Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 11 July 2012

FELISTA MSOKA AAPISHWA RASMI KUWA WAKILI WA KUJITEGEMEA NA JAJI MKUU OTHMAN CHANDE.!!!


Wakili Felista Msoka
Wakili Felista Msoka akiwa na Mawakili wenzake siku ambayo aliapishwa kuwa Wakili wa kujitegemea.

Wakili Felista Msoka wa katikati na kushoto ni kaka yake Gilbert Msoka na kulia ni rafiki na ndugu wa karibu wa familia ya Msoka ambaye alisoma na kaka yake.
Wakili Felista Msoka akiwa na pacha wake wa kuzaliwa ambaye pia ni Wakili Bi. Yusta Msoka, kwa pamoja wakiwa na furaha kwa kuwa Mawakili.

Wakili Felista Msoka aliapishwa tarehe 6/07/2012 na Jaji Mkuu Othman Chande pamoja na mawakili wengine 286 akiwemo na Waziri wa sheria na Katiba Mh. Mathias Chikawe na kufanya idadi ya mawakili nchini kufikia 2602.
Mtandao huu unapenda kumpongeza kwa mafanikio hayo.

HONGERA SANA.

Tuesday, 10 July 2012

Mswahili Wetu Leo; Da'EMMY KOSGEI,Ameanzia Wapi na Anaendeleaje,Msikileze!!!

Emmy Kosgei;Amepata Tunzo ya Nyimbo Bora ya Injili Barani Afrika 2012.Nyimbo;OLOLO.
Waungwana Mswahili Wetu Leo ni Emmy.
Yeye anatumia Lugha ya  kikuyu kwenye kuimba nyimbo zake,
Pia Mavazi yake Zaidi ni ya Ki Afrika.
 Mimi ananivutia sanaaa na da'Emmy 
 Nimetokea sana kupenda midundo,Mirindimo, Sauti na..... Lakini KIKUYU IMEPIGA CHENGA!!!

Vipi wewe Muungwana Emmy anakuvutia? Zaidi nini?

Ebu Tumsikilize kidogo yeye ni Nani na Ameanzia wapi na Anafanyaje!!!!!

Swahili NA Waswahili Pamoja Sana!!!!
Shukrani; Africanacts na k24Tv
Wimbo Alio upatia Tunzo Ololo!!!!
Emmy akiwa Uk.

Sunday, 8 July 2012

Siku kama ya Leo da'Rukia.H.Penza Alizaliwa,Burudani-Tuselebuke!!!!!!!!!!

Mwenyewe Wifi/da'Rukia
Bibi na Bwana Penza
 
hehehee kaka wa mimi hachezi mbali, hapo chini kaweka mkia wa Taa, nasikia alirithi kwa ba'Mkubwa!!

Waungwana Siku kama ya Leo miaka Kadhaa iliyopita, Bibi na Bwana Haidari walipata mtoto wa kike na Wakamwita Rukia.
Kwanza tunawapongeza Wazazi/Walezi kwa yoote.
Asante pia kwa kumzalia Mke kaka Mashaka!!!!!

Wifi/da'Rukia Tunakutakia kila lililojema leo na siku zote Maishani .
Mungu azidi kukubariki na kukulinda na Akupe Miaka Mingi ili ufanikishe Malengo yako.Uwe Baraka kwa Watu wooote.

Swali:Waungwana;Eti ni kweli kuolewa na mume mwenye dada wengi ni karaha na si Raha?
 Anapo penda kaka ni hapo tuu.........Endelea na Tuselebuke aeeee ......mimi nakuja.......
"SWAHILI na WASWAHILI"Pamoja sana!!


Nawatakia J'Pili Njema;Burudani - Taunet Nelel,Hakuna Mungu kama wewe na Mapambio Meengiii!!!

Wapendwa Nawatakia J'Pili yenye Baraka, Amani na Upendo!!!!
Neno la Leo;Zaburi:67;1-7;
Mungu na Atufadhili na kutubariki,Na Kutuangazia uso wake.Endelea..........

Saturday, 7 July 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Mafikizolo - ndihamba nawe na nyingine nyingiii!!!!!!

Waungwana; Leo ngoja tuwaangalie Hawa "Mafikizolo",
 Jee wewe wanakubamba/Unawapenda?
Nini zaidi kina kuvutia katika Muziki wao?.
Sina Mengi zaidi Nakusikiliza wewe.Twende sote sasa!!
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

EXTRA BONGO WAFUNIKA MBAYA KATIKA UZINDUZI WA UKUMBI WAO MPYA NEW WHITE HOUSE A.K.A BONGO RESORT KIMARA KOROGWE NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.!!!


Rais wa bendi ya Extra Bongo Ally Choki akiimba mbele ya wapenzi na washabiki wa bendi yake ndani ya ukumbi wao mpya New White House aka Bongo Resort Kimara Korogwe jana.

Rogert Hegga Katapila akiimba mbele ya washabiki wao katika ukumbi wao mpya uliopo Kimara Korogwe Dar es salaam.
Ally Choki na Henry

Mnenguaji mahiri wa Extra bongo akiwapagawisha washabiki wao ndani ya Kimara Korogwe.

Wakata nyonga wa kiume wa Extra Bongo wakiwakimbiza washabiki wao ndani ya ukumbi wao mpya Bongo Resort Kimara Korogwe.

 la Extra Bongo Banza Stone A.K.A Makaveli, Generale akipagawisha wapenzi wao ndani ya White Inn Kimara Korogwe.Jembe

Mwanamuziki wa BAIKOKO akiimba mbele ya washabiki wa Extra Bongo ndani ya Kimara Korogwe.

Tunda Man naye hakuwa nyuma katika kuwaburudisha mashabiki wa Extra Bongo.

Mwanamuzi wa Kizazi kipya Bongo Fleva Sheta akiwakimbiza washabiki wake ndani ya ukumbi mpya wa Extra Bongo katika uzinduzi wa ukumbi huo.

Extra Bongo jana walizindua ukumbi wao mpya New White House a.k.a Bongo resort uliopo kimara Korogwe. Uzinduzi huo ulisindikizwa na kundi la bendi ya taarabu Coast modern Taarab chini ya omary tego na Maua Tego, Tunda Man, Cheta na kundi maarufu la BAIKOKO ambalo linapiga muziki wenye maadhi ya utamaduni wa makabila ya watu kutoka Mkoa wa Tanga.

Friday, 6 July 2012

MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE!!!!!


ELCT/KARAGWE DIOCESE
Kwa wadau wote wa Maendeleo
Mkoa wa Kagera
Yah: MAOMBI YA MCHANGO KUFANIKISHA MALENGO YA SHEREHE YA MIAKA 100 YA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA KARAGWE
- NYAKAHANGA DDH
Somo hapo juu linahusika.
Hospitali tajwa inaadhimisha miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma za tiba na afya katika wilaya ya Karagwe. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: Shabaha Yetu ni Huduma Bora za Afya na Tiba
Maadhimisho hayo yatafanyika tangu tarehe 27 Agosti na kilele kuwa tarehe 2 Septemba. Katika wiki hii, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutakuwa na maonyesho yatakayoenda sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kwa wananchi watakotembelea mabanda yaliyoandaliwa.
Uchunguzi wa afya kama vile Kisukari, moyo, shinikizo la damu, upimaji wa VVU, uchunguzi wa saratani ya matiti kwa akina mama, huduma za macho na uzazi n.k zitatolewa kwa kushirikiana na wataalam wa ndani na nje ya nchi.
Mbali na huduma hizo, malengo makubwa ya hospitali katika kuadhimisha miaka 100, ni kupambana na changamoto zilizopo wilayani na nchini kwa ujumla katika kutoa huduma bora za afya.
Baadhi ya changamoto hizo ni upungufu wa wataala wa kada mbalimbali na uchakavu wa miundo mbinu.
Kupitia sherehe hizi, hospitali ina mpango wa kuanzisha chuo cha taaluma za afya na tiba wilayani Karagwe mapema mwakani.
Chuo hicho kitatoa wataalam katika fani za Uuuguzi, Uganga, wataalam wa Maabara na Maafisa afya.
Ш Faida za Chuo hiki:
o Kusaidia kupunguza upungufu wa wataalam Mkoani Kagera na nchini kwa ujumla.
o Kusaidia vijana wanaomaliza elimu ya sekondari kupata elimu ya taaluma kwa gharama nafuu, zingatia mkoa hauna chuo cha waganga, ni gharama kubwa kwa wazazi kupeleka watoto wao nje ya mkoa kusomea taaluma hio.
o Chuo kitatoa nafasi nzuri kwa watumishi waliopo kazini kuweza kujiendeleza wakingali katika mazingira ya familia zao hivo kupunguza gharama na usumbufu wa kusomea nje.
o Chuo kitasaidia kuongeza ajira hivo kusaidia katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla.
Katika kufanikisha malengo hayo, jumla ya shilingi 1.8 billion zinahitajika. Ikiwa ni kwa ajili ya uendeshaji wa maadhimisho (utoaji wa huduma bure kwa wiki ya maadhimisho), ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa chuo.
Kwa niaba ya menejiment ya hospitali, nakuomba ewe mpenda maendeleo uchangie kufanikisha malengo haya kwa maendeleo ya sekta ya afya.
Wote watakao changia wataorodheshwa katika kitabu maalum cha kumbukumbu.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu kwa Mganga Mkuu: 0762 751 335 / 0712 916 800 / 0787 785 969
Shukrani
Dr. Andrew Cesari
Mganga Mkuu
Nyakahanga Hospital