Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 7 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..25

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah..!Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru na kumsifu daima..
Mungu wetu,Baba yetu Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwa nguvu zetu wala uelewa wetu Baba wa Mbinguni sisi kuwa hivi tulivyo ni kwa Neema/Rehema zako Mungu wetu..


Tunakuja mbele zako tukijinyeyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mfalme wa Amani..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..



Mfano wa mtumishi asiyesamehe
21Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, “Je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?” 22Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba. 23Ndiyo maana ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake. 24Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta 10,000. 25Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe. 26Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, ‘Unisubiri nami nitakulipa deni lote’. 27Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.
28“Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha dinari 100. Akamkamata, akamkaba koo akisema, ‘Lipa deni lako!’ 29Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, ‘Unisubiri nami nitakulipa’. 30Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.
31“Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia. 32Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote. 33Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?’
34“Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote. 35Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.”

Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Jehovah tuyaweka maisha yetu mikononi mwako..
tunaomba utubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na yote tunayoenda kufanya/kutenda tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi utupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..

tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mfalme wa Amani ukatupe kama inavyokupendeza wewe..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Mungu wetu tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu na ukawaponye wote wataabikao,wenye shida/tabu,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,wagonjwa na wafiwa ukawe mfariji wao 
na ukawape neema ya kusimamia Neno lako Amri na sheria zako ...

wakapate kuwa huru rohoni na mwilini..

Roho Mtakatifu akatuongoze vyema,tusiwe watu wa kuhukumu wengine,tusiwe watu wa kudharau wengine na kukatisha tamaa..
tukawe na upendo wa kweli na kiasi katikayote..


Usimhukumu ndugu yako
1Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi. 2Watu hutofautiana: Mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu; lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani. 3Mtu ambaye hula kila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kula kila kitu; naye ambaye hula tu mboga za majani asimhukumu anayekula kila kitu, maana Mungu amemkubali. 4Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
5Mtu anaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maana zaidi kuliko nyingine; mtu mwingine aweza kuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja na afuate msimamo wa akili yake. 6Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu. 7Maana hakuna mtu yeyote miongoni mwetu aishiye kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe 8maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana. 9Maana Kristo alikufa, akafufuka ili apate kuwa Bwana wa walio hai na wafu. 10Kwa nini basi, wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. 11Maana Maandiko yanasema:
“Kama niishivyo, asema Bwana,
kila mtu atanipigia magoti,
na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.”
12Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu.


Asante Mungu Baba ...Sifa na utukufu ni wako..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa kwakuwa nami/kunisoma..
Mungu aendelee kuwa nayi daima..
Nawapenda.


Waisraeli na Baali wa Peori
1Waisraeli walipokuwa huko Shitimu, wanaume walianza kuzini na wanawake wa Moabu. 2Wanawake hao waliwaalika Waisraeli washiriki matambiko waliyotambikia miungu yao, nao Waisraeli wakala chakula na kuiabudu miungu yao. 3Ndivyo Waisraeli walivyojiunga na mungu Baali wa Peori, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi yao. 4Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.” 5Mose akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu amuue mtu yeyote miongoni mwenu ambaye amejiunga na mungu Baali wa Peori.”
6Wakati huohuo mtu mmoja akamleta mwanamke mmoja Mmidiani nyumbani kwake, Mose na jumuiya yote ya watu wa Israeli wakiwa wanaomboleza penye lango la hema la mkutano. 7Basi, Finehasi mwana wa Eleazari mwana wa kuhani Aroni alipoona hayo, aliinuka akatoka katika hiyo jumuiya, akachukua mkuki 8na kumfuatia yule Mwisraeli mpaka hemani, akawachoma mkuki wote wawili tumboni. Maradhi mabaya yaliyokuwa yamewaangamiza Waisraeli yakakomeshwa. 9Waliokufa kutokana na maradhi yale mabaya walikuwa watu 24,000.
10Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 11“Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, ameizuia hasira yangu dhidi ya Waisraeli; miongoni mwenu ni yeye tu aliyeona wivu kama nilio nao mimi. Ndio maana sikuwaangamiza Waisraeli wote kwa hasira yangu. 12Kwa hiyo mwambie kwamba ninafanya naye agano la amani. 13Naagana naye kwamba yeye na wazawa wake watakuwa makuhani milele kwa sababu aliona wivu kwa ajili yangu, Mungu wake, akawafanyia upatanisho Waisraeli.”
14Huyo Mwisraeli aliyeuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani aliitwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa mojawapo katika kabila la Simeoni. 15Na huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa aliitwa Kozbi binti Suri, aliyekuwa kiongozi wa ukoo fulani huko Midiani.
16Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 17“Wachokoze Wamidiani na kuwaangamiza, 18kwa sababu waliwachokoza nyinyi kwa hila zao, wakawadanganya kuhusu jambo la Peori, na kwa sababu ya Kozbi, binti yao, aliyeuawa wakati maradhi mabaya yalipozuka kule Peori.


Hesabu25;1-18


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.


Sunday 6 August 2017

Natumaini Jumapili ilikuwa/inaendelea Vyema;[Shukrani zangu kwenu]..Burudani-Mercy Masika & Angel Benard - Huyu Yesu,SINACH - I KNOW WHO I AM,EBEN-VICTORY...

Wapendwa/Waungwana nimatumaini yangu wote hamjambo na Mungu anawatendea sawasawa na mapenzi yake..
Hapa tulipo Jumapili inaendelea vyemakabisa na Bwana ametupa kibali cha kuungana na wengine katika Ibada..
Natumaini nawe unayesoma hapa umepata neema/kibali cha kushiriki na wenzio..
na kama ulikosa Mungu akakupe neema ya kuweza kushiriki wakati mwingine..


Shukrani zangu kwa wote mlioniombea na kunitakia heri kwa Anniversary yetu mimi na Isaac..
Pia kwa Birthday yangu..Asanteni sana na Mungu aendelee kuwabariki na kuongezea zaidi ya mlipojiatoa..
Tulikuwa na wakati mzuri sana na Tunamshukuru Mungu kwa neema na kibali alichotupa cha kuendelea kufikia hapa tulipo..
Shukrani kwa wazazi wangu,Mume wangu na watoto wetu,Ndugu,Jamaa na marafiki wote..
Nawapenda...!

Neno La Shukrani;

Nakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu, kwa moyo wangu wote, naimba sifa zako mbele ya miungu. Ninasujudu kuelekea hekalu lako takatifu; nalisifu jina lako, kwa sababu ya fadhili zako na uaminifu wako; kwa sababu umeweka jina lako na neno lako juu ya kila kitu. Nilipokulilia, wewe ulinijibu; umeniongezea nguvu zangu. Wafalme wote duniani watakusifu, ee Mwenyezi-Mungu, kwa sababu wameyasikia maneno yako. Wataimba sifa za matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, kwa maana utukufu wako ni mkuu. Ingawa wewe ee Mwenyezi-Mungu, uko juu ya wote, unawaangalia kwa wema walio wanyonge; nao wenye kiburi huwaona kutoka mbali. Hata nikikumbana na taabu, wewe wanilinda; waunyosha mkono wako dhidi ya hasira ya maadui zangu wakali; kwa nguvu yako kuu wanisalimisha. Ee Mwenyezi-Mungu, utatimiza yote uliyoniahidi. Fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, zadumu milele. Usisahau kazi ya mkono wako mwenyewe.
Zaburi 138:1-8


Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani. Nikiketi au nikisimama, wewe wajua; wajua kutoka mbali kila kitu ninachofikiria. Watambua nikienda au nikipumzika; wewe wazijua shughuli zangu zote. Kabla sijasema neno lolote, wewe, ee Mwenyezi-Mungu, walijua kabisa. Uko kila upande wangu, mbele na nyuma; waniwekea mkono wako kunilinda. Maarifa yako yapita akili yangu; ni makuu mno, siwezi kuyaelewa. Nikimbilie wapi ambako roho yako haiko? Niende wapi ambako wewe huko? Nikipanda juu mbinguni, wewe upo; nikijilaza chini kuzimu, wewe upo. Nikiruka hadi mawio ya jua, au hata mipakani mwa bahari, hata huko upo kuniongoza; mkono wako wa kulia utanitegemeza. Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, kwako giza si giza hata kidogo, na usiku wangaa kama mchana; kwako giza na mwanga ni mamoja. Wewe umeniumba, mwili wangu wote; ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu. Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa. Umbo langu halikufichika kwako nilipotungwa kwa siri na ustadi ndani ya dunia. Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza. Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno; hayawezi kabisa kuhesabika. Ningeyahesabu yangekuwa mengi kuliko mchanga. Niamkapo, bado nipo pamoja nawe.


                                                Amina...!!!


 Neno La Leo;

Maadamu Kristo aliteseka kimwili, nanyi pia mnapaswa kujiimarisha kwa nia hiyo yake; maana mtu akisha teseka kimwili hahusiki tena na dhambi. Tangu sasa, basi, maisha yaliyowabakia kuishi hapa duniani yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, sio na tamaa za kibinadamu. Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu. Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo wanawatukaneni. Lakini watapaswa kutoa hoja juu ya jambo hilo mbele yake Mungu aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa! Ndiyo maana Habari Njema ilihubiriwa hata kwa hao waliokufa, ili baada ya kuhukumiwa katika maisha yao ya kimwili kama wengine, waishi kwa ajili ya Mungu kwa njia ya Roho. Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na kukesha ili muweze kusali. Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi. Muwe na ukarimu nyinyi kwa nyinyi bila kunung'unika. Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine kama wakili mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguv
u anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina. Wapenzi wangu, msishangae kuhusu majaribio makali mnayopata kana kwamba mnapatwa na kitu kisicho cha kawaida. Ila furahini kwamba mnashiriki mateso ya Kristo ili muweze kuwa na furaha tele wakati utukufu wake utakapofunuliwa. Heri yenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina la Kristo; jambo hilo lamaanisha kwamba Roho mtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa nanyi. Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa sababu ni mwuaji, mwizi, mhalifu au mwovu. Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi, asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo. Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi, mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu? Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Ni vigumu kwa watu waadilifu kuokolewa; itakuwaje basi, kwa wasiomcha Mungu na wenye dhambi?” Kwa hiyo, wale wanaoteseka kufuatana na matakwa ya Mungu, wanapaswa, kwa matendo yao mema, kujiweka chini ya Muumba wao ambaye ni wa kuaminika kabisa.

1 Petro 4:1-19
Mungu aendelee kuwabariki na kuwalinda wakati wote..
Wenu Rachel-siwa na kwaniaba ya familia yangu
tunasena Asanteni Sana.



















"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Friday 4 August 2017

Mahojiano ya Mubelwa Bandio na Maduhu Emmanuel ndani ya Kilimanjaro Studios



Emmanuel Maduhu ni mtangazaji wa Morning Star Radio na Televisheni jijini Dar Es Salaam
Mwezi Julai 2017 alifanya ziara ya kikazi nchini Marekani, ambapo alitembelea majimbo kadhaa.
Mwishoni mwa ziara yake, alipata fursa kuketi na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production ndani ya Kilimanjaro Studios na kujadili mambo mbalimbali kuhusu kazi, ziara, maisha nk
Karibu ujiunge nasi


Kwa simu toka :London- Mahojiano Mafupi Kuhusu Kenya London


Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha
Mwito kwa Watanzania Kuchacharuka London









Mwito kwa Watanzania kufanya tamasha kama la Wakenya na Waghana London. Mjasiria mali wa Nyorido Fashion atoa ndogo ndogo. Kuh "Kenya in the Park"

Zaidi ingia;Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha



Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..24


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu na kimbilio letu..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Mfalme wa Amani Baba wa Upendo..Utukuzwe Baba wa Rehema..
Unastahili sifa na kuabudiwa daima..
wewe Ndimi Mwenyezi-Mungu..Muumba wa vyote..!
Wewe ni Alfa na Omega..!
Sifa na Utukufu ni wako Jehovah..!

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..!
Asante kwa ulinzi wako wakati wote...
Asante kwa kutuamsha salama na wenye afya tayari kwakuendelea na majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuiona leo hii..
Si kwamba sisi ni wema sana ,si kwamba wazuri mno au ni kwanguvu zetu..
Hapana Mungu wetu ni kwa Neema/Rehema zako tuu sisi kuwa hivi tulivyo..
Jehovah tunakuja mble zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..

Ukatubariki na Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu Baba ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Mfalme wa Amani ukawaponye na kuwagusa na mkono wako wenye nguvu wote wanaopitia magumu/majaribu,shida/tabu..Ukawape neema ya kusimamia Amri,sheria zako na Neno lako nalo likawaweke huru..



Yesu alipokwisha sema hayo, alitazama juu mbinguni, akasema, “Baba, ile saa imefika! Mtukuze Mwanao ili naye Mwana apate kukutukuza. Maana ulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote ili awape uhai wa milele wote hao uliompa. Na uhai wa milele ndio huu: Kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa niifanye. Sasa, Baba, nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuumbwa ulimwengu. “Nimekufanya ujulikane kwa watu wale ulionipa kutoka duniani. Walikuwa watu wako, nawe ukanipa wawe wangu; nao wamelishika neno lako. Sasa wanajua kwamba kila ulichonipa kimetoka kwako. Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa, nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako, na wanaamini kwamba wewe ulinituma. “Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea wale ulionipa, maana ni wako. Yote niliyo nayo ni yako, na yako ni yangu; na utukufu wangu umeonekana katika hao ulionipa. Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja. Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia. Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu. Mimi nimewapa ujumbe wako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu. Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu. Waweke wakfu katika ukweli; neno lako ni ukweli. Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni; na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ili nao pia wafanywe wakfu katika ukweli. “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao. Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma. Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja; mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi. “Baba! Nataka hao ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili wauone utukufu wangu ulionipa; kwa kuwa ulinipenda kabla ya kuumbwa ulimwengu. Baba Mwema! Ulimwengu haukujui, lakini mimi nakujua. Hawa nao wanajua kwamba wewe ulinituma. Nimekufanya ujulikane kwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”




Jehovah ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
tuliyoyanena na tusiyoyanena Mfalme wa Amani unayajua na kutujua sisi zaidi ya tunavyojijua..
Utukuzwe milele..Uabudiwe daima..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa kwakuwa nami..
Mungu aendelee kuwabariki katika yote yampendezayo..
Nawapenda.



1Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena, akawa anaangalia jangwani. 2Alitazama juu akawaona Waisraeli wamepiga kambi, kila kabila mahali pake. Kisha roho ya Mungu ikamjia, 3naye akatamka kauli hii ya kinabii:
Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peori
kauli ya mtu aliyefumbuliwa24:3 aliyefumbuliwa: Au aliyefumbwa, au aonaye vema. macho;
4kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu
mtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu,
mtu anayesujudu na kuona wazi.
5Hema zako zapendeza namna gani enyi watu wa Yakobo;
naam, kambi zenu enyi watu wa Israeli!
6Ni kama mabonde yanayotiririka maji,
kama bustani kandokando ya mto,
kama mishubiri aliyopanda Mwenyezi-Mungu,
kama mierezi kandokando ya maji.
7Watakuwa na hazina ya kutosha ya maji,24:7 Yatapata … kutosha: Kiebrania: Maji yatatiririka kutoka ndoo zake.
mbegu yao itapata maji mengi,
mfalme wao atakuwa mkuu kuliko Agagi,
na ufalme wake utatukuka sana.
8Mungu aliwachukua kutoka Misri,
naye huwapigania kwa nguvu kama nyati.
Atayateketeza mataifa yaliyo adui zao,
atavunjavunja mifupa yao,
atawachoma kwa mishale yake.
9Ataotea na kulala chini kama simba,
nani atathubutu kumwamsha?
Abarikiwe yeyote atakayewabariki nyinyi Waisraeli,
alaaniwe yeyote atakayewalaani.
10Balaki akawaka hasira dhidi ya Balaamu, akakunja mikono kwa ghadhabu na kumwambia, “Nilikuita uwalaani adui zangu, lakini mara hizi zote tatu umewabariki! 11Sasa! Nenda zako. Nilikuwa nimekuahidi kukupa zawadi nyingi, lakini Mwenyezi-Mungu hakukujalia kupata zawadi hizo, amekunyima!”
12Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikuwaambia wajumbe uliowatuma kwangu 13kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
14“Sasa ninarudi kwa watu wangu, lakini kabla sijaondoka, acha nikuambie mambo ambayo watu hao watawatendea watu wako siku zijazo.” 15Basi, Balaamu akatamka kauli hii:
“Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Beori,
kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho,
16kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu,
na mtu ajuaye maarifa ya Mungu Mkuu,
mtu aonaye maono ya Mungu Mwenye Nguvu,
mtu anayesujudu, macho wazi.
17Ninamwona, atakayekuja, lakini baadaye,
namwona, lakini hayuko karibu.
Nyota itatokea kwa wazawa wa Yakobo,
atatokea mfalme miongoni mwa Waisraeli.
Kwa fimbo yake atawachapa viongozi wa Wamoabu
atawaangamiza wazawa wote wa Sethi.
18Edomu itamilikiwa naye,
Seiri itakuwa mali yake,
Israeli itapata ushindi mkubwa.
19Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawala
naye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.”
20Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii:
“Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote,
lakini mwishoni litaangamia kabisa.”
21Kisha Balaamu akawaangalia Wakeni, akatoa kauli hii:
“Makao yenu ni salama, enyi Wakeni,
kama kiota juu kabisa mwambani.
22Lakini mtateketezwa, enyi Wakeni.
Mtachukuliwa mateka na Ashuru mpaka lini?”24:22 aya ya 22 makala ya Kiebrania si dhahiri.
23Tena Balaamu akatoa kauli hii:
“Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo?
24Meli zitafika kutoka Kitimu,
wataishambulia Ashuru na Eberi,
lakini nao pia wataangamia milele.”
25Basi, Balaamu akaondoka, akarudi nyumbani; Balaki pia akaenda zake.


Hesabu24;1-25


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 3 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..23


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Mungu wetu Baba yetu,Baba wa Mbinguni,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...!
Mfalme wa Amani Tunakuja mbele zako tukijinyeyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Jehovah...
Asante kwa wema na fadhili zako Mungu Baba..Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii...
Asante Mungu wetu kwa ulinzi wako wakati wote..
Utukuzwe Mungu wetu,Uabudiwe milele,Unastahili sifa,Unatosha Jehovah..Hakuna kama wewe..
Mungu wa wajane,Baba wa yatima,Baba wa Upendo,Muweza wa yote..Alfa na Omega..!!

Yahweh..!Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah.. nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Mungu wetu utuepushe katika majaribu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...

Mfalme wa Amani tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Ukabariki Kazi za mikono yetu na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Mungu Baba tukatende sawasawa na mapenzi yako..tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kamainavyokupendeza wewe..
Ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na amapenzi yako..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..


Endeleeni kupendana kindugu. Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua. Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao. Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi. Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.” Ndiyo maana tunathubutu kusema: “Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?” Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao. Yesu Kristo ni yuleyule jana, leo na milele. Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata. Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi hawana haki ya kula vitu vyake. Kuhani mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa tambiko kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi. Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji. Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu tambiko ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa kwa midomo inayoliungama jina lake. Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu. Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu. Mtuombee na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima. Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi Waebrania 13:1-19

Tazama wenye shida/tabu,wagonjwa na wenyedhiki,waliokatika vifungo vya yule mwovu..Mungu wetu tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye  kiroho na kimwili pia..ukawape neema ya kusimamia neno lako na kufuata Amri Sheria zako wakapate kujua jinsi wewe ulivyo na wakawe huru..
Sifa na utukufu tunakurudishia wewe mwenyezi-Mungu


Mungu amemfufua katika wafu Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele. Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.


Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa Mungu awe nanyi daima..
Nawapenda.




1Balaamu akamwambia Balaki, “Nijengee madhabahu saba hapa kisha uniletee fahali saba na kondoo madume saba.”2Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema. Basi, wakatoa juu ya kila madhabahu kafara fahali mmoja na kondoo dume mmoja.3Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima. 4Mungu akakutana naye. Balaamu akamwambia, “Nimetayarisha madhabahu saba na kutoa kafara fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.”
5Mwenyezi-Mungu akampa Balaamu maneno atakayosema na kumwambia arudi kwa Balaki. 6Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama palepale karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, pamoja na maofisa wote wa Moabu.
7Balaamu akamtolea Balaki kauli yake, akasema,
“Balaki amenileta hapa kutoka Aramu,
naam, mfalme wa Moabu amenileta kutoka milima ya mashariki.
‘Njoo uwalaani watu wa Yakobo kwa ajili yangu,
naam, njoo uwalaumu Waisraeli!’
8Nitamlaanije mtu ambaye Mungu hakumlaani?
Nitawalaumuje watu ambao Mwenyezi-Mungu hakuwalaumu?
9Kutoka vilele vya majabali nawaona;
kutoka juu ya milima nawachungulia.
Hilo taifa likaalo peke yake,
lisilojiona kuwa sawa na mataifa mengine.
10Nani awezaye kuwahesabu wingi wa watu wa Yakobo,
au kukisia umati wa Waisraeli?
Nife kifo cha waadilifu,
mwisho wangu na uwe kama wao.”
11Hapo, Balaki akamwambia Balaamu, “Umenifanyia nini? Nimekuleta hapa uwalaani adui zangu, lakini badala yake umewabariki!” 12Balaamu akamwambia Balaki, “Sina budi kusema maneno aliyonipa Mwenyezi-Mungu.”
Unabii wa pili wa Balaamu
13Baadaye, Balaki akamwambia Balaamu, “Twende mahali pengine ambapo utaweza kuwaona; hata hivyo utaona tu sehemu yao, hutaweza kuwaona wote. Kisha uwalaani kutoka huko kwa niaba yangu.” 14Basi, Balaki akamchukua Balaamu kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Hapo akajenga madhabahu saba na kutoa juu ya kila madhabahu kafara ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.
15Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende kule ngambo kukutana na Mwenyezi-Mungu.” 16Mwenyezi-Mungu akakutana na Balaamu, akampa maneno atakayosema, na kumwambia arudi kwa Balaki. 17Basi, Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na maofisa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza, “Mwenyezi-Mungu amekuambia nini?” 18Hapo, Balaamu akamtolea Balaki kauli yake:
“Inuka, Balaki, usikie,
nisikilize ewe mwana wa Sipori.
19Mungu si mtu, aseme uongo,
wala si binadamu, abadili nia yake!
Je, ataahidi kitu na asikifanye,
au kusema kitu asikitimize?
20Tazama, nimepewa amri ya kubariki,
naye amebariki wala siwezi kuitangua.
21Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo,
wala udhia kwa hao wana wa Israeli.
Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao,
Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao,
yeye huzipokea sifa zao za kifalme.
22Mungu aliyewachukua kutoka Misri,
huwapigania kwa nguvu kama za nyati.23:22 kwa nguvu … nyati: Au lina nguvu kama ya nyati.
23Hakika ulozi hauwezi kuwapinga watu wa Yakobo,
wala uchawi dhidi ya watu wa Israeli.
Sasa kuhusu Israeli, watu watasema,
‘Tazameni maajabu aliyotenda Mungu!’
24Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike,
wanasimama kama simba dume.
Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake,
na kunywa damu ya mawindo.”
25Ndipo Balaki akamwambia Balaamu, “Basi, usiwalaani wala usiwabariki kabisa!” 26Lakini Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikukuambia kwamba anachosema Mwenyezi-Mungu ndicho ninachopaswa kufanya?”
27Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo; nitakupeleka mahali pengine. Labda Mungu atakubali uwalaani watu hao kutoka huko kwa ajili yangu.” 28Basi, Balaki akamchukua Balaamu mpaka kwenye kilele cha Mlima Peori, ambapo mtu akisimama anaona jangwani. 29Balaamu akamwambia Balaki, “Nijengee madhabahu saba hapa, unitayarishie fahali saba na kondoo madume saba.”30Balaki akafanya kama alivyoambiwa na Balaamu, kisha akatoa juu ya kila madhabahu kafara fahali mmoja na kondoo dume mmoja.

Hesabu23;1-30


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.