Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 5 March 2012

Wanawake na Mitindo Leo-Da'SUBIRA WAHURE DESIGNS!!!!!!



Waungwana Wanawake wa leo wapo mbio sana kutafuta/Kusaidiana katika Maisha.
Da'Subira anaomba  wenye mapenzi mema,wamsaidie kufikisha Ujumbe huu.
Hizo ndizo kazi afanyazo.
Ukitaka kumfahamu zaidi ingia.http://www.subirawahure.blogspot
  Hongera sana da'Subira,Kazi nzuri na Mungu akubariki kwa kazi zaMikono yako!!
                         























Sunday, 4 March 2012

Nawatakia J'Pili Njema!!Burudani- Sauti Ikatoka na Mimi Yesu!!!!!!


Mzee kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli;Wala si mimi peke yangu,Bali na wote waijuao ile kweli.2Kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu,Nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.Neno la Leo:WARAKA WA PILI WA YOHANA..Nawatakia J'Pili yenye Upendo na Amani!!!!

Saturday, 3 March 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Ngoma & Kidumbak na Ahmada Umelewaaaa!!

Haya Waungwana  pata Burudani Muruwaaaaa!!!!!Mambo ya Zenji au?? Ngoma ya Kidumbaku,, na Kingine ni Ahmada Umelewaa, sijui hii ni chakacha au Taarabu, Jibu utalipa ukisikiliza, na unaweza kutujuza nasie!!!Karibuni sana. Waungwana kila J'Mosi kuna chaguo la Mswahili,si mimi Pekeyangu nawe kama unataka Kuchagua Mziki,Ngoma na......Ruksa nitumie Email, rasca@hotmail.co.uk  Swahili na Waswahili Waungwana  au Vipi?Twende Sote sasa!!!!!

Tuesday, 28 February 2012

Jikoni Leo -Bamia,Kwanini Wanaume wengi Hawali?Burudani- Nshomile!!!!!

Bamia za kukaanga na mafuta,Hapo naongeza na nyanya.

Mimi hupenda na Ugali.



Bamia za Kuchemsha[Mrenda]
Waungwana hivi ni kwanini mboga hii ya Bamia Wanaume wengi Hawali/Hawaipendi? Jee wewe Unapenda Bamia na Unapikaje?Wengine wanatia na nyanyachungu,Kwenye Samaki Wakavu na....Jee Unaweza kula Bamia na Ugali wa Muhogo? Karibuni sana!!!!

Monday, 27 February 2012

Mtoto Wetu Leo-Sabrina!!!!!!

katika Poziii
Alikuwa MC
Mifugo ni adimu kwao,weee paka njoo hapa!!!
Kwanini jana ulikimbia?utahama humu oohh,haya niamkie..
                                          Kama hutaki ngoja nikuamkie wewe!!!
Waswahili wanasema vyakurithi Vinazidi jee ni kweli?
Jee Watoto wanaweza kurithi Vituko,Ucheshi,Upole na Ugomvi?
Na kwanini baadhi ya misemo ya watoto inafanana kama Maji,kuwa Mma,Nyonyo na.....?
Kunawakati unaweza cheka na Mtoto mdogo au Kulia kwa mambo yake!!!!
Wengine hawapendi kula,kulala Usiku na mambo mengi.Pia kuwa na Mtoto kuna Raha yake!!

Kama wewe huna Mtoto na Unahitaji,Mungu yu Mwema  Uskate Tamaa!!!!

Sunday, 26 February 2012

Nawatakia J'pili Njema,Burudani-Unastahili Kuabudiwa !!!!

Naye alipowaona Makutano,alipanda mlimani;na alipokwisha kuketi,Wanafunzi wake walimjia;.Akafumbua kinywa chake,akawafundisha,akisema,Heri walio maskini wa Roho Maana ufalme wa mbinguni ni wao.Heri Wenye huzuni;Maana hao Watafarijika.Neno la  Leo;Mathayo Mtakatifu:5;1-16.Mbarikiwe sana!!!

Saturday, 25 February 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Muzina yaTabu ley,Zaiko Langalanga na Bozi boziana!!!

Leo nimekurudisheni nyuma kidoogo,Vipi  kuhusu vibao hivi leo,kuna lolote unalokumbuka?Twende Sote na Burudani !!!!!Nawatakia week end Njema.