Friday, 27 April 2012
Wednesday, 25 April 2012
Swali kutoka kwa Mwanamke wa Shoka[da'Mija] na Blogger wa Kwanza Mwanamke Mswahili!!!
Kwangu mimi ni Mwanamke wa Shoka huyu dada,Kichwa,mama Vipaji.
Ni Mwanamke wa Kwanza Blogger Mswahili mimi kumfahamu.blog yake http://damija.blogspot.co.uk
Da'Mija na Wanawake wa Shoka.
Swali;wewe Unafikiri Wanawake wa Shoka Wakoje?.Mama MM[Jina lake linaanzia na M,Mume wake M, watoto wao M.M] |
Kidada zaidi au vipi!!Una mbwembwe wewe dadake.
Nanukuu.."Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au Kuto OA Kabisa?."
Nami ngoja niulize kulingana na swali.."Kwani nafasi ya mwanamke ni ipi katika ndoa..Je ni kupika na kufanya kazi za ndani? au kwa maana nyingine ni kwa nini hasa mwanaume huamua kuoa?
Wanaume tungependa majibu yenu zaidi hapa...
Monday, 23 April 2012
Siku kama ya leo kaka Twahil Alizaliwa na Siku kama ya Leo Tulimpoteza baba yetu Kipenzi!!!!!!
Siku kama ya leo,Bibi na Bwana M.S.Kiwinga wa Ilala Sharifu Shamba,Dar-es-salaam.Walipata mtoto wa kiume na wakamwita Twahil.Mtoto huyu Siku alipofikisha umri wa miaka 9.Ndiyo Siku ambayo baba yetu, Kipenzi chetu,Muhimili Wetu,Faraja yetu,Rafiki yetu, yaani ni kila kitu Maishani mwetu,Marehemu M.S.KIWINGA.Aliga DUNIA!!! Ohhhhh Siku ambayo Familia hii hatuwezi kuisahau kamweee.
Tunamshuru Mungu kwa kila jambo.Kwani yeye huyu Mungu ndiye alisimamia makuzi yetu mpaka leo hii.
Hongera sana kaka Twahil, Mungu azidi kukubariki na kukulinda kila iitwapo Leo.
Tupo pamoja katika Siku yako hii muhimu japo ni siku ngumu kwetu.
Hongereni Wooote Mliozaliwa Leo na Pia Poleni sana mliopoteza Wapendwa wenu/wetu Leo.
Mungu awabariki na kuwalinda.
Wenu Rachel-siwa[Mwanapenza]hili mwanapenza ni jina la mama wa baba yangu mzazi[BIBI, Asha Penza]. Basi baba yetu alikuwa hupenda kutuita watoto wa kikeMAMA.
PAMOJA SANA,UPENDO DAIMA!!!!!!

Sunday, 22 April 2012
J'Pili iwe njema kwa Wote!!Burudani-Jehovah You are the most high God na-Igwe Midnighi Crew!!!!
Akawagawanyia Lea, na Rahel, wale vijakazi wawili,wana wao.
Neno la leo;Mwanzo33:1-11.
Pamoja sana katika yote Wapendwa.
Saturday, 21 April 2012
Chaguo la Mswahili Leo;Professor Jay -Anasema- hapo vipi?kama Ipo,Ndiyo Mzee!!!!!!!
Burudani na Maneno muruwaaa kutoka kwake Mswahili Professor Jay-Msikilize kwa makini.NDIYO MZEE!!.
Pamoja Sana, Hapo Vipi?
Thursday, 19 April 2012
MWAKILISHI MKAAZI WA UNOPS NDUGU OMARY MJENGA AKIBADILISHANA MIKATABA YA UJENZI WA HOSPITALI YA WATOTO NCHINI SIERA LEONE
Ndugu Mjenga wakijadiliana jambo na Naibu Mwakilishi wa UNICEF Bw Gopal Sharma wa nchini Siera Leone
Kutoka kulia ni Bwana Omar Mjenga, Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, akibadilisha mikataba ya ujenzi wa hospitali tatu za kisasa za watoto na Naibu Mwakilishi wa UNICEF Bw Gopal Sharma aliyemwakilisha Bw Mahimbo Mdoe ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Nchini Sierra Leone na Kushoto, ni mwakilishi wa Waziri wa Afya wa Siera Leone.
Bw Mahimbo ni Mtanzania mwingine mwenye cheo cha uwakilishi. Mtanzania mwingine mwenye cheo cha uwakilishi ni Bw Gabriel Rugalema, ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa FAO Nchini Sierra Leone. Tanzania inazidi kutamba katika nyanja za kimataifa
Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog. http://kapingaz.blogspot.co.uk
Ahsanteni sana.

Wednesday, 18 April 2012
Jikoni Leo ni Kakazzz,Burudani-Tmk wanaume family - Dar mpaka moro!!!!!!
Kina kaka walioandaa huu msosi. |
Kachumbari |
Samaki au dagaa? |
vipi hapo ugali utaisha? |
Mimi nafikiri mboga za leo mwenzake Nguna/Ugali,Jee mwenzangu? |
Mboga ya Majani. Jee ukishiba utashushia na nini? |
Kumbe wakiamua wanaweza,Huko nyuma tulijadili kuhusu ''WANAUME NA JIKO'',Kaka S. [Sam mwana wa Mbogo]Alielezea vyema sana, Hasa yeye anavyohusika Jikoni.Pia akasema Wanawake wengi wakisaidiwa huwa Wanatabia ya Kujisahau.
Kaka zangu hawa nao wanasema wao hupenda kujipikia zaidi kuliko kupikiwa.
Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au Kuto OA Kabisa?.
Jee wewe Mwenzangu una Maoni,Ushauri Gani? Pamoja sana!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)