Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 8 March 2012

Nawatakia kheri na Baraka, Wanawake wote!!Burudani,Vicky Kamata - Wanawake Maendeleo


Namshukuru Mungu kwa kuniumba  Mwanamke,Najivunia kuwa Mwanamke!Nawatakia Wanawake wenzangu woote Kheri,Baraka,Upendo,Utuwema,Fadhili na Yootee yanayostahili.Wanawake Tujiheshimu na Kuheshimu Wengine,Tupendane na Tujipende,Tushirikianae na Kuelimishana,Tusamehe nasi Tusamehewe.Wanawake wa Zamani hata akiwa mama wa Nyumbani lakini alikuwa anakitu kidogo cha kufanya,kama, Kusuka ukili,Kufuma vitambaa,Biashara ndogo ndogo,Kushona na mambo meengi ili kuongezea kipato.Hata Wanawake wa sasa hatuja chelewa, kama hakuna Ajira basi Tunaweza Kusjishughulisha,hakuna asiyeweza kufanya lolote na hakuna aliye zaliwa anaweza.Japo masoko yamekuwa magumu,lakini Tusikate Tamaa.Pale tunapokwama tusisite kutafuta Ushauri na maelekezo, Kwani kuuliza si Ujinga.Mungu awabariki sana,WANAWAKE JUUU!!!!!

Tuesday, 6 March 2012

Kaka Farid atimiza miaka 14-Ona mambo yake!!!

                                               Poziii
                                     Mpirani
                          Shughulika baba!!!!
                                             Vituko
                                           Mapenzi kwa mama.
Hongera sana kaka Faridi kwa kutimiza miaka 14,Mungu akubariki na kukulinda wakati wote.
Uwe baraka kwa wazazi na watu wote.
Hongera pia Wazazi na Mungu awape Maarifa, Usimamizi na Mema  Yote kwenye Malezi.


Waungwana; Eti watoto Wengi  wa  Kiume ni rafiki/wapo karibu  sana na MAMA kuliko BABA?
Pamoja Wapendwa!!

Monday, 5 March 2012

Wanawake na Mitindo Leo-Da'SUBIRA WAHURE DESIGNS!!!!!!



Waungwana Wanawake wa leo wapo mbio sana kutafuta/Kusaidiana katika Maisha.
Da'Subira anaomba  wenye mapenzi mema,wamsaidie kufikisha Ujumbe huu.
Hizo ndizo kazi afanyazo.
Ukitaka kumfahamu zaidi ingia.http://www.subirawahure.blogspot
  Hongera sana da'Subira,Kazi nzuri na Mungu akubariki kwa kazi zaMikono yako!!
                         























Sunday, 4 March 2012

Nawatakia J'Pili Njema!!Burudani- Sauti Ikatoka na Mimi Yesu!!!!!!


Mzee kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli;Wala si mimi peke yangu,Bali na wote waijuao ile kweli.2Kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu,Nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.Neno la Leo:WARAKA WA PILI WA YOHANA..Nawatakia J'Pili yenye Upendo na Amani!!!!

Saturday, 3 March 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Ngoma & Kidumbak na Ahmada Umelewaaaa!!

Haya Waungwana  pata Burudani Muruwaaaaa!!!!!Mambo ya Zenji au?? Ngoma ya Kidumbaku,, na Kingine ni Ahmada Umelewaa, sijui hii ni chakacha au Taarabu, Jibu utalipa ukisikiliza, na unaweza kutujuza nasie!!!Karibuni sana. Waungwana kila J'Mosi kuna chaguo la Mswahili,si mimi Pekeyangu nawe kama unataka Kuchagua Mziki,Ngoma na......Ruksa nitumie Email, rasca@hotmail.co.uk  Swahili na Waswahili Waungwana  au Vipi?Twende Sote sasa!!!!!

Tuesday, 28 February 2012

Jikoni Leo -Bamia,Kwanini Wanaume wengi Hawali?Burudani- Nshomile!!!!!

Bamia za kukaanga na mafuta,Hapo naongeza na nyanya.

Mimi hupenda na Ugali.



Bamia za Kuchemsha[Mrenda]
Waungwana hivi ni kwanini mboga hii ya Bamia Wanaume wengi Hawali/Hawaipendi? Jee wewe Unapenda Bamia na Unapikaje?Wengine wanatia na nyanyachungu,Kwenye Samaki Wakavu na....Jee Unaweza kula Bamia na Ugali wa Muhogo? Karibuni sana!!!!