Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Mungu mwenye nguvu,Mungu wa wa walio hai,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mfalme wa amani,Muweza wa yote,Alfa na Omega..
Utukuzwe ee Mungu wetu, Uabudiwe Baba wa Mbinguni,Usifiwe Yahweh,Uhimidiwe Jehovah,Neema yako yatutosha Mungu wetu
Hakuna kama wewe Yahweh,Hakuna lisilowezekana mbele zako Jehovah,Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu..!!
“Ewe Mwenyezi-Mungu, ni nani kati ya miungu anayelingana nawe? Ni nani aliye kama wewe uliye mtakatifu mkuu, utishaye kwa matendo matukufu, unayetenda mambo ya ajabu?
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu..
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..!!
Kulitokea ubishi kati ya hao mitume kuhusu nani miongoni mwao anayefikiriwa kuwa mkuu kuliko wengine. Yesu akawaambia, “Wafalme wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, nao huitwa wafadhili wa watu. Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi. Kwa maana, ni nani aliye mkuu: Yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi. “Nyinyi ndio mliobaki nami wakati wote wa majaribu yangu; na, kama vile Baba yangu alivyonikabidhi ufalme, vivyo hivyo nami ninawakabidhi nyinyi ufalme. Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu na kuketi katika viti vya enzi kuyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote
Baba wa mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Jehovah utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.
“Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetani alitaka kuwapepeta nyinyi kama mtu anavyopepeta ngano. Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako.” Naye Petro akamjibu, “Bwana, mimi niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani, na hata kufa.” Yesu akamjibu, “Nakuambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikana mara tatu.”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah tukatende sawasawa na mapenzi yako
Mungu wetu tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhutaji..
Baba wa Mbinguni tunaomba tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Jehovah ukatupe kama inavyokupendeza wewe..
Kisha, Yesu akawauliza wanafunzi wake, “Wakati nilipowatuma bila mfuko wa fedha wala mkoba wala viatu, mlitindikiwa chochote?” Wakajibu, “La.” Naye akawaambia, “Lakini sasa, yule aliye na mfuko wa fedha auchukue; na aliye na mkoba, hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga, auze koti lake anunue mmoja. Maana nawaambieni, haya maneno ya Maandiko Matakatifu: ‘Aliwekwa kundi moja na wahalifu,’ ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusu yanafikia ukamilifu wake.” Nao wakasema, “Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili.” Naye akasema, “Basi!”
Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Jehovah tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwavyote tunavyovimiliki
Mungu wetu tunaomba tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Yahweh ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Jehovah ukavifunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Jehovah tuaomba ukatamalaki na kutuatamia,Mungu wetu tukawe salama moyoni,Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya rohoni na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu,Upendo ukadumu kati yetu,hekima,busara na tukapate kutambua/kujitambua,Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
yahweh ukaonekane popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni..
Jehovah tuka nene yaliyo yako,Mungu wetu tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..
Ukatufanye chombo chema Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlima wa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata. Alipofika huko akawaambia, “Salini, msije mkaingia katika kishawishi.” Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe, akapiga magoti, akasali: “Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.” Hapo, malaika kutoka mbinguni akamtokea ili kumtia moyo. Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini. Baada ya kusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakuta wamelala, kwani walikuwa na huzuni. Akawaambia, “Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi.”
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaponye wagonjwa Yahweh ukawape uvumili na imani wanaowauguza,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu wenye shida/tabu Jehovah tunaomba ukawavushe salama wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Yahweh ukawaokoe walio katika vifungo vya yule mwovu
Mungu wetu ukawatendee waliomagerezani pasipo na hatia Baba wa Mbinguni haki ikatendeke
Yahweh tunaomba ukawalishe wenye njaa Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki mashamba/vyanzo vyao..
Jehovah tunaomba ukawe tumaini kwa waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu na mashaka Mungu wetu ukawe mfariji kwa wafiwa Yahweh ukawape nguvu na uvumilivu ..
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe wote waliokwenda kinyume nawe na wakatubu na kukurudia wewe...
Yahweh ukawarudishe waliopotea/walioanguka wakasimame tena na kufuata njia zako..Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea na kusimamia Neno lako nalo liwaweke huru..
Neema yako na mwanga wako ukaangaze katika maisha yao
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika shida zao
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Yahweh ukapokee sala/maombi yetu Baba wa Mbinguni ukawatendee sasawa na mapenzi yako..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na utukufu hata Milele..
Amina..!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwa kuwa nami
Mungu andelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi daima..
Nawapenda.
|