(Lifestyle)Jamii,Tamaduni ,Matukio,Maisha ya Waswahili. Wapendao Kiswahili/Waswahili,Marafiki wa Swahili na Waswahili, Na Mengineyo ya Karibu, Yahitajikayo Kujuzwa Waswahili.Karibuni sana!!!!!!!
Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Mchague
JOSEPH LUKAZA ili aweze kuibuka mshindi katika shindano la EXCEL WITH
GRAND MALT katika chuo kikuu cha Dodoma katika Category ya Innovation
Nominee
Jinsi ya kushiriki kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa simu unaandika
"INV UDOM JOSEPH LUKAZA 3rd year" alafu unatuma kwenda namba 0653202000.
Muonekano wa kitabu cha mapishi cha"A Taste of Tanzania".
Cover ame-Design Mwenyewe na Picha amepiga mwenye.Kitabu kitatoka hivi karibuni.
Utakipataje;Ataweka wazi jinsi gani unaweza kupata Kitabu.Ukiingia pale kwake kunasehemu ya mawasiliano,Unaweza kuwasiliana nae Zaidi kupitia http://www.tasteoftanzania.com
Jee da'Miriam anajua KISWAHILI?JIBU;Ndiyo,anakichapa haswa, kama ulivyoona kwenye ile post iliyopita niliandika ni Mswahili.
Nafikiri nimewajibu nijuavyo Waungwana mlionitumia Email na mlionitumia Messages kwenye sim.Na nimeweka hapa kama kuna wengine waliokuwa na maswali kama haya nao Wamepata Jibu.
Haya Waungwana pata mapishi ya UJI na FUTARI kutoka kwa da'Miriam Rose.Hapo juu.
Hapo chini;Mapishi ya "VITUMBUA"Kutoka kwa da'Cecy anapatikana http://mapishinacecy.blogspot.co.uk.
Mswahili mimi kupika vikorombwezo saaaana siweziiiiii,Najua kupika kiasi cha Kula MUBENA yangu na Watoto yangu na Wageni kidogo tuu,Si kila mtu anaweza kila kitu jamani, Watu na VIPAJI Vyao.MIMI nitakuwa nakurushia Matukio tuu hapa.Na nikipata Muda nitaweza Kuwatembelea Wapishi Nyumbani kwao na Kuwawekea MAZUNGUMZO na MAPISHI HAPA!!AU VIPI WAUNGWANA.SWAHILI NA WASWAHILI!!!PAMOJA SANA TUU.
imi huwa navutiwa mnoo na kazi zake dada huyu.Huwa sisiti kumuuliza pale nitakapo kujua zaidi.Sijapata nafasi ya k HayaWaungwana leo nimewaletea da'Mriam Rose wa Kinunda.
Mukutana nae,Lakini kwa mawasiliano tuu kwangu ni mtu asiye na Majivuno,dharau,Umimi/Ubinafsi.Ni dada Mcheshi na mwenye Upendo, na meeengi.
Hongera sana na Ahsante sana da'Miriam Rose kwa yooote,Mungu azidi kukubariki.
Kufahamu zaidi kazi zake na yeye ni nani ingia "Taste of Tanzania" http://www.tasteoftanzania.com
Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake. Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.
Wimbo
huu unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI
YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu
umerekodiwa kuhamasisha na kumchangia Sajuki. Kutoa ni moyo bado
hujachelewa. Unaweza kutuma mchango wako kupitia AKIBA BANK A/C # 050000003047 A/C ni ya mke wake Sajuki, Wastara Juma au unaweza kutuma kupitia M PESA 0762189592.
Mimi na wewe tunahitajika katika hili.
Habari zaidi na Picha,utazipata. http://www.jestina-george.com