Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 27 January 2012

Watoto wa Kiume na Wakike Wanamajukumu Sawa?


Nimatumaini yangu woote Muwazima!!!na Kama kunamgonjwa Pole sana na Mungu akuponye.
Waungwana Eti watoto wa kijijini wa Kiume na Wakike wanamajukumu sawa?Yaani si lazima wote waende kuchota maji pamoja,basi kama huyu anafagia mwingine aoshe vyombo,na ikifika saa ya kujisomea wote wanasoma,ikifika saa ya kucheza wote wanacheza.Najua kila familia inamalezi yake,Jee vipi kwa malezi ya kileo huko kijijini yameweza kubadili muonekano/Majukumu ya watoto? kama si kijiji kizima basi kuna nafuu?na kama hakuna jee tunaweza kuwasaidiaje?Sawa Mwanamke ni mwanamke, Mwanaume ni Mwanaume hilo naliheshimu pia.Jee Vipi na Watoto hawa wa Mjini?

Karibuni sana Wapendwa, kwa Mawazo,Ushauri,Kuelimishana  kwa Upendo.

Wednesday, 25 January 2012

Wanawake na Urembo,Unapenda Shanga?

                                Wengine wanavaa Kiunoni.
                                     Wengine wanavaa Shingoni
                            Wengine Kichwani,Mikononi...........
Nimatumaini yangu wote muwazima!!!
Haya wapendwa leo tuangalie Urembo huu wa Shanga,Jee wewe Mama,Dada wapenda Shanga?
Nawe Baba,kaka Unapenda Mkeo,Mchumba wako ajipambe kwa Shanga?
Kuna wanaopenda kuvaa Miguuni,kuna Mikanda, Bangili,Hereni naa........,Jee wewe Unapenda/Ungependa Uvae/Avae wapi?Wengine wanapenda za Bendera ya Taifa na......Vyovyote vile ilimradi SHANGAAA!.
Kitamaduni zaidi au Vipi?

Karibuni sana Waungwa!!!!!

Tuesday, 24 January 2012

Siku kama ya leo da'Nancy Alizaliwa!!!!!!

Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita,Da'Nancy Bibi ya Nyotu Alizaliwa!!!
Tunakutakia kila la kheri na baraka katika maisha yako,Mungu azidi kukubariki sana,
Upendo,Utu wema,Fadhili,Busara,Ucheshi na Mengine mengi Mungu amekujalia dada Nancy.
Wewe ni Rafiki wa nyakati zote kwa shida na Raha,Kupitia wewe nimejifunza meeengi sana sana.
Uwe na wakati mwema kila iitwapo Leo.
Familia ya Isaac Tunakupendaaa na kukuthani sanasana sana.
Mungu awe nasi Daima.




Wednesday, 18 January 2012

Ulale kwa Amani da'Regia!!!!!



 Poleni sana Ndugu,Jamaa,Marafiki na Taifa pia.Bwana alitoa na Bwana Ametwaa.