Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 28 November 2011

Wanawake na Urembo!!!!!!!!

                        Huyu kapaka sijui manjano.......
                        Huyu kawa wa pinki
                        Huyu na manyonyo
                                               Huyu kakaba shingo
                                                Huyu kachora .
Haya Wapendwa Wanawake na Urembo,kila siku yanazuka mapya,Pia ya Zamani yanarudi kama si kukumbukwa.Nao zamani kulikuwa na yao mengi tuu,Zazuu,Kuchoma nywele,Kusukia Rafya[sijui kama nimepatia]na Mengine Meeeeeeengi.

Wasasa kuna wanaopenda Maziwa makubwa mpaka kuyaongeza,Kujichubua/Mkorogo,Kujichora kwa sasa si hina tuu kuna Tattoo tena mpaka kwenye Nyusi, Wananyoa na kuweka tattoo ili wasipate shida ya kupaka Wanja.Kuna wanaoongeza Kope,Kunakuweka Vidubwasha ndani ya macho  na kubadili Lenzi kuwa kama ya Wadhungu. Na Mengine meeengi labda sikuweza kuyaandika au Siyajui Yote hayo kwa SABABU YA UREMBO!
Haya sasa  Mwanamke wewe;Katika hayo yote wewe unapenda nini ili uwe Mrembo au unaweza kuongezea ambayo hayapo hapo nasi Tufunguke,Pia unachukia kipi?

Wewe Mwanaume jee unapenda Mkeo,Mchumba,Rafiki yako wa Kike atoke vipi katika hayo na Unaweza kutujuza ambayo hayapo ili awe Mrembo na Unachukia kipi?

Duuhh Lakini Urembo mwingine unataka Moyo!!
Karibuni sana Wapendwa  kwa Mawazo/Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo!!!!!




Friday, 25 November 2011

CITE- NA MIAKA 50 ya UHURU WA TANZANIA!!!!

Watanzania waishio Uingereza Kufanya Maombi ya Kumshukuru Mungu Kwa MIAKA 50 ya UHURU.

Waandaaji wa maombi ya ya Miaka 50 ya Uhuru chini Uingereza ”Association of Tanzanian Christians in Europe(CITE)” Wakiwa na Mwl Christopher Mwakasege wakati wa Summer Confference 2009.
Mithali 14:34 Biblia inasema Haki ya Mungu huinua Taifa na huu ndio mstari wa kusimamia katika Maombi hayo yanayowajumuisha watanzania wote waishio nchini Uingereza Hususani katika jiji la London. Kwa Mujibu Wa Mchungaji Emmanuel Chatawe ambaye ni mmoja wa waratibu wa Maombi hayo maombi hayo yatahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali.

Pamoja na Maombi hayo pia kutakuwepo na vikundi mbalimbali vya kusifu na kuabudu.Maombi hayo yameandaliwa na Umoja wa wakristo watanzania waishio bara la Ulaya(CITE).

TAREHE:10 Dec 2011

VENUE: Vision Gospel Ministry International 68 Wallis ROAD Hackney Wick London E9 5LH

TIME :13:00 – 18:00 HRS



Wakati Watumishi wa Mungu Kutoka  Tanzania  waishio nchini Uingereza wakijipanga kwa Maombi hayo, Kwa Upande wa Wakristo wa Watanzania Waishio Nchini Marekani wao wanatarajia kufanya Maombi hayo Tarehe 10 Dec 2011 .Kwa Maelezo zaidi juu ya Kusanyiko la Maombi ya Uhuru wa miaka 50 nchini Marekani Fuata LINK hapa chini.


http://hosannainc.blogspot.com/search/label/Watanzania%20Wahudumuo%20Nje


Thursday, 24 November 2011

Miaka 50 ya Uhuru - Kijitonyama Evangelical Choir!!!!!

Wanakwambia Tujibweteke aaa,Turudi Nyuma mmm,Tusonge Mbele namnamnam,
Haya wapendwa mmejiaandaje na miaka 50 ya Uhuru? Mablogger nao sijui watatoka vipi/wameandaa nini?
kwani  nimeona Vyama, Vikundi vya ngoma,Muziki,Kwaya na mengine mengi kuhusu Miaka 50 ya UHURU. Uwe Huru na mwenye Amani na kila lililo jema!!!Usisite kutujuza Nasi Umejiaandaje au Unalipi kuhusu MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA. NA VISIWANI TUUNGANE PAMOJA!!

Tuesday, 22 November 2011

Siku kama ya Leo dada Akhram wa Billy Alizaliwa!!!!

Siku kama ya leo Familia ya Bibi na Bwana Billy, Walipata mtoto wa kike na wakamwita Akhram!!
dada huyu ni mtu wakucheka wakati wote mpole na mwenye heshima,Si muoengeaji sana mpaka akuzoee sana,Nakuongea kwake uwe na muda ili mmalize hayo maongezi kwani ni taratibu mnoo,Ukiona kafunga mdomo bila tabasamu ujue NJAAA Kwenye sekta ya msosi ahaaa hana Tabu kabisa!!!Usikivu,samahani na kufanya vyema darasani kwake ni maisha  ya kawaida.
Mungu awabari wazazi na awape hekima katika Malezi yenu.


Swahili na Waswahili tunakutakia kila lililo jema mwanakwetu!!!!

Thursday, 17 November 2011

SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA JUMA PENZA[JP]!!!


Marehemu JUMA PENZA enzi za uhai wake.
Familia ya Juma Penza ya Gongo la Mboto Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana  nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa, aliyefariki dunia tarehe 12/10/2011 katika hospitali ya Hindu Mandal na kuzikwa tarehe 13/11/2011 katika makaburi ya Kisutu. 



Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. J.M. Kikwete, CCM Makao Makuu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na kwa namna mlivyoshiriki katika shughuli zote za mazishi.  Shukrani za pekee ziwaendee Dr. Macha Ocean Road, wauguzi na madaktari  wa Hindu Mandal.


Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru  kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi  mzipokee  wote kwa mikono miwili  kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha  shughuli nzima ya msiba wa baba yetu mpendwa Mzee JP.


Tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu  nasi  kwa dua  na maombi wakati wote  hadi tulipompumzisha baba yetu kipenzi .


Vilevile  tunapenda  kuwakaribisha  katika  mkesha  wa dua  itakayofanyika  Ijumaa usiku  Novemba 18 kuamkia siku ya Jumamosi Novemba 19 ambapo khitma  itasomwa  nyumbani kwa marehemu  Gongo la Mboto Dar es es Salaam wote mnakaribishwa .


Tunawakaribisha wote kwenye Arobaini ya marehemu. Mkesha na kisomo utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/11/2011 na kufuatiwa na  Khitma itakayosomwa Jumamosi tarehe 19/11/2011 kuanzia saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.Inna lilah Wainna Ilaih Rajiun