Thursday, 29 December 2011
Ulale kwa Amani da'Halima Mchuka!!!!!
DADA HALIMA WAKATI WA UHAI WAKE.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA, HALIMA MCHUKA alikimbizwa katika hospitali ya DAR GROUP na baadae katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI hapo jana baada ya kuanguka ghafla akiwa katika kituo chake cha kazi eneo la PUGU ROAD Jijini DSM.
MCHUKA alikuwa mtangazajii wa kwanza wa kike wa mpira AFRIKA MASHARIKI.
Poleni sana Familia ya Mchuka kwa wakati huu mgumu kwenu.
Wednesday, 28 December 2011
MKESHA MKUBWA WA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA DESEMBA 31 MWAKA HUU, SERIKALI YAPONGEZWA KUKATAA USHOGA.
Umoja
wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania ChristianFellowship of
Churches) umeandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya dua maalum kwa taifa kwa
lengo la kumshukuru Mungu kwa kulivusha taifa katika kipindi cha miaka
50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine ambapo mgeni rasmi katika mkesha
huo atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati
ya maandalizi ya Mkesha mkuu kutoka Tanzania Christian Fellowship of
Chrches Askofu Godfrey Emmmanuel Malasi amesema watanzania wanapaswa
kujua Mungu anakusudi gani na taifa la Tanzania katika kipindi hiki
ambacho Taifa limetimiza miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine na
kutoa wito kwa kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kushiriki
katika uchumi wa taifa.
Amesema
serikali inazo sera nzuri za kuweza kuwamilikisha wananchi rasilimali
ziliizopo nchini ili waweze kuishi maisha bora na kuongeza kuwa
wananchi wanapaswa kutambua majira na wakati uliopo sasa wakati taifa
linapoanza miaka 50 mingine ya uhuru kwa kuzitumia fursa zilizopo
kujiletea maendeleo.
“Kila
mmoja anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa
taifa letu ambalo sasa limemaliza miaka 50 ya uhuru, kila mtu anapaswa
kutambua nafasi yake, tusikae kwa kubweteka, tusikae kwa kulalamika
kila mtu ajue ni wakati wa kumiki na kurithishwa rasilimali zilizopo
katika taifa hili”
Amesema
mwaka huu dua maalum kwa taifa litafanyika katika mikoa 14 ya Tanzania
ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro, Singida Iringa,
Mbeya ,Iringa, Kagera, Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na visiwa vya
Zanzbar na Pemba.
Amefafanua
kuwa katika mkesha huo viongozi mbalimbali wa taifa ,vyama vya siasa
na balozi mbalimbali zipatazo 37 zilizopo nchini zimearikwa kushiriki
mkesha huo na kuongeza kuwa tayari baadhi ya balozi zimethibitisha
kushiriki mkesha huo.
Kuhusu
maadalizi ya mkesha huo askofu Godfrey Malasi amesema yanaendelea
vizuri na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika dua hiyo
maalum na kuongeza kuwa mkesha huo utaambatana na tukio maalum la
watoto 50 kusimama uwanjani na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo
ikiwa ni ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania.
Kwa
upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya mkesha mkuu wa Taifa Askofu
Keneth Damas ameipongeza serikali kwa kuwa na msimamo wa kupinga suala
la ndoa za jinsia moja (ushoga) katika mikutano ya kimataifa
iliyofanyika hivi karibuni na kuuita uamuzi huo kuwa ni ushindi mkubwa
kwa taifa la Tanzania na watu wake katika kuheshimu utu na utamaduni wa
taifa na uukataaji wa vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kuwa wao
kama viongozi wa dini wataendelea kuonya na kufundisha watu wajue
athari za dhambi hiyo.
“Sisi
kama viongozi wa makanisa katika nchi hii tunapinga kwa nguzu zote
vitendo vya ushoga ndani ya taifa letu, vitendo vya ushoga ndivyo
vilivyosababisha Sodoma na Gomora kuchomwa moto kwa kuwa vilimchukiza
sana Mungu, Sisi kama viongozi wa dini katika kizazi chetu na vizazi
vijavyo hatutaki kufikia hapo na kuona taifa letu likichomwa moto”
Tuesday, 27 December 2011
Waswahili na Maisha yao -Ibada ya Kiswahili Columbus,Mungu awabariki sana!!
Picha zaidi utazipata kwenye blog ya VIJIMAMBO!!
Ahsante sana.
Ahsante sana.
Sunday, 25 December 2011
Jikoni Leo na Xmas,Wazee wa kazi hawataki ulalamishi!!!!!!!
Kaka Asulwisye hapa anageuza!!
Hapa zamu ya kaka Hamza kugeuza.
Haya wapendwa mambo ya Xmas hayo,kaka zangu leo wameniambia,unafikiri wewe kutokuwepo watu hatuli?Wameingia wenyewe!!!!hii ndiyo hali halisi ya kwetu kwenye swala la kupika hakuna JINSIA.
Nami nawaunga mkono naona kitu si chakawaida hicho,mimi mwenyewe hapa mate yananitoka!!!
Mpendwa nawe Xmas yako imekwenda/inakwendaje? maana masaa yanatofautiana.
Wengine wameshakula na Wengine wanaandaa.
Tushirikishe basi!!!!Karibuni sana wapendwa.
Hapa zamu ya kaka Hamza kugeuza.
Haya wapendwa mambo ya Xmas hayo,kaka zangu leo wameniambia,unafikiri wewe kutokuwepo watu hatuli?Wameingia wenyewe!!!!hii ndiyo hali halisi ya kwetu kwenye swala la kupika hakuna JINSIA.
Nami nawaunga mkono naona kitu si chakawaida hicho,mimi mwenyewe hapa mate yananitoka!!!
Mpendwa nawe Xmas yako imekwenda/inakwendaje? maana masaa yanatofautiana.
Wengine wameshakula na Wengine wanaandaa.
Tushirikishe basi!!!!Karibuni sana wapendwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)