Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 15 August 2011

Waswahili wa Mji wa Cork,Ireland na Futari ya Pamoja!!!!!

                         Mji wa Cork katika picha.
     Wanawake wakipika na kina baba wakijiandaa kupokea wageni.
           Waandazi/waandaaji wakiwa tayari.
              Waswahili hawa nao walikuwepo.
         Watoto wa kiswahili wametulia.
   Shekhe akisisitiza Upendo na Umoja kwa Waswahili.
     Waswahili wakisaidiana ili mambo yawe sawa.
         Kina mama na kina kaka wakiendelea na maandalizi.
 Wakiendelea na Futari.
         
  Kina mama wakishughulika.
    Lete Uji hapa!
    Vipi mko sawa!
    Baada ya kumaliza msosi.
   Wakisikiliza maongezi.
    Watu wa karibu baada ya wageni kuondaka wakijipongeza!
                                      Maalim akitoa Shukrani kwa wote waliofika na wasiofika,Mungu awabariki sana na kuwaongezea kila lililo jema na Amani.Anawatakia Funga njema na anawapenda wote.

Shughuli hii ya Futari ya pamoja iliandaliwa na Maalim picha ya chini mwenye kanzu.Kwa kumshukuru Mungu na kuunagana na familia,pia kuwashukuru Wasawhili na jamaa zake kwa kuwa naye pamoja kwa kila jambo.

Thursday, 4 August 2011

Mswahili Wetu Leo ni Bi Zaituni wa Mrisho; Anaishi ILALA!!!!!!!

Bi Zaituni wa Mrisho katika Picha ndiyo Mswahili wetu wa Leo,Anaishi Ilala mtaa wa Mwanza.
Bibi huyu ana hadithi na habari nyingi sana za maisha na siasa,Leo  anaongelea kuhusu ULIMBUKENI!!
Anasema watu wanaharibikiwa sana kwa kukataa yote ya zamani na kuingia kwenye mitindio mipya tuu,kwamba si yote mapya mabaya la! bali na yazamani pia yakumbukwe hasa yale mazuri, Na tuwe tunawafundisha watoto wetu,Asema utakuta mtu kazaliwa na kukulia kwenye familia ya kiswahili lakini mwaka mmoja tuu akienda nje ya nchi,anajifanya kasahau kabisa Kiswahili, mara oohh yah oohh yes, pia hawapendi hata watoto wao wanaowazaa huko au kukulia huko kuwafundisha KISWAHILI, tena na kujisifia wakipiga simu huku nyumbani mwanangu hajui/kasahau kabisa Kiswahili,Kama baba na mama Waswahili iweje mtoto wako asiongee Kiswahili?
Mwisho anawatakia Waislam wote duniani Funga njema yenye baraka na amani.

Nami nasema Ahsante sana bi Zaituni  wa Mrisho na kaka Mtaruke[mjuukuu wa binti Mrisho] yeye ndiye aliyetuunganisha na BIBI huyu.
Haya wapendwa Waswahili neno hilo kutoka kwa bibi unalionaje? Karibuni sana kwa kuchangia,kuelimishana  na.....
Kama una lolote jema na kuelimishana , Unataka kuwaambia Waswahili wenzio karibu  sana unaweza kutumia email hii Rasca@hotmail.co.uk. katika kipengele hiki cha Waswahili na Maisha yao ndani ya Swahili na Waswahili.
Nawatakia Swaumu njema kwa Waliofunga!!

Monday, 1 August 2011

Siku kama ya Leo Rachel-Siwa Alizaliwa!!!!!!!!

Siku kama ya leo, Familia ya Bibi na Bwana M.S. Kiwinga walibahatika kupata mtoto  wa kike ;Rachel-siwa.
Nawashukuru sana Wazazi wangu kwa Malezi yenu mema na  yote mliyonitendea.
Pia nakushukuru sana kaka yangu R.Kiwinga kwa kupokea ulezi na kunitunza, Tangu pale Baba alipofariki mpaka pale uliponikabidhi kwa Mume,Sina cha kukulipa bali sitoacha kukuombea.


Ahsante sana Mume wangu Issac kwa yote na kuwapamoja siku zote mpaka 27/07/11 yaani j'tano iliyopita tumetimiza miaka 15 ya ndoa yetu,Mungu atubariki sana katika maisha yetu.

Basi niwashukuru Ndugu,Jamaa,Marafiki zangu woooooteee, kwa Yote,kwani nikiandika hapa hapatatosha.


NENO LA LEO; Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika,kama sina Upendo,nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao.Tena nijapokuwa na unabii,na kujua siri zote na maarifa yote,nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina Upendo,si  kitu mimi.Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina Upendo, hainifaidii kitu. Upendo Hufadhili; Upendo Hauhusudu; Upendo Hautakabari; Haujivuni; Haukosi kuwa na adabu; Hautafuti mambo yake; Hauoni uchungu; Hauhesabu mabaya; Haufurahii udhalimu,bali Hufurahia pamoja na kweli.!!!


MUNGU ATUBARIKI SOTE!!!!!!!!!

Tuesday, 26 July 2011

Kaka Joel Ahitimu!!!!!!!!!

                          Kaka Joel mwenye Furaha.
                                 Duhh sitakuwa nao tena rafiki zangu,hii sasa mbaya kwangu!
                        Dada Jolen akimpongeza kaka.
               Nimeshakuwa mwanakijiji sasa!


Kaka Joel Amehitimu Nursery tayari kwa kuanza/kuingia Reception hapo September.
Joel!! Baba na Mama pamoja na Familia ya Mwasanjala na Shushu,Wanakutakia kila lililo jema katika safari yako ya kutafuta Elimu.


Rafiki[dada] yako kipenzi Tracey anakutakia mema katika masomo yako!


Nasi SwahilinaWaswahili tunakuombea Mungu awe pamoja nawe katika yote.


Mpendwa wewe ulipitia VIDUDU/Nursery?...Je unakumbukumbu gani katika hayo ni Uji,Nyimbo,Kulialia,Ulikutana na watoto Wababe au wewe ndiyo ulikuwa Mbabe!!!!!!


Karibuni sana Waungwana katika Yote!!!!!!!!

Sunday, 17 July 2011

Sandra Atimiza miaka 13!!!!!!

                                 Sandra-Neema, akishangaa duh13!

                         Leo natimiza 13,kweli siku hazigandi,kaka Brian akihakikisha.
                    Sandra na Tracey, mwenzangu tumekuwa sasa.
                 Wageni kutoka Birmingham nao walikuwepo.
                               Dada Damari akisimamia watoto wa Swahili Fellowship.
                   Joel,Jolin na Tracey katika poziiiiii.
                     Manjula,Eireen,Shambara na mgeni wao hawakukosa.
                        Miriam na kaka Ebeneza nao walikuwepo.
                                      Sandra &Tracey wakishukuru wageni kwakuwa nao pamoja.
                   Mama na Sandra Tunamalizia.
Familia ya Isaac tuna Mshukuru sana Mungu kwa Yote aliyotutendea,Pia tunawashukuru wote mlio jumuika nasi kwa namna moja au nyingine.Shukrani za pekee kwa Uongozi wa Watoto wetu Coventry Swahili Fellowship,Chini ya Mwenyekiti Da'Mija na msaidizi wake da'Damari.
Mungu awabariki  wote na Tunawapenda sana.

Wednesday, 13 July 2011

Bucha Zetu/Utumbo Wenyewe Twalia ......!!!!

Wapendwa hivi kwanini  Bucha nyingi TZ/Bongo, zipo katika mazingira machafu?UTUMBO ndiyo kabisa  Sehemu nyingi zinazouzwa Utumbo ni chafu sana.Kama kwenye maduka kuchafu, Je Machinjioni kutakuwaje?
Na nimesikia[sina uhakika] kwenye kununua uwe makini,Kwani wanaongeza kitu au kufanyia maalifa kwenye Mzani ili kuongezea uzito na kuibia wateja.Kama ulinunu kilo mmoja basi utapata pungufu.


Jewewe Unamawazo gani katika hili, Tuache kula Utumbo,waelimishwe,Wafungiwe au wenyewe tumeshazoea na Vichafu kwani tutapika na kuua Vijidudu?
Utumbo wenyewe twalia Ndizi!!!!!

Saturday, 9 July 2011

Mtoto Wetu leo ni Arianna Mbwambo!!!!!!!

                                            dada Arianna katika poziiii
                               Nina mapozi yakutosha.
                                 Nikibeba kipochi jee?

Watoto wa leo na mapozi yao!Wapendwa hivi hawa watoto haya mapozi wanayatoa wapi?
wanayaona kwenye Tv,kwa Wazazi/walezi,kwa rafiki zao au.......

Hata wakubwa nao wana mapozi ,Wengine kunyanyua mguu juu,kushika kiuno,kuweka dole,mikono kifuani na....
zile picha zetu za Studio kushika maua,je mpendwa wewe unazo?.



Karibuni sana Waungwana!!!!!