Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 22 May 2012

Wa Afrika na Sherehe Zao;Nigerian Bride (Traditional Wedding) and Gele Styles!!!!

Swali; Jee WaTanzania tunaweza kuvaa nini kwenye Ndoa,Siku ya Posa,Siku ya kuagwa, K/party au Sherehe yoyote inayotakiwa Kuonyesha Utanzania Wetu?

Nimeshaona wengi wakivaa kimasi, Jee Vazi hili linaweza kututambulisha?

Waungwana karibuni sana katika Kuelimishana,Kushauriana  na Mapenzi yako katika Vazi la Nyumbani.
Pamoja sana .Swahili na Waswahli!!!!!

Monday, 21 May 2012

Jikoni Leo. Mswahili; da'Sophi na Tupike Pamoja!!! Angalia Video!!!!




Karibuni "tupikepamoja.com"


Habari utakazo zipata katika tovuti hii ni picha za video na maelezo ya kina kuhusu namna ya kupika mapishi na vyakula vizuri vya kimataifa muhimu zaidi ni rahisi kupika.
Tovuti hii ni kwa ajili ya watu wanaopenda kupika, kujaribu vyakula vipya na ladha mpya ili kuwashangaza rafiki na familia zao kwa ladha hizo. Maelekezo ya mapishi utakayopata hapa ni kwa ajili ya meza kuu ingawa wakati mwingine tunashirikiana nawe katika vinywaji na viburudisho (deserts & sweets).
kwa kuanzia ni matumaini yetu utafurahia kupika kama sisi.
Pia usisahau kututumia maoni yako, maswali na ujumbe tuweze kuboresha na kutimiza mahitaji yako, Asante kwa ushirikiano wako
Furahia chakula chako!

Kujua zaidi Mtembelee.www.tupikepamoja.com
Haya Waungwana Mambo hayo kazi kwenu na "Tupike Pamoja"

Hongera da'Sophi kazi nzuri.

Sunday, 20 May 2012

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani;Sarah K - Liseme.The Christ Ambassadors-Moyoni Mwangu na Kazi Tufanye!!!!!!



Watoto wa KKkT Kijito Nyama
Nawatakia J'Pili yenye Baraka, Upendo,Amani, Umoja na Furaha.
1;Haleluya.Msifuni Mungu katika Patakatifu pake;
Msifuni katika anga la uweza wake.
Neno la Leo:Zaburi ya 150:1-6. 

6;Kila mwenye Pumzi na Amsifu BWANA.
Haleluya!!!!!!!!!.

Saturday, 19 May 2012

Chaguo la Mswahili Leo;Celine&R.kelly- I'm Your Angel, The Step in the Name of Love. Na nyingineee!!!



 Waungwana Nawatakia j'Mosi yenye Amani na Furaha daima!!.
Leo ngoja Tuangalie/twende Pande hii.
 Sina Mengi Zaidi Nakusikiliza wewe tuu.Baada ya Burudani, Umekumbuka nini,Umeguswa,Umefurahi,Umenuna au? "Swahili na Waswahili" Pamoja sana

Friday, 18 May 2012

MTANZANIA DR ENGINEER SHABAN KACHUA ATUNUKIWA RASMI SHAHADA YAKE YA UDAKTARI WA FALSAFA NCHINI CANADA.


Dr Engineer Shaban Kachua mwenye joho lenye rangi nyekundu na Bluu akiwa na waafrika wenzake wakati wa alipotunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa falsafa Nchini Canada.
Hapa Dr Kachua akiwa amekaa mstari wa mbele kabisa na wahitimu wenzake.
Mama Mzazi wa Dr Kachua (mwenye blauzi nyeusi), akiwa na Mama mkwe wake, wote kwa pamoja walishiriki katika tukio la kihistoria la kutunukiwa Shahada ya PHD kwa mtoto wao nchini Canada.
Mrs Dr Shaban Kachua (Jemima) akiwa na furaha pamoja na watoto wao walishiriki katika shughuli ya kutunukiwa Mume wake shahada ya udaktari wa Falsafa (PHD).

Kwa sasa Dr Shaban Kachua anaishi Nchini Canada pamoja na familia yake. Sisi kama watanzania wenzake tunapenda kumpongeza sana kwa kuweza kuipeperusha vema Bendera yetu, tunapenda kumshauri pia, elimu yake hiyo aweze kuitumia pia kulisaidia Taifa lake la Tanzania hasa katika nyanja hiyo ya Sayansi, kwa kutambua zaidi tuna upungufu mkubwa wa wanasayansi katika Taifa letu.

HONGERA SANA
Asanteni sana KapingaZ http://kapingaz.blogspot.co.uk/

Thursday, 17 May 2012

Watoto na Vituko;Pata na Burudani!!!!!!

Waungwana Mambo hayo, sina la kusema,Zaidi unayo wewe!!!!!!
Pamoja sana sana.Swahili na Waswahili!!!!!!!!

Wednesday, 16 May 2012

Mswahili;SAM MACHOZI - MY ANGEL.{OFFICIAL VIDEO}

Hii ni yenu.....!! ni video yangu ya kwanza kama sam machozi nigependa sana saport zenu wa TZ ili niweze kuipeleka bendera yetu mbele kimataifa zaidi tuamini kama tunaweza na tutaweza mungu yupo na sisi milele amine... ni sam machozi`TO ALL MY BEAUTIFUL PEOPLE...!




Hayo ni Maneno yake kaka Sam Machozi.

Pamoja sana Waungwana!!! Swahili na Waswahili.