VITENDO HIVI VYA KIKATILI VYA WATU KUPIGWA NONDO VITAISHA LINI MBEYA?
Bwana Elia
Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole akiwa hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1
baada ya kupigwa nondo hivi karibuni.
Bwana Zefania
Mwangwale mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Uyole akiwa katika hospitali ya Rufaa
mkoani Mbeya baada ya kupigwa nondo pia.
Vitendo vya watu kupigwa nondo kwa Jiji la Mbeya
vimekua kama ni vitendo vya kawaida, ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu
kila mwaka lazima hivi vitendo vitokee na kupelekea watu wengi wa jiji la Mbeya
kuishi katika maisha ya wasi wasi sana.
KAPINGAZ Blog inapenda kuviomba vyombo vyote vya
usalama Jijini Mbeya kuona kama hivi vitendo kama ni janga kubwa kwa watu wa
Mbeya.