Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 12 June 2012

Habari kuhusu kaka Med-Mod[Mbuko]Hajafa Yupo Hospitalini,Tuzidi Kuombea!!

Waungwana Habari nilizozipata sasa hivi, kwamba kaka Mbuko hajafa,Yupo Hospitalini, Tuungane pamoja katika KuMuombea apate kupona haraka.Nitawajulisha kinachoendelea.Mungu azidi kukupigania kaka Mbuko.

Sunday, 10 June 2012

Nawatakia J'Pili Yenye Furaha,Burudani;Kijitonyama Evangelical Choir !!!!!


Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;kwa maana Fadhili zake niza Milele.

Mshukuruni Mungu wa Miungu;kwa maana Fadhili zake ni za milele.

Waungwana  muwe na J'pili yenye Baraka,Amani,Shukrani na Fadhili.
Neno la Leo;Zaburi136:1-26. "Swahili na Waswahili".Pamoja sana!!!!!

Mswahili wetu Leo;kaka Mod-Med[Mbuko]Raha Jipe mwenyewe!!!!!!

Mswahili Kaka Mbuko akijipa Raha mtaani Huko Holland[Uholanzi],Raha tele Tabu ya nini?

"Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!


Saturday, 9 June 2012

MASHUJAA MUSICA BENDI WAZIDI KUPAA NDANI YA BUSINESS CENTRE CHINI YA UONGOZI WA CHAZ BABA.




Kiongozi na mwimbaji wa Bendi maarufu wa Mashujaa Chaz Baba jana akizikonga nyoyo za mashabiki wake kwa nyimbo zake mpya ndani ya ukumbi wa Business Centre Maeneo ya makumbusho.
Mpiga tumba maarufu Afrika Mashariki wa Bendi ya Mashujaa MCD akipafomu ndani ya Business Centre jana Usiku.


Maua ya Mashujaa Band yakiwachengua mamia ya washabiki wao ndani ya Business centre jana usiku.

Bendi ya Mashujaa ni moja ya Bendi maarufu Nchini ambazo zinakuja juu katika medani ya muziki wa bendi na kuthamini thamani ya mwanamuziki.
habari zaidi utazipata.KapingaZBlog.

Asanteni.

Chaguo la Mswahli Leo;Mchanganyiko;ZAY B,DataZ,Mez B&RaYC,Cat-Z,AY,FA,Gk&Pauline Zongo na...Safi hiyooooo!!!!!!

Waungwana Leo hakuna Maneno Meengii, Ni Burudani tuu!!!!
Lakini hawa wengine wako wapi?
je Unakumbuka chochote kuhusu Burudani ya Leo?
 kibao kipi? na nini kinachokukumbusha?Tujuze basi.
Twende Sote sasa Safi hiyoooooo!!!!!!
"Swahili na Waswahili" Pamoja sana tuu.

Thursday, 7 June 2012

"Sing" for HM Queen Elizabeth II (Diamond Jubilee)!!!!!!!

Mmmmhhh Umoja ni Nguvu na Penye Wengi Pana Mengi!!!"Sauti tamuuu Twende Sote Waungwana,Lalalalalaaaaaaaaaaa.....Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!

Wednesday, 6 June 2012

Jikoni Leo; ni da'Maidana wa Tmark!!!!!!!!!

Mwenyewe da'Maidana,mamake na Taqqiyyah
Samaki na Mazagazaga na ameungwa/tiwa Nazi
Kitu Samaki kimepakuliwa
Samaki wa Kubanikwa
Visheti,Kashata,Keki, hivyo vyenye kidoti mie naviitaga vibata, sijui vyaitwaje?Hapa bado Ufuta jamani duuhh
Mikate,sijui wewe utaitaje kwani hapa kwangu kila mtu anajina lake!
                                           Ipo kwa umbo tofauti

Waungwana karibuni tena  "JIKONI LEO".Leo Mpishi wetu si Mwingine ni da'Maidana,Ni blogger Mwenza,Pia ni MjasiriaMali,Ukitaka kujua zaidi. Anapatikana.http://tmark-turn.blogspot.co.uk

Nimegundua Waswahili Wengi Wanapenda kupika na kujifunza Mapishi Mbalimbali.
Vipi wewe mwenzangu unapenda kupika?jee mbali na kupika Unapenda/Unaweza Kufanya  nini kwa Mikono yako?



Karibuni sana Waungwana katika yoote!!!!!!
"Swahili na Waswahili" pamoja sana!!!!