Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 28 September 2011

Mtoto Cecilia Edward Aenda India kwa Matibau!!!!!!!









Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarim akiwa amemshika mkono Cesilia Edward (14) mwenye tatizo la moyo linalosababisha kuvimba tumbo akitoka Hospitali ya Regency jana tayari kwa safari ya New Delhi, India kwa matibabu.






CECILIA AWASHUKURU WATANZANIA
   Mtoto Cecilia Edward ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo amewashukuru kwa moyo mkunjufu watanzania waliojitokeza katika kumsaidia kwa hali na mali mpaka kufanikiwa kupata hela tayari kwa matibabu anayotarajia kwenda kuyapata nchini India.
   Cecilia amesafiri kuelekea katika hospitali iitwayo Fortis inayopatikana New Delhi -India kwa matibabu, jumatatu ya tarehe 26 mwezi septemba mwaka huu.
   Aidha walezi wa Sesilia familia ya mzee Kambaliko inatoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa moyo kumsaidia binti yao kwa kutoa pesa, mavazi na hata waliowapa maneno ya faraja pamoja na wale wote wanaoikumbuka familia hiyo katika maombi.
   Kabla ya safari yake hiyo, hali ya kiafya ya sesilia ilikuwa ikiendelea vizuri, kwani alikuwa anaweza kupumua na kukaa, tofauti na awali kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha maji katika tumbo lake hospitalini Regency alipolazwa kwa ajili ya matayarisho kabla ya kuanza safari yake kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.
   Mtoto huyu aliondoka hapa nchini jumatatu ya tarehe 26 na ndege ya shirika la Quatar Airways akifuatana na daktari mmoja kutoka hospitali ya regency, pamoja  na mlezi mmoja mpaka nchini India alipotarajia kupokelewa  na madaktari tayari kwa uchunguzi wa kina na kisha kuanza matibabu yake.
   Kipindi cha Mimi na Tanzania kinapenda kuwashukuru Watanzania wote pamoja na makampuni mbalimbali yaliyojitolea katika kumsaidia Sesilia kwa ajili ya matibabu. Shukrani za pekee ziifikie hospitali ya regency hasa daktari Kanabar kwa uvumilivu na huduma nzuri kwa Sesilia. Pia kwa mchango wao wa kulipia nauli ya kwenda nchini India kwa Sesilia, mzazi na daktari ikiwa ni pamoja na matibabu ya awali anayoyapata hivi sasa.
   Watanzania, pamoja tumeweza tena. Sesilia ni mmoja tu kati ya watoto milioni moja wanaosumbuliwa na tatizo hili, hebu tujitolee kuwasaidia watoto hawa bila ya kuchoka, pia tusimsahau binti huyu kwa maombi ili upasuaji anaotarajia kufanyiwa umalizike salama na kwa mapenzi yake Mungu mtoto huyu arudie katika hali ya kawaida kama watoto wengine.
Mungu mbariki Sesilia.Amen!
        :Swahili na Waswahili tunakuombea cecilia,Mungu asimamie Matibabu yako na upone haraka.


Habari hii kutoka kwa Zainul.A.Mzinge wa www.mohammedewji.com/blog.





-

Monday, 26 September 2011

Kaka Joel Atimiza Miaka 5!!!!!!!!

             Mwenyewe kaka Joel.
             Kaka Joel akiwaza juu ya miaka 5.
            Akikata keki na da'Tracey akishuhudia.
            Kaka Vin ndiye aliyetuongozea sala ya Chakula.
           da'Manjula akiwa kwenye Sala.
             Hakukuwa na Shani leo ni juisi.
         Kama kawaida ya da'Damari yupo makini kwa watoto.
            da'Damari akihakikisha kila mmoja hakosi keki.
        Mwenyekiti na msimamizi mkuu wa watoto wa Swahili Fellowship, da'Mija Mwanamke wa Shoka.
   da'Josephine ,Mdhungu Mswahili mwenye vituko alikuwepo.
    Wamama waliwakilishwa na Mke wa Mwenyekiti wa Swahili Felloship da'Edna.


Familia ya Bwana Godfrey[Mzee wa Fellowship] na bibi Mellanie wa Coventry,U.k.
Wanamshuru sana Mungu kwa kumtunza mtoto wao Joel na Mungu azidi kumsimamia katika makuzi yake,
Awe baraka kwao na kwa Jamii pia.
Shukrani za pekee ziwaendee Watoto wote wa Coventry Swahili Fellowship,Mwenyekiti da'Mija na msaidizi wake da'Damari, Bila kuwasahau Wazazi/Walezi na wote waliofanikisha sherehe ya kaka Joel.
Mungu awabariki sana na wanawapenda sana.

Familia ya Isaac na Cuthbert wa Coventry nao wanamtakia kila lililojema kaka Joel na Mungu awenawe daima,Pia wanasema asanteni sana Familia ya Godfrey kwa yoteeeee!!!Mungu awaongezee kila inapoitwa Leo.


Mengineyo; Kaka Joel anapenda sana Magari na kuyajua mnoo,Mpaka ananishinda mimi jamani, kila aonapo Gari  alipendalo atakwenda kumwambia Mjomba Isaac na Wazazi wake, kutwa anatafuta Magari kwenye Computer, kama uonavyo hapo kwenye keki alikosa Gari kapachika ka'Pikipiki.


Swali; je kupenda huku ni kwasababu ni mtoto wa kiume,akikua anaweza kufanya kazi ya Udereva au zinazohusiana na Magari au ni Utoto tuu akikuwa ataacha?.

Wewe mpendwa kunakitu ulikuwa unapenda wakati wa Utoto na mpaka Leo unakipenda/kukifanya?
Karibuni sana!!!














Saturday, 24 September 2011

Mshumaa uliozimika.Leo ni BRENDA FASSIE, Sikiliza (Vul'indlela / ...!!!

Mungu wape Faraja  Yatima ,Wajane na  wote walioondokewa na wapendwa wao.

Tuesday, 20 September 2011

kweli kulea Kazi!!!!!!!

Hata sijui nini anatafuta huko jamani, Mmmmhhh Tumetoka mbali sana.
Mpendwa unayakumbuka makabati ya vyombo ya Zamani yenye wavu kama wa dirisha?
mama yangu aliweka Ufuta huko,umetengenezwa kama vigorori hivi,mimi na kaka yangu tulikuwa tunautaka,
mama akasema tutapewa tukimaliza kula chakula,tumemaliza chakula mama kaondoka,lakini tunajua ulipo,mwenzangu  mimi nikaambiwa niupandie, hahahahaha kama wewe BINGWA panda,Sifa zikaniponza, nikaupandia weee nikala mweleka wa nguvu na kabati juu yangu, wenzangu wakatimua mbio,badala ya kuniokoa, Sasa na huyu naye yange mkuta yaliyonikuta jee? Kweli Kulea Kazi jamani, Wazazi /Walezi tuwe makini sana na Watoto.

Mpendwa huna kisanga kilichokukuta unachokumbuka?
Hujapitia mambo yakutaka  kuwa Bingwa/Mshindi?.

Karibuni sana.











Sunday, 18 September 2011

Siku kama ya Leo dada Levina Alizaliwa!!!!!!!

Leo ni Siku muhimu kwa  da'Levina Kimwaga.
Siku kama ya Leo familia ya Bibi na Bwana Kimwaga, Walipata mtoto wa kike na Wakamwita LEVINA!!!


Tunakutakia kila la kheri,Baraka na Mafanikio kila inapoitwa Leo.


Mungu awe nawe daima.
Karibuni Waungwana Tuduwage pamoja.





Saturday, 17 September 2011

Pole Zanzibar PoleTanzania!!!!!!!!

Ukatili Mbeya!!!!!!!!

VITENDO HIVI VYA KIKATILI VYA WATU KUPIGWA NONDO VITAISHA LINI MBEYA?

Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole akiwa hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo hivi karibuni.

Bwana Zefania Mwangwale mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Uyole akiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya baada ya kupigwa nondo pia.

Vitendo vya watu kupigwa nondo kwa Jiji la Mbeya vimekua kama ni vitendo vya kawaida, ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu kila mwaka lazima hivi vitendo vitokee na kupelekea watu wengi wa jiji la Mbeya kuishi katika maisha ya wasi wasi sana.
KAPINGAZ Blog inapenda kuviomba vyombo vyote vya usalama Jijini Mbeya kuona kama hivi vitendo kama ni janga kubwa kwa watu wa Mbeya.