|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana.. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kupitia kitabu cha "WIMBO ULIO BORA" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika na kutupa mwanga/kuelewa kwenye kitabu hiki...
Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha"ISAYA"tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake... Ee Mungu tunaomba ukatuongoze...!! Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Ndipo wakapatana hivi: “Hatutapata kisingizio chochote cha kumshtaki Danieli isipokuwa kama kisingizio hicho kitakuwa kinahusu sheria ya Mungu wake.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Basi, hao wakuu na maliwali kwa pamoja, wakamwendea mfalme na kumwambia, “Uishi ee mfalme Dario!
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Sisi wakuu uliotuweka, wasimamizi, maliwali, washauri na wakuu wa mikoa, sote tumepatana kuwa inafaa, ee mfalme, utoe amri na kuhakikisha inafuatwa kikamilifu. Amuru kwamba kwa muda wa siku thelathini kusiwe na mtu yeyote atakayeruhusiwa kuomba kitu chochote kwa mungu yeyote au kwa mtu yeyote, isipokuwa kutoka kwako wewe, ewe mfalme. Mtu yeyote atakayevunja sheria hii na atupwe katika pango la simba.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
1 Maono aliyoyaona Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na mji wa Yerusalemu, nyakati za utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.
Mungu awakemea watu wake
2Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Sikilizeni enyi mbingu,
tega sikio ee dunia.
Mimi nimewalea wanangu wakakua,
lakini sasa wameniasi!
3Ngombe humfahamu mwenyewe,
punda hujua kibanda cha bwana wake;
lakini Waisraeli hawajui,
watu wangu, hawaelewi!”
4Ole wako wewe taifa lenye dhambi,
watu waliolemewa na uovu,
wazawa wa wenye kutenda maovu,
watu waishio kwa udanganyifu!
Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu,
mmemdharau Mtakatifu wa Israeli,
mmefarakana naye na kurudi nyuma.
5Kwa nini huachi uasi wako?
Mbona wataka kuadhibiwa bado?
Kichwa chote ni majeraha matupu,
na moyo wote unaugua!
6Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu,
umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu,
navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.
7Nchi yenu imeharibiwa kabisa;
miji yenu imeteketezwa kwa moto.
Wageni wananyakua nchi yenu mkiona kwa macho,
imeharibiwa kama uharibifu wa Sodoma.1:7 Sodoma: Kiebrania: Wageni, Taz Kumb 29:33; Yer 49:18.
8Mji Siyoni umeachwa kama kibanda shambani,
kama kitalu katika shamba la matango,
kama mji uliozingirwa.
9Mwenyezi-Mungu wa majeshi asingalituachia wachache,
tungalikwisha kuwa kama watu wa Sodoma,
tungalikuwa hali ileile ya Gomora.1:9 Gomora: Taz Mwa 19:24; Roma 9:29.
10Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu
enyi watawala waovu kama wa Sodoma!
Sikilizeni mafunzo ya Mungu wetu
enyi watu waovu kama wa Gomora!
11 1:11-14 Taz Amo 5:21-22 Mwenyezi-Mungu asema hivi;
“Wingi wa tambiko zenu ni kitu gani kwangu?
Nimezichoka sadaka zenu za kondoo wa kuteketezwa
na mafuta ya wanyama wenu wanono.
Sipendezwi na damu ya fahali,
wala ya wanakondoo, wala ya beberu.
12Mnapokuja mbele yangu kuniabudu
nani aliyewataka mkanyagekanyage nyua zangu?
13Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana;
ubani ni chukizo kwangu.
Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya,
Sabato na mikutano mikubwa ya ibada;
sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.
14Sikukuu zenu za mwezi mpya na nyinginezo
moyo wangu wazichukia.
Zimekuwa mzigo mzito kwangu,
nami nimechoka kuzivumilia.
15“Mnapoinua mikono yenu kuomba
nitauficha uso wangu nisiwaone.
Hata mkiomba kwa wingi sitawasikia,
maana mikono yenu imejaa damu.
16Jiosheni, jitakaseni;
ondoeni uovu wa matendo yenu mbele yangu.
Acheni kutenda maovu,
17jifunzeni kutenda mema.
Tendeni haki,
ondoeni udhalimu,
walindeni yatima,
teteeni haki za wajane.”
18Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Njoni, basi, tuhojiane.
Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi,
mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji;
madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu,
mtakuwa weupe kama sufu.
19Mkiwa tayari kunitii,
mtakula mazao mema ya nchi.
20Lakini mkikaidi na kuniasi,
mtaangamizwa kwa upanga.
Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
Mji uliojaa dhambi
21Jinsi gani mji uliokuwa mwaminifu
sasa umegeuka kuwa kahaba!
Wakati mmoja haki ilitawala humo,
lakini sasa umejaa wauaji.
22Fedha yenu imekuwa takataka;
divai yenu imechanganyika na maji.
23Viongozi wako ni waasi;
wanashirikiana na wezi.
Kila mmoja anapenda hongo,
na kukimbilia zawadi.
Hawawatetei yatima,
haki za wajane si kitu kwao.
24Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu,
Mwenye Nguvu wa Israeli:
“Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu,
nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.
25Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu;
nitayeyusha uchafu wenu kabisa,
na kuondoa takataka yenu yote.
26Nitawapeni waamuzi wenu kama kwanza
na washauri wenu kama pale awali.
Ndipo Yerusalemu utakapoitwa ‘Mji wa Uadilifu’
utaitwa ‘Mji Mwaminifu’”
27Mji Siyoni utakombolewa kwa haki,
uadilifu utawaokoa watakaotubu humo.
28Lakini waasi na wenye dhambi
wote wataangamizwa pamoja;
wanaomwacha Mwenyezi-Mungu watateketezwa.
29Mtaionea aibu hiyo mialoni mliyoipenda sana;
mtafadhaika kwa sababu ya bustani mlizofurahia.
30Mtakuwa kama mwaloni unaonyauka majani;
kama shamba lisilo na maji.
31Wenye nguvu watakuwa kama majani makavu,
matendo yao yatakuwa kama cheche za moto.
Watateketea pamoja na matendo yao,
wala hapatakuwa na mtu wa kuwaokoa.
Isaya1;1-31
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.