Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana.. Tumshukuru katika yote..
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu.. Utukuzwe ee Baba wa Mbinguni,Usifiwe Jehovah,Uhimidiwe Yahweh, Uabudiwe Mungu wetu,Unatosha Yahweh,Neema yako yatutosha Jehovah Jireh,Jehovah Nissi,Jehovah Raah,Jehovah Rapha,Jehovah Shammah,Jehovah Shalom,Emunueli-Mungu pamoja nasi..!!
Sasa, Wafilisti walikusanya majeshi yao huko Soko, mji ulioko katika Yuda, tayari kwa vita. Walipiga kambi katika sehemu moja iitwayo Efes-damimu kati ya Soko na Azeka. Shauli pamoja na Waisraeli walikusanyika, na kupiga kambi katika bonde la Ela. Wakajipanga tayari kupigana na Wafilisti. Wafilisti walisimama mlimani upande mmoja na Waisraeli walisimama mlimani upande mwingine, katikati yao kulikuwa na bonde. Kutoka kwenye kambi ya Wafilisti, alijitokeza shujaa mmoja aitwaye Goliathi, mwenyeji wa mji wa Gathi. Urefu wake ulikaribia mita tatu. Kichwani alivaa kofia ya shaba, na deraya ya shaba kifuani yenye uzito wa kilo 57. Miguu yake pia ilikuwa na kinga ya shaba na mabegani pake alibeba mkuki wa shaba. Mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumanguo, na chembe cha mkuki huo, kilikuwa na uzito wa kilo saba. Ngao yake ilibebwa na mtu mwingine aliyemtangulia. Goliathi alisimama na kuwapigia kelele wanajeshi wa Israeli, akisema, “Mnafanya nini hapo? Je, mmekuja kupigana vita? Mimi ni Mfilisti, nyinyi ni watumwa wa Shauli. Chagueni mtu mmoja wenu aje kupigana nami. Akinishinda na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu. Lakini nikimshinda na kumuua basi, nyinyi mtakuwa watumwa wetu na kututumikia.” Kisha Mfilisti huyo aliendelea kusema kwa majivuno, “Nawataka wanajeshi wa Israeli siku hii kumtoa mtu mmoja aje kupigana nami.” Shauli pamoja na wanajeshi wote wa Israeli walipoyasikia maneno hayo ya Mfilisti huyo, walifadhaika na kuogopa sana.
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni.. Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua.. Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea.. Mfalme wa amani tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh tunaomba utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote.. Mungu wetu tunaomba ututakase miili yetyu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Jehovah tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika ufanyaji/utendaji Mungu wetu tukatende sawasawa na mapenzi yako.. Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji.. Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu Yahweh tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe..
Mungu Baba tunaomba ukabariki maisha yetu Yahweh tunaomba ukatamalaki na kutuatamia,Mungu wetu tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki,Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka,Yahweh ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetuYesu Kristo vyote tunavyoenda kugusa/kutumia.. Mungu wetu ukatupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Yahweh tukanene yaliyo yako,Mungu wetu ukaonekane popote tupitapo Yahweh na ijulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni.. Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu,Baba wa Mbinguni upendo ukadumu kati yetu,tukawe salama moyoni Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya kuona,masikio ya kisikia sauti yako na kuitii.. Ukatufanye chombo chema Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Daudi alikuwa mtoto wa Yese, Mwefrathi kutoka Bethlehemu katika Yuda. Yese alikuwa na watoto wanane wa kiume. Wakati Shauli alipokuwa mfalme, yeye alikuwa tayari mzee, mtu mwenye umri mkubwa. Wana wakubwa watatu wa Yese, Eliabu mzaliwa wa kwanza, Abinadabu aliyefuata na Shama wa tatu, walikuwa wamekwenda pamoja na Shauli vitani. Daudi alikuwa ndiye mdogo wa wote. Wale watoto watatu wakubwa walikuwa wamekwenda na Shauli. Ingawa Daudi mara kwa mara alikwenda kwa Shauli, alirudi nyumbani Bethlehemu kuchunga kondoo wa baba yake. Kwa muda wa siku arubaini, asubuhi na jioni, yule Mfilisti Goliathi alijitokeza hadharani, akasimama na kuwakejeli wanajeshi wa Israeli. Siku moja, Yese alimwambia mwanawe Daudi, “Wapelekee kaka zako bisi kilo kumi na mikate kumi. Wapelekee haraka huko kambini. Na yule kamanda wao wa kikosi cha wanajeshi elfu mpelekee jibini hizi kumi. Kawaangalie kaka zako kama wanaendelea vizuri na kisha uniletee habari zao.” Wakati huo mfalme Shauli, kaka zake Daudi na wanajeshi wote wa Israeli walikuwa kwenye bonde la Ela, wanapigana na Wafilisti. Kesho yake, Daudi aliamka asubuhi na mapema, na kondoo akamwachia mchungaji. Alichukua chakula na kwenda kama alivyoagizwa na baba yake Yese. Alipofika kwenye kambi ya Waisraeli, aliwakuta wanajipanga kwenye sehemu yao ya vita na wanapiga kelele za vita. Majeshi ya Waisraeli na ya Wafilisti walijipanga tayari kupigana vita, majeshi yakiwa yanakabiliana ana kwa ana. Daudi alimkabidhi chakula mtu aliyetunza mizigo, akawakimbilia wanajeshi, akaenda kwa kaka zake na kuwasalimia. Alipokuwa anaongea nao, Goliathi yule shujaa wa Wafilisti kutoka Gathi alijitokeza mbele ya wanajeshi wa Israeli kama alivyozoea. Naye Daudi alimsikiliza vizuri sana. Waisraeli walipomwona Goliathi, walimkimbia, na kumwogopa sana. Waliambiana, “Je, mmemwona yule mtu aliyejitokeza? Ama kweli, amejitokeza kuwakejeli Waisraeli. Mfalme Shauli atampa mtu yeyote atakayemuua mtu huyo utajiri mwingi. Zaidi ya yote, atamwoza binti yake. Tena, watu wa jamaa ya baba yake watakuwa huru, hawatalipa kodi.” Daudi akawauliza wale waliokuwa karibu naye, “Je, mtu atakayemuua Mfilisti huyu na kuikomboa Israeli kutokana na aibu hii atafanyiwa nini? Ni nani huyu Mfilisti, mtu asiyetahiriwa, anayethubutu kuyatukana majeshi ya Mungu aliye hai?” Watu wakamwambia kama walivyokuwa wamesema hapo awali juu ya mtu atakayemuua Goliathi. Lakini Eliabu, kaka mkubwa wa Daudi alipomsikia Daudi akiongea na watu, alimkasirikia Daudi, akasema, “Kwa nini umekuja? Je, wale kondoo wachache umemwachia nani kule nyikani? Najua ujeuri wako na uovu wako. Umekuja tu kutazama vita.” Daudi akamjibu, “Sasa nimefanya nini? Je, siwezi kuuliza swali tu?” Daudi akamgeukia mtu mwingine akamwuliza swali hilohilo; na kila alipouliza, alipata jibu lilelile. Watu fulani ambao walimsikia Daudi alivyosema, walikwenda kumwambia Shauli. Naye Shauli akaagiza aitwe. Daudi akamwambia Shauli, “Mtu yeyote asitishike moyoni mwake kutokana na Mfilisti huyu. Mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana naye.” Shauli akamwambia Daudi, “Wewe huwezi kwenda kupigana na Mfilisti yule. Wewe ni kijana tu, lakini mtu huyo amekuwa vitani tangu ujana wake.” Daudi akasema, “Mimi mtumishi wako nimezoea kuchunga kondoo wa baba yangu. Kila wakati simba au dubu akija na kukamata mwanakondoo mimi humfuata na kumshambulia, nikamwokoa mwanakondoo kinywani mwake. Kama simba au dubu akinishambulia, mimi humshika ndevu zake, nikamwangusha na kumuua. Mimi mtumishi wako nimekwisha ua simba wengi na dubu wengi. Sasa, hata yule Mfilisti asiyetahiriwa, ambaye ameyatukana majeshi ya Mungu aliye hai, atakuwa kama hao. Mwenyezi-Mungu ambaye ameniokoa makuchani mwa simba na dubu, ataniokoa kutoka kwa Mfilisti huyu.” Shauli akamwambia, “Nenda; naye Mwenyezi-Mungu awe pamoja nawe.” Shauli akamvisha Daudi mavazi yake ya kivita, akamvika kofia yake ya shaba kichwani na koti lake la kujikinga kifua. Daudi akajifunga upanga wa Shauli, akajaribu kutembea; lakini akashindwa kwa kuwa hakuyazoea mavazi kama hayo. Akamwambia Shauli, “Siwezi kwenda vitani nikiwa nimevaa mavazi haya, kwani mimi sijayazoea.” Kwa hiyo, akayavua. Daudi akachukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe matano mazuri kutoka kwenye kijito, akayatia katika mfuko wake wa mchungaji. Kombeo lake likiwa tayari mkononi mwake, akaanza kumwendea Goliathi Mfilisti.
Mungu wetu tunarudisha sifa na utukufu kwako.. Yahweh tunakushukuru kwa matendo yako makuu.. Mungu wetu tulikulilia nawe ukatufuta machozi Baba wa Mbinguni tulikuomba nawe ukajibu... Mfalme wa Amani tulikuita nawe ukaja.. Jehovah tuliomba nawe ukasikia na ukatutendea Uponyaji wako ni furaha na tunazidi kutii na kukutukuza daima Uponyaji wako umezidi kutufunulia na kutupa shauku zaidi ya kukutafuta wewe.. Mungu wetu tumeuona mkono wako,Baba wa Mbinguni umetutendea Yahweh hakuna kama wewe,Mungu wetu unatosha..!!
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawatendee na wengine wanaokuomba kwa bidii na imani Yahweh ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu Mungu wetu ukawaponye na kuwaweka huru,Mfalme wa amani ukatawale maisha yao,Jehovah ukaonekane katika mapito yao.. Mungu wetu ukawasamehe waliokwenda kinyume nawe... Baba wa Mbinguni tunaomba ukawape neema ya kujiombea.. Yahweh wafuate njia zako nazo ziwaweke huru.. Mungu wetu ukasikie kilio chao na ukawafute machozi watoto wako Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu Yahweh ukawatendee sawasawa na mapenzi yako.. Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.. Amina..!!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami Mungu Baba akaonekane katika maisha yenu,upendo wenu si bure Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea kama inavyompendeza yeye Nawapenda. |