Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 22 July 2012

J'Pili ya Leo Tumsikilize;Masanja Mkandamizaji - Albam Hakuna Jipya, Zaburi ya Wani Fifte!!!!!

Masanja ndiye anayetupa Neno na Burudani J'pili ya leo.
Neno la Leo zaburi :150;1-6;Haleluya.Msifuni MUNGU katika Patakatifu pake;Msifuni katika anga la uweza wake,Endelea...

Nawatakia J'Pili yenye Baraka,Amani,Furaha,Upendo,Unyenyekevu na Fadhili!!
Na kila Mwenye pumzi na  amsifu BWANA.
HALELUYA!!!!!!!

Saturday, 21 July 2012

Chaguo la Mswahili Leo;Marijani Raajab - Salama,Mwajuma,Mwanameka-DDC na kitu cha-Hiba!!!

DJ Wa Swahili NA Waswahili Leo!!

Waungwana "CHAGUO LA MSWAHILI LEO"
 Turudi nyuma kidoogo Tuangalie/Tusikilize Bendi zetu , jee unaonaje Bendi hizi?
 Zinaklukumbusha nini na jee Zinakubamba/Unazipenda?
 Vipi Bendi za kileo na za zamani Tofauti iko wapi?

 Na jee zasasa wanafanya vyema zaidi kwa sababu ya usasa au wanakwenda Kinyume?

Twende sote sasa....... oohh mwajuma pesa hupatikana kwatabu...oohh mwajuma pesa hupatikana kwa shidaaaaa...Bwana Mashakaaaa wachakulalamika oohh kama amekushinda mrudishe kwaooo.......

Mhhhhh  ngoja niishie hapa na Chumvi nimeacha nisije pata Safura bure!!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja sana.

Thursday, 19 July 2012

MWANAFUNZI WA IFM AFARIKI KIFO CHA KUTATANISHA: AOKOTWA MAENEO YA KOKO BEACH AKIWA HAJITAMBUI!!!!


Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake.
Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).

Mwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri.

Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni.



Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.


Aliyevaa Koti jeusi ndio baba mzazi wa Agnes Bwana Bernard King'unza.




Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Baba Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza.


Hawa ni baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM.

Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.

Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.


"Swahili NA Waswahili" inawapa pole wafiwa.
Ulale kwa Amani da'Agnes

Tuesday, 17 July 2012

How to make fresh coconut-milk (Tui la Nazi) - By Miriam Rose Kinunda!!!!!


Waungwana "JIKONI LEO"Si mwingine ni da'Miriam Rose  Kinunda wa "TASTE OF TANZANIA"
Leo anatuletea jinsi ya kuandaa Tui la Nazi.
Pia kaa Tayari kwa Video mpya zinakuja,Kitabu pia Kipo Njiani.
Kipende chako au........Kujua Zaidi Ingi http://tasteoftanzania.com/blog

Jamani eehh Nazi za Kopo,Box,Unga mzipumzishe haswa mliokuwa Nje ya Nyumbani.
Tena Mwezi wa Ramadhani unakuja kwa Wenzetu Wanaofunga Nazi ndiyo yenyewe au vipi?

Mimi hicho Kibao  cha Mbuzi hapa ninapoishi sijakiona,Lakini sina Hofu Jirani  yangu anaweza kuwa nacho si wanasema mpende Jirani yako? hahahhaa..
Na jee kwanini kiliitwa Kibao cha Mbuzi?

Jee wewe Unapenda Nazi? na Unapenda kuunga/kuweka kwenye Chakula Gani?

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaana!!!

Monday, 16 July 2012

Da'Sandra-Neema Atimiza Miaka14!!!!!!!


                      Duuhh miaka 14 si mchezo!!!!!

                     da' Sandra na Rafiki yake da'Frida[Swahili ya Tz na Swahili ya Kenya] wakiwa Drayton Manor ndipo alipofanyia sherehe ndogo na Wanafunzi wenzie.
Shukrani sana kwa Wanafunzi ,Walimu wa Blue Coat

Familia ya Isaac Tunamshukuru sana MUNGU kwa Mema yoote anayotutendea.Asante sana MUNGU kwa kutujalia na kututunzia Sandra.Tunamuweka Mikononi mwako kwa kila Jambo.Wewe watosha BABA.
Asante sana kwa Woote wanaojumuika nasi kwa namna moja au nyingine katika malezi yetu.

MUNGU Azidi kukubariki sana Sandra-Neema,Uwe Baraka kwetu na kwa Watu Wote.

MUNGU Awajalie pia wanaotafuta Watoto.

MUNGU NI MWEMA!!!!!!!!

Unakata Logo/ Wapi utatengenezewa?Fuatana nami!!!!!!!

 
within three days, using the very best professional logo tools designer.

 Logo nzuri ni moja ya njia muhimu na ya pekee kujitambulisha katika soko la bidhaa zako.
 Logo ndio kielelezo cha kampuni yako, na ndio kioo cha kutambulisha bidhaa zako.
 Logo ndio Alama pekee yenye nguvu, na ndio yenye kuzungumza na wateja wako kabla ya kuwasiliana au kukutana nao.
 Basi ili uweze kuwavutia wateja wa bidhaa zako, yakupasa uwe na kielelezo kitakachosema kabla ya wewe kuzungumza.
 Kitu icho si kingine ni ile alama ya utambulisho wa kipekee, aidha ni Logo au lebo za bidhaa zako. Ili uweze kufikia malengo yako ya kibiashara, unaweza kuwasiliana na 99graphix wabunifu wa aina mbali mbali za logo (Nembo).


 99Graphix Design Email: 99graphix@gmail.com http://99graphixdesign.blogspot.com/


Ndiyo waliotengeneza hiyo "Swahili Na Waswhili" hapo juu.
        Pamoja sana.

Jikoni Leo-Mapishi ya coated chicken with chutney - Recipe of (Swahili)!!!!

Waungwana "JIKONI LEO"Si wengine ni "TUPIKE PAMOJA"
Leo wametuletea Mapishi ya Coated Chicken With Chutney.Mmmmhhhh Tamu Sanaaa!!
Hii ni Video Mpya Waungwana Usikose kupitia www.tupikepamoja.com kwa vipimo na kujua zaidi.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja saaaana!!!