Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 18 March 2012

J'Pili ya leo ni Maombi kwa Wajane,Yatima , Wenye shida na Tabu; Kabula anasema Dhihirisha na Upendo anasema Hapa Nilipo!!!!!!!


Leo ni siku ya Mama,Tuwaweke kwenye Maombi,Sala,Dua, Wajane,Yatima, Wenye Shida na Tabu.Mungu awasimamie katika Maisha yao Wajane na Yatima,Mungu uwaguse wenye Shida na Tabu, Wengine wanahitaji Watoto,Wanahitaji kuwa MAMA/BABA,Kuna wanohitaji Wenza/Ndoa,Elimu,Chakula,Malazi,Upendo,Faraja.Wagonjwa walio Hospitalini na Majumbani.Waliokata Tamaa.Waliopoteza Wapendwa wao katika Majanga mbalimbali.Walio vitani.Na mengine Meengi. Mungu uwaguse kwa Mkono wako wenye Nguvu.

Neno la leo;Matendo ya Mitume:9;36-43.Na Mwanafunzi mmoja alikuwa Yafa Jina lake Tabitha,Tafsiri yake ni Dorkasi[yaani Paa];Mwanamke huyu  alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.Endelea na Uwe na wakati mwema.

Saturday, 17 March 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Congo - Pepe Kalle!!!!!!!

Nawatakieni J'mosi njema!Kumbuka Enzi zako, hahah wapi dada Mwasu KLM, my Wifi Neema Nyanyile, Mama Kisa na da' Nana Msilie wapendwa wangu,Enzi hairudi ikipita imepita, kumbukumbu ipo lakini..Waungwana nini Mnakumbuka kukisiliza nyimbo hizi?.Twende sote sasa Anakala Manzeeeeee!!!!!!!!.Pamoja sana.

Thursday, 15 March 2012

Mswahili Wetu Leo; DR. SHABANI KACHUA MTANZANIA ANAEIPEPERUSHA VEMA BENDERA YA TANZANIA NCHINI CANADA



Dr. Engineer Shabani G Kachua akijiandaa kuingia kwenye Professional Engineer Induction Ceremony nchini Canada
Hapa Dr. Kachua akionyesha moja ya Nishani aliyotunukiwa siku hiyo
Dr Kachua akiwa amesimama kwa nyuma na Mainjinia wenzake
Akipiga picha ya pamoja kwa kumbukumbu na mainjinia wenzake.
Kwa niaba ya Watanzania ninapenda kukupongeza kwa kuipeperusha vema Bendera ya Tanzania.

Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.http://kapingaz.blogspot.com/

Ahsante sana.

Wednesday, 14 March 2012

Watoto na Urembo,Wanapaka Shedoooooo!!!!!!

Wazazi/Walezi hapo vipi?Kuna msemo sikuhizi; Aku babu najiremba mie napishana na Uzee!Nao Watoto sasa;Aku bibi nakufuata hukohuko!!Mambo ya kileo hayo, Zamani ulikuwa huruhusiwi kupaka,Wanja,Poda na vipodozi vingine, mpaka siku ya KUOLEWA!!Eti ukipaka  kabla,Siku ya Arusi hautapendeza!!Na walikuwa Wakisuka Nywele Ufunge kilemba mpaka MUMEO kwanza Aone!!''Hizi hadithi mie nazisikia''.Hahahahahha Ohiiii Leo hii nani umfungishe Kilemba?Tena ukienda salon ndiyo unafunga kilemba kama nywele zimeharibika, ukimaliza tuu kilemba kuleeee,Wataanza kuona kina baba/mama John,Juma,Neema,Pili na mnaopishana Njiani, hee dada wewe Umependeza, Umetoka Chicha na..Nani kakusuka dada mmoja anaitwa YASINTA NGONYANI!!!Muwe na Wakati Mwema Waungwa, Karibu Sana sana.

Tuesday, 13 March 2012

Wanawake na Mitindo ya Nywele,Pata na kideo Jinsi ya kuweka Nywele Bandia!!!!!!

Haya Waungwana Mitindo ya Nywele kwa Wanawake, Mmmh lakini kwa sasa hakuna cha Wanaume wala cha Wanawake, kila mmoja  anajaribu kuingilia Mitindo ya Jinsia nyingine,Au labda mimi ndiyo sielewi, kwamba hakuna Mitindo ya Wanawake na Wanaume Wote ni Sawa!!!!Wewe uliyepita hapa unaonaje?
Swali ;Wanaume wengi Wanaofanya Kazi  SALON zA Wanawake Wengi wao/Baadhi yao ni MASHOGA?

Sunday, 11 March 2012

Nawatakia j'Pili Njema Wapendwa,Burudani,Rose Muhando-Tamalaki''Na nyingine Mpya!!



Mzee,kwa Gayo mpenzi,nimpendaye katika kweli.2Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo.Neno linapatikana;WARAKA WA TATU WA  YOHANA:soma 1-13.15;Amani kwako,Rafiki zetu wakusalimu.Wasalimu hao rafiki zetu,kila mtu kwa jina lake.Mbarikiwe sana!!!mimi nabarikiwa sana na nyimbo nyingi kupitia hapa kwa Kaka yangu Matondo.http://nyimbozadini.blogspot.com/