Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 12 July 2012

Watoto na Vipaji;Aliyah Kolf -Finale Holland's Got Talent na Natalie Okri-Britain's Got Talent!!!!!!

Waungwana, Wazazi/Walezi; Leo tuangalie Vipaji vya Watoto.
Nafikiri kila mtoto anakipaji chake, Jee unajua kipaji cha mtoto wako?Jee unawezaje kujua mtoto wako anakipaji gani?

 Wewe unakipaji Gani na Nani aligundua Kipaji chako?

Pia Watoto/Watu wengi wanapokuwa/Walipokuwa wadogo wana/Walikuwa na Ndoto ya kuwa/kufanya kitu Ukubwani jee NDoto hizi niza kitoto tuu au Wapo Waliofanisha/Wanaweza kumefanikisha NDOTO zao?

 Jee ulipokuwa Mdogo Ulitamani kuwa Nani/Kufanya Kazi Gani ukiwa mkubwa?Mwalimu,Polisi,Nesi,Mama Ntilie,Muimbaji au........!!
 "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Vituko;FUNNY BEST UGANDAN FEMALE LAWYER on DjDinTV!!!!!!

Wednesday, 11 July 2012

FELISTA MSOKA AAPISHWA RASMI KUWA WAKILI WA KUJITEGEMEA NA JAJI MKUU OTHMAN CHANDE.!!!


Wakili Felista Msoka
Wakili Felista Msoka akiwa na Mawakili wenzake siku ambayo aliapishwa kuwa Wakili wa kujitegemea.

Wakili Felista Msoka wa katikati na kushoto ni kaka yake Gilbert Msoka na kulia ni rafiki na ndugu wa karibu wa familia ya Msoka ambaye alisoma na kaka yake.
Wakili Felista Msoka akiwa na pacha wake wa kuzaliwa ambaye pia ni Wakili Bi. Yusta Msoka, kwa pamoja wakiwa na furaha kwa kuwa Mawakili.

Wakili Felista Msoka aliapishwa tarehe 6/07/2012 na Jaji Mkuu Othman Chande pamoja na mawakili wengine 286 akiwemo na Waziri wa sheria na Katiba Mh. Mathias Chikawe na kufanya idadi ya mawakili nchini kufikia 2602.
Mtandao huu unapenda kumpongeza kwa mafanikio hayo.

HONGERA SANA.

Tuesday, 10 July 2012

Mswahili Wetu Leo; Da'EMMY KOSGEI,Ameanzia Wapi na Anaendeleaje,Msikileze!!!

Emmy Kosgei;Amepata Tunzo ya Nyimbo Bora ya Injili Barani Afrika 2012.Nyimbo;OLOLO.
Waungwana Mswahili Wetu Leo ni Emmy.
Yeye anatumia Lugha ya  kikuyu kwenye kuimba nyimbo zake,
Pia Mavazi yake Zaidi ni ya Ki Afrika.
 Mimi ananivutia sanaaa na da'Emmy 
 Nimetokea sana kupenda midundo,Mirindimo, Sauti na..... Lakini KIKUYU IMEPIGA CHENGA!!!

Vipi wewe Muungwana Emmy anakuvutia? Zaidi nini?

Ebu Tumsikilize kidogo yeye ni Nani na Ameanzia wapi na Anafanyaje!!!!!

Swahili NA Waswahili Pamoja Sana!!!!
Shukrani; Africanacts na k24Tv
Wimbo Alio upatia Tunzo Ololo!!!!
Emmy akiwa Uk.

Sunday, 8 July 2012

Siku kama ya Leo da'Rukia.H.Penza Alizaliwa,Burudani-Tuselebuke!!!!!!!!!!

Mwenyewe Wifi/da'Rukia
Bibi na Bwana Penza
 
hehehee kaka wa mimi hachezi mbali, hapo chini kaweka mkia wa Taa, nasikia alirithi kwa ba'Mkubwa!!

Waungwana Siku kama ya Leo miaka Kadhaa iliyopita, Bibi na Bwana Haidari walipata mtoto wa kike na Wakamwita Rukia.
Kwanza tunawapongeza Wazazi/Walezi kwa yoote.
Asante pia kwa kumzalia Mke kaka Mashaka!!!!!

Wifi/da'Rukia Tunakutakia kila lililojema leo na siku zote Maishani .
Mungu azidi kukubariki na kukulinda na Akupe Miaka Mingi ili ufanikishe Malengo yako.Uwe Baraka kwa Watu wooote.

Swali:Waungwana;Eti ni kweli kuolewa na mume mwenye dada wengi ni karaha na si Raha?
 Anapo penda kaka ni hapo tuu.........Endelea na Tuselebuke aeeee ......mimi nakuja.......
"SWAHILI na WASWAHILI"Pamoja sana!!


Nawatakia J'Pili Njema;Burudani - Taunet Nelel,Hakuna Mungu kama wewe na Mapambio Meengiii!!!

Wapendwa Nawatakia J'Pili yenye Baraka, Amani na Upendo!!!!
Neno la Leo;Zaburi:67;1-7;
Mungu na Atufadhili na kutubariki,Na Kutuangazia uso wake.Endelea..........

Saturday, 7 July 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Mafikizolo - ndihamba nawe na nyingine nyingiii!!!!!!

Waungwana; Leo ngoja tuwaangalie Hawa "Mafikizolo",
 Jee wewe wanakubamba/Unawapenda?
Nini zaidi kina kuvutia katika Muziki wao?.
Sina Mengi zaidi Nakusikiliza wewe.Twende sote sasa!!
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.