Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 13 June 2012

Waswahili Wetu Leo;Twiga Stars: Tanzania's Soccer Sisters,Wanawake Wanaweza!!!!

Waungwana "Waswahili Wetu Leo";
Leo tuwaangalie Wanawake Waswahili Wanaocheza Mpira wa Miguu.
Wanawake hawa Wanavipaji au Wanalazimisha kwasababu ya  Maisha Magumu?
Jee Umeona Wanayopitia mpaka kufikia hapo?Unafikiri Wazazi sasa ni Wakati wa Kuamka na Kutambua hakuna Michezo ya Wanawake au Wanaume?
Jee Wewe Unaushauri,Maoni Gani kwa Wachezaji wetu wa Kike?.

Wewe unapenda Mpira? au Michezo/Ni Mchezo gani unapendelea kuangalia au kuucheza/ulicheza?jee Unaumudu?

Karibuni sana Waungwana katika Yote.Kujua zaidi kuhusu timu hii ya Twiga Stars ingia;www.twigastars.com
 "Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!!!!

Tuesday, 12 June 2012

Habari kuhusu kaka Med-Mod[Mbuko]Hajafa Yupo Hospitalini,Tuzidi Kuombea!!

Waungwana Habari nilizozipata sasa hivi, kwamba kaka Mbuko hajafa,Yupo Hospitalini, Tuungane pamoja katika KuMuombea apate kupona haraka.Nitawajulisha kinachoendelea.Mungu azidi kukupigania kaka Mbuko.

Sunday, 10 June 2012

Nawatakia J'Pili Yenye Furaha,Burudani;Kijitonyama Evangelical Choir !!!!!


Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;kwa maana Fadhili zake niza Milele.

Mshukuruni Mungu wa Miungu;kwa maana Fadhili zake ni za milele.

Waungwana  muwe na J'pili yenye Baraka,Amani,Shukrani na Fadhili.
Neno la Leo;Zaburi136:1-26. "Swahili na Waswahili".Pamoja sana!!!!!

Mswahili wetu Leo;kaka Mod-Med[Mbuko]Raha Jipe mwenyewe!!!!!!

Mswahili Kaka Mbuko akijipa Raha mtaani Huko Holland[Uholanzi],Raha tele Tabu ya nini?

"Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!


Saturday, 9 June 2012

MASHUJAA MUSICA BENDI WAZIDI KUPAA NDANI YA BUSINESS CENTRE CHINI YA UONGOZI WA CHAZ BABA.




Kiongozi na mwimbaji wa Bendi maarufu wa Mashujaa Chaz Baba jana akizikonga nyoyo za mashabiki wake kwa nyimbo zake mpya ndani ya ukumbi wa Business Centre Maeneo ya makumbusho.
Mpiga tumba maarufu Afrika Mashariki wa Bendi ya Mashujaa MCD akipafomu ndani ya Business Centre jana Usiku.


Maua ya Mashujaa Band yakiwachengua mamia ya washabiki wao ndani ya Business centre jana usiku.

Bendi ya Mashujaa ni moja ya Bendi maarufu Nchini ambazo zinakuja juu katika medani ya muziki wa bendi na kuthamini thamani ya mwanamuziki.
habari zaidi utazipata.KapingaZBlog.

Asanteni.

Chaguo la Mswahli Leo;Mchanganyiko;ZAY B,DataZ,Mez B&RaYC,Cat-Z,AY,FA,Gk&Pauline Zongo na...Safi hiyooooo!!!!!!

Waungwana Leo hakuna Maneno Meengii, Ni Burudani tuu!!!!
Lakini hawa wengine wako wapi?
je Unakumbuka chochote kuhusu Burudani ya Leo?
 kibao kipi? na nini kinachokukumbusha?Tujuze basi.
Twende Sote sasa Safi hiyoooooo!!!!!!
"Swahili na Waswahili" Pamoja sana tuu.

Thursday, 7 June 2012

"Sing" for HM Queen Elizabeth II (Diamond Jubilee)!!!!!!!

Mmmmhhh Umoja ni Nguvu na Penye Wengi Pana Mengi!!!"Sauti tamuuu Twende Sote Waungwana,Lalalalalaaaaaaaaaaa.....Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!