Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 14 December 2011

Jikoni Leo ni Halwaa!!!!!!

Haya wapendwa leo ni kitu Halwaa kwa Kahawa,kuna inayochanganywa na Ufuta,pia kuna ya Karanga, hizi ndizo nilizowahi kula, kama kuna nyingine wewe unajua Tufahamishane!Vipi lakini Kitu Halwaa na Kahawa Vinapanda/Unapenda? au Hujafanikiwa kuonja?
Karibuni sana Waungwana!!!

Monday, 12 December 2011

Watoto wa Kiume na Mitindo!!!!!!

                                        Kaka Mohamed kapozi
                                  hapa na Tabasam
                                              hapa katulia.
Wapendwa Watoto wa kiume na Mitindo yao!!Nakumbuka zamani kulikuwa na Kaunda Suti,Ngwabi,Mchelemchele,Jinzi za Chatu/kujikunjakunja hivi,Mashati ya drafti na nyingine nyingiii,pia watoto wengi walikuwa wanashonewa hizo Suti kwa Fundi tena SareSare,Viatu Moro shoes,Vimokasini,Raba Mtoni, Ndopa/Lakupanda.Pia kulikuwa na viatu vya Bora sijui kama bado lipo hili duka.Pia naona kama mitindo inajirudia .

Wewe unakumbuka nini/kuvutiwa na nini vya wakati ule na Wakati wa sasa jee?

Karibuni sana Waungwana!!!!!

Friday, 9 December 2011

Kheri ya Miaka 50 yaUhuru,Na Siku kama ya Leo da'Halima Kiwinga Alizaliwa!!!

Nawatakia Kheri ya  Miaka 50 ya Uhuru!Pia Siku kama ya Leo Familia ya M.S.Kiwinga wa Ilala,Sharifu/Shamba,  Ilipata Mtoto wa kike na Wakamwita HALIMA!!!Leo ametimiza miaka 50!!!!!Hongera sana dada yetu mpendwa,Mungu akubariki sana katika yote,Sisi wadogo zako Tunakupenda,kukujali,kukuthamini na Tunajidai kuwa na dada kama wewe .Da'HALIMA Uwe na Wakati mzuri  Leo na siku zote za Maisha yako.MUNGU NI PENDO.Kwaniaba ya Familia ya Marehemu Mzee Kiwinga ni mimi Rachel-Siwa.

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU JIJINI DAR PART - 2