Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 4 July 2012

Wanawake na Urembo-Kunyoa Nyusi -Burudani Kipepeo!!!!!!



Waungwana Leo tuangalie Unyoaji Nyusi, Sikuhizi hata Waume wananyoa Nyusi.
Jee wewe  Unapenda kunyoa nyusi?
 Ungependa Mkeo/Mumeo,Mpenzi wako Anyoe Nyusi?


Jee unatumia njia gani?Jee unapenda kutoa zote au unapunguza tuu?


Hivi Watu wa Zamani nao walinyoa Nyusi?
Kunyoa Nyusi kunaweza kusababisha madhara yoyote kiafya?


Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.


"Swahili NA Waswahili" Pamoja sana!!!

Monday, 2 July 2012

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-Mapishi ya Cold Vegetable Soup - Recipe of (Swahili)!!!!!!


Waungwana "JIKONI LEO" Pata video mpya kutoka "TUPIKE PAMOJA" Wanakuletea mambo ya Supu!!
Supu si Nyama tuu, Ungana nao kupitia www.tupikepamoja.com pia unaweza kuungana nao You tube.
Mhhh Tamu sana!!!!!!!!
 Unaswali au Maoni? Usisite kuongea nao ,Usife nalo....hahahaaha "Pamoja sana Swahili NA Waswahili"

Sunday, 1 July 2012

J'Pili ya leo, Tujifunze kupitia kaka Mubelwa na Mch.F.Shideko !!!!!!!!



Kaka Mubelwa Bandio[Mzee wa Changamoto]

Sijawahi kuhusika na mwisho wa maisha ya mwanadamu kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Kaka Domitian Rutakyamirwa. Na katika kuhusika huku, (tangu kuugua mpaka harakati zilizofuata baada ya kifo chake) nimegundua na kujifunza mengi kuhusu mtu, utu na watu. Ni kwa kupitia maisha ya mwisho ya Kaka Domi, nimeweza kujiakisi na kuakisi mengi yanayoendelea katika maisha yetu wanadamu na kuweka bayana “ndivyo-sivyo” ya maisha yetu.
Binafsi nimeshuhudia maisha yangu yakikaribia kifo tena cha ghafla katika matukio tofauti na bado sikuona ama kujifunza nililojifunza sasa.
Nakumbuka kauli ya mwisho niliyoisikia ikitoka kinywani mwa Kaka Domi ni ile ya kutubu aliyoongozwa na Mchungaji akiwa wodini.
Katika matukio yote niliyokumbana nayo, na ambayo wenzangu baadhi walipoteza maisha, hakuna kati yao aliyepata nafasi ya kutubu na kumuomba Mungu kama alivyofanya Kaka yangu huyu.
Na kama alivyohubiri Mchungaji kwenye ibada ya mazishi, mambo makuu matatu aliyosisitiza ni kuwa
1: Hatujui tutaondoka lini.
2: Hatujui tutaondokea wapi.
3: Hatujui tutaondoka vipi
Domitian, aliyekuwa Kaka, rafiki, Mume, mzazi na mlezi kwa wengi aliishi maisha ambayo yamekuja kudhihirika katika wakati wa uhitaji wake.
ASANTENI NYOTE
Maisha ya Domi yamedhihirisha UMOJA unaotamaniwa na waTanzania hasa wa Washington DC na vitongoji vyake ambao kwa namna moja ama nyingine unakwamishwa na mambo mbalimbali, lakini pale inapotokea tofauti zetu zikawekwa kando kwa ajili ya

 mtu aliyekuwa nasi sote licha ya tofauti zetu, tunaona matunda ya umoja. UMATI unaojitolea kufanikisha jambo kwa namna ya kipekee sana.

Inaendelea.ingia http://changamotoyetu.blogspot.co.uk
                             Marehemu;Domitian Rutakyamirwa; Ulale kwa Amani.[Rafiki wa kaka Mubelwa]

Mahubiri ya Mch. Ferdinand Shideko kwenye ibada ya kumuaga Ndg Domitian Rutakyamirwa iliyofanyika Jumatano June 27, 2012 kwenye kanisa la
The Way Of The Cross Gospel Ministries (at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 2074

U.S.A

Wapendwa; muwe na j'Pili yenye Amani,Baraka,Pendo na Umoja.

Samehe Usamehewe,Mungu atusaidie katika Msamaha!!!!!

            "Swahili NA Waswahili" Nimesamehe na Nawapenda Wooote!!!!!!!

ENGINEER DEUSDEDIT MALULU NA DORIS KASAKA WAMEREMETA KATIKA NDOA YAO TAKATIFU ILIYOFUNGWA JANA.!!!!!


Engineer Deusdedit Malulu akiwa na mke wake kipenzi Doris Joseph Malulu, kwa pamoja wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa Takatifu jana katika kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Mavurunza Kimara.

Engineer Deusdedit Malulu akimvisha pete ya ndoa mke wake mpenzi Doris Kasaka aliyefunga nae ndoa takatifu jana.


Familia ya Mzee Njelu Kasaka wakipiga picha ya kumbukumbu na watoto wao wapendwa Doris Kasaka Malulu na Engineer Deusdedit Malulu waliofunga ndoa takatifu jana jioni.

Maharusi kwa nyuso za furaha wakipiga picha na Mtoto wao.



Engineer Deusdedit Malulu na Mkewe Doris wakikata Keki kwa pamoja kuonyesha kuonyesha ishara ya umoja na mapendo.
Meza kuu ya Familia ya Engineer Deusdedit Malulu

Meza kuu ya Wazazi wa Doris Kasaka.


Engineer Deusdedit Malulu na Doris Kasaka walifunga ndoa takatifu katika kanisa la Katoliki Parokia ya Mavurunza Kimara jana Tarehe 30/06/2012 na baadae kwenye Sherehe ya nguvu iliyofanyka katika ukumbi wa Luxery Mbezi Mwisho.

Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Shirika la ugavi wa Umeme (TANESCO) Makao Makuu na Bi Harusi ni mwajiriwa wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ZANTEL Dar es salaam.


Swahili na Waswahili Tunawatakia Maisha mema yenye Furaha,Amani na Baraka.

Wednesday, 27 June 2012

SHEREHE YA SENDOFF YA DORIS KASAKA (KAPINGA) ILIVYOFANA USIKU WA JANA NDANI YA DELUXE HALL SINZA!!!!!!!!!!


Doris Kasaka (Kushoto) akiwa na mpambe wake jana ndani ya Deluxe Hall Sinza wakati wa sherehe ya kumuaga (Sendoff) na kumpongeza kwa kufanya maamuzi mazuri.

Mama Mkubwa wa Doris Mama Angelina Mwami akiwakaribisha wageni wakati wa sherehe ya Binti yake ndani ya ukumbi wa Deluxe Sinza.

Baba Mkubwa wa Doris Mzee Njelu Kasaka akiwakaribisha wageni katika sherehe ya kumuaga Binti yake ndani ya Ukumbi wa Deluxe Sinza jana usiku.

Meza kuu ya wazazi wa Doris kutoka kulia ni Mama Njelu Kasaka, Mzee Njelu Kasaka, Dr Mwami na mwisho kushoto ni Mama Mwami.
Doris akipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wenzake kutoka Zantel.


"Swahili na Waswahili" Tunakutakia Safari njema na kila lililo jema na Maandalizi mema ya Ndoa.


Pamoja sana KapingaZ!!!!!!!



Watoto na Malezi-Tatizo la Ndoa za Watoto;Pata Video!!!!!!!

Waungwana "WATOTO NA MALEZI".
Wazazi/Walezi leo Tuangalie NDOA ZA UTOTONI.


Kwanza nikuulize swali;Jee wewe ulilazimishwa kuolewa/Kuoa?jee Mume/Mke uliyenaye ni chaguo lako? .Jee wewe Umekeketwa?.


Sasa turudi kwa Watoto wetu ndugu zetu,wadogo zetu,Jee unafikiri kukeketwa kunawafaa?
Jee Unaushauri,Maoni,Ujumbe gani kwa Wazazi/Walezi na Jamii kwa ujumla kuhusina na Ndoa hizi za Watoto?.


Karibuni sana Tuelimishane kwa Upendo.
"SWAHILI na WASWAHILI" Pamoja sana.