Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 11 February 2012

OMARY MJENGA AKIWA NA FAMILIA YA BALOZI MDOGO WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA MH. CHABAKA KILUMANGA




Kutoka kulia ni Mtoto wa Balozi Mdogo nchini Uingereza anaitwa Maya, anaefuata ni Mwakilishi wa UNOPS Siera Leone Ndugu Omary Mjenga, anaefuata ni Mke wa Balozi Mdogo Uingereza, anaefuata ni Balozi mdogo wa Tanzania Nchini Uingereza Mh. Chabaka Kilumanga, na wa mwisho ni Aziz Msuya mtoto wa Balozi wetu Pretoria Afrika ya kusini.
Mjenga yuko Nchini Uingereza kuhudhuria moja Kikao ambacho kiko ndani ya majukumu yake ya kikazi.

Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.
Ahsante sana.

Friday, 10 February 2012

Harambee ya Msiba wa Mtanzania Mwenzetu,Washington DC.Kutoa ni Moyo!!!

Marehemu Christavina Kusaga Cryor
Familia ya Kusaga inawaomba watanzania wote walioko Marekani na hasa eneo la Washington DC na vitongoji vyake kushirikiana nao katika harambee (fundraising) ili kupata pesa ya mazishi ya mtanzania mwenzetu Christavina Kusaga Cryor aliyefariki February 7, 2012 kwa sarakani ya utumbo.

Marehemu alikuwa akiishi Landover, MD. Ameacha mume na watoto wawili- mvulana wa miaka 4 na msichana wa miaka 2. Alikuwa akisumbuliwa na cancer ya utumbo.

Tafadhali fika tushirikiane kusaidia mume wake na watoto na familia wamzike mpendwa wao. Jumla ya gharama za mazishi ni $11,000, na mpaka sasa tuna $3,000. Tunashukuru kwa waliokwisha saidia.

Harambee itakuwa Jumapili February 12, 2012, kuanzia saa 8.30 mchana (2.30pm).

Anuani ni: 3621 Campus Drive, College Park, MD 20740.

Kwa wale wa mbali au wasioweza kuhudhuria tafadhali tusaidie mchango wako kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing # 255071981. Jina la Account ni Lavorn Cryor. Tafadhali eneza habari hii kwa ndugu na marafiki wote. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu katika wakati huu mgumu.

Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile (240.938.3177); Teddy (301.254.4169); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au Rebecca (202.580.4648).

M/Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen

Thursday, 9 February 2012

Wednesday, 8 February 2012

Waswahili na Maisha yao -Nyimbo za Mipasho[Rusha Roho]!!!!!!!

Waungwana vipi kuhusu nyimbo hizi za MIPASHO,[RUSHA ROHO]Zinajenga au Zinabomoa?jee nahii michezaji vipi?kwani mpaka tukukatike na kugusana?jee hizi  ni Taarabu,Chakacha au ni Mitindo gani?Wenyewe wanaema meseji Send wewe unasemaje?Duuhh SWAHILI NA WASWAHILI AU VIPI? KARIBUNI SAAANA.

Tuesday, 7 February 2012

Wanawake na Mitindo ni Mswahili-Maskat Designs!!!


Leo wanawake na Mitindo ni da'Maskat,yeye ni Desings,mimi nimevutiwa sana na kazi zake.
unaweza kuangalia zaidi kazi zake kupitia http://www.zib-fashion.blogspot.com.

Jikoni Leo ni Chai ya Waswahili!pata na Burudani; Ray C-Mama Ntilie!!!!!!!


Waungwana leo tuangalie chai za Waswahili.Unapenda kufumgua kinywa/Chai na nini Asubuhi?
Kuna wanaopenda Viporo,Vitu vya kuchemsha,Vyakukaanga,Kuungwa,Uji,Supu na vingine Vingii.
Jee upo kwenye lipi? na jee hapo ulipo unavipata kwa Urahisi kama kununua vilivyopikwa au unapika mwenyewe?na jee Kifungua kinywa chako kina Faida kiafya?.
Karibuni sana Waungwana katika Yote!!!!

Sunday, 5 February 2012

Nawatakia J'Pili Njema na Burudani-YUMWEMA ANGEL CHOIR

Hali ya Hewa baadhi ya Sehemu iko hivi,Isiwe sababu ya kutokwenda  kwenye Nyumba za ibada Wapendwa,Mungu awabariki sana, na Muwe na J'Pili njema yenye Baraka,Amani na Upendo. Mungu yu Mwema Maishani mwetu,wenyekuamini hivyo na Tuseme AMINA!!