Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 17 June 2012

EXTRA BONGO WAZEE WA KIZIGO WAZIDI KULITIKISA JIJI NDANI YA MEEDA SINZA.




Ally Choki akiwaburudisha washabiki na wapenzi wa Extra Bongo ndani ya Meeda usiku wa kuamkia leo
Choki akichea show na wanenguaji wake wa Extra bongo ndani ya Meeda Sinza.
Banza Stone Mwana wa Masanja - AKA Jenerale akiimba nyimbo yake ndani ya Meeda Sinza.

Mmiliki wa KAPINGAZ Blog Henry Kapinga alikuwepo ndani ya Meeda Sinza, hapa akishoo luv na kuwapa Big Up Ally Choki na Banza Stone wakati Extra Bongo walipokuwa wanapamofu usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi huo.
Rapa maarufu namba moja Afrika mashariki wa Extra Bongo Kaba Tano akirap ndani ya Meeda Sinza usiku wa kuamkia leo

Saturday, 16 June 2012

Watoto na Kujifunza Lugha-Pata video ya Mtoto wetu Wa Burundi!!!!

Wazazi/Walezi hapo vipi?Leo sina Mengi nasubiri kutoka kwenu,Mjumbe Hauawiii!!!!"
SWAHILI na WASWAHILI "Pamoja sana!!!!!!!!!!

Friday, 15 June 2012

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-How to cook Russian salad (In Swahili)!!!!!!!

Waungwana; "JIKONI LEO;"Ni Tupike Pamoja wametoa Mapishi mapya ya Russian Salad,kwa njia ya Video.Lugha ni Kiswahili.
 Usikose kujifunza kupitia "TUPIKE PAMOJA" Mmmmmhh Tamu Saaaana.
Kuona mengi zaidi ingia;www.tupikepamoja.com au hapo pembeni kuna nembo yao bonyeza tuu.

 Pamoja sana Waungwana. "SWAHILI na WASWAHILI"

Thursday, 14 June 2012

Siku Kama Ya Leo da'Rehema [RayK] Alizaliwa,Burudani-Hakunaga by Suma Lee!!!!

Mwenyewe RayK
Bibi na Bwana Kiwinga!!!!!
Uzuri tangu Utotoni,ya Kale ni Dhahabu
Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita da'Rehema Alizaliwa.Tunakutakia kila lililo jema katika Maisha yako,Mungu azidi kukulinda wewe na Familia yako.Uwe Baraka kwa watu woote.Tunakupenda na kukuthamini.
Asante kwa yooote,Hakunaga Wifi wa mimi Pamoja Daima.

Swali kwa Waungwana; Hivi nini kinasababisha Mtu na Wifi zake wasielewane?Wivu,Chuki,Tamaa au.......


Karibuni sana kwa Maoni,Mawazo,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

Angalizo; Wifi zangu Sitaki kujifunza Kuharibu Nyumba zenu Akuuu hahahhahhaahahah!!!!!!!

Hakunaga hakunaga hakunaaaaa hakunaaa"Swahili na Waswahili" Pamoja sana.

Wednesday, 13 June 2012

TuMpigie Kura Christina SHUSHO;Viva Shusho Viva Tanzania!!!!!!!!

Waungwana;Tumpigieni Kura Christina Shusho aweze kupata tuzo ya Africa Gospel Music Award 2012
Jinsi ya kupiga kura nenda,
www.africagospelawards.com/nominate.html

VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA   "pamoja Tunaweza"

Waswahili Wetu Leo;Twiga Stars: Tanzania's Soccer Sisters,Wanawake Wanaweza!!!!

Waungwana "Waswahili Wetu Leo";
Leo tuwaangalie Wanawake Waswahili Wanaocheza Mpira wa Miguu.
Wanawake hawa Wanavipaji au Wanalazimisha kwasababu ya  Maisha Magumu?
Jee Umeona Wanayopitia mpaka kufikia hapo?Unafikiri Wazazi sasa ni Wakati wa Kuamka na Kutambua hakuna Michezo ya Wanawake au Wanaume?
Jee Wewe Unaushauri,Maoni Gani kwa Wachezaji wetu wa Kike?.

Wewe unapenda Mpira? au Michezo/Ni Mchezo gani unapendelea kuangalia au kuucheza/ulicheza?jee Unaumudu?

Karibuni sana Waungwana katika Yote.Kujua zaidi kuhusu timu hii ya Twiga Stars ingia;www.twigastars.com
 "Swahili na Waswahili" Pamoja sana!!!!!!!

Tuesday, 12 June 2012

Habari kuhusu kaka Med-Mod[Mbuko]Hajafa Yupo Hospitalini,Tuzidi Kuombea!!

Waungwana Habari nilizozipata sasa hivi, kwamba kaka Mbuko hajafa,Yupo Hospitalini, Tuungane pamoja katika KuMuombea apate kupona haraka.Nitawajulisha kinachoendelea.Mungu azidi kukupigania kaka Mbuko.