Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 30 April 2012

Wimbo Mpya "Uhuru wa Habari" kutoka Ngoma Africa band aka FFU





                  FFU wa Ngoma Africa Band wameachia Jipya "Uhuru wa Habari"
                  Unasikika at www.ngoma-africa.com


Kwa kawaida wanahabari na vyombo vyao ndio wanarusha hewani habari za
matukio mbali mbali pamoja wasanii na burudani zao kwa jamii,
Lakini bendi maarufu Ngoma Africa aka FFU imewageuzia kibao !!
Kuliweka hewani song jipya "Uhuru wa habari" wimbo huo mpya
utunzi wake kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na
kijana Christian Bakotessa aka Chris-B,ambaye pia ni mpiga
gitaa la solo(mtutu) wa kikosi kazi iko.
Bendi hiyo maarufu Ngoma Africa yenye makao yake kule ujerumani,
miezi michache tu iliachia hewani CD ya "Miaka 50 ya Uhuru" na sasa
wanarusha hewani "Uhuru wa habari" ,
Taarifa za kuhaminika zinaeleza kuwa Remix ya wimbo huo pia itakua
hewani siku za usoni,katika Remix hiyo kutakua na majina mengi ya wa
dau wa habari ambao wanachangia kuijulisha jamii habari mbali mbali.
Sikiliza na pata burudani ya bure katika ffu camp at www.ngoma-africa.com
au http://www.ngoma-africa.com


















Sunday, 29 April 2012

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani-liko lango moja wazi,Bwana Usehemu Yangu,Si Mbali



Nawatakia J'Pili Yenye Furaha,Upendo,Uvumilivu,Fadhili,Busara,Kiasi na Shukrani.
Utamlinda yeye ambaye moyo wake  Umekutegemea katika Amani Kamilifu,Kwa kuwa Anakutumaini
Neno la Leo;Isaya 26:3-4.
Mbarikiwe Woooote.

Friday, 27 April 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Sweet Mother ,Wagadu Gu,Colombia,!!!!!!!!



Wakaka na Karikiti!!!!
Haya Waungwa, yakale ni Dhahabu Waswahili wanasema au?
Kuna lolote unakumbuka hapa?


Inavuka soxxxx kinabakia kiatuuuu.
Muwe na wakati mwema!!!!!!!!

Wednesday, 25 April 2012

Swali kutoka kwa Mwanamke wa Shoka[da'Mija] na Blogger wa Kwanza Mwanamke Mswahili!!!

Kwangu mimi ni Mwanamke wa Shoka huyu dada,Kichwa,mama Vipaji.
Ni Mwanamke wa Kwanza Blogger Mswahili mimi kumfahamu.blog yake http://damija.blogspot.co.uk
Da'Mija na Wanawake wa Shoka.
Swali;wewe Unafikiri Wanawake wa Shoka Wakoje?.

Haya tukiachana na hayo, Shuka Chini uone Swali lake analotaka KuJibiwa,Linatokana na  Mada ya Jikoni leo ni Kakazz.
Mama MM[Jina lake linaanzia na M,Mume wake M, watoto wao M.M]
Kidada zaidi au vipi!!Una mbwembwe wewe dadake.
Nanukuu..
"Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au Kuto OA Kabisa?."


Nami ngoja niulize kulingana na swali.."Kwani nafasi ya mwanamke ni ipi katika ndoa..Je ni kupika na kufanya kazi za ndani? au kwa maana nyingine ni kwa nini hasa mwanaume huamua kuoa?


Wanaume tungependa majibu yenu zaidi hapa...

        

Monday, 23 April 2012

Siku kama ya leo kaka Twahil Alizaliwa na Siku kama ya Leo Tulimpoteza baba yetu Kipenzi!!!!!!

Siku kama ya leo,Bibi na Bwana M.S.Kiwinga wa Ilala Sharifu Shamba,Dar-es-salaam.Walipata mtoto wa kiume na wakamwita Twahil.Mtoto huyu Siku alipofikisha umri wa miaka 9.Ndiyo Siku ambayo baba yetu, Kipenzi chetu,Muhimili Wetu,Faraja yetu,Rafiki yetu, yaani ni kila kitu Maishani mwetu,Marehemu M.S.KIWINGA.Aliga DUNIA!!! Ohhhhh Siku ambayo Familia hii hatuwezi kuisahau kamweee.

Tunamshuru Mungu kwa kila jambo.Kwani yeye huyu Mungu ndiye alisimamia makuzi yetu mpaka leo hii.


Hongera sana kaka Twahil, Mungu azidi kukubariki na kukulinda kila iitwapo Leo.
Tupo pamoja katika Siku yako hii muhimu japo ni siku ngumu kwetu.


Hongereni Wooote Mliozaliwa Leo na Pia Poleni sana mliopoteza Wapendwa wenu/wetu Leo.
Mungu awabariki na kuwalinda.


Wenu Rachel-siwa[Mwanapenza]hili mwanapenza ni jina la mama wa baba yangu mzazi[BIBI, Asha Penza]. Basi  baba yetu  alikuwa hupenda kutuita watoto wa kikeMAMA.
                       PAMOJA SANA,UPENDO DAIMA!!!!!!

Sunday, 22 April 2012

J'Pili iwe njema kwa Wote!!Burudani-Jehovah You are the most high God na-Igwe Midnighi Crew!!!!

Muwe na J'pili njema yenye Amani na Baraka.
Akawagawanyia Lea, na Rahel, wale vijakazi wawili,wana wao.
Neno la leo;Mwanzo33:1-11.
Pamoja sana katika yote Wapendwa.