Sunday, 22 January 2012
Friday, 20 January 2012
Thursday, 19 January 2012
Wednesday, 18 January 2012
Monday, 16 January 2012
Utafiti;Eti kuangalia TV kwa saa Moja kunapunguza dakika22 za Maisha Yako!!!
- Ukifuata kila linalosemwa na wanasayansi utashindwa kuishi. Leo watasema kunywa kahawa kunapunguza msongo wa mawazo. Kesho watasema kunywa kahawa huko huko kunaongeza shinikizo la damu na uwezekano wa kupata pigo la kiharusi. Leo watasema hiki na kesho watasema kile ali mradi ni vurugu tupu. Kibaya zaidi ni ukimya wao kuhusu nini cha kufanya hasa pale tafiti zao zinapotoa matokeo yanayokinzana.
- Kwa vile nyingi ya tafiti hizi hufanyika huko Ulaya na Marekani, Waafrika inabidi kuyapokea matokeo ya tafiti hizi kwa uangalifu sana kwani huwa hayazingatii mazingira yetu na mtindo wetu wa maisha (japo sasa tunajitahidi sana kuwaiga kwa kila kitu).
- Utafiti uliofanywa mwaka jana na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Queenesland unaonyesha kwamba kuangalia runinga kwa watu wenye umri wa miaka 25 na kuendelea kuna madhara makubwa kiafya na kunapunguza muda wa kuishi. Utafiti huu unaonyesha kwamba kwa kila saa moja unayoitumia ukiangalia runinga basi unajipunguzia dakika 22 katika maisha yako. Hii ni sawa na kuvuta sigara mbili.
- Wanasayansi
hawa wanasema kwamba tatizo hasa siyo kuangalia tv bali madhara ya
kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ambako kunasababisha magonjwa ya
moyo, kisukari, kunenepeana na matatizo mengine ya kiafya
yanayosababishwa na mtindo wa maisha ya kubweteka (sedentary lifestyle).
Kufanya mazoezi, hata kama ni dakika 15 tu kwa siku ni jambo la muhimu
na kumeonyeshwa kuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza siku tatu katika maisha yako.
Kusoma zaidi habari hii ingia kwa Blog ya kaka Matondo[MMN]http://www.matondo.blogspot.com
Ahsante kaka Matondo.
Saturday, 14 January 2012
Siku kama ya leo kaka Isaac Alizaliwa!!!!!!
Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita, Kaka Isaac, babake Sandra na Tracey,Mume ya MadameRachel-siwa,Alizaliwaaa!!!
Tunamshukuru sana Mungu kwa yote juu yako,Mungu akubariki na kukulinda kila inapoitwa Leo.
Akuongezee Miaka Mingi na Ufanikishe malengo yako.Uzidi kuwa Baraka kwetu na Kwa Watu wote.
Tunakupenda saaana,Wako Rachel,Sandra,Tracey[ Rasca].
Tunamshukuru sana Mungu kwa yote juu yako,Mungu akubariki na kukulinda kila inapoitwa Leo.
Akuongezee Miaka Mingi na Ufanikishe malengo yako.Uzidi kuwa Baraka kwetu na Kwa Watu wote.
Tunakupenda saaana,Wako Rachel,Sandra,Tracey[ Rasca].
Friday, 13 January 2012
Wanawake na Urembo!!!!!!!!
Nimatumaini yangu woote wazima,
Haya Waungwana Wanawake na Urembo! Kuna mengi kwenye hizi picha na kwa Wanawake kwa Ujumla,
Mimi leo si msemaji saana,Kazi kwenu nyie na Mitazamo yenu,kipi wewe umependa hapo/Kukuvutia na kipi hujapenda hapo,yaani kama ingekuwa wewe hapo ungeongezea nini au ungepunguza nini,Pia wewe Mwanaume kama ni Mkeo,dada,shangazi na...Ungependa nini aongeze au apunguze nini?Na jee labda unapenda lakini hujui ufanyeje uwe/awe kama hivyo,au kunakingine unapenda hapo hakipo,Basi usisite kusema/Kutoa Mawazo,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.
Karibuni sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)