Mrembo wa enzi hizooooo |
Nipe siri ya urembo huu |
Waungwa Leo nimewaletea Mrembo wa zamani kidogo,lakini mimi kwangu bado wananibamba sana.
Angalia hajajichubua,Hana makoroooombwezo meengi,Shedo za kuwaaakaa,Jee Hajapendeza?
Na sasa naona kama vimitindo tindo vya zamani vinarudi, Sijui kukosa ubunifu, Ya metushinda au kukumbukia Enzi?
Huyu yeye hakuweka dawa Nywele wala kusuka,Lakini wapo pia wazamani waliokuwa wakisuka,Nywele za Uzi,Rafya,Jicho la mke wenza,Kilimanjaro, walibana Mchicha, waliweka Zazuuu, wali roli , Waliweka Kan'ta, Walifunga Vilemba na..... duuuh nimengi nao Walikuwemo sana tuu.
Jee kunachochote cha Mitindo ya Zamani wewe bado Unapenda au Kukumbuka? na nini Kimekugusa/Kuvuti, kwa huyu Mrembo?
Unapicha za BABA/MAMA za Wakati huo wakiwa Vijana na Unapenda Tujifunze Mitindi yao?
Usiwe na Tabu Unaweza kututumia Kupitia email.rasca@hotmail.co.uk
Karibuni sana Waungwa!!!!!