Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana...
Tunamshukuru Mungu wetu kwa kutupa neema ya kuweza
kupitia kitabu cha "Wafalme" Asante sana Mungu wetu kwa nafasi hii
Kwa imani yote tuliyojifunza kupitia kitabu hiki yatakuwa ndani yetu
pia na faida kwetu na kwa wengine....
Leo tunaanza Kitabu cha "1Mambo ya Nyakati"Mungu wetu tunaomba
tunapoanza kusoma Neno lako kupitia kitabu hiki,ukatupe macho
ya rohoni,masikio,uelewa na kutambua..
Mungu wetu tukasome na kuhifadhi pia elimu hii ikawafae na wengine
Ee Baba tunaomba ukatuongoze...!!
Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe. Sensa hiyo ilikuwa mara ya kwanza, wakati Kurenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria. Basi, wote waliohusika walikwenda kuhesabiwa kila mtu katika mji wake. Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi. Alikwenda kuhesabiwa pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mjamzito. Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia, akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Tunakushukuru Mungu wetu kwa siku hii pia
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali
cha kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana,wala si kwamba sisi
ni wazuri mno,si kwa nguvu zetu wala utashi wetu
Si kwa uwezo wala akili zetu sisi kuwa hivi tulivyo
Ni kwa neema/rehema zako ni kwa mapenzi yako Mungu wetu
Sifa na Utukufu tunakurudishia Baba wa Mbinguni...!!
Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao. Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana. Malaika akawaambia, “Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kubwa itakayowapata watu wote. Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana. Na hiki kitakuwa kitambulisho kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini.” Mara kundi kubwa la jeshi la mbinguni likajiunga na huyo malaika, wakamsifu Mungu wakisema: “Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu anaowafadhili!”
Tazama jana imepita Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho
ni siku nyingine Jehovah
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuokoe na yule mwovu
na kazi zake zote
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Mungu wetu utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu
Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate
kupona...
Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: “Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha.” Basi, wakaenda mbio, wakamkuta Maria na Yosefu na yule mtoto mchanga amelazwa horini. Hao wachungaji walipomwona mtoto huyo wakawajulisha wote habari waliyokuwa wamesikia juu yake. Wote waliosikia hayo walishangaa juu ya habari walizoambiwa na wachungaji. Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake. Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni ukatupe kama inavyokupendeza wewe...
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu
familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Baba wa Mbinguni tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote
tunavyovimiliki
Jehovah tunaomba ukatamalaki na kutuatamia
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana
wetu Yesu Kristo..
Mungu wetu tukawe salama rohoni
Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya kuona na masikio ya
kusikia sauti yako na kuitii
Jehovah ukatupe neema ya kufuata njia zako Mungu wetu tukasimamie
Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Yahweh ukatupe akili ya kutamnbua mema na mabaya
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu
Neema yako na Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
mkono wako wenye nguvu ukatuguse ee Mungu wetu
Ukatufanye chombo chema Baba wa Mbinguni nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi
Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
Tazama wenye shida/tabu Mungu wetu
Tazama watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba ukamguse kila mmoja na mahitaji yake
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Baba wa Mbinguni ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Mungu wetu tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia
zako Mungu wetu ukawape macho ya rohoni
Yahweh tunaomba ukasikie kulia kwao Mungu wetu tunaomba
ukawafute machozi yao
Baba wa Mbinguni tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukapokee sala/maombi yetu Jehovah ukawatendee
sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwa kuwanami/kunisoma
Baba wa Mbinguni akawabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye..
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukawe nanyi Daima...
Nawapenda. |