aroni waliwahesabu wakisaidiwa na wale viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila kiongozi akiwakilisha ukoo wake. 45Hivyo jumla ya wanaume wote wa Israeli wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini nchini Israeli 46ilikuwa watu 603,550.
47Lakini Walawi hawakuhesabiwa pamoja na yale makabila mengine, 48kwa sababu Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 49“Usihesabu kabila la Lawi wala usiwafanyie sensa kati ya watu wa Israeli; 50bali utawateua wawe waangalizi wa hema la ushuhuda, vyombo vyake vyote na kila kitu kilichomo ndani yake; watakuwa wakilibeba pamoja na vyombo vyake vyote. Watahudumu humo ndani na kupiga kambi yao kwa kulizunguka. 51Tena wakati wa hema kungolewa Walawi ndio watakaolingoa na wakati wa hema kusimikwa Walawi ndio watakaolisimamisha. 52Waisraeli wengine wote watapiga kambi zao makundimakundi, kila mtu katika kundi lake na chini ya bendera yake. 53Lakini Walawi watapiga kambi zao kulizunguka hema la maamuzi, wakililinda ili mtu yeyote asije akalikaribia na kusababisha ghadhabu yangu kuwaka dhidi ya jumuiya ya watu wa Israeli; basi Walawi watalitunza hema la maamuzi.” 54Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Hesabu1;1-54


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 3 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..27...Mwisho wa Kitabu cha Walawi

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!

Asante Baba wa Mbinguni kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Tazama jana imepita Mungu Baba Leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine..
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwakutulinda na kutuamsha salama wenye Afya na kuendelea kwa majukumu yetu..
Si kwamba sisi ni wema sana au ni wazuri mno hapana ni kwa neema/rehema zako tuu Mungu wetu..


Tunakuja mbele zako Jehovah..!Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote..

Tilizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Yahweh tunaomba utuepushe na majaribu na utuokoe na mwovu na kazi zake zote..

Ututakase Miili yetu na Akili zetu Mungu  Baba na utufunike kwa Damau  ya mwanano Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
yeye aliteseka kwanza ilisisi tupate kupona..



Kwa vile sheria ni kivuli tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu! Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na tambiko hizo zote zingekoma. Lakini tambiko hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao. Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi. Ndiyo maana Kristo alipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambia Mungu: “Hukutaka tambiko wala sadaka, lakini umenitayarishia mwili. Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi. Hapo nikasema: ‘Niko hapa, ee Mungu, kutimiza matakwa yako kama ilivyoandikwa juu yangu katika kitabu cha sheria.’” Kwanza alisema: “Hutaki wala hupendezwi na tambiko, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na sheria. Kisha akasema: “Niko hapa, ee Mungu, tayari kufanya matakwa yako.” Hivyo Mungu alibatilisha tambiko za zamani na mahali pake akaweka tambiko nyingine moja. Kwa kuwa Yesu Kristo alitimiza matakwa ya Mungu, sisi tunatakaswa dhambi zetu kwa ile tambiko ya mwili wake aliyotoa mara moja tu, ikatosha. Kila kuhani Myahudi hutoa huduma yake ya ibada ya kila siku na kutoa tambiko zilezile mara nyingi, tambiko ambazo haziwezi kuondoa dhambi. Lakini Kristo alitoa tambiko moja kwa ajili ya dhambi, tambiko ifaayo milele, kisha, akaketi upande wa kulia wa Mungu, anangoja maadui zake wafanywe kama kibao chini ya miguu yake. Basi, kwa tambiko yake moja, amewafanya kuwa wakamilifu milele wote wale wanaotakaswa dhambi zao. Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema: “Hili ndilo agano nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao.” Kisha akaongeza kusema: “Sitakumbuka tena dhambi zao, wala vitendo vyao vya uhalifu.” Basi, dhambi zikisha ondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoa tambiko za kuondoa dhambi.


Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Mungu wetu ukatupe neema ya kusimamia Neno lako na kufuata sheria na Amri zako..
Kwa moyo  mnyofu na imani timilifu tuzingatie tumaini na ahadi zako kwani wewe ni mwaminifu na wakuabudiwa..
Ukatufanye Chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Ukatubariki tuingiapo/tutokapo na ukabariki kazi zetu na vyote tunavyoenda kutenda/kufanya Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu na ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Tazama Yatima na wajane Mungu ukawabariki na wasipungukiwe katika mahitaji yao..
Wenye shida/tabu,wagonjwa na wote wanaopita magumu/majaribu,waliokatika vifungo mbalimbali Mungu wetu ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawape neema ya kukujua wewe na kufuata njia zako,waijue kweli yako nayo ikawaweke huru..Ukawaponye na kuwaokoa..

wafiwa ukawe mfariji wao na ukawape nguvu na uvumilivu...

Mungu wetu tunashukuru hata kwakumaliza/kupitia/kusoma na kujifunza katika kitabu hiki..leo tumefikia mwisho lakini ikawe ndiyo mwanzo wa kujituma zaidi na  utupe neema ya kujifunza zaidi na kurudia kila wakati ili tuishi kwa sheria na misingi yako..
tupate pia shauku ya kupenda kusoma na kujifunza na kuendelea kusoma Neno lako kila wakati..
si kwa uwezo wetu bali ni kwa neema  yako Mungu..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu..
Tukiami na kushukuru daima..

kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina..!!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa pamoja..
Leo tumefikia mwisho wa kitabu hiki lakini usiwe mwisho wakuendela kujifunza na kusoma vitabu vingine na pia tuwe tunarudia ili kuhifadhi na kujifunza zaidi..
Ninawashukuru sana na sina neno zuri zaidi ya kusema..
Nawapenda na Mungu aendelee kutuongoza.

Sheria kuhusu matoleo

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Waambie Waisraeli hivi: Mtu akiweka nadhiri ya kumtolea Mwenyezi-Mungu binadamu, mtu huyo anaweza kuondoa nadhiri yake kwa kulipa kiasi cha fedha kinachokadiriwa kama ifuatavyo: 3Mwanamume wa miaka ishirini hadi miaka sitini atakombolewa kwa fedha shekeli 50 kulingana na kipimo cha mahali patakatifu. 4Kama ni mwanamke, atakombolewa kwa fedha shekeli 30. 5Kama mtu huyo ni wa miaka kati ya mitano na 20 atakombolewa kwa fedha shekeli 20 kama ni mvulana na shekeli 10 za fedha kama ni msichana. 6Ikiwa ni mtoto wa umri wa kati ya mwezi mmoja na miaka mitano atakombolewa kwa shekeli 5 za fedha kama ni mvulana na shekeli 3 za fedha kama ni msichana. 7Ikiwa mtu huyo umri wake ni zaidi ya miaka sitini, thamani yake itakuwa ni shekeli 15 za fedha kama ni mwanamume na shekeli 10 za fedha kama ni mwanamke. 8Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini na hawezi kulipa gharama yake, basi, mtu huyo atapelekwa kwa kuhani. Kuhani atampima thamani yake kulingana na uwezo wa huyo aliyeweka nadhiri.
9“Ikiwa nadhiri yenyewe inahusu mnyama wa namna ambayo watu humtolea Mwenyezi-Mungu sadaka, basi mnyama huyo huwa kitu kitakatifu. 10Hairuhusiwi kumbadilisha mnyama huyo kwa mwingine awaye yeyote, mzuri kwa mbaya au mbaya kwa mzuri. Kama akimbadilisha kwa mnyama mwingine, wote wawili watakuwa watakatifu.
11“Kama nadhiri hiyo yahusu mnyama najisi, wa aina ambayo si halali kumtolea Mwenyezi-Mungu, basi, mtu aliyemtoa, atamleta kwa kuhani, 12naye kuhani ataamua thamani yake kulingana na uzuri au ubaya wake. Jinsi atakavyoamua kuhani, ndivyo itakavyokuwa. 13Lakini ikiwa mwenyewe anataka kumkomboa, basi, ataongeza asilimia ishirini ya thamani ya mnyama huyo.
14“Mtu akiiweka wakfu nyumba yake kuwa takatifu kwa Mwenyezi-Mungu, kuhani ataamua thamani yake kulingana na uzuri au ubaya wake. Jinsi atakavyoamua, ndivyo itakavyokuwa. 15Kama huyo mtu aliyeiweka wakfu akitaka kuikomboa hiyo nyumba, basi, ataongeza asilimia ishirini ya thamani yake, nayo itakuwa mali yake.
16“Mtu akiiweka ardhi yake, ambayo ni urithi wake, wakfu kwa Mwenyezi-Mungu basi, thamani yake itapimwa kulingana na mbegu zinazotumika kulipanda shamba hilo; kwa kila kilo ishirini za shayiri thamani yake itakuwa shekeli hamsini za fedha. 17Kama akiliweka wakfu shamba lake katika mwaka wa kuadhimisha miaka hamsini, thamani yake ni lazima ilingane na vipimo vyenu. 18Lakini kama akiliweka wakfu baada ya mwaka huo, basi, kuhani ataamua thamani yake kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na thamani yake ipunguzwe. 19Kama mwenyewe akitaka kulikomboa, basi, ni lazima aongeze asilimia ishirini ya thamani ya shamba hilo, na kisha litakuwa mali yake. 20Lakini kama hataki kulikomboa au amemwuzia mtu mwingine, basi, shamba hilo lisikombolewe tena. 21Katika mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini shamba hilo litaachiliwa na kuwa lake Mwenyezi-Mungu milele. Kuhani ndiye atakayelimiliki.
22“Kama mtu akiweka wakfu shamba alilonunua, yaani sio lake kwa urithi, 23kuhani ataamua thamani ya shamba hilo kwa kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na mtu huyo atalazimika kulipa thamani yake kama ni kitu kitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu. 24Lakini katika mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini, shamba hilo ni lazima arudishiwe yule mtu aliyeliuza. 25Kila thamani itapimwa kwa kipimo cha uzito cha shekeli kulingana na kipimo cha mahali patakatifu: Uzito wa gera 20 ni sawa na uzito wa shekeli moja.
26“Hairuhusiwi kumweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa wanyama; kisheria huyo ni wake Mwenyezi-Mungu; awe ni ng'ombe au kondoo. 27Kama anayehusika ni mnyama najisi, mwenyewe atamnunua kwa kulingana na mnavyompima na ataongeza asilimia ishirini ya thamani ya mnyama huyo. Kama hakombolewi, basi, atauzwa kulingana na vipimo vyenu.
28 # Taz Hes 18:14 “Lakini kitu chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, kiwe ni mtu au mnyama au kitu kilichopatikana kwa urithi, hakitauzwa wala kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu ni kitakatifu kabisa. 29Mtu yeyote aliyewekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu ili aangamizwe, asikombolewe; sharti auawe.
30 # Taz Hes 18:21; Kumb 14:22-29 “Zaka za mazao iwe ni nafaka au matunda ya miti, yote ni mali ya Mwenyezi-Mungu; ni takatifu kwa Mwenyezi-Mungu. 31Kama mtu akitaka kuikomboa zaka yake, atalipa thamani yake na kuongeza asilimia ishirini ya thamani ya zaka hiyo. 32Kuhusu mifugo, inapohesabiwa, kila mnyama wa kumi ni mtakatifu kwa Mwenyezi-Mungu. 33Mtu yeyote hana ruhusa kuuliza kama mnyama huyo ni mzuri au mbaya wala mnyama huyo kamwe hatabadilishwa kwa mwingine. Kama akibadilishwa kwa mwingine, wanyama wote wawili watakuwa watakatifu; hawatakombolewa.”
34Hizo ndizo amri ambazo Mwenyezi-Mungu alimwamuru Mose ili awaambie Waisraeli, mlimani Sinai.

Mambo Ya Walawi27;1-34


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday 30 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..26...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Mungu wetu ,Baba yetu,Muumba wetu, Muumba wa Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Baba wa uzima,Mungu unayeponya,Mungu usiyesinzia wala kulala..!!
Ee ,Mwenyezi-Mungu,Mungu wetu hakuna Mungu mwingine kama wewe, wewe ni mwaminifu...!


Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutuamsha salama na wenye afya..

Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii...

Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..

Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..

Ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo yeye aliteseka ili sisi tupate kupona...
Ee Mungu wetu tunaomba ututimizie maombi yetu tunayokuomba leo..Ee Mungu wetu utuhurumie na usikie  upokee maombi ya watu wako wanapoomba kwa unyenyekevu na ukawasamehe pale walipokosea,ukawape neema ya kufuata njia zako na  ukawabariki..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Mungu wetu utuchunge na kutupa neema ya kusimamia Neno lako..
Mungu wetu tunaomba utubariki na ukabariki nyumba zetu/ndoa,watoto wetu na familia nzima..
Baba wa mbinguni tunaomba ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda na ukatuongoze vyema tukatende sawasawa na mapenzi yako..Baba wa Mbinguni ukajiinue na kunyoosha mkono wako wenye nguvu na uponyaji kwa wote wanaopitia magumu/majaribu,Magonjwa,shida/tabu,waliokatika vifungo mbalimbali na ukatupe neema ya kujua jinsi ulivyo..
Jehovah..ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako

Sala ya Solomoni

(1Fal 8:22-53)
Kisha, Solomoni alisimama mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu halafu mbele ya jumuiya yote ya watu wa Israeli, aliinua mikono yake juu. Solomoni alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba ambalo aliliweka katikati ya ua. Urefu na upana wake ulikuwa mita mbili na robo, na kimo chake mita moja na robo. Alipanda jukwaani na kupiga magoti mbele ya jumuiya yote ya Israeli, akainua mikono yake kuelekea mbinguni. Aliomba akisema, “Ee, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu mwingine kama wewe, mbinguni ama duniani. Wewe ni mwaminifu, kwani umetimiza agano lako na kuwaonesha fadhili zako watumishi wako wanaoishi wakikutii kwa moyo wao wote. Umetimiza ahadi uliyotoa kwa mtumishi wako baba yangu Daudi; naam, yale uliyonena umeyatimiza leo kwa uwezo wako mwenyewe. “Kwa hiyo sasa, Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ninakuomba pia utimize ile ahadi uliyomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu, ukisema, ‘Siku zote utakuwa na mzawa wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, iwapo wazawa wako watafuata kwa uangalifu sheria yangu kama wewe ulivyofanya mbele yangu.’ Sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nakusihi utimize yote uliyomwahidi mtumishi wako Daudi. “Lakini, ee Mungu kweli utakaa humu duniani na binadamu? Hata mbingu zenyewe, wala mbingu za mbingu za juu sana hazikutoshi, itakutoshaje nyumba hii ambayo nimeijenga? Hata hivyo, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, mimi mtumishi wako, nakuomba unisikilize na kunitimizia ombi langu ninalokuomba leo. Ichunge nyumba hii mchana na usiku, mahali ambapo umechagua watu wako waliabudu jina lako. Unisikie mimi mtumishi wako ninapokuja mahali hapa kuomba. Sikia maombi yangu mimi mtumishi wako na ya watu wako Israeli wanapoomba wakielekea mahali hapa. Usikie maombi kutoka huko mbinguni na ukisha sikia, utusamehe. “Mtu akimkosea mwenzake, naye akaletwa apate kuapa mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii, na akiapa tafadhali wewe usikie kutoka huko mbinguni, uchukue hatua na kuwahukumu watumishi wako. Aliye na hatia umwadhibu kadiri ya makosa yake; asiye na hatia umwachilie na kumpatia tuzo kadiri ya uadilifu wake. “Wakati watu wako Israeli watakaposhindwa na maadui zao, kwa sababu ya dhambi walizotenda dhidi yako, nao wakitubu kwako na kukiri jina lako, wakiomba msamaha wako kwa unyenyekevu katika nyumba hii, basi, usikie kutoka huko mbinguni. Usamehe dhambi zao na uwarudishe katika nchi uliyowapa wao na babu zao. “Mvua isiponyesha kwa sababu wametenda dhambi dhidi yako, wakiomba wakielekea mahali hapa na kulikiri jina lako, pia wakiziacha dhambi zao, tafadhali uwasikie kutoka huko mbinguni, na usamehe dhambi zao watumishi wako watu wako Waisraeli, huku ukiwafundisha kufuata njia nyofu, ukanyeshe mvua katika nchi yako hii ambayo uliwapa watu wako iwe mali yao. “Iwapo kuna njaa nchini au tauni, ukame, ugonjwa wa mimea, nzige au viwavi, au ikiwa watu wako wamezingirwa na maadui zao katika mji wao wowote ule; ikiwa kuna pigo lolote au ugonjwa wowote, tafadhali usikie maombi yoyote yatakayoombwa na mtu yeyote au watu wako wote wa Israeli, kila mtu akijua taabu yake na huzuni yake akikuomba huku akinyosha mikono yake kuelekea nyumba hii. Basi usikie kutoka kwako mbinguni, utoe msamaha, pia umtendee kila mtu kadiri anavyostahili, kwani ni wewe tu ujuaye mawazo ya mioyo ya wanadamu wote. Hivyo watakutii na kuenenda katika njia zako wakati wote wanapoishi katika nchi uliyowapa babu zetu. “Vivyo hivyo wakati mgeni asiye mmoja wa watu wako Israeli atakuja kutoka nchi ya mbali kwa ajili ya jina lako kuu, na kwa sababu ya nguvu na ulinzi wako, kuomba katika nyumba hii, nakusihi umsikie toka huko kwako mbinguni, na umjalie huyo mgeni yote atakayokuomba kusudi watu wote ulimwenguni wapate kujua jina lako na kukutii kama wafanyavyo watu wako Israeli na wapate kufahamu kwamba nyumba hii ambayo nimeijenga inajulikana kwa jina lako. “Watu wako wakienda vitani kupigana na maadui zao kokote kule utakakowapeleka, nao wakikuomba wakielekea mji huu uliouchagua na nyumba ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako, nakusihi usikie sala yao na maombi yao ukiwa huko mbinguni na uwapatie ushindi vitani. “Ikiwa watatenda dhambi dhidi yako, maana hakuna mtu asiyetenda dhambi, na ukiwakasirikia na kuwaacha washindwe na adui, hata wapelekwe mateka mpaka nchi ya mbali au ya karibu; kama watakapokuwa huko uhamishoni watajirudi kwa roho yao yote na kwa moyo wao wote na kutubu na kukuomba msamaha, wakisema, ‘Tumetenda dhambi; tumepotoka na kufanya maovu’; pia kama watatubu kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote wakati watakapokuwa katika nchi ya uhamisho, na kama watakuomba wakielekea nchi yao ambayo uliwapatia babu zao, mji huu ambao uliuchagua na nyumba hii ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako; basi, nakusihi usikie huko mbinguni uliko sala yao na maombi yao na uwapatie haki zao, uwasamehe watu wako ambao wametenda dhambi dhidi yako. “Sasa ee Mungu wangu, tuangalie na upokee maombi tutakayoomba mahali hapa. Sasa inuka ee Bwana Mungu, uingie mahali pako pa kupumzika wewe pamoja na sanduku la agano la nguvu zako. Makuhani wako ee Bwana Mungu, wapate wokovu, na watakatifu wako wafurahie wema wako. Ee Bwana Mungu, usimpige kisogo masiha wako. Kumbuka fadhili zako kwa mtumishi wako Daudi.”
Asante Baba wambinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana kwakuwa nami/kunisoma
Mungu akawabariki na kuwaongoza katika yote..
Nawapenda.




Baraka kwa utiifu

(Kumb 7:12-24; 28:1-14)
1“Msijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, msishike sanamu zao za kuchonga wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa nchini mwenu na kuvisujudu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. 2Shikeni sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
3 # Taz Kumb 11:13-15; 28:1-14 “Kama mkifuata masharti yangu na kuzishika amri zangu, 4nitawanyeshea mvua wakati ufaao, nchi ipate kuzaa mavuno kwa wingi, nayo miti ya mashambani matunda yake. 5Kupura nafaka kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, na uvunaji zabibu mpaka wakati wa kupanda mbegu. Mtakuwa na chakula tele na kuishi kwa usalama nchini mwenu. 6Nitawapeni amani nchini hata muweze kulala bila ya kuogopeshwa na chochote. Nitawaondoa wanyama wakali katika nchi na nchi yenu haitakumbwa na vita. 7Mtawafukuza adui zenu na kuwaua kwa upanga. 8Watano wenu watawafukuza adui 100 na 100 wenu watawafukuza adui 10,000. Adui zenu wataangamia mbele yenu kwa upanga. 9Nitawafadhili na kuwajalia mpate watoto wengi na kuongezeka; nami nitaliimarisha agano langu nanyi. 10Wakati wa mavuno mtakuwa bado mnakula mazao ya zamani; tena itawalazimu kuondoa yaliyobaki kupata nafasi ya kuhifadhi mavuno mapya. 11Nitaweka maskani yangu miongoni mwenu, wala sitawaacheni. 12#Taz Nya 6:16 Nitatembea kati yenu na kuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. 13Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa nchini Misri ili msiwe watumwa wa Wamisri. Mimi nimevunja nira mliyofungiwa shingoni mwenu na kuwafanya mtembee wima.

Laana

(Kumb 28:15-68)
14“Lakini kama hamtanisikiliza wala kufuata amri zangu, 15kama mkidharau masharti yangu na kuchukia kwa roho maagizo yangu mkaacha kuzitii amri zangu zote na kuvunja agano langu, 16basi, mimi nitafanya hivi: Nitawapiga kwa kuwaletea hofu kuu ya ghafla, kifua kikuu na homa itakayowapofusha macho na kuwadhoofisha. Mtapanda mbegu zenu bila mafanikio kwani adui zenu ndio watakaokula. 17Mimi nitawakabili, nanyi mtapigwa na adui zenu; mtatawaliwa na wale wanaowachukia. Mtatishwa na kukimbia hata kama hakuna mtu yeyote anayewafukuza. 18Na Kama hata baada ya kuadhibiwa hivyo, hamtanisikiliza, basi, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. 19Kiburi chenu nitakivunjilia mbali kwa kuzifanya mbingu huko juu kuwa ngumu kama chuma, na nchi yenu bila mvua iwe ngumu kama shaba. 20Mtatumia nguvu zenu bure maana mashamba yenu hayatatoa mavuno na nchi yenu haitazaa matunda.
21“Kama mkiendelea kunipinga na kukataa kunisikiliza, nitazidisha tena adhabu yenu mara saba kadiri ya wingi wa dhambi zenu. 22Nitawapeleka wanyama wakali kati yenu ambao watawanyakulieni watoto wenu na kula mifugo yenu; na kukata idadi yenu hata njia zenu zigeuke kama jangwa.
23“Kama hata baada ya adhabu hiyo bado hamnigeukii mimi, ila mnazidi kupingana nami, 24basi, nami nitapingana nanyi na kuwaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. 25Nitawaleteeni upanga ambao utalipiza kisasi juu ya agano mlilovunja. Nyinyi mtakimbilia katika miji yenu, lakini nitawapelekea maradhi mabaya na kuwatia mikononi mwa adui zenu. 26Chakula chenu nitakipunguza hata wanawake kumi watumie jiko moja tu kuoka mikate. Watawagawia kwa kipimo. Na hata baada ya kula bado mtakuwa na njaa tu.
27“Na kama hata baada ya hayo yote bado hamtanisikiliza mkaendelea kunipinga, 28basi nami nitapingana nanyi kwa hasira kali, na kuwaadhibu mimi mwenyewe mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. 29Ndipo mtakula watoto wenu, wa kiume na kike. 30Nitapaharibu mahali penu pa ibada milimani, nitazibomoa madhabahu zenu za kufukizia ubani, na kuzitupa maiti zenu juu ya sanamu za miungu yenu. Roho yangu itawachukia kabisa. 31Miji yenu nitaiteketeza mahali penu patakatifu nitapafanya jangwa na harufu zenu nzuri za sadaka kamwe sitazikubali. 32Nitaiteketeza nchi yenu hivyo kwamba hata adui wanaohamia humo watashangaa. 33Nitawatawanya nyinyi miongoni mwa watu wa mataifa na kuchomoa upanga dhidi yenu. Nchi yenu itakuwa ni ukiwa na miji yenu uharibifu.
34“Nyinyi mtakapokuwa mikononi mwa adui zenu, hapo ndipo nchi itakapozifurahia sabato zake wakati itakapokuwa hali ya ukiwa. Nchi itapumzika na kufurahia sabato zake. 35Kadiri itakapokuwa hali ya ukiwa itapata kiasi ambacho haikupata katika sabato zenu mlipokuwa mkiishi humo. 36Na kwa baadhi yenu watakaosalimika nitawaletea woga mioyoni mwao, katika nchi ya adui zao hata jani linalopeperushwa litawakimbiza. Watakimbia kama mtu anayekimbia vita. Watakimbia na kuanguka hata kama hamna mtu anayewafukuza. 37Wataangukiana ovyo kama mtu anayekimbia vita hata kama hamna anayewafukuza. Hamtakuwa na nguvu yoyote kuwakabili adui zenu. 38Mtaangamia kati ya mataifa na nchi za adui zenu zitawameza. 39Kama baadhi yenu wakisalimika katika nchi za adui zenu watadhoofika kwa sababu ya uovu wao; na kwa sababu ya uovu wa wazee wao.
40“Lakini kama wakitubu uovu wao na uovu wa wazee wao juu ya uasi waliotenda dhidi yangu na pia juu ya kupingana kwao nami, 41wakatambua kwa nini nilipingana nao na kuwapeleka katika nchi ya adui zao; kama kweli moyo wao mkaidi ukinyenyekea na kutubu uovu wao, 42#Taz Mwa 17:7-8; 26:3-4; 28:13-14 basi, hapo nami nitalikumbuka agano langu na Abrahamu, Isaka na Yakobo; na kuikumbuka ile nchi niliyowaahidia.
43“Wakati watakapokuwa nje ya nchi yao, nchi hiyo itafurahia sabato zake hapo itakapokuwa hali ya ukiwa. Wakati huo wao watatubu uovu wao wa kupuuza maagizo yangu na kuyachukia maagizo yangu. 44Lakini, kwa hayo yote, wawapo katika nchi ya adui zao; mimi sitawatupa wala kuwachukia hata kuwaangamiza kabisa na kulivunjilia mbali agano langu. 45La! Kwa ajili yao nitalikumbuka agano nililofanya na wazee wao ambao niliwatoa katika nchi ya Misri, mataifa yakishuhudia, ili mimi niwe Mungu wao. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.” 46Hayo ndiyo masharti, maagizo na sheria ambazo Mwenyezi-Mungu aliwapa watu wa Israeli kule mlimani Sinai kwa njia ya Mose.

Mambo Ya Walawi26;1-46


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.