Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 3 June 2012

Nawatakia J'Pili Njema,Burudani- Upendo Nkone,Abihudi Misholi!!!!!!


6.Lakini nasema neno hili,Apandaye haba atavuna haba;Apandae kwa Ukarimu Atavuna kwa Ukarimu.
7.Kila mtu na Atende kama alivyokusudia Moyoni mwake,si kwa Huzuni,wala si kwa Lazima;Maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa Moyo wa Ukunjufu.
Neno la Leo:Wakorintho9:6-15.

Mungu atubariki Sote!!!!

Saturday, 2 June 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Tupo Burundi;Ndugu zangu wa Buyenzi Mpo?!!!!!

 Bibi na Bwana Billy.Hongereni sana Kwa kupata mtoto wa kiume.Mungu amlinde na kumkuza vyema.Nanyi awape hekima katika malezi yenu.Ngoja leo niwasogeze nyumbani.
 

Waungwana "CHAGUO LA MSWAHLI LEO" Nimewapeleka BURUNDI.
Haya umeona waRundi waishio CANADA wanavyofunza watoto wao Utamaduni wao?Jee wewe unaonaje kuhusu hili la kuwafundisha watoto mambo yakwenu?

Jee unao wakati wa kuwafundisha watoto hata Kibuzi,Kinyunyu,Ukuti,Rede,Nyimbo hata zile za Mchakamchaka?Au Muda hautoshi?

Nakumbuka kama wikimbili 2 tulikutana Waswahili kwenye Mnuso Mmoja hivi, Baada ya Kushiba Tukaanza kuimba hii Nyimbo.

Alisemaaa  Alisemaaa,Alisema Nyerere Alisema,Vijana wangu wote Mmeleegea, Sharti Tuanze Mchaka Mchaka.................Hahahahaa

 Swahili na Waswahili Waungwana.

 Kama unalolote utahitaji kuwajuza wenzio. Tutumie Kupitia Email.rasca@hotmail.co.uk.Pamoja sana!!!!!!

Wednesday, 30 May 2012

Jikoni Leo; ni Wasomali na Darasa la Mapishi na Utamaduni wao;Wazazi wa Marekani.na Da'Mariam!!!!!!

Waungwana "Jikoni Leo" ni Wasomali;
Wazazi/Walezi wa Marekani Wakiwafundisha Watoto wao Jinsi ya Kupika na Tamaduni za Kwao.


Pia da'Mariam naye Hayuko Nyuma kuonyesha/Kuwafunza watu wengine Jinsi "East Africa" wapikavyo.
 

Hapa nimeona Wasomali wanajitahidi kuwafundisha kupika watoto wa kike tuu,Sijui watoto wa kiume kwao Hawapiki?au bado wanamambo yaleee mtoto wakike "LAKE JIKO".

Waungwana Mmejifunza nini kwa haya ya Wenzetu Wasomali?

Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

Pamoja sana."Swahili na Waswahili."

Tuesday, 29 May 2012

Wa Afrika na Sherehe zao;Leo ni Wadigo wedding , Kenya!!!!!!

Hahhahahhah Kadala,Mwanamke wa shoka, Mwanakwetu,Kadoda,Ndugu wa mimi na Waungwana Woooote,
Mambo hayo ya kupetipeti!!
Sina lazaidi Mengi Mnayo Wenyewe Yakheeeeee!!!!


Karibuni sana. "Swahili na Waswahili".Pamoja sana tuu.

Monday, 28 May 2012

Da'Tracey-Sarah,Atimiza Miaka 11!!!!!!!

Da'Tracey-Sarah
Da'Sandra akiandaa Keki
Tumtangulize Mungu kwanza katika Yote!!!

Leo umezima 11,mungu akulinde uzime 100!!!
Anaitwa Mkama; kwakuzima Mishumaa hayuko nyuma,Kama mtoto wako anasuasua kuzima,Tuwasiliane!!
da'Tracey akikata keki na da'Mija akihakikisha mambo yako sawa!!!

da'Elizabeth na da'Mija wakiandaa keki,watu tule!!kweli watoto wa Shoka,Mungu awabariki sana!!
Mama akimlisha Mwana!!
Da'Mija akilishwa na Rafiki yake kipenzi,Mungu azidi kuwaunganisha daima!!
Da'Tracey akilishwa na dada yake!!
Da'Sandra akilishwa na Mdogo wake, duuh kuna haja ya kuongeza sijui!!
Da'Anita akilishwa,Chezea yeye!!!
Da'Asiimwe akilishwa,huwa hana haraka wala maneno mengi,jicho tuu linaongea!!
Da'Manjula aliamua kupanda juu ya kiti,Ale kwa raha,nani anapenda Ufupi?
Kamanda Mkama a.k.a.Mzee wa Next,Akipata kipande chake!!!
Dada Mkubwa,Eliza naye akijipatia keki!!
Pamoja daima!!!!
Katuni/Vibonzo lazima tuangalie!!!
Mapoziiiiiii
Unahitaji wanamitindo? Tuwasiliane.....hahahahaha
Na muziki tulisakata, sikunyingine nitaweka Video!!!Lakini Zilipendwa waligomaaa!!!
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi,da'Mija[Mia] akipozi baada ya kazi kubwa!!
Da'Tracey[Sarah]Akipozi  na Kuwashukuru Wazazi,Ndugu,Jamaa na Marafiki kwa yooote!!!



Familia ya Isaac,Tunamshukuru sana Mungu kwa Mema Mengi aliyotutendea,Asante kwa kumtunza na kumlinda Mtoto wetu Tracey-Sarah na Familia pia.
Asante kwa Kumaliza SAT'S,Salama,wewe ulimlinda akiwa Shule ya Msingi pia Tunamuweka Mikononi mwako Aendapo Secondary.

Shukrani Nyingi Ziwaendee,Familia ya Nyotu[Kamau].Familia ya Manju[Da'Mija Mwanamke wa Shoka].Kaka Don,baba Eliza na Familia yako. Da'Maggie[dadake]Asante sana.

Mungu awabariki sana kwa Moyo wenu wa Upendo na Kutumia Muda wenu kuwa nasi.

Pamoja sana Wapendwa,MUNGU NI PENDO APENDA WATU.Nasi TUNAWAPENDA WOOOOOTE.

Friday, 25 May 2012

Waswahili wetu Leo;WaTanzania na Madawa ya Kulevya!!!!!!!

Haya Waungwana;Hawa ni Ndugu zetu,Jamaa zetu,Rafiki zetu,
Jee nani Alaumiwe? Muuzaji au Mtumiaji?
"Swahili na Waswahili" Pamoja sana.

Tuesday, 22 May 2012

Wa Afrika na Sherehe Zao;Nigerian Bride (Traditional Wedding) and Gele Styles!!!!

Swali; Jee WaTanzania tunaweza kuvaa nini kwenye Ndoa,Siku ya Posa,Siku ya kuagwa, K/party au Sherehe yoyote inayotakiwa Kuonyesha Utanzania Wetu?

Nimeshaona wengi wakivaa kimasi, Jee Vazi hili linaweza kututambulisha?

Waungwana karibuni sana katika Kuelimishana,Kushauriana  na Mapenzi yako katika Vazi la Nyumbani.
Pamoja sana .Swahili na Waswahli!!!!!