Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 5 April 2012

Watoto na Mitindo,Kutoboa/Kutoga Masikio!!!!

Haya Waungwana;Wazazi/Walezi Unaonaje watoto kutoboa/kutoga masikio wakiwa Wadogo?jee Tunawafurahisha au Tunajifurahisha?ni vyema atoboe/kutoga yeye mwenyewe akikua au bora tuwafanyie labda wakikua watatulaum?
Karibuni Sana kwa Maoni na Ushauri.Pamoja!!!!!!

Tuesday, 3 April 2012

Shilingi ya ua tena Maua!!!!!!!


Waungwana sina la kuongezea hapo!!Jee Pesa ni kila kitu?Karibuni sana kwa Maoni na Kuelimishana kwa Upendo.

NDG. OMARY MJENGA MWAKILISHI WA UNOPS NCHINI SIERA LEONE AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI.


Ndg. Omary Mjenga akipiga picha ya kumbukumbu wakati alipokwenda kumtembelea na kumuaga Rais Jakaya Kikwete jana Ikulu.
Hapa ndugu Mjenga akipiga picha na Naibu Waziri wa Jinsia, Watoto na maendeleo ya jamii, wakati alipokwenda kumtembelea.

Baada ya kutoka kuonana na Viongozi hao alishiriki Dinner Party na Wanafunzi wenzake aliosoma nao Shule ya Sekondari Songea Boys ndani ya viunga vya Rose Garden akiwemo na Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mh. Philipo Mulugo.
Picha zaidi mtazipata baadae za tukio hili la kihistoria, ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika katika Pub ya KAPINGAZ Pub wakati huo tukimpongeza Naibu Waziri Mh. Mulugo kwa kuteuliwa.
Wana BOX 2 (Wana Luhila) walimpendekeza Ndg. Henry O. Kapinga kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mpaka pale tutakapo itisha uchaguzi Rasmi.

Omary Mjenga anaondoka leo kurudi Siera Leone tayari kwa kuendelea na kazi zake za UNOPS.

Habari kutoka http://kapingaz.blogspot.co.uk/
Ahsante sana.

Sunday, 1 April 2012

Nawatakia J'Pili Njema,Burudani-AIC Chang'ombe na Bahati Bukuku,Sikiliza mwenyewe!!


Wapendwa muwe na J'Pili yenye Amani na Baraka Tele!!!!!!Neno la Leo;zaburi:12;1-8.Bwana UokoeMaana Mcha Mungu amekoma,Maana Waaminifu wametoweka katika Wanadamu.....Endelea.

Saturday, 31 March 2012

Chaguo la Mswahili Leo,mambo ya Taarab-Utalijua Jiji!

Haya Waungwana mambo hayo, hahaaaa Mambo ya Taarab... Swahili na Waswahili twende Sote sasa!!

Thursday, 29 March 2012

MAZISHI YA MAREHEMU DENIS OSWALD KAPINGA


Ndg. Joseph Oswald Kapinga

Ndugu Joseph Kapinga pichani hapo juu anapenda kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki kuwa Ratiba ya mazishi ya mpendwa mdogo wetu Denis O. Kapinga yatafanyika leo Tarehe 29/03/2012 katika makaburi ya Sinza karibu na ukumbi wa mwika.

Ratiba itakuwa kama ifuatavyo:

Mwili wa marehemu utafika Nyumbani maeneo ya Sinza karibu na New White Inn Bar bara bara ya Sinza uzuri mnamo saa 6.00 Mchana kutoka Hospitali ya Mwananyamala.

Mwili utaagwa nyumbani saa 7.00 Mchana na baadae utapelekwa kanisa la Roman Catholic Sinza kwa Ibada.

Baada ya hapo Saa 8.30 Mchana mwili wa marehemu utapelekwa Makaburi ya Sinza kwenye nyumba yake ya milele.

"BWANA ALITOA NA BWANA 

Poleni sana Familia ya Kapinga.
Swahili na Waswahili tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu kwenu.

Mungu awatie Nguvu.
Ulale kwa Amani kaka Denis.O.Kapinga.