Saturday, 21 July 2012
Thursday, 19 July 2012
MWANAFUNZI WA IFM AFARIKI KIFO CHA KUTATANISHA: AOKOTWA MAENEO YA KOKO BEACH AKIWA HAJITAMBUI!!!!
Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake.
Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).
Mwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri.
Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni.
Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.
Aliyevaa Koti jeusi ndio baba mzazi wa Agnes Bwana Bernard King'unza.
Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Baba Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza.
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM.
Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.
Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
"Swahili NA Waswahili" inawapa pole wafiwa.
Ulale kwa Amani da'Agnes
"Swahili NA Waswahili" inawapa pole wafiwa.
Ulale kwa Amani da'Agnes
Tuesday, 17 July 2012
How to make fresh coconut-milk (Tui la Nazi) - By Miriam Rose Kinunda!!!!!
Waungwana "JIKONI LEO"Si mwingine ni da'Miriam Rose Kinunda wa "TASTE OF TANZANIA"
Leo anatuletea jinsi ya kuandaa Tui la Nazi.
Pia kaa Tayari kwa Video mpya zinakuja,Kitabu pia Kipo Njiani.
Kipende chako au........Kujua Zaidi Ingi http://tasteoftanzania.com/blog
Jamani eehh Nazi za Kopo,Box,Unga mzipumzishe haswa mliokuwa Nje ya Nyumbani.
Tena Mwezi wa Ramadhani unakuja kwa Wenzetu Wanaofunga Nazi ndiyo yenyewe au vipi?
Mimi hicho Kibao cha Mbuzi hapa ninapoishi sijakiona,Lakini sina Hofu Jirani yangu anaweza kuwa nacho si wanasema mpende Jirani yako? hahahhaa..
Na jee kwanini kiliitwa Kibao cha Mbuzi?
Jee wewe Unapenda Nazi? na Unapenda kuunga/kuweka kwenye Chakula Gani?
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaana!!!
Monday, 16 July 2012
Da'Sandra-Neema Atimiza Miaka14!!!!!!!
da' Sandra na Rafiki yake da'Frida[Swahili ya Tz na Swahili ya Kenya] wakiwa Drayton Manor ndipo alipofanyia sherehe ndogo na Wanafunzi wenzie.
EXTRA BONGO NEXT LEVEL YAWAAGA WAPENZI NA WASHABIKI WAKE KWA SHOW KALI ILIYOSINDIKIZWA NA MATONYA, Q CHIF NA CHID BENZ NDANI YA UKUMBI WAO MPYA NEW WHITE HOUSE - KIMARA KOROGWE JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba mbele ya mamia ya washabiki wake jana usiku ndani ya Ukumbi wa New White House Kimara Korogwe
Msanii wa kizazi kipya Bongo Fleva Matonya akiwarusha mashabiki wa Extra bongo usiku wa kuamkia leo ndani ya New white house Kimara Korogwe.
Q chif akiimba kwa hisia kali usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa New white house Kimara Korogwe katika show kali ya Extra bongo ya kuwaaga mashabiki wao, usiku wa leo wanaelekea Finland kwa mwaliko rasmi wa kwenda kufanya show kadhaa huko.
Chid Benz kama kawa akiwarusha mashabiki wake.
Matonya na Q Chif
Choki na Chid Benz
Ally Choki akimsikiliza kwa umakini mdhamini mkuu wa Bendi yake Chif Kiumbe, wakati wa show ya kuwaaga washabiki na wapenzi wao iliyofanyika ndani ya ukumbi wa New white house Kimara Korogwe
Subscribe to:
Posts (Atom)