Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 18 October 2011

SAKATA LA MGOMO WA WANACHUO WA IMTU UNIVERSITY HATMA YAKE LINI?




Geti kuu la kuingia Chuo kikuu cha Afya IMTU kilichopo Mbezi Beach.

Wanachuo hao hapa wakiwa katika moja ya maandamano ya mgomo huo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Kawambwa

Sakata hili lilitolewa miezi michache iliyopita na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu mgomo huu wa wanachuo hawa.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa Madaktari, kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa umekamilisha miezi miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila hitimisho la mgomo huu.

Kwa kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuongoza  ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi ni kulipa Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti na vyuo vingine vya binafsi (private).

Sisi kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na Serikali ya Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara ya elimu,Tanzania Commision of Universties na Higher Education Student Loan Board tunawaomba waumalize mzozo huu.
Pesa nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha wanafunzi hawa Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikia hili tatizo ili tuweze kuendelea na Masomo na mwisho tuende kujenga taifa letu changa lenye upungufu mkubwa wa Madaktari.


Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog.
Asante.

Thursday, 13 October 2011

Mazishi ya Mpendwa Wetu; Baba Mzee Juma Penza, katika Picha

                       Marehemu Mzee Penza wakati wa Uhai wake.
     Kaka Mashaka akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Kaka Mustapha akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Kaka Iddy akiweka Mchanga wa Mwisho.
                   Rais Jakaya Kikwete akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Mzee Janguo akiweka Mchangawa Mwisho.
             Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa, akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Wajukuu nao hawakuwa nyuma kufanikisha Mazishi ya babu yao.


Shukrani kwa Wote Mliofanikisha Mazishi ya Mpendwa baba Yetu Mzee Juma Penza[JP].
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI;AMINA.


Rachel-siwa[Mwanapenza]na Timu Yote ya SwahilinaWaswahili;MAJONZINI.




picha kwa hisani ya Michuzi blog,Asante sana.

Ulale kwa Amani baba Mzee Juma Penza!!!!!!!

Mzee wetu mpendwa Umetutoka tukiwa bado tunakuhitaji.
Leo sina mengi ya kusema;
Mungu akulaze mahali pema peponi Amina.

Poleni ndugu zangu wote mliopo nyumbani Tanzania na Wote tuliopo nje ya Tanzania,
Tuungane pamoja kwa wakati huu Mgumu kwetu Mgumu.

wako Rachel-Siwa[Mwanapenza].


Wednesday, 12 October 2011

Tamara Sibusisiwe Phiri's birthday Party,Ilivyokuwa,Umewasikia Watoto wa Bondeni/Afrika kusini?Pata Uhondo!!!

HALI YA MTOTO CESILIA NI MBAYA ARUDI BILA KUFANYIWA OPERESHENI.




Mtoto Cecilia wakati akiwaomba wasamalia wema waweze kumsaidia.

Hapa Mtoto Cecilia akitoka Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na afisa mmoja wa Channel Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya kwenda India.

Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.

Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi .Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.

Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapemakwa uchunguzi tunaweza tukawahepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
Habari hii kutoka Kapingaz Blog