Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 16 May 2012

Mswahili;SAM MACHOZI - MY ANGEL.{OFFICIAL VIDEO}

Hii ni yenu.....!! ni video yangu ya kwanza kama sam machozi nigependa sana saport zenu wa TZ ili niweze kuipeleka bendera yetu mbele kimataifa zaidi tuamini kama tunaweza na tutaweza mungu yupo na sisi milele amine... ni sam machozi`TO ALL MY BEAUTIFUL PEOPLE...!




Hayo ni Maneno yake kaka Sam Machozi.

Pamoja sana Waungwana!!! Swahili na Waswahili.

Tuesday, 15 May 2012

Siku kama ya Leo da'Masika na Bw'Jamal,Waliungana na Kuwa Mke na Mume. Burudani: Nitadumu nae!!!!

                                  Nakuvisha/kuvalisha Pete[Pingu] hii..............
                                     Bwana Jamal James Umekubali..............
                                  Mke mkeo kaka J .J
                               Mama Masika katikati, Hongera mama.
                    Mwenyewe da'Masika, Raha jipe Mwenyewe!!!
                                  Mwenye Bw'J.J.Mwakitalu.
                           Shughuli Watu na Watu Walikuwepo.
BIBI na BWANA MWAKITALU.
Na Wamejaaliwa kupata Watoto Wawili
.
Tunawatakia kila lililo jema katika Maisha yenu,Mungu azidi kuwabariki na Ndoa hii Idumu!!!!

Kama una lolote unataka kushiriki nasi, tuma kupitia Email.rasca@hotmail.co.uk
                         Pamoja sana Waungwana.

Monday, 14 May 2012

Wanawake na Urembo;Ya kale ni Dhahabu!!!Burudani-Rangi ya Chungwa,Pamelah!!

Mrembo wa enzi hizooooo
Nipe siri ya urembo huu


Waungwa Leo nimewaletea Mrembo wa zamani kidogo,lakini mimi kwangu bado wananibamba sana.
Angalia hajajichubua,Hana makoroooombwezo meengi,Shedo za kuwaaakaa,Jee Hajapendeza?

Na sasa naona kama vimitindo tindo vya zamani  vinarudi, Sijui kukosa ubunifu, Ya metushinda au kukumbukia Enzi?

Huyu yeye hakuweka dawa Nywele wala kusuka,Lakini wapo pia wazamani waliokuwa wakisuka,Nywele za Uzi,Rafya,Jicho la mke wenza,Kilimanjaro, walibana Mchicha, waliweka Zazuuu, wali roli , Waliweka Kan'ta, Walifunga Vilemba  na..... duuuh nimengi nao Walikuwemo sana tuu.

Jee kunachochote cha Mitindo ya Zamani wewe bado Unapenda au Kukumbuka? na nini Kimekugusa/Kuvuti,  kwa huyu Mrembo?
Unapicha za BABA/MAMA za Wakati huo wakiwa Vijana na Unapenda Tujifunze Mitindi yao?

Usiwe na Tabu Unaweza kututumia Kupitia email.rasca@hotmail.co.uk

Karibuni sana Waungwa!!!!!

Sunday, 13 May 2012

Nawatakia J'Pili Njema na Hongera kina MAMA!!Burudani; mwaitege-mama ni mama.Bahati-Mapito!!!

Da'Rehema na Mwanawe Chance
Wifi'Rehema na Mwanawe Farid.


Nawatakia J'Pili na Hongera kina MAMA Woote popote Mlipo!!
 Kila lenye Kheri,Baraka,Upendo,Uvumilivu,Utuwema,Umoja,Huruma na REHEMA!!!

Wengine tulisha Sheherekea, lakini si Mbaya tukiungana Nanyi tena.

Leo da'REHEMA na wifi REHEMA ndiyo wanaotuwakilisha SWAHILI na WASWAHILI.katika Siku ya MAMA.

3;REHEMA na kweli zisifarakane nawe.6;Katika njia zako zote mkiri yeye,Naye atakuonyesha MAPITO yako.
Neno la Leo;Mithali:3;1-7

Saturday, 12 May 2012

Chaguo la Mswahili Leo;Kutoka kwa Familia ya Penza.Burudani;Diamond - Moyo wangu,Mbagala,Mawazo!!!!!



Diamond na Chance
Diamond na da'Phoibe[Mwana Penza]
Waungwana Leo sipo mbaali sana,yaani si za Kale,Kijana anabamba/anafanya vyema katika Kazi yake, au vipi.
Jee wewe Muungwana Kijana Almasi anakubamba/unapenda kazi yake?Zaidi ni Sauti,Maneno,Muonekano,Uchezaji, Manjonjooo kama si Vionjooo?

Twende Sootee sasaaa, Moyo Wanguuu ooh Moyo wanguuu oooohhh.....Makuti na Mkoleeeeee duuhh mpaka Mkoleeeee!!

Pamoja sana na muwe na J'Mosi njema!!!!!!

Friday, 11 May 2012

Wanawake na Shughuli;Burudani-Bembeleza,Pii pii!!!!


mwanamke akifanya vitu vyake.Picha kwa hisani ya da'Jane Siame wa http://j2wisdom.blogspot.co.uk


Waungwana  natumai wote Hamjambo.

"Wanake na Shughuli " Kumekuwa na Shughuli nyiingi sana zinazohusishwa wanawake tuu.Jee Wanaume Hampendi/Hawapendi Shughuli/kujichanganya peke yenu/Yao?


Au sisi Wanawake ndiyo haswaa tunatakiwa kujichanganya,kufurahi,kukutana wenyewe?


Na jee kwanini tunapoalikana hizo shughuli tunaambiana kuwa ni ya "WANAWAKE TUU" Sasa basi ukienda huko unakuta Dj,Mchukua matukio, Mara kaka,Mjomba kaja na mengine meeengi yanafanywa na "WANAUME".Jee kweli wanawake wa leo hakuna wakutosha kufanya hizo kazi?
Je na hawa MASHOGA  Tumeshawaweka kwenye kundi Letu?

Vipi unapoaga Nyumbani kwa baba Ngina[mume] unaenda kwenye Shughuli za Wanawake tuu, nae anakupeleka na kuishia mlangoni anarudi Nyumbani.
 Akikufuata anakutana na Wanaume kibao wanatoka humo kwa Shughuli jee hii imekaaje?


Mpenzi Msomaji wewe una Mawazo,Maoni,Ushauri Gani katika hili?


Karibuni sana Tuelimishane  Kwa Upendo!!!!

Thursday, 10 May 2012

Mchague Joseph Lukaza !!!!!!!


Mchague JOSEPH LUKAZA ili aweze kuibuka mshindi katika shindano la EXCEL WITH GRAND MALT katika chuo kikuu cha Dodoma katika  Category ya Innovation Nominee
Jinsi ya kushiriki kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa simu unaandika
"INV UDOM JOSEPH LUKAZA 3rd year" alafu unatuma kwenda namba 0653202000.
Na unaweza kupiga kura kwa kutumia tovuti