Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 3 May 2011

Waswahili wa Holland na Qeen Day!!!!!!!!


































 Waswahili wa Holland wakisherekea Qeen day.Hii ni Siku muhimu kwa watu wa Holland,Waswahili wa huko nao wakaona vyema kujumuika na wenyeji wao.Tunawatakia Maisha mema na Ushirikiano mzuri.
Je wewe msomaji  huko unapoishi,  Unapenda kuungana na wenyeji wako katika siku zao muhimu?Karibuni sana  Waswahili wote popote mlipo,Mnaweza kutuma picha /matukio yenu.

Friday, 29 April 2011

Waswahili na Royal Wedding





















Wazazi/Walezi na Watoto wanaosoma Henley Green Primary School,Coventry,UK.Jana walijumuika pamoja na Walimu wao kwa Kusheherekea Royal Wedding.Wengi wao kama si wote waliokwenye picha hizi wanazungumza Kiswahili,Ni Waswahili wa Tanzani,Kenya,Burundi,Rwanda na Congo. kama uonavyo Kanga ,Vikoi,Mikeka vilitandikwa chini Waswahili wakajiachi.

Swahili na Waswahili inawatakia mapumziko mema na Ndoa njema kwa maharusi.

Wednesday, 27 April 2011

Mpendwa da Mija!!!!!!!!

YouTube



Sisi sote ni kazi ya Mikono yake Mungu!

Hata na wewe Mpendwa da Mija ni kazi ya Mikono yake Pia. Mimi na Familiya yangu tunakutakia kila la kheri na baraka kwa siku yako hii ya Kuzaliwa na Siku zoteeeee!

Mija kwetu ni zaidi ya Rafiki!!!!!Tunakupenda na kukuthamini maishani! SEBHA AKJHIWE SANAAAA!
Pata kibao hicho!.
Karibuni sana wapendwa Tuselebuke na da Mija!!!!!!!!!!!
© 2011 YouTube, LLC
901 Cherry Ave, San Bruno, CA 94066

Monday, 25 April 2011

Wazazi wa sasa na Malezi!!!!!!!


Katika pitapita zangu nimekutana na malezi tofauti ya Watoto.Hasa ya kule Nyumbani Afrika/Tanzania na Wanaoishi nje ya Nchi.Watoto wa Nyumbani wengi wao bado wanaheshima kwa wakubwa wote awe mzazi au jilani,kwa Mgeni au Mwenyeji,Akufahamu/kukujua au Asikufahamu/Kukujua.Unyenyekevu na Usikivu. na mengine mengi.
Watoto wa waishio nje ya Afrika/Ng'ambo Wengi wao ni wabinafsi, wanauthubutu wa kukujibu lolote analoweza,anaweza asikusalimie,hawana karibu wala heshima kwa wakubwa,wanamaamuzi zaidi na matakwa yao,Akisema sitaki na hataki,Na  baadhi ya wazazi wao wanawasilkiliza zaidi, Hata  hawana Aibu kwa matendo ya watoto wala Hofu.
Je Msomaji wewe unamawazo gani katika haya,je ni Mazingira,Maendeleo,Malezi ya kisomi au ni nini kwa hawa wa Nje?.
Na jee hawa wa Nyumbani ni Waoga,Hofu,Kutojiamini au Washamba na wanapitwa na wakati?
Karibuni sana  kwa Kuelimishana na Kufundishana .