Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 10 June 2012

Mswahili wetu Leo;kaka Mod-Med[Mbuko]Raha Jipe mwenyewe!!!!!!

Mswahili Kaka Mbuko akijipa Raha mtaani Huko Holland[Uholanzi],Raha tele Tabu ya nini?

"Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!


Saturday, 9 June 2012

MASHUJAA MUSICA BENDI WAZIDI KUPAA NDANI YA BUSINESS CENTRE CHINI YA UONGOZI WA CHAZ BABA.




Kiongozi na mwimbaji wa Bendi maarufu wa Mashujaa Chaz Baba jana akizikonga nyoyo za mashabiki wake kwa nyimbo zake mpya ndani ya ukumbi wa Business Centre Maeneo ya makumbusho.
Mpiga tumba maarufu Afrika Mashariki wa Bendi ya Mashujaa MCD akipafomu ndani ya Business Centre jana Usiku.


Maua ya Mashujaa Band yakiwachengua mamia ya washabiki wao ndani ya Business centre jana usiku.

Bendi ya Mashujaa ni moja ya Bendi maarufu Nchini ambazo zinakuja juu katika medani ya muziki wa bendi na kuthamini thamani ya mwanamuziki.
habari zaidi utazipata.KapingaZBlog.

Asanteni.

Chaguo la Mswahli Leo;Mchanganyiko;ZAY B,DataZ,Mez B&RaYC,Cat-Z,AY,FA,Gk&Pauline Zongo na...Safi hiyooooo!!!!!!

Waungwana Leo hakuna Maneno Meengii, Ni Burudani tuu!!!!
Lakini hawa wengine wako wapi?
je Unakumbuka chochote kuhusu Burudani ya Leo?
 kibao kipi? na nini kinachokukumbusha?Tujuze basi.
Twende Sote sasa Safi hiyoooooo!!!!!!
"Swahili na Waswahili" Pamoja sana tuu.

Thursday, 7 June 2012

"Sing" for HM Queen Elizabeth II (Diamond Jubilee)!!!!!!!

Mmmmhhh Umoja ni Nguvu na Penye Wengi Pana Mengi!!!"Sauti tamuuu Twende Sote Waungwana,Lalalalalaaaaaaaaaaa.....Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!

Wednesday, 6 June 2012

Jikoni Leo; ni da'Maidana wa Tmark!!!!!!!!!

Mwenyewe da'Maidana,mamake na Taqqiyyah
Samaki na Mazagazaga na ameungwa/tiwa Nazi
Kitu Samaki kimepakuliwa
Samaki wa Kubanikwa
Visheti,Kashata,Keki, hivyo vyenye kidoti mie naviitaga vibata, sijui vyaitwaje?Hapa bado Ufuta jamani duuhh
Mikate,sijui wewe utaitaje kwani hapa kwangu kila mtu anajina lake!
                                           Ipo kwa umbo tofauti

Waungwana karibuni tena  "JIKONI LEO".Leo Mpishi wetu si Mwingine ni da'Maidana,Ni blogger Mwenza,Pia ni MjasiriaMali,Ukitaka kujua zaidi. Anapatikana.http://tmark-turn.blogspot.co.uk

Nimegundua Waswahili Wengi Wanapenda kupika na kujifunza Mapishi Mbalimbali.
Vipi wewe mwenzangu unapenda kupika?jee mbali na kupika Unapenda/Unaweza Kufanya  nini kwa Mikono yako?



Karibuni sana Waungwana katika yoote!!!!!!
"Swahili na Waswahili" pamoja sana!!!!

Tuesday, 5 June 2012

SHUKRANI KUTOKA KWA MCHUNGAJI JOHN KUPAZA WA KANISA LA BAPTIST TANGA.


Marehemu Mama Mchungaji John Kupaza
Familia ya Mchungaji John Kupaza wa Kanisa la Baptist Kisosora Tanga anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa wale wote waliojaribu kuokoa maisha ya Mke wake Mpendwa Marehemu Mama Mchungaji Kupaza na wale walioshiriki kwa dhati katika shughuli za mazishi.
Mchungaji J. Kupaza anapenda shukrani zake za dhati ziwafikie Baptist Convention of Tanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya Kuu ya Wanawake wa Baptist Tanzania, Dr. Lugano Mtafya, Umoja wa Makanisa ya Baptist Dar es salaam, Baptist Kanda ya Kaskazini, Umoja wa Makanisa Tanga, Manesi na Wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili, Hospitali ya Cancer ya Ocean Road, Hospitali ya Bombo Tanga, Madaktari na wauguzi wa Magomeni Baptist Center, Majirani wote wa Mchungaji Kupaza na watoto wa Marehemu Sarah, Samwel, Rosemary, Dr. Lawi, Potinna, David na Tumaini wote kwa pamoja wanawashukuru wote mlioshirikiana nao katika kipindi hiki kigumu. Mungu awabariki wote.
Marehemu Mama Mchungaji Kupaza alifariki Tar. 18/05/2012 Jijini Dar es slaam na kuzikwa Tarehe 21/05/2012 Jijini Tanga katika makaburi ya Bombo.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
AMEN.

Monday, 4 June 2012

Mambo ya Igatanzania!!Ungana nami kujua zaidi!!!!!!

Haya Waungwana mambo ya Igatanzania hayo!!!
Niwauzaji wa T-shirt,Jezi,Kanga,Vitenge,Viatu vya shanga,Bangili,Makembe na vitu vyooote vya urembo kutoka nyumbani Tanzania.

 Pia ni Wapishi wa vitafunwa/Vitafunio,Vyakula vyooote ujuavyo vya kiswahili.
Pata kitu Roho inapenda na waswahili wa "Igatanzania"

Wapo Coventry u.k.

kwa mawasiliano zaidi piga namba hii.07730008921.

KARIBUNI SANA WAUNGWANA.