Sunday, 24 June 2012
Saturday, 23 June 2012
Thursday, 21 June 2012
Watoto na Malezi;Violence Against Children [Ukatili Kwa Watoto]!!!!!!!
Makala hii inaonyesha ukatili dhidi ya watoto na jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakishirikiana na wadau mbalimbali kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.
Makala hii imetengenezwa ikiwa ni mwitikio wa hali ya unyanyasaji na ukatili ambayo watoto wanakabiliana nayo. Makala hii imeandaliwa sambamba na uzinduzi wa ripoti ya ukatili kwa watoto ambalo ni agizo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutokomeza ukatili kwa watoto. Ripoti hii ilizinduliwa na Dr. Asha Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Waungwana;Wazazi/Walezi Mnamaoni,Ushaurigani katika haya?
Shime Wazazi/Walezi;"Tutokomeze Ukatili kwa watoto" Tuungane Pamoja katika kuwapenda,kuwatunza,kuwapa Malezi bora,kuwapatia Elimu na Kuwasikiliza.
"Mtoto wa mwenzio ni wako"."SWAHILI na WASWAHILI" Pamoja sana!!!!
Wednesday, 20 June 2012
RATIBA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU WILLIAM FOFO MAPUNDA!!!!!
WILLIAM FOFO MAPUNDA (FOFO)
MWILI WA MAREHEMU WILLIAM FOFO MAPUNDA UTAAGWA RASMI LEO TAREHE 20/06/2012 NYUMBANI KWAKE TABATA KISUKULU TAYARI KWA KUPELEKWA NYUMBANI KWAO MANDA LUDEWA KWA MAZISHI, AMBAYO YATAFANYIKA KESHO TAREHE 21/06/2012 SIKU YA ALHAMISI.
RATIBA:
SAA 5.00 ASUBUHI: - MWILI KUWASILI NYUMBANI KWAKE TABATA KISUKULU
SAA 6.00 - 7.00 MCHANA: - CHAKULA KWA WOTE
SAA 7.00 - 8.30 MCHANA: - SALAMU ZA MWISHO (LAST RESPECT)
SAA 8.30 - 9.00 ALASIRI: - MWILI KUFIKA KANISANI (KANISA LA ANGLIKANA TABATA KISUKULU KARIBU NA BAR YA MAZDA)
SAA 9.00 - 10.30 JIONI: - IBADA NA KUAGA KWA WALE AMBAO WATAKUWA WAMECHELEWA NYUMBANI
SAA 10.30 JIONI: - KUANZA SAFARI YA KWENDA MANDA LUDEWA
WILLIAM FOFO MAPUNDA ALIFARIKI GAFLA USIKU WA KUAMKIA JANA NYUMBANI KWAKE TABATA KISUKULU, KWA TAARIFA TULIZOZIPATA KUTOKA KWA MADAKTARI WA HOSPITALI YA AMANA ILALA, KIFO CHAKE KIMESABABISHWA NA KUPATWA NA BLOOD PRESSURE GAFLA.
KWA TAARIFA YOYOTE PIGA NAMBA: 0713-254553
Tuesday, 19 June 2012
TAARIFA YA MSIBA: WILLIAM FOFO MAPUNDA HATUNAYE TENA!!!!!!
Marehemu William Fofo enzi za uhai wake.
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde Ndugu yetu, Rafiki yetu William Fofo maarufu kwa jina la FOFO amefariki dunia usiku huu akiwa nyumbani kwake Tabata.
Taarifa kamili za sababu ya kifo chake bado hatujazipata, pindi tutakapozipata tutawajulisha, kwa sasa taratibu zote inaendelea nyumbani kwake Tabata na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana Ilala Dar es salaam.
Monday, 18 June 2012
Wa Afrika na Sherehe zao,LeoTupo Malawi ni-Kachitsa na Farayi;Tradditional Wedding!!!!
Mwenyewe bi Arusi Mtarajiwa,da'Farayi |
Bwana Arusi Mtarajiwa kaka Willy Kachitsa,Huingii hapo mmpaka utoe pesa!!! |
MmePendeza sana Wapendwa!!!!! |
Mmmmhh Mapenzi Motomoto!!!! |
Nasi tunawatakia kila lililojema katika maandalizi yao.Mungu asimamie kila hatua na Twasubiri kwa Hamu siku yenyewe!!!!!.
Waungwana; Sherehe hizi za WaAfrika zinafanana eehh? vipi kuhusu mambo ya kutoa pesa/Kufichua kabla ujaingia kwa wakwe na Mengine Meengi, Mila/Tamaduni za ndoa. zipi ninyi mnatumia/mlitumia?
jee bado zina nguvu/Kufaa/Kufuatwa au mmezitupa?.
Jee wewe una Maoni ,Ushauri,gani kuhusu Tamaduni/Mila hizo nivyema kuzitunza na kuzifuata au Zimepitwa na Wakati?.
[To; Willy&farayi;May Good bless you!!!
We are still waiting for the big day!!
With Love From Isaac's Family.]
"SWAHILI na WASWAHLI"Pamoja sana!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)