(Lifestyle)Jamii,Tamaduni ,Matukio,Maisha ya Waswahili. Wapendao Kiswahili/Waswahili,Marafiki wa Swahili na Waswahili, Na Mengineyo ya Karibu, Yahitajikayo Kujuzwa Waswahili.Karibuni sana!!!!!!!
Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Hii ni yenu.....!! ni video yangu ya kwanza kama sam machozi nigependa
sana saport zenu wa TZ ili niweze kuipeleka bendera yetu mbele
kimataifa zaidi tuamini kama tunaweza na tutaweza mungu yupo na sisi
milele amine... ni sam machozi`TO ALL MY BEAUTIFUL PEOPLE...!
Waungwa Leo nimewaletea Mrembo wa zamani kidogo,lakini mimi kwangu bado wananibamba sana.
Angalia hajajichubua,Hana makoroooombwezo meengi,Shedo za kuwaaakaa,Jee Hajapendeza?
Na sasa naona kama vimitindo tindo vya zamani vinarudi, Sijui kukosa ubunifu, Ya metushinda au kukumbukia Enzi?
Huyu yeye hakuweka dawa Nywele wala kusuka,Lakini wapo pia wazamani waliokuwa wakisuka,Nywele za Uzi,Rafya,Jicho la mke wenza,Kilimanjaro, walibana Mchicha, waliweka Zazuuu, wali roli , Waliweka Kan'ta, Walifunga Vilemba na..... duuuh nimengi nao Walikuwemo sana tuu.
Jee kunachochote cha Mitindo ya Zamani wewe bado Unapenda au Kukumbuka? na nini Kimekugusa/Kuvuti, kwa huyu Mrembo?
Unapicha za BABA/MAMA za Wakati huo wakiwa Vijana na Unapenda Tujifunze Mitindi yao?
Usiwe na Tabu Unaweza kututumia Kupitia email.rasca@hotmail.co.uk
Waungwana Leo sipo mbaali sana,yaani si za Kale,Kijana anabamba/anafanya vyema katika Kazi yake, au vipi.
Jee wewe Muungwana Kijana Almasi anakubamba/unapenda kazi yake?Zaidi ni Sauti,Maneno,Muonekano,Uchezaji, Manjonjooo kama si Vionjooo?
Twende Sootee sasaaa, Moyo Wanguuu ooh Moyo wanguuu oooohhh.....Makuti na Mkoleeeeee duuhh mpaka Mkoleeeee!!
mwanamke akifanya vitu vyake.Picha kwa hisani ya da'Jane Siame wa http://j2wisdom.blogspot.co.uk
Waungwana natumai wote Hamjambo.
"Wanake na Shughuli " Kumekuwa na Shughuli nyiingi sana zinazohusishwa wanawake tuu.Jee Wanaume Hampendi/Hawapendi Shughuli/kujichanganya peke yenu/Yao?
Au sisi Wanawake ndiyo haswaa tunatakiwa kujichanganya,kufurahi,kukutana wenyewe?
Na jee kwanini tunapoalikana hizo shughuli tunaambiana kuwa ni ya "WANAWAKE TUU" Sasa basi ukienda huko unakuta Dj,Mchukua matukio, Mara kaka,Mjomba kaja na mengine meeengi yanafanywa na "WANAUME".Jee kweli wanawake wa leo hakuna wakutosha kufanya hizo kazi? Je na hawa MASHOGA Tumeshawaweka kwenye kundi Letu?
Vipi unapoaga Nyumbani kwa baba Ngina[mume] unaenda kwenye Shughuli za Wanawake tuu, nae anakupeleka na kuishia mlangoni anarudi Nyumbani. Akikufuata anakutana na Wanaume kibao wanatoka humo kwa Shughuli jee hii imekaaje?
Mpenzi Msomaji wewe una Mawazo,Maoni,Ushauri Gani katika hili?
Mchague
JOSEPH LUKAZA ili aweze kuibuka mshindi katika shindano la EXCEL WITH
GRAND MALT katika chuo kikuu cha Dodoma katika Category ya Innovation
Nominee
Jinsi ya kushiriki kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa simu unaandika
"INV UDOM JOSEPH LUKAZA 3rd year" alafu unatuma kwenda namba 0653202000.