Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 18 June 2012

Wa Afrika na Sherehe zao,LeoTupo Malawi ni-Kachitsa na Farayi;Tradditional Wedding!!!!


Mwenyewe bi Arusi Mtarajiwa,da'Farayi
Bwana Arusi Mtarajiwa kaka Willy Kachitsa,Huingii hapo mmpaka utoe pesa!!!
MmePendeza sana Wapendwa!!!!!
Mmmmhh Mapenzi Motomoto!!!!
Waungwana Leo Tupo Malawi, kaka KACHITSA na da'FARAYI wanatarajia kuwa mwili mmoja hivi karibuni.
Nasi tunawatakia kila lililojema katika maandalizi yao.Mungu asimamie kila hatua na Twasubiri kwa Hamu siku yenyewe!!!!!.

Waungwana; Sherehe hizi za WaAfrika zinafanana eehh? vipi kuhusu mambo ya kutoa pesa/Kufichua kabla ujaingia kwa wakwe na Mengine Meengi, Mila/Tamaduni za ndoa. zipi ninyi mnatumia/mlitumia?
 jee bado zina nguvu/Kufaa/Kufuatwa au mmezitupa?.

Jee wewe una Maoni ,Ushauri,gani kuhusu Tamaduni/Mila hizo nivyema kuzitunza na kuzifuata au Zimepitwa na Wakati?.

[To; Willy&farayi;May Good bless you!!!
We are still waiting for the big day!!
With Love From Isaac's Family.]


"SWAHILI na WASWAHLI"Pamoja sana!!!

Sunday, 17 June 2012

Tumalize J'Pili vyema,Burudani-Anita John (Jehovah Jireh) swahili !!!!!!!!!

Waswahili wakisifu na Kuabudu,Da'Anita mwenye blauzi ya maua yenye pink
Natumaini mlikuwa na J'pili njema, Mungu azidi kuwabariki wooote!!!
Tumalizie siku na Zaburi ya 23:1-6;Bwana ndiye Mchungaji wangu,Sitapungukiwa na kitu!.!!!!!
Nawapenda Wooote.!
"SWAHILI na WASWAHILI"   Pamoja sana....

EXTRA BONGO WAZEE WA KIZIGO WAZIDI KULITIKISA JIJI NDANI YA MEEDA SINZA.




Ally Choki akiwaburudisha washabiki na wapenzi wa Extra Bongo ndani ya Meeda usiku wa kuamkia leo
Choki akichea show na wanenguaji wake wa Extra bongo ndani ya Meeda Sinza.
Banza Stone Mwana wa Masanja - AKA Jenerale akiimba nyimbo yake ndani ya Meeda Sinza.

Mmiliki wa KAPINGAZ Blog Henry Kapinga alikuwepo ndani ya Meeda Sinza, hapa akishoo luv na kuwapa Big Up Ally Choki na Banza Stone wakati Extra Bongo walipokuwa wanapamofu usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi huo.
Rapa maarufu namba moja Afrika mashariki wa Extra Bongo Kaba Tano akirap ndani ya Meeda Sinza usiku wa kuamkia leo

Saturday, 16 June 2012

Watoto na Kujifunza Lugha-Pata video ya Mtoto wetu Wa Burundi!!!!

Wazazi/Walezi hapo vipi?Leo sina Mengi nasubiri kutoka kwenu,Mjumbe Hauawiii!!!!"
SWAHILI na WASWAHILI "Pamoja sana!!!!!!!!!!

Friday, 15 June 2012

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-How to cook Russian salad (In Swahili)!!!!!!!

Waungwana; "JIKONI LEO;"Ni Tupike Pamoja wametoa Mapishi mapya ya Russian Salad,kwa njia ya Video.Lugha ni Kiswahili.
 Usikose kujifunza kupitia "TUPIKE PAMOJA" Mmmmmhh Tamu Saaaana.
Kuona mengi zaidi ingia;www.tupikepamoja.com au hapo pembeni kuna nembo yao bonyeza tuu.

 Pamoja sana Waungwana. "SWAHILI na WASWAHILI"

Thursday, 14 June 2012

Siku Kama Ya Leo da'Rehema [RayK] Alizaliwa,Burudani-Hakunaga by Suma Lee!!!!

Mwenyewe RayK
Bibi na Bwana Kiwinga!!!!!
Uzuri tangu Utotoni,ya Kale ni Dhahabu
Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita da'Rehema Alizaliwa.Tunakutakia kila lililo jema katika Maisha yako,Mungu azidi kukulinda wewe na Familia yako.Uwe Baraka kwa watu woote.Tunakupenda na kukuthamini.
Asante kwa yooote,Hakunaga Wifi wa mimi Pamoja Daima.

Swali kwa Waungwana; Hivi nini kinasababisha Mtu na Wifi zake wasielewane?Wivu,Chuki,Tamaa au.......


Karibuni sana kwa Maoni,Mawazo,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

Angalizo; Wifi zangu Sitaki kujifunza Kuharibu Nyumba zenu Akuuu hahahhahhaahahah!!!!!!!

Hakunaga hakunaga hakunaaaaa hakunaaa"Swahili na Waswahili" Pamoja sana.

Wednesday, 13 June 2012

TuMpigie Kura Christina SHUSHO;Viva Shusho Viva Tanzania!!!!!!!!

Waungwana;Tumpigieni Kura Christina Shusho aweze kupata tuzo ya Africa Gospel Music Award 2012
Jinsi ya kupiga kura nenda,
www.africagospelawards.com/nominate.html

VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA   "pamoja Tunaweza"