Saturday, 11 June 2011
Wednesday, 8 June 2011
Wanawake na Urembo!!!!!!!!
Haya wapendwa Urembo wakati mwingine unataka Moyo! Kama unavyoona kwenye picha.
Wewe mwanamke/dada unapenda kujiremba na unapendelea nini kuongezea Urembo wako?
Wewe baba/kaka unapenda wanawake/kina dada wanaojiremba na unapenda nini waongezee katika Urembo wao?.
Na jee kwenye Picha hizo nini kimekuvutia na nini Kimekuchukiza?.
Kwa wanaopenda kujiremba, Wanajiremba ili iweje? Ni kujiweka nadhifu,kumfurahisha mpenzi,kujipenda au.......
Na wasiopenda kujiremba, Nini sababu, Nikujiamni, kutojipenda,wapenzi wao hawapendi,kuona Aibu au.....
Karibuni sana Waungwana kwa kuelimishana.
Sunday, 5 June 2011
Mtoto Wetu Leo ni Frank- Jayden!!!!!!!!!!!!!!!!
Hapa anawaza leo nianze na Mchezo upi au nikacheze wapi Sijui?
Nimekuja kunywa maji tuu,Wao wameshanibana nisiende tena kucheza je hii ni haki jamani?
Nimeshindwa kutoka tena,ahhh ngoja nioge zangu tuu!!!!!
Sasa watajuta kunifungia ndani ,mimi naungana na huyu ni kelele tuu mpaka kieleweke!!!!!!
Wakaona wanitoe kidogo hata kwa Mangi nipate walau Soda!!!!!!!
Hapa sasa mambo poa watu wangu, Asanteni kwa Ofa baba na mama!!!!!!!!
Ngoja nikatafute Elimu , Eti yule babu wanaemuita sijui NYERERE [R.I.P] Nimeambiwa alisema Elimu ni Uti wa Mgongo,Sasa sijui kama nikweli au maneno tuu.
Waungwana kila Mtoto anavituko vyake,Hata wewe kwenye Utoto wako ulipitia mambo mengi sana mpaka kufikia hapo ulipo.Katika hayo ya Mtoto wetu Frank-Jayden, Umeguswa/kumbushwa na nini katika Maisha ya Utoto?. Karibuni sana kwa Ushauri na kuelimishana katika malezi ya Watoto wetu!!!!!!!

Wednesday, 1 June 2011
Mapenzi/Mahusiano ya Jinsia Moja!!!!!!
Kumekuwa na Ongezeko la Mahusiano ya kimapenzi ya Jinsia Moja, Mpaka kutaka /kufunga Ndoa za jinsia Moja.Kuna baadhi ya Nchi wanapinga mpaka kutaka kuwadhuru au kuwaua kabisa.Na kunawanaoandamana kwa kupinga Mauaji hayo, Nakutaka wapewe haki zao za Kuoana au Kuendeleza Mapenzi/Mahusiano yao ya Jinsia Moja.
Je wewe Mpenzi msomaji unamawazo/mchango gani katika hili? Karibuni sana Waungwana!!!!!!!
Je wewe Mpenzi msomaji unamawazo/mchango gani katika hili? Karibuni sana Waungwana!!!!!!!
Tuesday, 31 May 2011
Siku kama ya Leo dada Upendo Penza Alizaliwa!!!!!!!!
Dada/Mdogo wetu Upendo[Mwana Penza].Siku kama ya leo alizaliwa na kuongeza idadi ya watoto wa Familia ya Bibi na Bwana J,Penza.Pia idadi ya Wajukuu wa Penza.Upendo ana Upendo na Mtu wa Vichekesho na Utani mwingi sana,Pia ana huruma na niwakujitoa sana kwa kila jambo,Liwe la Familia,Marafiki na Majirani. Kama mwanafamilia ninakuwa na wakati mzuri sana kuwa nae popote, Hasa kwenye mikusanyiko ya kifamilia,Hata ikiwa ya majonzi basi baada ya muda kidogo mtacheka tuu.
Upendo, Tunakutakia kila la kheri na baraka katika maisha yako na uwe na wakati mzuri leo na siku zote.
Je mpenzi msomaji eti jina linaendana na Matendo ya mtu?kama vile ukimpatia mtoto jina la Shida na kweli Shida zitamuandama? au Imani za Waswahili/Watu?.

Saturday, 28 May 2011
Wednesday, 25 May 2011
Je Utoto wako Ulipitia huku???.
Kunamambo mengi sana watu hupitia katika safari ya Maisha ya Utoto mpaka Ukubwani.Kama Udokozi wa mboga,pesa,Sukari.Pia Kujaribu kuvuta Sigara,Bangi.Utoro shuleni,Ugomvi/Ubabe,Matusi na mengi mabaya ambayo hayapendeezi katika jamii.Je wewe ulikuwa katika kundi lipi katika haya na je ulibadilika mwenyewe au kwa msaada wa Wazazi/walezi?. Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana.
Subscribe to:
Posts (Atom)