kusafisha vyumba vyao.
kusaidia kusafisha na sehemu nyinngine
Wabaki na Furaha/Amani.
Ni matumaini yangu wote wazima,
Haya wapendwa,Wazazi/walezi wenzangu,vipi watoto kufanya/kusaidia kazi za nyumbani,
Hii imekaaje/wewe unaonaje?kazi kama kusafisha vyumba,kuosha vyombo,kuaanda vyakula na kazi nyingine nyingi,Jee wewe unafikiri ni Umri gani uliosahihi kwa mtoto kuanza kumfundisha kazi ndogondogo?naje huu ni Unyanyasaji au ni malezi ya kawaida? naje Kuna kazi za watoto wa kiume na wakike?kama ndiyo jee sisi wenye watoto wa jinsia moja je?Unafikiri watoto wote wanapenda kazi? je kama hataki?.
Mimi binafsi kazi nyingine sikuwa nazipenda kufanya nilipokuwa mtoto,lakini mama alikuwa ananilazimisha, jee alikuwa ananikosea au ndiyo malezi?Jee wewe unapenda/ulipenda kazi zote ufanyazo/ulizokuwa unafanya?.Mwana Umleavyo ndivyo akuavyo au.......
Karibuni sana Waungwana katika kusaidiana Kimawazo,Kujadili na Kuelekezana kwa Upendo!!