Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 27 March 2012

Jikoni Leo-Ni kwa Mama Mwakitalu!!!Pata na Burudani ya Ngoma!!!!![Mwanamke jiko au Mwaume Jiko?]



Da'Masika/mama Mwakitalu
Mboga za Majani Mchanganyiko,Majani ya Kunde na Majani ya Maboga
Mchuzi wa Samaki Umeungwa/wekwa Nazi na nyanyachungu

Maandaziiiiii na hapo chini ni Mahindi ya Kuchemsha.

Haya Waungwa,vipi wewe unapenda kupika?au Unapika kwasababu ni lazima upike na ule?Kwenye kazi za Nyumbani kila mmoja kuna kazi anapenda kuifanya, Na kuna baadhi ya Kazi hatuzipendi,Lakini tunafanya kwa sababu ni lazima zifanywe,Na utasikia duuh yule kaka/dada au Mama/Baba anajua Kupika sana,Hivi kujua kupika ni Chakula kiive au?
Kwani Utamu/Radha ya chakula wewe unaweza kupendezwa nacho na mwingine asipendezwe nacho.
Jee Kazi/Ujuzi wa Kupika ni kwa Wanawake tuu?Kwani mara nyingi utasikia Mwanamke jiko na si Mwanaume Jiko,Hasa kwa Maisha ya Leo,
 kwa Maisha ya Zamani wengi wao Mama/Dada kazi yao kubwa ni Upishi na Baba wengi ndiyo walikuwa wanafanya Kazi hasa Mijini, Kwa Vijijini Woote BABA na MAMA Wanaenda shambani lakini Kupika ni MAMA.Jee Leo Tunaweza Thubutu kusema MWANAUME JIKO? AU TUTAKUA TUMEWADHALILISHA?Kwani wapo Wanakarangiza haswaaaa kutushinda au Hamjakutana nao?.


Karibuni Waumgwana kwa Mawazo na Kuelimisha na Kwa upendo.

MWAKILISHI WA UNOPS NCHINI SIERA LEONE NDUGU OMARY MJENGA AKISALIMIANA NA RAIS KIKWETE WAKATI WA MAZISHI YA MKUU WA WILAYA YA LIWALE MAREHEMU VICTOR P. CHIWILE JANA KIBAHA.


Mmoja wa waombolezaji akimsalimia Rais Kikwete kwa kuibusi Pete yake, kulia ni Ndugu Omary Mjenga akishuhudia tukio hilo.
Rais akisalimiana na Ndugu Omary Mjenga jana walipokutana kwenye mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale.
Ndugu Mjenga alikuwa Personal Secretary wa Rais Kikwete wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje kabla hajawa Rais.

Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog. http://kapingaz.blogspot.co.uk/
Ahsante Sana.

Sunday, 25 March 2012

Nawatakia J'Pili Njema Woote!!Burudani-AIC Chang'ombe Vijana Choir - Hakuna

Nawatakiaeni J'pili njema yenye kheri,Baraka,Upendo na Utu wema.
Neno la Leo;Zaburi ya 121:1-8.Nitayainua Macho yangu niitazame Milima,Msaada wangu Utatoka Wapi?Endelea.
Nijambo Gani linalomshinda MUNGU BABA?.

Saturday, 24 March 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Twanga Pepeta - Mtu Pesa na nyingine nyingi!!!

Papaa Sunday, Yeye ndiyo aliyenianzishia wana Twangwa leo, Ahsante kaka yangu, Duhh Pia nimekumbuka Mengi sana Ndugu yangu. Papaa Huyu tumecheza nae sana Mpira wa Makaratasi,Makonzi , Hahahahhaaha Enzi za Masonge muuza Mihogo,Mzee wasiwasi ooohhiiii. Tumetoka mbali sanaaaaa!!Hili nitalikumbushia siku nyingine, Pata Burudani na Nawatakia J'mosi Njeeeeeemaaa!!!Mimi nawapenda Wooote Waungwana. Twende Sote sasa.Twanga pepeta Inapendaga Watu Woteeee ehhhh ohhhhh Ehhhheee!!!!!!!

Wednesday, 21 March 2012

Waswahili na Maisha Yao - Zanzibar na Mwaka Kogwa Festiva-Burudani Marashi ya Pemba!!


Waungwana Waswahili wa Zenji wanamambo yao,Unajua kuhusu Mwaka Kogwa?Sijui ni Matambiko,Michezo,Sherehe au?Jee mpenzi msomaji Umeshawahi kukutana,Kuona,Kushiriki Mwaka Kogwa?Hivi wanavyotandikana, Kama kunamtu unasababu nae si ndiyo Utamtandika Kwa hasira?Jee Mwaka Kogwa wanaruhusu kushiriki mtu yeyote au mpaka uwe Mzaliwa wa huko?
Karibuni sana Waungwa!!

Waswahili na Maisha yao!!!!!!!

Hakuna linaloshindikana au?Asante mwanangu Amina kwa kazi nzuri,Joto sasa basi.Kumbe inawezekana!!!!

Sunday, 18 March 2012

J'Pili ya leo ni Maombi kwa Wajane,Yatima , Wenye shida na Tabu; Kabula anasema Dhihirisha na Upendo anasema Hapa Nilipo!!!!!!!


Leo ni siku ya Mama,Tuwaweke kwenye Maombi,Sala,Dua, Wajane,Yatima, Wenye Shida na Tabu.Mungu awasimamie katika Maisha yao Wajane na Yatima,Mungu uwaguse wenye Shida na Tabu, Wengine wanahitaji Watoto,Wanahitaji kuwa MAMA/BABA,Kuna wanohitaji Wenza/Ndoa,Elimu,Chakula,Malazi,Upendo,Faraja.Wagonjwa walio Hospitalini na Majumbani.Waliokata Tamaa.Waliopoteza Wapendwa wao katika Majanga mbalimbali.Walio vitani.Na mengine Meengi. Mungu uwaguse kwa Mkono wako wenye Nguvu.

Neno la leo;Matendo ya Mitume:9;36-43.Na Mwanafunzi mmoja alikuwa Yafa Jina lake Tabitha,Tafsiri yake ni Dorkasi[yaani Paa];Mwanamke huyu  alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.Endelea na Uwe na wakati mwema.