mwanamke akifanya vitu vyake.Picha kwa hisani ya da'Jane Siame wa http://j2wisdom.blogspot.co.uk |
Waungwana natumai wote Hamjambo.
"Wanake na Shughuli " Kumekuwa na Shughuli nyiingi sana zinazohusishwa wanawake tuu.Jee Wanaume Hampendi/Hawapendi Shughuli/kujichanganya peke yenu/Yao?
Au sisi Wanawake ndiyo haswaa tunatakiwa kujichanganya,kufurahi,kukutana wenyewe?
Na jee kwanini tunapoalikana hizo shughuli tunaambiana kuwa ni ya "WANAWAKE TUU" Sasa basi ukienda huko unakuta Dj,Mchukua matukio, Mara kaka,Mjomba kaja na mengine meeengi yanafanywa na "WANAUME".Jee kweli wanawake wa leo hakuna wakutosha kufanya hizo kazi?
Je na hawa MASHOGA Tumeshawaweka kwenye kundi Letu?
Vipi unapoaga Nyumbani kwa baba Ngina[mume] unaenda kwenye Shughuli za Wanawake tuu, nae anakupeleka na kuishia mlangoni anarudi Nyumbani.
Akikufuata anakutana na Wanaume kibao wanatoka humo kwa Shughuli jee hii imekaaje?
Mpenzi Msomaji wewe una Mawazo,Maoni,Ushauri Gani katika hili?
Karibuni sana Tuelimishane Kwa Upendo!!!!